歷代志下 29 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

歷代志下 29:1-36

猶大王希西迦

1希西迦二十五歲登基,在耶路撒冷執政二十九年。他母親叫亞比雅,是撒迦利雅的女兒。 2希西迦效法他祖先大衛,做耶和華視為正的事。

潔淨聖殿

3希西迦元年一月,他開啟耶和華殿的門,重新修理。 4他把眾祭司和利未人召集在東邊的廣場, 5對他們說:「利未人啊,請聽我說!現在你們要潔淨自己,也要潔淨你們祖先的上帝耶和華的殿,除去聖所中的污穢之物。 6我們的祖先行事不忠,做我們的上帝耶和華視為惡的事,背棄祂,轉臉背向祂的居所。 7他們封鎖殿廊的門,吹滅燈火,不在聖所裡向以色列的上帝燒香、獻燔祭。 8因此,耶和華的烈怒臨到猶大耶路撒冷,使他們的遭遇令人恐懼、震驚、嗤笑,正如你們親眼所見的。 9所以我們的祖先死在刀下,我們的妻兒也被擄去。 10現在我決心要與以色列的上帝耶和華立約,好使祂的烈怒轉離我們。 11我的孩子們啊,不要懈怠!因為耶和華揀選你們站在祂面前事奉祂,向祂燒香。」

12於是,利未人開始供職。其中哥轄宗族有亞瑪賽的兒子瑪哈亞撒利雅的兒子約珥米拉利宗族有亞伯底的兒子基士耶哈利勒的兒子亞撒利雅革順宗族有薪瑪的兒子約亞約亞的兒子伊甸13以利撒反宗族有申利耶利亞薩宗族有撒迦利雅瑪探雅14希幔宗族有耶歇示每耶杜頓宗族有示瑪雅烏薛15他們召集其他利未人一起潔淨自己,並遵照王的吩咐和耶和華的命令,進去潔淨耶和華的殿。 16祭司們進入耶和華的殿,把所有污穢之物搬到耶和華殿的院子裡,然後再由利未人運到外面的汲淪溪丟掉。 17他們一月一日開始潔淨的工作,到一月八日已經潔淨到耶和華殿的走廊,又用八天潔淨耶和華的殿,一月十六日完成潔淨的工作。

重新奉獻聖殿

18然後,他們晉見希西迦王,說:「我們已經潔淨了整個耶和華的殿、燔祭壇以及壇上的一切器皿、供餅的桌子及桌子上的一切器皿。 19我們已備齊亞哈斯王對上帝不忠時所廢棄的器皿,並潔淨了它們,現在都放在耶和華的壇前。」

20希西迦王清早起來,召集城中官員一同上到耶和華的殿。 21他們牽來七頭公牛、七隻公綿羊、七隻羊羔和七隻公山羊,作國家、聖所和猶大人的贖罪祭。王吩咐做祭司的亞倫子孫把這些牲畜獻在耶和華的壇上。 22他們宰了公牛,祭司取過血來灑在壇上,然後宰了公綿羊並把血灑在壇上,又宰了羊羔並把血灑在壇上。 23有人把作贖罪祭的公山羊牽到王和會眾面前,他們就將手按在公山羊身上。 24祭司宰了公山羊,把血灑在壇上作贖罪祭,為所有以色列人贖罪,因為王吩咐要為所有以色列人獻上燔祭和贖罪祭。

25王又分派利未人在耶和華的殿裡敲鈸、鼓瑟、彈琴,正如大衛王、王的先見迦得和先知拿單的指示,即耶和華藉先知所吩咐的。 26利未人拿著大衛的樂器侍立在那裡,祭司拿著號角侍立在那裡。 27希西迦下令在壇上獻燔祭。開始獻燔祭時,伴隨著號角聲和以色列大衛的樂器聲,響起了頌讚耶和華的歌聲。 28全體會眾伴著歌聲和號角聲俯伏敬拜,直到獻完燔祭。 29獻完燔祭後,王和所有在場的人都俯伏敬拜。 30希西迦王與眾官員又吩咐利未人用大衛亞薩先見的詩詞頌讚耶和華。他們歡喜地歌唱,並低頭敬拜。

