尼希米記 1 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

尼希米記 1:1-11

尼希米的禱告

1以下是哈迦利亞的兒子尼希米的記述。

波斯亞達薛西二十年基斯流月1·1 基斯流月」即希伯來曆的九月,陽曆是十一月中旬到十二月中旬。,我在書珊城裡。 2猶大來了我的一個兄弟哈拿尼和一些人,我問他們有關從流亡之地歸回的猶太餘民和耶路撒冷的情況。 3他們回答說:「那些從流亡之地歸回猶大省的人深陷苦難,飽受凌辱。耶路撒冷的城牆已經倒塌,城門也被燒毀。」

4我一聽見這消息,就坐下痛哭,悲傷了好幾天。我在天上的上帝面前禁食禱告,說:

5「天上的上帝耶和華啊,你是偉大而可畏的上帝,你向愛你、守你誡命的人守約,施慈愛。 6僕人在你面前晝夜為你的眾僕人以色列民祈禱,求你睜眼察看,側耳傾聽。我承認以色列人向你所犯的罪,以及我和我的家族所犯的罪。 7我們行事敗壞,沒有遵守你賜給你僕人摩西的誡命、律例和典章。 8求你顧念你對你僕人摩西所說的話,『如果你們不忠,我必把你們驅散到列邦中。 9但如果你們轉向我,謹遵我的誡命,即使你們流落天涯,我也必從那裡把你們召集到我選為我名所在之地。』 10我們是你的僕人、你的子民,是你用大能大力救贖的。 11主啊,求你側耳聽你僕人的禱告,垂聽那些喜愛敬畏你名的眾僕人的祈求,使你僕人今天亨通,在王面前蒙恩。」

我是王的侍酒總管。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Nehemia 1:1-11

Maombi Ya Nehemia

11:1 Neh 10:1; Ezr 7:8; Zek 7:1; Dan 8:2; Neh 2:1; Es 1:2Maneno ya Nehemia mwana wa Hakalia:

Katika mwezi wa Kisleu1:1 Kisleu ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiyahudi; katika kalenda yetu ni Novemba/Desemba (ona pia Zekaria 7:1). katika mwaka wa ishirini, wakati nilikuwa ngomeni katika jumba la kifalme la Shushani, 21:2 Neh 7:2; 2Fal 21:4; Neh 7:6; Yer 52:28Hanani, mmoja wa ndugu zangu, alikuja kutoka Yuda akiwa na watu wengine, nami nikawauliza kuhusu mabaki ya Wayahudi wale walionusurika kwenda uhamishoni na pia kuhusu Yerusalemu.

31:3 Law 26:31; Mao 2:9; Yer 5:10; Law 26:31; 2Fal 25:10; Neh 2:3, 13, 17; Isa 22:9Wakaniambia, “Wale walionusurika kwenda uhamishoni, wale ambao wamerudi kwenye lile jimbo, wako katika taabu kubwa na aibu. Ukuta wa Yerusalemu umebomoka, na malango yake yamechomwa moto.”

41:4 Za 137:1; 2Nya 20:3; Ezr 9:4; Dan 9:3Niliposikia mambo haya, niliketi, nikalia. Kwa siku kadhaa niliomboleza na kufunga na kuomba mbele za Mungu wa mbinguni. 51:5 Kum 7:21; Neh 4:14; Kum 7:9; 1Fal 8:23; Ebr 6:13-18Kisha nikasema:

“Ee Bwana, Mungu wa mbinguni, mkuu na mwenye kuogofya, ambaye hulishika agano lake la upendo na wale wampendao na kutii amri zake, 61:6 2Nya 7:15; 1Fal 8:30; 2Nya 6:40; 1Fal 8:47tega masikio yako, na ufungue macho yako, ili usikie maombi ya mtumishi wako anayoomba mbele yako usiku na mchana kwa ajili ya watumishi wako, watu wa Israeli. Ninaungama dhambi zetu sisi Waisraeli, pamoja na zangu na za nyumba ya baba yangu, tulizotenda dhidi yako. 71:7 Kum 28:14-15; Za 106:6Tumetenda uovu sana mbele zako. Hatukutii amri, maagizo na sheria ulizompa Mose mtumishi wako.

81:8 Mwa 8:1; Law 26:33; Kum 4:25“Kumbuka agizo ulilompa Mose mtumishi wako, ukisema, ‘Kama mkikosa uaminifu, nitawatawanya miongoni mwa mataifa, 91:9 Kum 30:4; Eze 20:34-38; Mik 2:12lakini mkinirudia na kutii amri zangu, ndipo hata kama watu wenu walio uhamishoni wako mbali sana katika miisho ya dunia, nitawakusanya kutoka huko na kuwaleta mahali ambapo nimepachagua kuwa makao kwa ajili ya Jina langu.’

101:10 Kum 9:29; Isa 51:9-11; Dan 9:15“Hawa ni watumishi wako na watu wako, uliowakomboa kwa nguvu zako kuu na mkono wako wenye nguvu. 111:11 2Nya 6:40; Mwa 40:1; 32:11; Isa 26:8Ee Bwana, tega sikio lako na usikie maombi ya huyu mtumishi wako, na maombi ya watumishi wako wanaofurahia kuliheshimu Jina lako. Nipe leo, mimi mtumishi wako, mafanikio kwa kunipa kibali mbele ya mtu huyu.”

Kwa maana nilikuwa mnyweshaji wa mfalme.