歷代志上 23 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

歷代志上 23:1-32

利未人的職務

1大衛年紀老邁,壽數將盡,就立他兒子所羅門以色列王。 2他召集了以色列的眾首領、祭司和利未人。 3凡三十歲以上的利未人都在統計之列,共有三萬八千男子, 4其中有兩萬四千人在耶和華的殿裡司職,六千人做官長和審判官, 5四千人守門,四千人用大衛提供的樂器頌讚耶和華。 6大衛利未革順哥轄米拉利的子孫分成班次。

7革順的兒子有拉但示每8拉但有長子耶歇,還有細坦約珥,共三個兒子, 9都是拉但族的族長。示每的兒子有示羅密哈薛哈蘭三人。 10示每的兒子還有雅哈細拿耶烏施比利亞四人。 11雅哈是長子,細拿是次子。耶烏施比利亞的子孫不多,所以合為一族。

12哥轄暗蘭以斯哈希伯崙烏薛四個兒子。 13暗蘭的兒子是亞倫摩西亞倫和他的子孫永遠被分別出來事奉耶和華,向祂獻至聖之物,在祂面前燒香,奉祂的名祝福,直到永遠。 14上帝的僕人摩西的子孫歸在利未支派的名下。 15摩西的兒子是革舜以利以謝16革舜的長子是細布業17以利以謝只有一個兒子利哈比雅,但利哈比雅子孫眾多。 18以斯哈的長子是示羅密19希伯崙的長子是耶利雅,次子是亞瑪利亞,三子是雅哈悉,四子是耶加緬20烏薛的長子是米迦,次子是耶西雅

21米拉利的兒子是抹利姆示抹利的兒子是以利亞撒基士22以利亞撒終生沒有兒子,只有女兒,同族人基士的兒子娶了她們為妻。 23姆示的三個兒子是末力以得耶利摩24以上是利未各宗族的子孫,他們登記在各自族長的名下,凡二十歲以上的男子都在耶和華的殿裡任職。 25大衛說:「以色列的上帝耶和華已使祂的子民安享太平,祂永遠住在耶路撒冷26利未人再不用抬聖幕和其中的器皿了。」 27按照大衛臨終時的囑咐,二十歲以上的利未人都已被統計。 28他們的任務是幫助亞倫的子孫在耶和華的殿裡司職,管理殿的院子和廂房,負責潔淨聖物等事務。 29他們還負責供餅、做素祭的細麵粉、無酵薄餅的調和、烤製、分量和尺寸。 30他們每天早晚要肅立、頌讚耶和華, 31每逢安息日、朔日23·31 朔日」即每月初一。或其他節期,他們要按照規定的數目將燔祭獻給耶和華, 32並負責看守會幕和聖所,幫助他們的親族——亞倫的子孫在耶和華的殿裡供職。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Nyakati 23:1-32

Jamaa Za Walawi Na Utendaji Wao

123:1 1Fal 1:30-33; 1Nya 28:5; 29:28; 29:22-25Daudi alipokuwa mzee aliyeshiba siku, akamfanya Solomoni mwanawe kuwa mfalme juu ya Israeli.

2Pia akawakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi. 323:3 Hes 8:24; 4:3-49Walawi waliokuwa na umri wa miaka thelathini au zaidi walihesabiwa, nayo hesabu ya wanaume ilikuwa 38,000. 423:4 Ezr 3:8; 2Nya 19:8; Kum 16:18; Eze 44:24; Kum 16:18; 1Nya 26:29Daudi akasema, “Miongoni mwa hawa, 24,000 watasimamia kazi ya Hekalu la Bwana na 6,000 watakuwa maafisa na waamuzi, 523:5 1Nya 15:16; Za 92:3; Neh 12:45; Amo 6:5; 2Nya 29:25-26na 4,000 watakuwa mabawabu, na wengine 4,000 watamsifu Bwana kwa ala za uimbaji nilizotoa kwa ajili ya kusudi hilo.”

623:6 2Nya 23:18; 29:25; 8:14; Kut 6:16; Hes 26:57; 2Nya 35:10; 31:2; Ezr 6:18Daudi akawagawa Walawi katika makundi kufuatana na wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.

Wagershoni

7Wana wa Wagershoni walikuwa wawili:

Ladani na Shimei.

8Wana wa Ladani walikuwa watatu:

Yehieli wa kwanza, Zethamu na Yoeli.

9Wana wa Shimei walikuwa watatu:

Shelomothi,23:9 Yaani Shelomithi; maana yake ni Mpenda amani. Hazieli na Harani.

Hawa watatu walikuwa viongozi wa jamaa za Ladani.

10Nao wana wa Shimei walikuwa wanne:

Yahathi, Zina,23:10 Tafsiri zingine zinamwita Ziza. Yeushi na Beria.

