約翰福音 3 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

約翰福音 3:1-36

論重生

1有一個法利賽人名叫尼哥德慕,是猶太人的官。 2一天晚上,他來見耶穌,說:「老師,我們知道你是上帝差來教導人的,因為如果沒有上帝的同在,沒有人能行你所行的神蹟。」

3耶穌說:「我實實在在地告訴你,人若不重生3·3 重生」或譯「生自上面」,7節同。,就不能看見上帝的國。」

4尼哥德慕說:「人老了,怎能重生呢?難道要再進母腹生一次嗎?」

5耶穌說:「我實實在在地告訴你,人如果不是從水和聖靈生的,就不能進上帝的國。 6從肉體生的還是肉體,從聖靈生的才是靈。 7所以我說你們必須重生,你不要驚奇。 8風隨意吹動,你聽見它的聲音,卻不知道它從哪裡來,往哪裡去。凡從聖靈生的人也是這樣。」

9尼哥德慕又問:「這怎麼可能呢?」

10耶穌說:「你是以色列人的教師,還不明白這事嗎? 11我實實在在地告訴你,我們所說的是自己知道的,所見證的是自己見過的,可是你們不肯接受我們的見證。 12我對你們說地上的事,你們尚且不信,要是說天上的事,你們怎麼會信呢? 13除了從天上降下來的人子3·13 從天上降下來的人子」有古卷作:「從天降下、仍舊在天的人子」。以外,沒有人到過天上。 14摩西在曠野怎樣舉起銅蛇,人子也必照樣被舉起來, 15叫一切信祂的人都得到永生。

16「因為上帝愛世人,甚至將祂獨一的兒子賜給他們,叫一切信祂的人不致滅亡,反得永生。 17上帝差祂的兒子到世上來,不是要定世人的罪,而是要藉著祂的兒子拯救世人。 18信祂的人不會被定罪,不信的人已經被定罪,因為他們不信上帝獨一的兒子。 19光來到世上,世人因為自己的行為邪惡而不愛光,反愛黑暗,這就是他們被定罪的原因。 20作惡的人恨光,不肯接近光,恐怕他們的罪行暴露出來。 21但遵行真理的人喜歡接近光,好顯明他所做的是靠上帝做的。」

施洗者約翰論耶穌

22這事之後,耶穌和門徒前往猶太地區,在那裡住下來給人施洗。 23-24那時約翰還沒有入獄,他在靠近撒冷哀嫩也給人施洗。那裡水多,眾人都去受洗。 25約翰的門徒和一個猶太人為了潔淨的禮儀爭辯起來, 26於是門徒來見約翰,說:「老師,你看,以前在約旦河對岸和你在一起、你為祂做見證的那位在給人施洗,眾人都去祂那裡了!」

27約翰回答說:「除非是從天上賞賜下來的,否則人什麼都得不到。 28你們自己可以為我做見證,我說過我不是基督,我只是奉差在祂前面預備道路的。 29娶新娘的是新郎,站在旁邊的朋友聽見新郎的聲音,就會歡喜快樂。因此,我現在也心滿意足了。 30祂必興旺,我必衰微。

31「從天上來的,超越一切;從地上來的,屬於地,他所談論的也不外乎地上的事。那來自天上、超越萬物的, 32要把所見所聞講給人聽,只是沒有人接受祂的見證。 33但已經接受祂見證的人證實了上帝是真實的。 34上帝所差來的,說的是上帝的話,因為上帝將聖靈無限量地賜給祂。 35父愛子,已把萬物交在祂手裡。 36信子的人有永生;不信子的人得不到永生,上帝的烈怒常在他身上。」

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yohana 3:1-36

Nikodemo Amwendea Yesu Usiku

13:1 Yn 7:50; 19:39; Lk 23:13Basi palikuwa na mtu mmoja Farisayo, jina lake Nikodemo, mmoja wa Baraza la Wayahudi3:1 Baraza la Wayahudi hapa ina maana ya Sanhedrin ambalo lilikuwa ndilo Baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi, lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu. lililotawala. 23:2 Yn 2:11; 9:16, 33; Mdo 2:22; 10:38Huyu alimjia Yesu usiku akamwambia, “Rabi, tunajua kuwa wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii uifanyayo wewe, kama Mungu hayuko pamoja naye.”

33:3 Yn 1:13; 1Pet 1:23Yesu akamjibu, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu anayeweza kuuona Ufalme wa Mungu kama hajazaliwa mara ya pili.”

4Nikodemo akauliza, “Awezaje mtu kuzaliwa wakati akiwa mzee? Hakika hawezi kuingia mara ya pili kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe!”