31希西迦說:「你們既然已經把自己獻給了耶和華,現在就把祭物和感恩祭帶到耶和華的殿裡來吧。」於是,會眾就把祭物和感恩祭送來,有些人甘心樂意地送來燔祭。 32會眾獻給耶和華作燔祭的有七十頭公牛、一百隻公綿羊、二百隻羊羔, 33獻為聖物的有六百頭公牛、三千隻綿羊。 34但祭司人數太少,剝不完燔祭牲的皮,於是他們的親族利未人就來幫助他們,直到獻完燔祭,並且別的祭司也潔淨了自己,因為利未人比祭司更誠心潔淨自己。 35他們獻上大量的燔祭,以及很多平安祭祭牲的脂肪和與燔祭同獻的奠祭。

從此,耶和華殿裡的事奉恢復了。 36希西迦和民眾因上帝為他們所做的而歡喜快樂,因為這事情很快成就了。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Nyakati 29:1-36

Hezekia Mfalme Wa Yuda

(2 Wafalme 18:1-12)

129:1 1Nya 3:13; 2Nya 26:5; 2Fal 18:1Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria. 229:2 2Nya 28:1; 34:2Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana kama Daudi baba yake alivyofanya.

329:3 2Fal 18:16; 2Nya 28:24; Mit 8:17Katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa kwanza wa utawala wa alifungua milango ya Hekalu la Bwana, na kuikarabati. 4Akawaingiza makuhani na Walawi ndani na kuwakutanisha katika uwanja upande wa mashariki 529:5 Law 11:44; Neh 13:9; Efe 5:26-27; 1Nya 15:12; 2Nya 35:6; Eze 36:25; Mt 21:12-13; 1Kor 3:16-17; 2Kor 6:16na kusema: “Nisikilizeni mimi, enyi Walawi! Jitakaseni nafsi zenu sasa, mkaitakase na nyumba ya Bwana, Mungu wa baba zenu. Ondoeni uchafu wote kutoka mahali patakatifu. 629:6 Eze 23:35; Dan 9:5-6; 1Nya 5:25; Eze 8:16; Yer 2:27Baba zetu hawakuwa waaminifu, walifanya maovu machoni pa Bwana Mungu wetu na wakamwacha yeye. Wakageuza nyuso zao mbali na Maskani ya Bwana wakamgeuzia visogo vyao. 729:7 2Fal 16:17-18; 2Nya 28:24Pia walifunga milango ya ukumbi wa Hekalu na kuzima taa zake. Hawakufukiza uvumba wala kutoa sadaka yoyote ya kuteketezwa katika mahali patakatifu kwa Mungu wa Israeli. 829:8 Kum 28:25; 2Nya 24:18; Law 26:32; Eze 8:16; Yer 18:16; 1Fal 9:8; Yer 19:8; 29:18Kwa hiyo, hasira ya Bwana ikashuka juu ya Yuda na Yerusalemu, naye akawa amewafanya kitu cha kutisha, cha kushangaza na kitu cha kufanyia mzaha kama mnavyoona kwa macho yenu wenyewe. 929:9 2Nya 28:5-8, 17; Law 26:17Hii ndiyo sababu baba zetu wameanguka kwa upanga na ndiyo sababu wana wetu na binti zetu, pia wake zetu wamekuwa mateka. 1029:10 2Fal 11:17; 2Nya 15:12; Neh 9:38; Ezr 10:3; 2Nya 23:16Sasa ninadhamiria moyoni mwangu kuweka Agano na Bwana, Mungu wa Israeli, ili hasira yake kali igeuziwe mbali nasi. 1129:11 Hes 3:6; 8:6-14; 1Nya 15:2; 1Kor 6:9Wanangu, basi msipuuze jambo hili sasa, kwa kuwa Bwana amewachagua ninyi msimame mbele zake na kumtumikia, mkawe watumishi wake na mkamfukizie uvumba.”

