列王紀下 19 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

列王紀下 19:1-37

希西迦向以賽亞求助

1希西迦王聽了就撕裂衣服,披上麻衣,進入耶和華的殿。 2他派身披麻衣的宮廷總管以利亞敬、書記舍伯那和祭司中的長者去見亞摩斯的兒子以賽亞先知, 3對他說:「希西迦說,『今天是遭難、蒙羞、受辱的日子,就像嬰兒要出生,產婦卻無力生產一樣。 4亞述王派他的將軍來辱罵永活的上帝,也許你的上帝耶和華聽見那些話,就會懲罰他。所以,請你為我們這些剩下的人禱告。』」 5希西迦王的臣僕說完這些話後, 6以賽亞對他們說:「告訴你們主人,耶和華這樣說,『你不要因亞述王的僕人那些褻瀆我的話而害怕。 7我必驚動19·7 驚動」希伯來文是「使靈進入」。亞述王的心,讓他聽見一些風聲後便返回本國,在那裡死於刀下。』」

希西迦向上帝禱告

8亞述的將軍聽說亞述王已離開拉吉,便回去見王,發現王在攻打立拿9亞述王聽說古實特哈加正前來攻打他,便再次派使者去對希西迦說: 10「不要讓你所倚靠的上帝愚弄你,說什麼耶路撒冷必不會被亞述王攻陷。 11你肯定聽過亞述諸王掃滅列國的事,難道你能倖免嗎? 12我先祖毀滅了歌散哈蘭利色提·拉撒伊甸人,這些國家的神明救得了他們嗎? 13哈馬王、亞珥拔王、西法瓦音城的王、希拿王和以瓦王如今在哪裡呢?」

14希西迦從使者手中接過信,讀完後走進耶和華的殿,在耶和華面前展開信, 15禱告說:「坐在二基路伯天使之上、以色列的上帝耶和華啊,唯有你是天下萬國的上帝,你創造了天地。 16耶和華啊,求你側耳垂聽!耶和華啊,求你睜眼察看!求你聽聽西拿基立派使者來辱罵永活上帝的話。 17耶和華啊,亞述諸王確實掃滅列國,使其土地荒涼, 18把列國的神像丟在火中。因為那些神像只是人用木頭石頭製造的,根本不是神。 19我們的上帝耶和華啊,現在求你從亞述王手中拯救我們,讓天下萬國都知道唯有你是耶和華。」

以賽亞給希西迦的信息

20亞摩斯的兒子以賽亞派人告訴希西迦:「以色列的上帝耶和華說,『我已經聽見你關於亞述西拿基立的禱告。 21以下是耶和華對他的判語,

錫安的居民藐視你,嘲笑你;

耶路撒冷的居民朝你逃竄的背影搖頭。

22你在侮辱、褻瀆誰呢?

你不放在眼裡、

高聲罵的是誰呢?

以色列的聖者!

23你藉你的使者辱罵主,

你說你率領許多戰車上到群山之巔,

上到黎巴嫩的巔峰,

砍下最高的香柏樹和上好的松樹,

征服最高的山和最美的樹林。

24你自誇已在外邦之地挖井取水,

已用腳掌踏乾埃及的河流。

25『難道你不知道這是我在太初所定、

在亙古就籌畫好的嗎?

如今我實現了所定的計劃——

藉著你使堅城淪為廢墟。

26城中的居民軟弱無力,

驚慌失措,羞愧難當,

脆弱如野草和菜蔬,

又像還未長大就被曬焦的房頂草。

27『你起你坐,你出你進,

你向我發怒,我都知道。

28因為你向我發怒,

你狂傲的話達到了我耳中,

我要用鉤子鉤住你的鼻子,

把嚼環放在你嘴裡,

使你原路返回。』

29希西迦啊,我要賜給你們一個兆頭,你們今年要吃野生的,明年也要吃自然生長的,後年要播種收割,栽種葡萄園,吃園中的果子。 30猶大的倖存者要再次向下扎根,向上結果。 31因為將有餘民從耶路撒冷出來,有倖存者從錫安山出來。耶和華必熱切地成就這事。

32「至於亞述王,耶和華說,『他必不能進這城或向這裡射一箭,必不能手持盾牌兵臨城下或修築攻城的高臺。 33他從哪條路來,也將從哪條路回去,他必進不了這城。這是耶和華說的。 34我必為自己和我僕人大衛而保護、拯救這城。』」

35當晚,耶和華的天使到亞述營中殺了十八萬五千人。人們清早起來,發現到處是屍體。 36亞述西拿基立便拔營回國,住在尼尼微37一天,亞述王在他的神明尼斯洛的廟裡祭拜時,他的兩個兒子亞得米勒沙利色用刀殺了他,逃往亞拉臘。他的另一個兒子以撒哈頓繼位。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Wafalme 19:1-37

Hezekia Autafuta Msaada Wa Bwana

(Isaya 37:1-20)