53:5 Tit 3:5Yesu akamwambia, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu yeyote anayeweza kuingia Ufalme wa Mungu kama hajazaliwa kwa maji na kwa Roho. 63:6 Yn 1:13; Mwa 5:3; Za 51:5Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho. 7Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna budi ‘kuzaliwa mara ya pili.’ 83:8 Mk 4:41; Mhu 11:5Upepo huvuma popote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uendako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa na Roho.”

93:9 Yn 6:52, 60Nikodemo akamuuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?”

103:10 Lk 2:46Yesu akamwambia, “Wewe ni mwalimu mashuhuri wa Waisraeli, nawe huelewi mambo haya? 113:11 Yn 1:18; 7:16-17Amin, amin ninakuambia, sisi tunazungumza lile tunalolijua na tunashuhudia lile tuliloliona. Lakini ninyi watu hamkubali ushuhuda wetu. 123:12 Lk 22:67Nimewaambia mambo ya duniani, nanyi hamkuniamini, mtaniaminije basi nitakapowaambia mambo ya mbinguni? 133:13 Mit 30:4; Efe 4:8-10; Ebr 4:14; 9:24Hakuna mtu yeyote aliyekwenda mbinguni isipokuwa yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu. 143:14 Hes 21:8-9; Yn 8:28; 12:32Kama vile Mose alivyomwinua yule nyoka kule jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu. 153:15 Mwa 15:6; Rum 3:22Ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele.

163:16 Rum 5:8; Efe 2:4; Yn 6:29, 40; 11:25-26“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 173:17 Yn 17:8, 21; 20:21; Isa 53:11; Rum 11:14Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kupitia kwake ulimwengu upate kuokolewa. 183:18 Yn 5:24; 1:18; 1Yn 4:9Yeyote amwaminiye hahukumiwi, lakini asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. 193:19 Yn 1:4; 8:12Hii ndiyo hukumu kwamba: Nuru imekuja ulimwenguni, nao watu wakapenda giza kuliko nuru kwa sababu matendo yao ni maovu. 203:20 Efe 5:11-13Kwa kuwa kila atendaye maovu huchukia nuru, wala haji kwenye nuru ili matendo yake maovu yasifichuliwe. 21Lakini yule aishiye kwa ukweli huja kwenye nuru, ili ionekane wazi kwamba matendo yake yametendeka katika Mungu.”

Ushuhuda Wa Yohana Mbatizaji Kuhusu Yesu

223:22 Yn 4:2Baada ya haya, Yesu na wanafunzi wake walikwenda katika nchi ya Uyahudi, nao wakakaa huko kwa muda na kubatiza. 233:23 1Sam 9:4; Mt 3:6Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni karibu na Salimu kwa sababu huko kulikuwa na maji tele. Watu wazima wakamjia huko ili kubatizwa. 243:24 Mt 4:12; 14:3(Hii ilikuwa kabla Yohana hajatiwa gerezani). 253:25 Yn 2:6Mashindano yakazuka kati ya baadhi ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja kuhusu suala la desturi ya kunawa kwa utakaso. 263:26 Mt 23:7; Yn 1:7Wakamwendea Yohana wakamwambia, “Rabi, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ngʼambo ya Mto Yordani, yule uliyeshuhudia habari zake, sasa anabatiza na kila mtu anamwendea!”

273:27 Ebr 5:4; 1Kor 4:7; Yak 1:17Yohana akawajibu, “Hakuna mtu yeyote awezaye kupata kitu chochote isipokuwa kile tu alichopewa kutoka mbinguni. 283:28 Yn 1:20-23; 3:9; Mt 9:15; Flp 2:2; 2Yn 12Ninyi wenyewe ni mashahidi wangu kwamba nilisema, ‘Mimi si Kristo,3:28 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. ila nimetumwa nimtangulie.’ 293:29 Mt 22:2; 2Kor 11:2; Efe 5:25, 27; Ufu 21:9; Wim 5:1Bibi arusi ni wa bwana arusi. Lakini rafiki yake bwana arusi anayesimama karibu naye na kusikiliza kutoka kwake, hufurahi sana aisikiapo sauti ya bwana arusi. Kwa sababu hii furaha yangu imekamilika. 303:30 2Sam 3:1Yeye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi nizidi kuwa mdogo.”

Yeye Aliyetoka Mbinguni

313:31 Yn 8:23; 1Yn 4:5“Yeye ajaye kutoka juu yu juu ya yote, yeye aliye wa duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya yote. 323:32 Yn 8:26; 15:15Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna yeyote anayekubali ushuhuda wake. 333:33 Rum 3:4; 1Yn 5:10Lakini yeyote anayekubali huo ushuhuda anathibitisha kwamba, Mungu ni kweli. 343:34 Isa 42:1; Mt 12:18Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, kwa kuwa Mungu humtoa Roho pasipo kipimo. 353:35 Mt 28:18; Yn 17:2Baba anampenda Mwana, naye ametia vitu vyote mikononi mwake. 363:36 Yn 5:24; 6:47Yeyote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake.”