耶利米書 16 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

耶利米書 16:1-21

耶和華降災難的日子

1耶和華對耶利米說: 2「你不可在這地方娶妻,也不可生兒育女。 3至於在這地方出生的孩子和他們的父母,耶和華說, 4『他們必死於惡疾,無人哀悼,無人埋葬,他們好像地上的糞便。他們必死於戰爭和饑荒,屍首必成為飛鳥和走獸的食物。』」 5耶和華對我說:「你不要進入喪家為他們哀悼悲傷,因為我已收回我賜給這百姓的平安、慈愛和憐憫。這是耶和華說的。 6他們無論尊卑都要死在這裡,無人埋葬,無人哀悼,也無人為他們的死而割傷身體、剃光頭髮。 7無人用食物和酒安慰哀悼者,甚至無人給喪父或喪母者一杯安慰酒。 8你不可進入宴樂之家與他們同坐吃喝。」 9以色列的上帝——萬軍之耶和華說:「在這百姓有生之年,我要使這地方的歡樂聲和新郎新娘的歡笑聲從他們眼前消失。

10「當你把這些話告訴他們的時候,他們會質問你,『耶和華為什麼給我們降這大災難?我們有什麼罪?我們哪裡得罪了我們的上帝耶和華?』 11你要對他們說,『耶和華說,你們的祖先背棄我,去跟隨、供奉、祭拜別的神明;他們背棄我,不遵守我的律法。 12可是,你們的行為比他們更邪惡,一意孤行,不聽從我。 13所以,我要把你們從這裡驅逐到你們和你們祖先都不認識的地方,你們在那裡要日夜供奉別的神明,因為我不再恩待你們。』」

14耶和華說:「時候將到,那時人不再憑把以色列人帶出埃及的耶和華起誓, 15而是憑把他們從流放之地——北方和列國領回來的永活的耶和華起誓。因為我必領他們回到我賜給他們祖先的地方。」

16耶和華說:「看啊,我要召來許多漁夫把他們捕撈上來,我要召來許多獵人去各山嶺和岩穴獵取他們。 17因為我鑒察他們的一切行為,他們無法隱藏,他們的罪惡逃不過我的眼晴。 18首先,我要讓他們因自己的罪與惡而受加倍的報應,因為他們用沒有生命氣息的可憎偶像玷污我的土地,使可厭之物充滿我的產業。」

19耶和華啊,你是我的力量,

是我的堡壘,

是我患難時的避難所。

萬國都要從地極來朝見你,

說:「我們祖先所拜的神像虛假無用,一無是處。

20難道人可以為自己製造神明嗎?

其實那些神明並不是真神。」

21耶和華說:「看啊,這一次我要讓他們知道我的權柄和能力,讓他們知道我是耶和華。」

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 16:1-21

Siku Ya Maafa

1Kisha neno la Bwana likanijia: 216:2 Mwa 19:14; Mt 19:12; 1Kor 7:26-27“Kamwe usioe na kuwa na wana wala binti mahali hapa.” 316:3 Yer 6:21Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana kuhusu wana na binti wazaliwao katika nchi hii, na kuhusu wale wanawake ambao ni mama zao, na wale wanaume ambao ni baba zao: 416:4 Yer 25:33; 9:22; Za 83:10; Kum 28:26; Za 79:1-3; Yer 14:15; 19:7“Watakufa kwa magonjwa ya kufisha. Hawataombolezewa wala kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyosambaa juu ya ardhi. Watakufa kwa upanga na kwa njaa, nazo maiti zao zitakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi.”

5Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana: “Usiingie katika nyumba ambayo kuna chakula cha matanga, usiende kuwaombolezea wala kuwahurumia, kwa sababu nimeziondoa baraka zangu, upendo wangu na huruma zangu kutoka kwa watu hawa,” asema Bwana. 616:6 Yer 9:21; Eze 9:5-6; Law 19:28; 21:5; Isa 22:12; 1:20“Wakubwa na wadogo watakufa katika nchi hii. Hawatazikwa wala kuombolezewa, na hakuna atakayejikatakata au kunyoa nywele za kichwa chake kwa ajili yao. 716:7 Mit 3:6; Eze 24:17; Hos 9:4; 2Sam 3:35; Yer 22:10; Mao 1:9, 16Hakuna yeyote atakayewapa chakula ili kuwafariji wale waombolezao kwa ajili ya wale waliokufa, hata akiwa amefiwa na baba au mama, wala hakuna yeyote atakayewapa kinywaji ili kuwafariji.