11Yahathi alikuwa wa kwanza na Ziza wa pili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; kwa hiyo walihesabiwa kama jamaa moja, wakapewa wajibu kwa pamoja.

Wakohathi

1223:12 Mwa 46:11; Kut 6:18-20; 1Nya 6:2Wana wa Kohathi walikuwa wanne:

Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

1323:13 Kut 30:7-10; 28:1; Kum 21:5; Hes 6:23; 16:40; Ebr 5:4; Hes 16:40; 1Sam 2:28Wana wa Amramu walikuwa:

Aroni na Mose.

Aroni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za Bwana, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la Bwana milele. 1423:14 Kum 33:1Wana wa Mose mtu wa Mungu walihesabiwa kama sehemu ya kabila la Lawi.

1523:15 Kut 18:4; 2:22Wana wa Mose walikuwa:

Gershomu na Eliezeri.

1623:16 1Nya 26:24-28Wazao wa Gershomu:

Shebueli alikuwa wa kwanza.

17Wazao wa Eliezeri:

Rehabia alikuwa wa kwanza.

Eliezeri alikuwa na mwana mmoja tu, lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.

18Wana wa Ishari:

Shelomithi alikuwa wa kwanza.

1923:19 1Nya 24:23; 26:31Wana wa Hebroni walikuwa:

Yeria alikuwa wa kwanza, wa pili Amaria, wa tatu Yahazieli, na wa nne Yekameamu.

20Wana wa Uzieli walikuwa:

Mika wa kwanza na Ishia wa pili.

Wamerari

2123:21 1Nya 6:19; 24:26Wana wa Merari walikuwa:

Mahli na Mushi.

Wana wa Mahli walikuwa:

Eleazari na Kishi.

2223:22 Hes 36:6Eleazari akafa bila ya kuwa na wana: alikuwa na binti tu. Binamu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.

2323:23 1Nya 24:30Wana wa Mushi:

Mahli, Ederi na Yeremothi; wote walikuwa watatu.

2423:24 Hes 4:3; 10:17-21Hawa walikuwa wazao wa Lawi kwa jamaa zao. Wakuu wa jamaa kama walivyoandikwa kwa majina yao na kuhesabiwa kila mmoja, yaani, wenye uwezo wa kufanya kazi kuanzia miaka ishirini au zaidi, waliohudumu katika Hekalu la Bwana. 25Kwa maana Daudi alikuwa amesema, “Kwa vile Bwana, Mungu wa Israeli amewapa watu wake raha na amekuja kuishi Yerusalemu milele, 26Walawi hawahitaji tena kubeba Maskani wala chombo chochote cha utumishi wake.” 27Kulingana na maagizo ya mwisho ya Daudi, Walawi waliohesabiwa ni wale wa kuanzia umri wa miaka ishirini au zaidi.

2823:28 Neh 13:9; Mal 3:3Wajibu wa Walawi ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aroni kuhudumu katika Hekalu la Bwana: Kuwa wasimamizi wa nyua, vyumba vya pembeni, kutakasa vyombo vitakatifu na utendaji mwingine wowote katika nyumba ya Mungu. 2923:29 Kut 25:30; Law 2:4-7; 6:20-23; 19:35-36; 1Nya 9:29-32Walikuwa wasimamizi wa mikate iliyowekwa mezani, unga kwa ajili ya sadaka za nafaka, mikate isiyotiwa chachu, uokaji na uchanganyaji, pamoja na vipimo vyote vya wingi na ukubwa. 3023:30 1Nya 9:33; Ufu 5:8-14; 2Nya 31:2; 1Nya 6:31-33; Za 135:1-3; Ufu 14:3Pia ulikuwa wajibu wao kila asubuhi kumshukuru na kumsifu Bwana. Iliwapasa pia kufanya hivyo jioni 3123:31 2Fal 4:23; Law 23:4; Kol 2:16; Hes 10:10; Za 81:3; Isa 1:13-14na wakati wowote sadaka za kuteketezwa zilipotolewa kwa Bwana siku za Sabato na kwenye sikukuu za Mwezi Mwandamo na katika sikukuu nyingine zilizoamriwa. Iliwapasa kuhudumu mbele za Bwana mara kwa mara kwa idadi maalum na kwa namna waliyokuwa wamepewa maelekezo.

3223:32 Hes 1:53; 1Nya 6:48; Hes 3:6-8; 2Nya 31:2; Eze 44:14Hivyo Walawi wakafanya wajibu wao katika Hema la Kukutania, katika Mahali Patakatifu chini ya uongozi wa ndugu zao wazao wa Aroni, kwa ajili ya utumishi katika Hekalu la Bwana.