士師記 8 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

士師記 8:1-35

基甸擒殺米甸二王

1後來,以法蓮人對基甸說:「你攻打米甸人時為什麼不召我們去?你為什麼這樣對待我們?」他們與他激烈地爭論起來。

2基甸說:「我怎能比得上你們呢?以法蓮人摘剩的葡萄豈不比我們亞比以謝族收穫的葡萄更好嗎? 3上帝把兩名米甸人的首領俄立西伊伯交在了你們手中,我所做的有哪一件能與這事相比呢?我怎能比得上你們呢?」基甸這麼一說,他們的怒氣就平息了。

4基甸率領他的三百人渡過約旦河,雖然疲憊不堪,仍緊追敵人。 5基甸疏割的人說:「我們在追趕西巴撒慕拿兩個米甸王,十分疲憊,請給我的軍隊一些餅吃。」

6疏割的首領卻說:「你還沒有抓到西巴撒慕拿,我們憑什麼給你的軍隊餅吃?」

7基甸說:「好吧,耶和華把西巴撒慕拿交在我們手中後,我必回來用荒野的荊棘抽打你們。」

8基甸又去毗努伊勒提出同樣的請求,也遭到拒絕。 9基甸對那裡的人說:「我凱旋歸來時,必拆毀你們的這座城樓。」

10那時,西巴撒慕拿率領東方各族的殘餘軍隊一萬五千人駐紮在加各,因為已經有十二萬刀兵被殺。 11基甸取道挪巴約比哈東邊遊牧者走的路,出其不意地突襲米甸人。 12米甸二王西巴撒慕拿逃跑,基甸追上去擒住他們,擊潰他們全軍。

13約阿施的兒子基甸從戰場返回,經過希列斯山坡時, 14抓住一個疏割的青年,問他疏割的首領和長老是誰,他就寫下疏割七十七位首領和長老的名字。 15基甸到了疏割,對那裡的人說:「你們曾經譏笑我說,『你還沒有抓到西巴撒慕拿,我們憑什麼給你疲憊的軍隊餅吃?』看!西巴撒慕拿在這裡!」 16說完,就捉住城中的長老,用荒野的荊棘抽打他們。 17他又去拆毀毗努伊勒的城樓,殺了城裡的人。

18基甸西巴撒慕拿:「你們在他泊山殺的人是什麼樣子?」他們回答說:「他們長得像你,都像王子一樣。」

19基甸說:「他們是我同母所生的兄弟,我憑永活的耶和華起誓,如果你們當初不殺他們,今天我就不殺你們了。」 20於是,基甸對長子益帖說:「你殺死他們。」但益帖年紀小,心中害怕,不敢動手。

21西巴撒慕拿基甸說:「你親自動手吧!這是男子漢做的事。」基甸便親手殺了他們,拿走了他們駱駝頸上的月牙飾物。

基甸造以弗得

22以色列人對基甸說:「你從米甸人手中救了我們,請你和你的子孫統治我們。」

23基甸回答說:「我和我子孫都不統治你們,統治你們的是耶和華。 24但我有一個要求,請你們把搶來的耳環都給我。」原來米甸人屬於以實瑪利族,都戴金耳環。

25他們欣然同意,便鋪開一件外衣,各自把搶來的金耳環都放在上面, 26重約二十公斤。此外,還有米甸王的月牙飾物、耳墜、紫袍以及駱駝頸上的金鏈。 27基甸用這些金子造了一件以弗得聖衣,放在自己的家鄉俄弗拉。後來,以色列人拜那件以弗得,玷污自己,使基甸及其全家陷入網羅。

28這樣,米甸人被以色列人征服了,從此一蹶不振。基甸在世之日,以色列境內安享太平四十年。

基甸去世

29約阿施的兒子耶路·巴力返回家鄉居住。 30他有許多妻子,生了七十個兒子。 31他的妾住在示劍,也給他生了一個兒子,他給孩子取名叫亞比米勒32約阿施的兒子基甸年高壽終,葬在亞比以謝族的俄弗拉,在他父親約阿施的墳墓裡。

33基甸剛去世,以色列人便又與眾巴力苟合,奉巴力·比利土為他們的神明, 34忘記了他們的上帝耶和華曾經從四圍的仇敵手中拯救他們, 35也沒有因耶路·巴力——基甸的功績而厚待他的家人。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Waamuzi 8:1-35

Ushindi Wa Gideoni Na Kulipiza Kisasi

18:1 Amu 6:11; Mwa 25:2; Amu 12:1; 2Sam 19:41Basi Waefraimu wakamuuliza Gideoni, “Mbona mmetutenda hivi? Kwa nini hukutuita ulipokwenda kupigana na Wamidiani?” Wakawalaumu kwa ukali sana.