1229:12 Hes 3:17-20; 2Nya 31:15Ndipo Walawi wafuatao wakaanza kazi:

Kutoka kwa Wakohathi,

Mahathi mwana wa Amasai na Yoeli mwana wa Azaria;

kutoka kwa Wamerari,

Kishi mwana wa Abdi na Azaria mwana wa Yahaleleli;

kutoka kwa Wagershoni,

Yoa mwana wa Zima na Edeni mwana wa Yoa;

1329:13 1Nya 6:36kutoka kwa wana wa Elisafani,

Shimri na Yeieli;

kutoka kwa wana wa Asafu,

Zekaria na Matania;

14kutoka kwa wana wa Hemani,

Yehieli na Shimei;

kutoka kwa wana wa Yeduthuni,

Shemaya na Uzieli.

1529:15 1Nya 23:28; Isa 1:25; 2Nya 30:12Walipomaliza kuwakusanya ndugu zao na kujiweka wakfu, wakaingia ndani ili kutakasa Hekalu la Bwana, kama vile mfalme alivyokuwa ameagiza, kwa kufuata neno la Bwana. 1629:16 2Sam 15:23Makuhani wakaingia patakatifu pa Hekalu la Bwana ili kupatakasa. Wakatoa nje penye ua wa Hekalu la Mungu kila kitu kichafu walichokikuta kwenye Hekalu la Bwana. Walawi wakavichukua na kuvipeleka nje katika Bonde la Kidroni. 1729:17 1Fal 6:3Walianza kazi ya utakaso siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza na kufikia siku ya nane ya mwezi huo wakawa wamefikia kwenye ukumbi wa Bwana. Kwa siku zingine nane wakalitakasa Hekalu lenyewe la Bwana wakakamilisha katika siku ya kumi na sita ya mwezi huo wa kwanza.

18Kisha wakaingia ndani kwa Mfalme Hezekia kutoa habari na kusema: “Tumelitakasa Hekalu lote la Bwana, madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa pamoja na vyombo vyake vyote, meza ya kupanga mikate iliyowekwa wakfu, pamoja na vyombo vyake vyote. 1929:19 2Nya 28:24Tumeviandaa na kuvitakasa vyombo vyote vile ambavyo Mfalme Ahazi, kwa kukosa uaminifu kwake, aliviondoa wakati alipokuwa mfalme. Sasa viko mbele ya madhabahu ya Bwana.”

Ibada Hekaluni Yarejeshwa

20Ndipo Mfalme Hezekia akainuka asubuhi na mapema, akakusanya pamoja maafisa wa mji wakakwea hekaluni mwa Bwana. 2129:21 Law 4:13-14Wakaleta mafahali saba, kondoo dume saba, wana-kondoo dume saba na mabeberu saba kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya ufalme, kwa ajili ya mahali patakatifu na kwa ajili ya Yuda. Mfalme akawaamuru makuhani, wazao wa Aroni, kuvitoa vitu hivyo sadaka katika madhabahu ya Bwana. 2229:22 Law 4:18; Hes 18:17; Ebr 9:21; Law 8:14-24Hivyo wakachinja wale mafahali, nao makuhani wakachukua ile damu na kuinyunyiza kwenye madhabahu, halafu wakawachinja wale kondoo dume saba na kunyunyiza hiyo damu yao kwenye madhabahu, kisha wakawachinja wale wana-kondoo dume na kunyunyiza damu yao kwenye madhabahu. 2329:23 Law 4:15, 24Wale mabeberu waliokuwa kwa ajili ya sadaka ya dhambi wakaletwa mbele ya mfalme na kusanyiko nao wakaweka mikono yao juu hao mabeberu. 2429:24 Kut 29:36; Law 4:20-26; Kol 1:20Ndipo makuhani wakawachinja hao mabeberu na kuweka damu yao kwenye madhabahu kwa ajili ya sadaka ya dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli yote, kwa sababu mfalme alikuwa ameamuru hiyo sadaka ya kuteketezwa na hiyo sadaka ya dhambi kwa ajili ya Israeli yote.

