撒母耳記上 18 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

撒母耳記上 18:1-30

掃羅嫉妒大衛

1大衛掃羅說完話後,又見了約拿單,二人一見如故,約拿單像愛自己一樣愛大衛2從那天起,掃羅大衛留在身邊,不讓他再回父親那裡。 3約拿單像愛自己一樣愛大衛,他與大衛立了盟約, 4並把身上的外袍、戰衣、刀、弓和腰帶都送給大衛5無論掃羅大衛辦什麼事,他都表現出色。掃羅派他做軍隊的將領,民眾和掃羅的臣僕都非常滿意。

6大衛殺死了非利士歌利亞以色列人凱旋歸來,婦女們擊鼓彈琴、載歌載舞地從以色列各城出來迎接掃羅王。 7她們跳舞歌唱:「掃羅殺死千千,大衛殺死萬萬。」 8掃羅聽了非常憤怒,說:「她們將萬萬歸功給大衛,將千千歸功給我,只剩我的王位沒有給他了!」 9掃羅從此對大衛起了嫉妒之心。

10第二天,從上帝那裡來的邪靈突然降在掃羅身上,他就在屋子裡叫鬧不停,大衛照常為他彈琴。掃羅當時手上拿著矛, 11他突然把矛投向大衛,心想:「我要把他刺透,釘在牆上。」他投了兩次,大衛都躲過了。

12耶和華離開了掃羅大衛同在,因而掃羅懼怕大衛13他把大衛調離自己身邊,立為千夫長,讓他領兵作戰。 14耶和華與大衛同在,因此他事事成功。 15掃羅看見大衛做事精明,就懼怕他。 16以色列人和猶大人都愛戴他,因為他帶領他們作戰。

17掃羅大衛說:「我要把大女兒米拉嫁給你,但你要英勇作戰,效忠於我,為耶和華爭戰。」掃羅心裡想:「我不要親自動手,我要藉非利士人的手殺他。」 18大衛說:「我算什麼?我的家族在以色列那麼卑微,我怎麼配做王的女婿呢?」 19到了婚禮的日子,掃羅卻把米拉嫁給了米何拉亞得列20掃羅的次女米甲愛上了大衛掃羅知道了非常高興。 21他心裡想:「我把這個女兒給大衛,讓他中圈套,好藉非利士人的手殺掉他。」於是,他對大衛說:「你現在還有一次機會做我的女婿。」 22他又吩咐臣僕,說:「你們私底下告訴大衛,說王很欣賞他,群臣都愛戴他,勸他做王的女婿。」 23掃羅的臣僕把這話告訴了大衛大衛卻說:「做王的女婿豈是一件小事呢?我不過是個貧窮卑微的人。」 24臣僕把這番話回報掃羅25掃羅說:「你們去告訴大衛,就說王只需要一百個非利士人的包皮作聘禮,好向他的敵人報仇。」掃羅想讓大衛死在非利士人的手上。 26臣僕把這番話告訴了大衛大衛欣然答應做王的女婿。期限到來之前, 27大衛和部下出去殺了二百個非利士人,把他們的包皮獻給掃羅,好做王的女婿。掃羅便把女兒米甲嫁給了大衛28掃羅知道耶和華與大衛同在,自己的女兒米甲也愛他, 29就更加懼怕大衛,終生與大衛為敵。

30非利士人的將領常來進犯,大衛每次作戰總比掃羅的其他臣僕出色,因而倍受尊重。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Samweli 18:1-30

Sauli Amwonea Daudi Wivu

118:1 1Sam 19:1; 20:16; 31:2; 2Sam 4:4; 1:26; Mwa 44:30; Kol 2:2; Kum 13:6; 1Sam 20:17; Mit 18:24; Yn 15:17-19; 1Yn 3:12-14Baada ya Daudi kumaliza kuongea na Sauli, roho ya Yonathani ikaambatana na roho ya Daudi, naye akampenda kama nafsi yake mwenyewe. 218:2 1Sam 8:11; 14:52; 17:15Kuanzia siku ile Sauli akamchukua Daudi naye hakumruhusu kurudi nyumbani kwa baba yake. 318:3 1Sam 20:8, 16, 17, 42; 22:8; 23:18; 24:21; 2Sam 21:7Yonathani akafanya agano na Daudi kwa sababu alimpenda kama nafsi yake mwenyewe. 418:4 Mwa 41:42; 2Sam 18:11Yonathani akavua joho alilokuwa amevaa na kumpa Daudi, pamoja na koti lake, silaha zake, hata pamoja na upanga wake, upinde wake na mshipi wake.

518:5 2Sam 5:2Lolote Sauli alilomtuma Daudi kufanya, alitenda kwa hekima, hata Sauli akampa cheo cha juu katika jeshi. Jambo hili likawapendeza watu wote, hata maafisa wa Sauli pia.

618:6 Kut 15:20; 2Sam 1:20; Za 68:25; Amu 11:34; Yer 31:4Watu walipokuwa wanarudi nyumbani baada ya Daudi kumuua yule Mfilisti, wanawake wakaja kutoka pande zote za miji ya Israeli kumlaki Mfalme Sauli kwa kuimba na kucheza, kwa nyimbo za furaha na kwa matari na zeze.

718:7 Kut 15:21; 1Sam 21:11; 29:5; 2Sam 18:3; Amu 5:3; 2Nya 5:13; Za 24:1-10; Isa 5:1Walipokuwa wanacheza, wakaimba:

“Sauli amewaua elfu zake,

naye Daudi makumi elfu yake.”

