民數記 27 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

民數記 27:1-23

女兒的繼承權

1西羅非哈約瑟之子瑪拿西的玄孫、瑪吉的曾孫、基列的孫子、希弗的兒子。他的女兒是瑪拉挪阿曷拉密迦得撒。她們前來, 2站在會幕門口對摩西以利亞撒祭司、眾首領和全體會眾說: 3「我們的父親死在曠野,他並沒有跟可拉一夥一起反叛耶和華,而是因自己的罪而死,沒有留下兒子。 4難道因為他沒有兒子,他的名字就要從族中消失嗎?請讓我們在父親的家族中分一份產業吧。」 5摩西就把她們的請求呈到耶和華面前。 6耶和華對摩西說: 7西羅非哈的女兒說得有理。你要從她們父親的家族中分一份產業給她們,讓她們繼承父親的產業。 8你要告訴以色列人,『人死後如果沒有兒子,就由女兒繼承產業; 9如果沒有女兒,就由其兄弟繼承; 10如果沒有兄弟,就由其父的兄弟繼承; 11如果其父沒有兄弟,就由其族中最近的親屬繼承。』」這是耶和華吩咐摩西頒佈給以色列人的律例。

約書亞接替摩西做首領

12耶和華對摩西說:「你上亞巴琳山去眺望我賜給以色列人的土地。 13看了以後,你就要像你哥哥亞倫一樣去祖先那裡了。 14因為會眾在曠野反叛我的時候,你們二人沒有按照我的指示取水,沒有在他們面前尊我為聖。」耶和華指的是米利巴泉事件,發生在曠野的加低斯15摩西對耶和華說: 16「耶和華啊,你是賜人生命的上帝,求你立一個人做會眾的首領, 17帶領他們或進或退,免得你的會眾像沒有牧人的羊群。」 18耶和華對摩西說:「的兒子約書亞心裡有聖靈,你把他召來,按手在他身上, 19讓他站在以利亞撒祭司和全體會眾面前,當著他們的面任命他做首領, 20把你的權柄賜給他,使以色列全體會眾都聽從他。 21遇到事情,他要去以利亞撒祭司那裡,讓祭司藉著烏陵為他求問我。他和全體會眾或進或出都要聽從以利亞撒的指示。」 22摩西遵命而行,把約書亞召來,讓他站在以利亞撒祭司和全體會眾面前, 23然後照耶和華的吩咐按手在他的頭上,任命他做首領。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hesabu 27:1-23

Binti Wa Selofehadi

127:1 Hes 26:33; Yos 17:2, 3; Hes 26:30; Mwa 50:23; 1Nya 2:21Binti za Selofehadi mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, walikuwa wa koo za Manase mwana wa Yosefu. Majina ya hao binti yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa. Walikaribia 227:2 Kut 40:2; Hes 9:6; 1:16; 31:13; 32:2; 36:1ingilio la Hema la Kukutania na kusimama mbele ya Mose, kuhani Eleazari, viongozi na kusanyiko lote, wakasema, 327:3 Hes 26:65; 16:2; 26:33“Baba yetu alikufa jangwani. Hakuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora, ambao walifungamana pamoja dhidi ya Bwana, lakini alikufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe na hakuacha wana. 4Kwa nini jina la baba yetu lifutike kutoka ukoo wake kwa sababu hakuwa na mwana? Tupatie milki miongoni mwa ndugu za baba yetu.”

527:5 Mwa 25:22; Kut 18:19; Hes 9:8; Kut 25:22; Law 24:12-13; Mit 3:5-6Kwa hiyo Mose akalileta shauri lao mbele za Bwana, 6naye Bwana akamwambia Mose, 727:7 Ay 42:15; 17:4; Hes 36:2“Wanachosema binti za Selofehadi ni sawa. Ni lazima kwa hakika uwape milki kama urithi miongoni mwa ndugu za baba yao, na kubadili urithi wa baba yao uwe wao.