2529:25 1Nya 28:19; 2Nya 8:14; 1Sam 22:5; 2Sam 24:11; 1Nya 16:4; 23:6; 25:6; 2Nya 30:12Akawaweka Walawi kwenye Hekalu la Bwana wakiwa na matoazi, vinubi na zeze kama ilivyoagizwa na Daudi na Gadi mwonaji wa mfalme pamoja na nabii Nathani kwani hili lilikuwa limeamriwa na Bwana kupitia manabii wake. 2629:26 1Nya 15:16-24; 23:5; Hes 10:10; 2Nya 12:13; Amo 6:5; 1Nya 16:6Hivyo Walawi wakasimama tayari wakiwa na ala za uimbaji za Daudi na makuhani walikuwa na tarumbeta zao.

2729:27 1Sam 16:16; 2Nya 23:18; 20:21Hezekia akatoa amri ya kutoa sadaka ya kuteketezwa madhabahuni. Walipoanza kutoa sadaka, wakaanza pia kumwimbia Bwana pamoja na tarumbeta na zile ala za uimbaji za Daudi mfalme wa Israeli. 28Kusanyiko lote wakaabudu kwa kusujudu, wakati waimbaji wakiwa wanaimba na wenye tarumbeta wakipiga tarumbeta zao. Yote haya yaliendelea mpaka walipomaliza kutoa ile dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa.

2929:29 2Nya 20:18; Rum 14:11Kutoa sadaka kulipomalizika, mfalme na kila mtu aliyekuwepo pamoja naye wakapiga magoti na kuabudu. 3029:30 Za 32:11; Flp 4:4Mfalme Hezekia na maafisa wake wakawaamuru Walawi kumsifu Bwana kwa maneno ya Daudi na ya Asafu mwonaji. Hivyo wakaimba sifa kwa furaha nao wakainamisha vichwa vyao na kuabudu.

3129:31 Ebr 13:15-16; Kut 35:22; 25:2; Law 7:12; 2Nya 13:9Kisha Hezekia akasema, “Sasa mmejiweka wakfu kwa Bwana. Njooni mlete dhabihu na sadaka za shukrani Hekaluni mwa Bwana.” Hivyo kusanyiko likaleta dhabihu na sadaka za shukrani, nao wote waliokuwa na mioyo ya hiari wakaleta sadaka za kuteketezwa.

32Idadi ya sadaka za kuteketezwa zilizoletwa na kusanyiko zilikuwa mafahali sabini, kondoo dume 100 na wana-kondoo dume 200. Wote hawa walikuwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa Bwana. 33Wanyama waliowekwa wakfu kwa sadaka ya kuteketezwa walikuwa mafahali 600, pamoja na kondoo na mbuzi 3,000. 3429:34 2Nya 35:11; Hes 8:15; 2Nya 30:3; Eze 44:11; 1Nya 29:17; Za 7:10Lakini makuhani walikuwa wachache sana kuweza kuchuna wale wanyama wote wa sadaka za kuteketezwa, kwa hiyo ndugu zao Walawi wakawasaidia mpaka kazi ile ikakamilika na mpaka makuhani wengine walipowekwa wakfu, kwa kuwa Walawi walikuwa makini kujiweka wakfu kuliko walivyokuwa makuhani. 3529:35 Mwa 4:4; 35:14; Hes 15:5-10; Law 3:16; 7:11-21; Kut 29:13Kulikuwa na sadaka nyingi za kuteketezwa, pamoja na mafuta ya wanyama ya sadaka za amani na sadaka za kinywaji ambazo ziliambatana na sadaka za kuteketezwa.

Kwa hiyo huduma ya Hekalu la Bwana ikarudishwa kwa upya. 3629:36 Za 118:23; Mdo 2:41Hezekia pamoja na watu wote wakafurahi kwa sababu ya lile Mungu alilolifanya kwa ajili ya watu wake, kwa kuwa lilitendeka papo hapo.