歷代志上 28 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

歷代志上 28:1-21

大衛對所羅門的囑咐

1大衛以色列的眾首領到耶路撒冷。於是,各支派的首領、各班將領、千夫長、百夫長、負責王和王子的財產及牲畜的官員、宮廷侍臣、顯貴和勇士都來了, 2大衛王站起來說:「我的弟兄,我的人民啊,請聽我說。我本想建造一座殿宇安放耶和華的約櫃,作我們上帝的腳凳,我已準備好建造的材料。 3但上帝對我說,『你不可為我的名建造殿宇,因為你是個戰士,曾流過人的血。』 4以色列的上帝耶和華從我父親家中揀選我做以色列的王,直到永遠。因為祂揀選了猶大支派做首領;在猶大支派中,祂揀選了我父親家;在我父親的眾子中,祂喜悅我,立我做以色列的王。 5耶和華賜給我許多兒子,祂在我眾子中揀選了所羅門,讓他坐以色列的王位,治理耶和華的國。 6耶和華對我說,『你兒子所羅門必建造我的殿宇和庭院,因為我揀選他做我的兒子,我也必做他的父親。 7倘若他像今天一樣繼續堅守我的誡命和典章,我必使他的國度永遠穩固。』 8現在,當著耶和華的會眾——全體以色列人的面,趁著我們的上帝在垂聽,你們要謹遵你們的上帝耶和華的一切誡命,以便你們可以擁有這片佳美之地,並且把它傳給你們的子孫作永遠的產業。

9「我兒所羅門啊,你要認識你父親的上帝耶和華,誠心樂意地事奉祂,因為祂洞察人心,知道人一切的心思意念。倘若你尋求祂,祂必讓你尋見;倘若你背棄祂,祂必永遠丟棄你。 10現在你要謹慎,因為耶和華揀選你來建造殿宇作聖所。你要堅定不移地去做。」

11大衛將殿的走廊、房舍、庫房、樓房、內室和安放施恩座的聖所的圖樣都交給所羅門12又將心裡構想的耶和華殿的院子、四周的房屋、殿的庫房和聖物庫房的圖樣都交給他。 13大衛還讓他知道祭司和利未人的班次、耶和華殿裡各樣的工作及一切所需的器皿, 14製造各種金器銀器所需金銀的分量—— 15金燈臺和金燈的分量,銀燈臺和銀燈的分量——按每座燈臺的用途酌定金銀的分量, 16放供餅的金桌子的分量,銀桌子的分量, 17純金的叉子、碗、瓶的分量,每個金碗和銀碗的分量, 18純金香壇的分量,以及在施恩座上展開翅膀遮蓋耶和華約櫃的基路伯天使的樣式。 19大衛說:「以上這一切都是耶和華親手指示我的,讓我明白工作的細節。」

20大衛又對兒子所羅門說:「你要堅定勇敢地去做!不要懼怕,也不要驚慌,因為我的上帝耶和華必不撇下你,也不丟棄你,祂必與你同在,直到聖殿的一切工作完畢。 21你看,在上帝殿裡司職的各班祭司和利未人已準備就緒,又有各種能工巧匠樂意在各種工作上幫你,眾首領和百姓都聽你調遣。」

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Nyakati 28:1-21

Maandalizi Ya Daudi Ya Kujenga Hekalu

128:1 1Nya 11:10; 29:6; Kut 18:25; 1Nya 27:16; Yos 23:2; 24:1; 1Nya 23:2; Kum 1:15Daudi akawaita maafisa wote wa Israeli wakusanyike huko Yerusalemu: yaani, maafisa walio juu ya makabila, majemadari wa vikosi katika utumishi wa mfalme, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, maafisa wanaosimamia mali zote na mifugo ya mfalme na wanawe, wakiwemo maafisa wa jumba la kifalme, mashujaa na askari wote walio hodari.

228:2 1Sam 10:7; 1Nya 17:2; Za 132:7; Isa 60:13; Ebr 2:11; Kum 17:20; 1Nya 11:1-3; Za 22:22; 2Sam 7:2; 1Fal 8:17; 2Nya 6:7-8Mfalme Daudi akainuka na kusema: “Nisikilizeni ndugu zangu nanyi watu wangu. Nilikuwa na nia ya kujenga nyumba ili iwe mahali pa kukaa Sanduku la Agano la Bwana kwa ajili ya kuwa mahali pa kuwekea miguu ya Mungu wetu, nami nikafanya maandalizi ya kuijenga. 328:3 2Sam 7:5; 1Nya 22:8; 1Fal 5:3; 1Nya 17:4Lakini Mungu akaniambia, ‘Wewe hutajenga nyumba kwa Jina langu, kwa sababu wewe umepigana vita na umemwaga damu.’

428:4 1Nya 17:23-27; 2Nya 6:6; 1Sam 16:1-13; Mwa 49:10; Hes 24:17-19“Hata hivyo, Bwana, Mungu wa Israeli, alinichagua mimi kutoka jamaa yangu yote niwe mfalme juu ya Israeli milele. Alimchagua Yuda kuwa kiongozi na kutoka nyumba ya Yuda akaichagua jamaa yangu na kutoka wana wa baba yangu ikampendeza kunifanya niwe mfalme juu ya Israeli yote. 528:5 1Nya 3:1; 2Sam 12:24; 1Nya 22:9; 14:4-7Miongoni mwa wanangu wote, naye Bwana amenipa wengi, amemchagua Solomoni mwanangu ili kukikalia kiti cha enzi cha ufalme wa Bwana juu ya Israeli. 628:6 2Sam 7:13; 1Nya 22:9-10Aliniambia, ‘Solomoni mwanao ndiye atakayejenga nyumba yangu na nyua zangu, kwa maana nimemchagua yeye kuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake. 728:7 1Nya 22:13; 1Fal 9:4; 11:11Nitaufanya imara ufalme wake milele kama akiendelea kuzishika amri zangu na sheria zangu, kama afanyavyo hivi leo.’