28:2 Hes 26:30Gideoni akawajibu, “Nilichofanya mimi ni nini kulinganisha na kile ninyi mlichofanya? Je, kuokoa masazo ya zabibu za Efraimu si bora kuliko mavuno kamili ya zabibu ya Abiezeri? 38:3 Amu 7:25; Mit 15:1Mungu amewatia Orebu na Zeebu, hao viongozi wa Wamidiani, mikononi mwenu. Je, mimi niliweza kufanya nini kulinganisha na mlichofanya ninyi?” Aliposema hili, hasira yao dhidi yake ikatulia.

48:4 Amu 7:25Gideoni akiwa pamoja na wale watu 300 waliofuatana naye, wakiwa wamechoka na wenye njaa lakini bado wakiwafuatia, wakafika Yordani na kuuvuka. 58:5 Mwa 33:17; Za 83:11; Yer 45:3; Ay 16:7; Za 6:6Akawaambia watu wa Sukothi, “Tafadhali lipatieni jeshi langu mikate, kwa maana wamechoka, nami ningali ninawafuatia Zeba na Salmuna, wafalme wa Midiani.”

68:6 1Sam 25:11Lakini maafisa wa Sukothi wakasema, “Je, mikono ya Zeba na Salmuna tayari mnayo sasa ili tuweze kulipatia jeshi lako mikate?”

7Gideoni akajibu, “Kwa ajili ya hilo tu, Bwana atakapowatia Zeba na Salmuna mkononi mwangu, nitaichana nyama ya miili yenu kwenye miiba ya nyikani na kwenye michongoma.”

88:8 Mwa 32:30; 1Fal 12:25Kutoka hapo alikwea mpaka Penieli na kutoa ombi lile lile, lakini nao watu wa Penieli wakamjibu kama watu wa Sukothi walivyokuwa wamemjibu. 9Hivyo akawaambia watu wa Penieli, “Nitakaporudi baada ya kushinda, nitaubomoa mnara huu.”

108:10 Amu 6:5; Isa 9:4Wakati huu Zeba na Salmuna walikuwa Karkori wakiwa na jeshi lenye watu wapatao 15,000 wale wote waliokuwa wamesalia wa mataifa ya mashariki, kwa kuwa watu wapatao 120,000 wenye panga walikuwa wameuawa. 118:11 Hes 32:42; 32:35Basi Gideoni akakwea kwa njia ya wasafiri mashariki ya Noba na Yogbeha na kulishambulia jeshi ambalo halikushuku lolote. 12Zeba na Salmuna, hao wafalme wawili wa Midiani, wakakimbia lakini yeye Gideoni akawafuata na kuwakamata, akalishinda hilo jeshi lao lote.

138:13 Amu 6:11; 1:35Gideoni mwana wa Yoashi akarudi kutoka vitani kwa kupitia Mwinuko wa Heresi. 148:14 Kut 3:16Akamkamata kijana mmoja wa Sukothi na kumuuliza maswali, naye yule kijana akamwandikia majina ya maafisa sabini wa Sukothi, ambao ni viongozi wa mji. 15Ndipo Gideoni akaja na kuwaambia watu wa Sukothi, “Tazama, hapa wapo Zeba na Salmuna mlionisimanga kwa ajili yao mkisema, ‘Je, mikono ya Zeba na Salmuna tayari mnayo sasa ili tuweze kulipatia jeshi lako mikate?’ ” 168:16 1Sam 14:12Akawachukua hao viongozi wa mji na kuwafundisha watu wa Sukothi somo kwa kuwaadhibu kwa miiba na michongoma ya nyikani. 17Pia akaubomoa mnara wa Penieli na kuwaua watu wa mji.

188:18 Yos 19:22; Amu 4:6Kisha akawauliza Zeba na Salmuna, “Ni watu wa aina gani mliowaua huko Tabori?”

Wakajibu, “Ni watu kama wewe, kila mmoja wao akiwa na nafasi ya uana wa mfalme.”