818:8 1Sam 13:14; 15:8; Mhu 4:4Sauli akakasirika sana; sehemu hii ya kurudia rudia ya wimbo huu ilimkasirisha sana. Akafikiri kuwa, “Wamempa Daudi makumi elfu, lakini mimi wamenipa elfu tu. Apate nini zaidi isipokuwa ufalme?” 918:9 Mwa 4:5; 31:2, 5; Mt 20:15; Lk 15:28Kuanzia wakati ule na kuendelea Sauli akawa na jicho la wivu juu ya Daudi.

1018:10 Amu 9:23; 1Sam 16:14; 10:5; 16:21; 19:7; 17; 6; 1Fal 18:29; Mdo 16:16Kesho yake roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Mungu ikaja kwa nguvu juu ya Sauli. Alikuwa akitabiri nyumbani mwake, wakati Daudi alikuwa akipiga kinubi, kama alivyozoea. Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake; 1118:11 1Sam 20:7, 33; 19:10; Za 132:1akautupa kwa nguvu, akijiambia mwenyewe, “Nitamchoma kwa mkuki abaki hapo ukutani.” Lakini Daudi akamkwepa mara mbili.

1218:12 1Sam 16:13; Yos 1:5; 1Sam 17:37; 20:13; 1Nya 22:11; Amu 16:20Sauli akamwogopa Daudi, kwa sababu Bwana alikuwa pamoja na Daudi, lakini alikuwa amemwacha yeye. 1318:13 Hes 27:17; 2Sam 5:2Kwa hiyo Sauli akamwondoa Daudi mbele yake na kumpa kuwa kiongozi wa watu elfu moja, naye Daudi akatoka na kuingia akiongoza vikosi katika vita. 1418:14 Mwa 39:2, 3; Hes 14:43; 2Sam 7:9; Yos 6:27Katika kila kitu alichofanya, Daudi alipata mafanikio makubwa, kwa sababu Bwana alikuwa pamoja naye. 15Sauli alipoona jinsi alivyokuwa akifanikiwa, akamwogopa. 1618:16 2Sam 5:2Lakini Israeli wote na Yuda walimpenda Daudi, kwa sababu ndiye alikuwa akiwaongoza katika vita vyao.

1718:17 1Sam 17:25; Mwa 29:26; Hes 21:14; 1Sam 20:33; 25:28Sauli akamwambia Daudi, “Huyu hapa binti yangu mkubwa Merabu. Nitakupa umwoe, endapo tu utanitumikia kwa ushujaa na kupigana vita vya Bwana.” Kwa maana Sauli alisema moyoni mwake, “Sitainua mkono wangu dhidi yake. Acha mkono wa Wafilisti uwe juu yake.”

1818:18 Kut 3:11; 1Sam 9:21; 2Sam 7:18; Rut 2:10; Mit 15:33Lakini Daudi akamwambia Sauli, “Mimi ni nani, nayo jamaa yangu ni nini au ukoo wa baba yangu katika Israeli, kwamba mimi niwe mkwewe mfalme?” 1918:19 2Sam 21:8; Amu 7:22Basi ulipofika wakati wa Daudi kupewa Merabu, binti Sauli, huyo binti aliozwa kwa Adrieli, Mmeholathi.

2018:20 Mwa 29:26Basi Mikali binti Sauli alimpenda Daudi, nao walipomwambia Sauli juu ya jambo hili, likampendeza. 2118:21 Kut 10:7; 7:16; Za 7:14-16; Mit 26:24-26; Yer 5:26; 9:8Sauli akawaza, “Nitampa Daudi binti yangu, ili apate kuwa mtego kwake, ili kwamba mkono wa Wafilisti upate kuwa juu yake.” Hivyo Sauli akamwambia Daudi, “Sasa unayo nafasi ya pili ya kuwa mkwe wangu.”

22Ndipo Sauli akawaagiza watumishi wake, akisema, “Zungumzeni na Daudi kwa siri na kumwambia, ‘Tazama, mfalme amependezwa nawe, nao watumishi wake wote wanakupenda. Basi na uwe mkwewe mfalme.’ ”

23Watumishi wa Sauli wakarudia hayo maneno kwa Daudi. Lakini Daudi akasema, “Je, mnafikiri ni jambo dogo kuwa mkwewe mfalme? Mimi ni mtu maskini tu, na nisiyejulikana sana.”

24Watumishi wa Sauli walipomweleza yale Daudi aliyoyasema, 2518:25 Mwa 34:12; Za 8:2; 44:16; Yer 20:10; Kut 22:17Sauli akajibu, “Mwambieni Daudi, ‘Mfalme hataki zawadi nyingine kuwa mahari isipokuwa magovi 100 ya Wafilisti, ili kulipiza kisasi juu ya adui zake.’ ” Mawazo ya Sauli yalikuwa Daudi akaanguke mikononi mwa Wafilisti.

26Watumishi walipomwambia Daudi mambo haya, ikampendeza kuwa mkwewe mfalme. Basi kabla siku iliyopangwa haijafika, 2718:27 2Sam 3:14; 6:16Daudi na watu wake walitoka na kuwaua Wafilisti mia mbili. Akayaleta magovi yao na kupeleka hesabu kamilifu kwa mfalme, ili kwamba apate kuwa mkwewe mfalme. Ndipo Sauli akamwoza Daudi Mikali binti yake.

28Sauli alipotambua kuwa Bwana alikuwa pamoja na Daudi na kwamba Mikali binti yake anampenda Daudi, 2918:29 1Sam 18:20; Mhu 4:4; Yak 2:13Sauli akazidi kumwogopa Daudi, naye Sauli akabaki kuwa adui yake siku zote za maisha yake.

3018:30 1Sam 11:1; Lk 21:15Majemadari wa jeshi la Wafilisti waliendelea kupigana vita na kadiri walivyoendelea kupigana, Daudi akazidi kutenda kwa hekima kuliko maafisa wengine wa Sauli, nalo jina lake likajulikana sana.