816:8 Kut 32:6; Mhu 7:2-4; Yer 15:17“Usiingie katika nyumba ambayo kuna karamu, na kuketi humo ili kula na kunywa. 916:9 Isa 51:3; Amo 6:4-7; Yer 7:34; Isa 22:12-14; Ufu 18:23; Eze 26:13Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, aliye Mungu wa Israeli: ‘Mbele ya macho yako na katika siku zako, nitakomesha sauti zote za shangwe na za furaha, na pia sauti za bibi arusi na bwana arusi mahali hapa.’

1016:10 Kum 29:24; Yer 5:19“Utakapowaambia watu hawa mambo haya yote na wakakuuliza, ‘Kwa nini Bwana ameamuru maafa makubwa kama haya dhidi yetu? Tumefanya kosa gani? Tumetenda dhambi gani dhidi ya Bwana, Mungu wetu?’ 1116:11 Amu 2:12-13; Za 106:35-43; 1Fal 9:9; Neh 9:26-29; Ay 31:27; Kum 29:25-26Basi waambie, ‘Ni kwa sababu baba zenu waliniacha mimi, wakafuata miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu. Waliniacha mimi na hawakuishika sheria yangu,’ asema Bwana. 1216:12 Kut 32:8; Amo 2:4; Mhu 9:3; Yer 13:10; 2Tim 3:13; Yer 7:26; Eze 20:30‘Lakini ninyi mmetenda uovu zaidi kuliko baba zenu. Tazama jinsi ambavyo kila mmoja wenu anafuata ukaidi wa moyo wake mbaya, badala ya kunitii mimi. 1316:13 Kum 4:26-28; Yer 15:4-5; 2Nya 20:7; Yer 5:19; Kum 28:36Kwa hiyo nitawaondoa katika nchi hii na kuwatupa katika nchi ambayo ninyi wala baba zenu hamkuijua, nako huko mtaitumikia miungu mingine usiku na mchana, kwa maana sitawapa fadhili zangu huko.’

1416:14 Kum 15:15; Yer 23:7-8; 29:10; 31:27, 38; 30:3“Hata hivyo, siku zinakuja,” asema Bwana, “wakati ambapo watu hawatasema tena, ‘Hakika kama Bwana aishivyo, aliyewapandisha Waisraeli kutoka Misri,’ 1516:15 Isa 11:11-12; Za 53:6; Yer 3:18; 23:8; 30:3; Eze 38:14; Yoe 3:1; Kum 30:3bali watasema, ‘Hakika kama Bwana aishivyo, aliyewatoa wana wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia.’ Maana nitawarudisha katika nchi niliyowapa baba zao.

1616:16 Amo 4:2; Hab 1:14-15; Amo 9:3; Mik 7:2; 1Sam 26:20“Lakini sasa nitawaagiza wavuvi wengi,” asema Bwana, “nao watawavua. Baada ya hilo, nitawaagizia wawindaji wengi, nao watawawinda kwenye kila mlima na kilima, na katika nyufa za miamba. 1716:17 Mhu 12:14; Mk 4:22; Mit 5:21; Sef 1:12; Yer 32:19; Mwa 3:8; Ebr 4:13Macho yangu yanaziona njia zao zote, hazikufichika kwangu, wala dhambi yao haikusitirika. 1816:18 Hes 35:34; Isa 40:2; Eze 43:7; Ufu 18:6; Isa 65:6; Yer 12:3; Za 101:3Nitawalipiza maradufu kwa ajili ya uovu wao na dhambi yao, kwa sababu wameinajisi nchi yangu kwa maumbo yasiyo na uhai ya vinyago vyao vibaya, na kuujaza urithi wangu na sanamu za kuchukiza.”

1916:19 Yer 3:17; Za 4:2; Isa 2:2; Za 18:2; 2Sam 22:3; Yer 14:22; Isa 40:19; 1Sam 12:21Ee Bwana, nguvu zangu na ngome yangu,

kimbilio langu wakati wa taabu,

kwako mataifa yatakujia

kutoka miisho ya dunia na kusema,

“Baba zetu hawakuwa na chochote zaidi ya miungu ya uongo,

sanamu zisizofaa kitu

ambazo hazikuwafaidia lolote.

2016:20 Isa 37:19; Rum 1:23; Gal 4:8; Za 115:4-7; Yer 2:11Je, watu hujitengenezea miungu yao wenyewe?

Naam, lakini hao si miungu!”

2116:21 Kut 3:15“Kwa hiyo nitawafundisha:

wakati huu nitawafundisha

nguvu zangu na uwezo wangu.

Ndipo watakapojua

kuwa Jina langu ndimi Bwana.