士師記 21 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

士師記 21:1-25

為便雅憫支派娶妻

1以色列人曾在米斯巴起誓不把女兒嫁給便雅憫人。 2他們來到伯特利,坐在上帝面前放聲痛哭,直到黃昏。 3他們說:「以色列的上帝耶和華啊,以色列為何少了一個支派呢?為何發生了這樣的事呢?」 4第二天,眾人清早起來在那裡築了一座祭壇,獻上燔祭和平安祭。 5他們彼此議論說:「我們到米斯巴聚集在耶和華面前的時候,各支派中誰沒有來呢?」原來,他們曾經起誓說:凡不到米斯巴聚集在耶和華面前的人都要被處死。 6以色列人為他們的同胞便雅憫人難過,說:「如今以色列絕了一個支派。 7我們曾經在耶和華面前起誓,決不把女兒嫁給便雅憫人,現在我們應該怎麼辦才能使他們剩下來的人得到妻子呢?」

8他們又查問各支派中誰沒有到米斯巴聚集在耶和華面前,結果發現基列·雅比人缺席, 9因為點兵的時候,沒有一個基列·雅比人在場。 10於是,會眾派出一萬二千精兵,命令他們殺掉基列·雅比人及其婦女和孩子。 11他們對精兵說:「你們所要做的就是消滅所有的男子和已婚婦女。」 12他們在基列·雅比的居民中找到四百名處女,把她們帶回迦南示羅營地。

13全體會眾又派人到臨門岩去跟便雅憫人講和。 14於是,便雅憫人返回了家鄉,以色列人把從基列·雅比居民中留下來的四百個處女給他們做妻子,但還是不夠。 15眾人為便雅憫支派難過,因為耶和華使以色列少了一個支派。

16會眾的長老說:「便雅憫支派的女子都死了,我們應該怎麼辦才能使餘下的人有妻子呢? 17便雅憫的餘民必須成家立後,以免以色列失去一個支派。 18可是我們又不能把女兒嫁給他們,因為我們曾經起誓,『把女兒嫁給便雅憫人的必受咒詛。』」 19有人想起在示羅每年都有耶和華的節期。示羅利波拿以南、伯特利以北至示劍的大路東面。 20於是,他們對便雅憫人說:「你們埋伏在葡萄園裡, 21見到示羅的女子出來跳舞時,就衝出去各自搶一個,帶回便雅憫做妻子。 22倘若她們的父親或弟兄前來抱怨,我們會說,『求你們恩待我們,因為我們從戰場上帶回的女子不夠分給他們做妻子。何況又不是你們把女兒嫁給他們的,所以罪不在你們。』」 23便雅憫人就依計行事,從跳舞的女子中各自搶了一個,帶回自己的家鄉做妻子。他們重建城邑,住在其中。 24於是,以色列人離開那裡,各回自己的支派、宗族和家園。

25那時候,以色列人沒有王,人人各行其是。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Waamuzi 21:1-25

Wabenyamini Watafutiwa Wake

121:1 Yos 9:18; 11:3; Amu 20:1Wana wa Israeli walikuwa wameapa kwa kiapo kule Mispa: “Hapana mtu yeyote atakayemwoza binti yake kwa Wabenyamini.”

2Watu wakaenda Betheli, wakaketi mbele za Mungu mpaka jioni, wakapaza sauti zao, wakalia sana. 3Wakasema, “Ee Bwana, Mungu wa Israeli, kwa nini jambo hili limewapata Waisraeli? Kwa nini kabila moja la Israeli limekosekana?”

421:4 Amu 20:26; 2Sam 24:25Kesho yake asubuhi na mapema watu wakajenga madhabahu na kuleta sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani.

521:5 Amu 5:23; 20:1Ndipo Waisraeli wakasema, “Ni kabila lipi la Israeli ambalo halikufika katika mkutano kumkaribia Bwana?” Kwa kuwa walikuwa wameweka kiapo kikuu kuwa yeyote asiyefika mbele za Bwana huko Mispa, kwa hakika angeuawa.