828:8 Kum 6:1; 4:1; 17:14-20“Hivyo basi ninawaagiza mbele za Israeli yote na kusanyiko hili la Bwana naye Mungu wetu akiwa anasikia: Kuweni na bidii kuzifuata amri za Bwana Mungu wenu, ili mpate kumiliki nchi hii nzuri na kuwaachia wana wenu kuwa urithi milele.

928:9 1Nya 29:19; 2Nya 6:30; Za 40:16; Yer 29:13; Kum 4:31; Yos 24:20; Za 9:10; Yer 9:24; Yn 17:3; 2Fal 20:3; Za 101:2; 1Sam 16:7; 1Fal 8:39; 1Nya 29:17; Ufu 2:23; 2Nya 15:2; Mt 7:7; Yak 4:8-10“Nawe Solomoni mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa kujitoa kwa moyo wote na kwa nia ya kumkubali, kwa maana Bwana huuchunguza kila moyo na kujua kila kusudi la kila fikira. Ukimtafuta, ataonekana kwako; bali kama ukimwacha, yeye atakukataa milele. 1028:10 1Nya 22:16; Mit 4:23Angalia basi, kwa maana Bwana amekuchagua wewe ili ujenge Hekalu kuwa mahali patakatifu. Uwe hodari ukafanye kazi hiyo.”

1128:11 Kut 25:9; Ebr 8:9; 1Fal 6:2Ndipo Daudi akampa Solomoni mwanawe kielelezo kwa ajili ya ukumbi wa Hekalu, nyumba zake, vyumba vyake vya hazina, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kufanyia upatanisho. 1228:12 1Nya 12:18; 26:12-20Akampa vielelezo vya yote Roho alikuwa ameviweka moyoni mwake kwa ajili ya kumbi za Hekalu la Bwana na vyumba vyote vilivyolizunguka, kwa ajili ya hazina za Hekalu la Mungu na kwa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu. 13Mfalme pia akampa Solomoni maelekezo kwa ajili ya migawanyo ya huduma za makuhani na Walawi, pia kwa ajili ya kazi zote za huduma katika Hekalu la Bwana. Akampa pia maelezo kuhusu vifaa vyote vya kutumika katika huduma ya Hekalu. 14Akamwagizia uzito wa dhahabu kwa ajili ya vitu vyote vya dhahabu vya kutumika katika huduma mbalimbali, uzito wa fedha kwa ajili ya vitu vyote vya fedha vya kutumika katika huduma mbalimbali. 1528:15 Kut 25:31Uzito wa dhahabu kwa ajili ya vinara vya dhahabu na taa zake, kukiwa na uzito kwa ajili ya kila kinara na taa zake, pamoja na uzito wa fedha kwa ajili ya kila kinara cha fedha na taa zake, kulingana na matumizi ya kila kinara; 1628:16 Kut 25:23; 1Fal 7:48; 2Nya 4:8uzito wa dhahabu kwa ajili ya meza ya mikate iliyowekwa wakfu, uzito wa fedha kwa ajili ya meza ya fedha; 1728:17 Kut 27:3uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya nyuma, mabakuli ya kunyunyizia na vikombe, masinia; uzito wa dhahabu kwa ajili ya kila bakuli la dhahabu; uzito wa fedha kwa ajili ya kila bakuli la fedha; 1828:18 Kut 30:1-10; 25:22; Eze 10:2; Za 68:17; 1Fal 6:23; Za 18:10na uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya madhabahu ya kufukizia uvumba. Pia alimpa kielelezo kwa ajili ya gari, yaani, wale makerubi wa dhahabu waliokunjua mbawa zao na kuweka kivuli juu ya Sanduku la Agano la Bwana.

1928:19 1Fal 6:38; Kut 25:9; 25:40; 26:30Daudi akasema, “Hii yote, ninayo kwa maandishi kutoka mkononi mwa Bwana ulio juu yangu, naye amenipa ufahamu kwa ajili ya habari zote za kielelezo hiki.”

2028:20 2Nya 29:11; Hag 2:4; Kum 4:31; Yos 24:20; 1Fal 6:14; Ebr 13:5; Kum 31:7; Yos 1:5-7; 1Nya 22:13; 1Kor 16:13Daudi pia akamwambia Solomoni mwanawe, “Uwe hodari na moyo mkuu, ukafanye kazi hii. Usiogope wala usifadhaike, kwa maana Bwana aliye Mungu, Mungu wangu yu pamoja nawe. Hatakuacha wala hatakupungukia mpaka kazi hii yote kwa ajili ya utumishi wa Hekalu la Bwana itakapokamilika. 2128:21 1Nya 25:1; Kut 35:25–36:5Migawanyo ya makuhani na Walawi iko tayari kwa ajili ya kazi yote katika Hekalu la Mungu, naye kila mtu mwenye moyo wa kupenda mwenye ustadi katika aina yoyote ya ufundi atakusaidia katika kazi yote. Maafisa na watu wote watatii kila agizo lako.”