8“Waambie Waisraeli, ‘Ikiwa mtu atakufa naye hakuacha mwana, utampa binti yake urithi wake. 9Ikiwa hana binti, wape ndugu zake wa kiume urithi wake. 10Ikiwa hana ndugu wa kiume toa urithi wake kwa ndugu za baba yake. 1127:11 Hes 35:29Ikiwa baba yake hakuwa na ndugu wa kiume, toa urithi wake kwa ndugu wa karibu katika ukoo wake, ili aumiliki. Hili litakuwa dai la sheria kwa Waisraeli, kama Bwana alivyomwamuru Mose.’ ”

Yoshua Kuchukua Nafasi Ya Mose

(Kumbukumbu 31:1-8)

1227:12 Hes 23:14; 33:47; Yer 22:20; Kum 3:23; 32:48-52; Law 14:34Kisha Bwana akamwambia Mose, “Panda juu ya mlima huu katika kilele cha Abarimu uione nchi ambayo nimewapa Waisraeli. 1327:13 Hes 20:12; 31:2; Kum 4:22; 31:14; 32:50; 1Fal 2:1; Hes 20:28Baada ya kuiona, wewe pia utakusanywa pamoja na watu wako kama ndugu yako Aroni alivyokusanywa, 1427:14 Hes 20:1; 20:12; Kut 17:7; Kum 1:37; 32:51; Za 106:32kwa kuwa jumuiya ilipoasi amri yangu kwenye maji katika Jangwa la Sini, wakati jumuiya ilipogombana nami, nyote wawili mliacha kuitii amri yangu ya kuniheshimu kama mtakatifu mbele ya macho yao.” (Haya yalikuwa maji ya Meriba huko Kadeshi, katika Jangwa la Sini.)

15Mose akamwambia Bwana, 1627:16 Hes 16:22; Ay 21:10; Ebr 12:9; Zek 12:1Bwana, Mungu wa roho zote za wanadamu, na amteue mtu juu ya jumuiya hii 1727:17 1Fal 22:17; 2Nya 18:16; Eze 34:5; Zek 10:2; Mt 9:36; Kum 31:2; 1Sam 8:20; 18:13; 2Nya 1:10; 18:16; Amu 3:10ili atoke na kuingia mbele yao, atakayewaongoza katika kutoka kwao na kuingia kwao, ili watu wa Bwana wasiwe kama kondoo wasio na mchungaji.”

1827:18 Mwa 41:38; Hes 11:25; Kum 34:9; Mdo 6:6; Amu 3:10Kwa hiyo Bwana akamwambia Mose, “Mchukue Yoshua mwana wa Nuni, mtu ambaye Roho yuko ndani yake, uweke mkono juu yake. 1927:19 Kum 3:28; 31:14; 31:7Msimamishe mbele ya kuhani Eleazari pamoja na kusanyiko lote, umpe maagizo mbele yao. 2027:20 Ay 1:16; Hes 11:17; 1Sam 10:6; 2Fal 2:15Mpe sehemu ya mamlaka yako ili jumuiya yote ya Waisraeli ipate kumtii. 2127:21 Mwa 25:22; Ay 9:14; Za 106:13; Isa 8:19; 1:13; Mal 2:7; 3:1; Kut 28:30; Yos 9:14; Amu 1:1; 20:18; Law 8:8; Kum 33:8; 1Sam 28:6Atasimama mbele ya kuhani Eleazari, ambaye atapokea maamuzi kwa ajili yake, kwa kuuliza mbele za Bwana kwa ile Urimu.27:21 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha. Kwa amri yake, yeye na jumuiya yote ya Waisraeli watatoka, na kwa amri yake, wataingia.”

22Mose akafanya kama Bwana alivyomwagiza. Akamtwaa Yoshua na kumsimamisha mbele ya kuhani Eleazari na kusanyiko lote. 2327:23 Kum 3:28; Isa 55:4Kisha akaweka mikono yake juu ya kichwa cha Yoshua na kumpa maagizo, kama vile Bwana alivyoelekeza kupitia kwa Mose.