6Basi Waisraeli wakaghairi kwa ajili ya ndugu zao Wabenyamini, wakasema, “Leo kabila moja limekatiliwa mbali na Israeli. 721:7 Yos 9:18Sasa tutawezaje kuwapa mabinti zetu wawe wake zao kwa hao waliobaki maadamu tumeapa kwa Bwana kuwa hatutawapa binti zetu kuwa wake zao?” 821:8 1Sam 11:1; 31:11; 2Sam 2:4; 21:1; 1Nya 10:11Ndipo wakasema, “Ni kabila lipi la Israeli ambalo halikufika mbele za Bwana huko Mispa?” Wakagundua kuwa hakuna hata mmoja aliyetoka Yabeshi-Gileadi aliyefika kambini kwa ajili ya kusanyiko la mkutano. 9Walipohesabu waliona hakuna mtu yeyote wa Yabeshi-Gileadi aliyekuwepo.

10Ndipo mkutano wakatuma askari 12,000 na wakawaamuru kwenda Yabeshi-Gileadi na kuwaua wale wote waishio huko, walikuwepo wake na watoto. 1121:11 Hes 31:7; 31:17-18Wakasema, “Hilo ndilo mtakalofanya. Ueni kila mtu mume na mke ambaye si bikira.” 1221:12 Yos 18:1Wakakuta kati ya watu walioishi Yabeshi-Gileadi wanawali mia nne ambao hawajakutana kimwili na mwanaume, nao wakawachukua kwenye kambi huko Shilo katika nchi ya Kanaani.

1321:13 Kum 2:28; Yos 15:35; Kum 20:10; Amu 20:47Ndipo mkutano ukatuma ujumbe wa amani kwa Wabenyamini huko katika mwamba wa Rimoni. 14Basi Wabenyamini wakarudi nyumbani mwao, wakapewa wale wanawali wa Yabeshi-Gileadi waliowaponya. Lakini hawakuwatosha wanaume wote.

15Waisraeli wakasikitika kwa ajili ya Wabenyamini, kwa kuwa Bwana ameweka ufa katika makabila ya Israeli. 16Viongozi wa kusanyiko wakasema, “Kwa kuwa wanawake wa Wabenyamini wameangamizwa, tufanyeje ili kuwapatia wake wale wanaume waliosalia? 17Wale waliopona wa Wabenyamini ni lazima tuwape wake, ili wawe na warithi, ili kabila lolote katika Israeli lisifutike. 1821:18 Yos 9:18Hatuwezi kuwapa binti zetu kuwa wake, kwa kuwa sisi Waisraeli tumeapa kiapo hiki: ‘Alaaniwe mtu yeyote ampaye Mbenyamini mke.’ ” 1921:19 Yos 18:1; 1Sam 1:3; Yos 16:1; 16:1; 17:7Ndipo waliposema, “Tazama iko sikukuu ya kila mwaka ya Bwana katika Shilo, kaskazini ya Betheli na mashariki mwa ile barabara itokayo Betheli kwenda Shekemu, upande wa kusini wa Lebona.”

20Hivyo wakawaelekeza Wabenyamini wakisema, “Nendeni mkajifiche kwenye mashamba ya mizabibu, 2121:21 Kut 15:20; Amu 11:34nanyi mwangalie. Wasichana wa Shilo watakapojiunga kwenye kucheza, ninyi tokeni kwenye hayo mashamba ya mizabibu na kila mmoja akamate mwanamke mmoja toka miongoni mwa hao wasichana wa Shilo na mwende nao katika nchi ya Benyamini. 22Baba zao au ndugu zao waume watakapotulalamikia, tutawaambia, ‘Kuweni wakarimu kwetu, nanyi mturuhusu tuwe nao kwa kuwa hatukuweza kumpa kila mtu mke tulipopigana. Lakini ninyi pia hamna hatia, kwa kuwa hamkuwapa wao binti zenu kuwa wake.’ ”

2321:23 Yos 24:28; Amu 20:48Basi hivyo ndivyo Wabenyamini walivyofanya. Wakati wasichana walipokuwa wakicheza, kila mtu akamkamata msichana mmoja akamchukua akaenda naye ili awe mke wake. Kisha wakarudi katika urithi wao na kuijenga upya miji na kuishi humo.

24Wakati huo Waisraeli wakaondoka sehemu ile na kwenda nyumbani kwao, kwenye makabila yao na kwa jamaa zao, kila mmoja kwenye urithi wake mwenyewe.

2521:25 Kut 12:8; Amu 17:6Katika siku hizo kulikuwa hakuna mfalme katika Israeli; kila mtu alifanya kile alichoona ni sawa machoni pake mwenyewe.