198:19 Hes 14:21Gideoni akajibu, “Hao walikuwa ndugu zangu, wana wa mama yangu hasa. Hakika kama aishivyo Bwana, kama mngekuwa mmewaacha hai, mimi nisingewaua ninyi.” 20Akamgeukia Yetheri, mwanawe mzaliwa wa kwanza, akasema, “Waue hawa!” Lakini Yetheri hakuufuta upanga wake, kwa sababu aliogopa, kwa kuwa alikuwa bado kijana mdogo tu.

218:21 Za 83:11; Isa 3:18Zeba na Salmuna wakasema, “Njoo ufanye hivyo wewe mwenyewe. ‘Alivyo mtu, ndivyo zilivyo nguvu zake.’ ” Hivyo Gideoni akatoka mbele na kuwaua, naye akayaondoa mapambo kwenye shingo za ngamia zao.

Kisibau Cha Gideoni

22Waisraeli wakamwambia Gideoni, “Ututawale, wewe, wanao na wana wa wana wako, kwa kuwa umetuokoa kutoka mikononi mwa Wamidiani.”

238:23 Kut 16:8; Hes 11:20; 1Sam 8:7; 12:12Lakini Gideoni akawaambia, “Mimi sitatawala juu yenu, wala wanangu hawatatawala juu yenu. Bwana ndiye atakayetawala juu yenu ninyi.” 248:24 Mwa 35:4; 49:27; 16:11; 25:13Naye akasema, “Ninalo ombi moja, kwamba kila mmoja wenu anipatie kipuli kutoka kwenye fungu lake la nyara.” (Ilikuwa desturi ya Waishmaeli kuvaa vipuli vya dhahabu.)

25Wakajibu, “Tutafurahi kuvitoa.” Hivyo wakatanda vazi chini na kila mwanaume akatupia juu yake pete kutoka kwenye fungu lake la nyara. 26Uzito wa pete za dhahabu alizoomba zilifikia shekeli 1,700,8:26 Shekeli 1,700 ni sawa na kilo 19.5. bila kuhesabu mapambo mengine, pete za masikio na mavazi ya zambarau yaliyovaliwa na wafalme wa Midiani, au mikufu iliyokuwa kwenye shingo za ngamia zao. 278:27 Kut 25:4; Amu 17:5; 18:14; Yos 18:23; Kut 10:7; 32:2; Za 106:39Gideoni akatengeneza kisibau kwa kutumia ile dhahabu, ambacho alikiweka katika mji wake, yaani, Ofra. Waisraeli wote wakafanya uasherati kwa kukiabudu huko, nacho kikawa mtego kwa Gideoni na jamaa yake.

288:28 Za 83:2; Amu 3:11; 5:31Hivyo Midiani ikashindwa mbele ya Israeli nayo haikuinua kichwa chake tena. Wakati wa siku za uhai wa Gideoni, nchi ikafurahia amani miaka arobaini.

Kifo Cha Gideoni

298:29 Amu 6:32; 7:1; 6:11Yerub-Baali mwana wa Yoashi akarudi kwenda kuishi katika nyumba yake. 308:30 Amu 9:2, 5, 18, 24; 12:14; 2Fal 10:1Alikuwa na wana sabini wa kwake mwenyewe, kwa kuwa alikuwa na wake wengi. 318:31 Mwa 22:24; Amu 9:1; 10:1; 2Sam 11:21Suria wake, aliyekuwa anaishi huko Shekemu, pia alimzalia mwana, ambaye alimwita Abimeleki. 328:32 Mwa 15:15Gideoni mwana wa Yoashi akafa akiwa na umri mzuri wa uzee, na akazikwa katika kaburi la Yoashi baba yake huko Ofra ya Waabiezeri.

338:33 Amu 2:11, 13, 19; 9:4, 27, 46Mara tu alipofariki Gideoni, Waisraeli wakarudia hali ya uovu na kufanya uasherati kwa kuabudu Mabaali. Wakamsimamisha Baal-Berithi kuwa mungu wao na 348:34 Amu 3:7; Neh 9:17; Za 78:11, 42wala hawakumkumbuka Bwana Mungu wao, aliyewaokoa kutoka mikononi mwa adui zao wote kutoka kila upande. 358:35 Amu 6:32; 9:16Pia wakashindwa kuitendea mema jamaa ya Yerub-Baali (yaani Gideoni) kwa ajili ya mambo yote mema aliyokuwa amefanya kwa ajili yao.