耶利米書 21 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

耶利米書 21:1-14

預言耶路撒冷的淪陷

1西底迦王派瑪基雅的兒子巴施戶珥瑪西雅的兒子西番雅祭司來見耶利米的時候,耶利米聽到了耶和華的話。當時,他們對耶利米說: 2「請你為我們求問耶和華,因為巴比倫尼布甲尼撒來攻打我們,或許耶和華會像以往一樣行神蹟,使敵人撤軍。」

3耶利米對他們說:「你們要告訴西底迦4以色列的上帝耶和華說,『看啊,你們與圍城的巴比倫王及其率領的迦勒底人作戰,我要把你們的兵器掉轉過來,我要把它們收集在城中心。 5我要在烈怒中伸出大能的臂膀下手擊打你們, 6我要擊打這城裡的居民和牲畜,使他們死於瘟疫。 7然後,我要把猶大西底迦及其臣僕以及城中逃過瘟疫、戰爭和饑荒的人都交給巴比倫尼布甲尼撒等仇敵,使他們落在想殺滅他們的人手中。巴比倫王必殘酷無情地殺戮他們。這是耶和華說的。』

8耶利米啊,你要告訴百姓,『耶和華說,看啊,我把生命之路和死亡之路擺在你們面前, 9留在這城裡的必死於戰爭、饑荒和瘟疫,出城向迦勒底人投降的必保全性命、逃過一死。 10我必嚴懲這城,向它降禍不降福。它必落在巴比倫王手中,被付之一炬。這是耶和華說的。』

11「你要對猶大的王室說,『你們要聽耶和華的話。 12大衛家啊,耶和華說,

『你們要天天秉公行義,

從壓迫者手中解救受剝削的人,

免得你們的惡行激起我的怒火,

如烈焰燃起,無人能滅。

13耶和華說,耶路撒冷啊,

你座落在山谷之上,

如平原的磐石,

自以為無人能攻擊你,

無人能闖入你的住處。

但我要攻擊你,

14照你的所作所為懲罰你;

我要點燃你的樹林,

燒光你周圍的一切。

這是耶和華說的。』」

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 21:1-14

Mungu Anakataa Ombi La Sedekia

121:1 2Fal 24:18; 1Nya 9:12; 2Fal 25:18; Yer 37:3; 52:1Neno lilimjia Yeremia kutoka kwa Bwana wakati Mfalme Sedekia alipowatuma Pashuri mwana wa Malkiya, na kuhani Sefania mwana wa Maaseya kwake, kusema: 221:2 Mwa 25:22; Yer 32:5; Za 44:1-4; Yer 32:17; Kut 9:28; 2Fal 22:18; Mwa 10:10“Tuulizie sasa kwa Bwana, kwa sababu Nebukadneza mfalme wa Babeli anatushambulia. Labda Bwana atatenda maajabu kwa ajili yetu kama nyakati zilizopita, ili Nebukadneza atuondokee.”

3Lakini Yeremia akawajibu, “Mwambieni Sedekia, 421:4 Yer 32:5; 37:8-10; Isa 13:4‘Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: Ninakaribia kuwageuzia silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo mnatumia kupigana na mfalme wa Babeli na Wakaldayo ambao wako nje ya ukuta wakiwazunguka kwa jeshi. Nami nitawakusanya ndani ya mji huu. 521:5 2Fal 22:13; Yer 6:12; Kut 6:6; 3:20; Yos 10:14; Eze 5:8Mimi mwenyewe nitapigana dhidi yenu kwa mkono wangu ulionyooshwa na mkono wa nguvu, kwa hasira na ghadhabu kali na ukali mwingi. 621:6 Yer 14:12; 7:20Nitawaangamiza waishio katika mji huu, watu na wanyama, nao watauawa kwa tauni ya kutisha. 721:7 Eze 12:14; 2Nya 36:10; Eze 29:19; Hab 1:6; Yer 39:5; 2Fal 25:7; Yer 52:9; 27:6Baada ya hayo, nitamtia Sedekia mfalme wa Yuda, maafisa wake na watu wa mji huu ambao walinusurika tauni, upanga na njaa, mkononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, na kwa adui zao wale wanaotafuta uhai wao. Atawaua kwa upanga; hatakuwa na rehema juu yao au huruma wala kuwasikitikia,’ asema Bwana.

8“Zaidi ya hayo, waambie watu hawa, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Tazama, naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti. 921:9 Yer 14:12; Eze 5:12; Yer 39:18; 45:5; 27:11; 40:9; 39:18Yeyote atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa au tauni. Lakini yeyote atakayetoka na kujisalimisha kwa Wakaldayo ambao wameuzunguka mji huu kwa jeshi, atanusurika, naye ataishi. 1021:10 Yer 20:4; Amo 9:4; Yer 22:3; Isa 1:31; 42:25Nimekusudia kuufanyia mji huu jambo baya, wala si jema. Utatiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto, asema Bwana.’

1121:11 Yer 13:18“Zaidi ya hayo, ambia nyumba ya mfalme ya Yuda, ‘Sikia neno la Bwana, 1221:12 Kut 22:22; Yer 22:3; Isa 1:31; 42:25Ewe nyumba ya Daudi, hili ndilo Bwana asemalo:

“ ‘Hukumuni kwa haki kila asubuhi,

mwokoeni mikononi mwa mdhalimu

yeye aliyetekwa nyara,

la sivyo ghadhabu yangu italipuka

na kuwaka kama moto

kwa sababu ya uovu mlioufanya:

itawaka na hakuna wa kuizima.

1321:13 Nah 2:13; Eze 5:8; 2Sam 5:6-7; Oba 1:3-4; Yer 49:4; 23:30; 50:31; 51:25Niko kinyume nawe, ee Yerusalemu,

wewe uishiye juu ya bonde hili

kwenye uwanda wa juu wa miamba,

asema Bwana,

wewe usemaye, “Ni nani awezaye kuja kinyume chetu?

Nani ataingia mahali pa kimbilio letu?”

1421:14 Mit 1:31; Isa 3:10-11; 2Nya 36:19; 2Fal 19:23; Mao 2:3; Eze 20:47; Yer 17:10Nitawaadhibu kama istahilivyo matendo yenu,

asema Bwana.

Nitawasha moto katika misitu yenu

ambao utateketeza kila kitu kinachowazunguka.’ ”