119:1 Mwa 37:34; Hes 14:6Mfalme Hezekia aliposikia haya, akararua nguo zake na kuvaa nguo ya gunia, naye akaenda katika Hekalu la Bwana. 219:2 Yer 19:1; Mwa 37:34Akawatuma Eliakimu msimamizi wa nyumba ya mfalme, Shebna mwandishi, na viongozi wa makuhani, wote wakiwa wamevaa nguo za magunia, waende kwa nabii Isaya mwana wa Amozi. 319:3 Hos 13:13Wakamwambia, “Hili ndilo asemalo Hezekia: Siku hii ni siku ya dhiki, ya kukaripiwa na ya aibu, kama wakati watoto wanapofikia karibu kuzaliwa na kumbe hakuna nguvu ya kuwazaa. 419:4 2Sam 16:12; Yer 37:3Yamkini Bwana, Mungu wako atayasikia maneno ya jemadari wa jeshi, ambaye bwana wake, mfalme wa Ashuru, amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai, tena kwamba atamkemea kwa maneno ambayo Bwana, Mungu wako ameyasikia. Kwa hiyo omba kwa ajili ya mabaki ambao bado wako.”

5Maafisa wa Mfalme Hezekia walipofika kwa Isaya, 619:6 Kum 3:2; Yos 1:9Isaya akawaambia, “Mwambieni bwana wenu, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Usiogope kwa hayo uliyoyasikia, yale maneno ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana nayo. 719:7 Kut 14:24; 2Nya 32:21Sikiliza! Nitatia roho fulani ndani yake ili atakaposikia taarifa fulani, atarudi nchi yake mwenyewe, nami huko nitafanya auawe kwa upanga.’ ”

819:8 2Fal 18:14; Hes 33:20Jemadari wa jeshi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru ameondoka Lakishi, alirudi, akamkuta mfalme akipigana na Libna.

9Basi Senakeribu akapata taarifa kwamba Tirhaka, Mkushi mfalme wa Misri, alikuwa anaenda kupigana naye. Basi akatuma tena wajumbe kwa Hezekia na neno hili: 1019:10 2Fal 18:5“Mwambieni Hezekia mfalme wa Yuda: Usikubali huyo Mungu unayemtumainia akudanganye wakati anaposema, ‘Yerusalemu haitatiwa mkononi mwa mfalme wa Ashuru.’ 11Hakika umesikia yale ambayo wafalme wa Ashuru wametenda kwa nchi zote, wakiwaangamiza kabisa. Je, wewe utaokolewa? 1219:12 2Fal 18:33; Mwa 11:31Je, miungu ya mataifa ambayo yaliangamizwa na baba zangu iliweza kuwaokoa, hiyo miungu ya Gozani, Harani, Resefu, na ya watu wa Edeni waliokuwa Telasari? 1319:13 2Fal 5:7Yuko wapi mfalme wa Hamathi, mfalme wa Arpadi, mfalme wa mji wa Sefarvaimu, au wa Hena au wa Iva?”

Maombi Ya Hezekia

1419:14 2Fal 5:7Hezekia akapokea barua kutoka kwa wale wajumbe, naye akaisoma. Kisha akapanda katika Hekalu la Bwana, akaikunjua mbele za Bwana. 1519:15 Mwa 3:24; Kut 25:22Naye Hezekia akamwomba Bwana akisema: “Ee Bwana, Mungu wa Israeli, uketiye juu ya kiti cha enzi kati ya makerubi, wewe peke yako ndiwe Mungu juu ya falme zote za dunia. Wewe umeumba mbingu na nchi. 1619:16 Za 31:2; Kut 3:16Tega sikio, Ee Bwana, usikie; fungua macho yako, Ee Bwana, uone; sikiliza maneno ambayo Senakeribu ametuma kumtukana Mungu aliye hai.

17“Ni kweli, Ee Bwana, kwamba wafalme wa Ashuru wameyaangamiza mataifa haya na nchi zao. 1819:18 Yer 10:3-10; Mdo 17:29Wameitupa miungu yao kwenye moto na kuiangamiza, kwa kuwa haikuwa miungu, bali miti na mawe tu iliyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. 1919:19 1Sam 12:10; Yos 4:24Sasa basi, Ee Bwana Mungu wetu, tuokoe kutoka mkononi mwake, ili falme zote duniani zipate kujua kwamba wewe peke yako, Ee Bwana, ndiwe Mungu.”

Isaya Anatoa Unabii Wa Kuanguka Kwa Senakeribu

(Isaya 37:21-38)

2019:20 1Fal 9:3Kisha Isaya mwana wa Amozi akapeleka ujumbe kwa Hezekia, akasema: “Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: Nimesikia maombi yako kuhusu Senakeribu mfalme wa Ashuru. 2119:21 Isa 47:1; Mao 2:13; Ay 16:4Hili ndilo neno ambalo Bwana amelisema dhidi yake:

“ ‘Bikira Binti Sayuni anakudharau na kukudhihaki.

Binti Yerusalemu anatikisa kichwa chake unapokimbia.

2219:22 Law 19:2; Hos 11:9Ni nani uliyemtukana na kumkufuru?

Ni nani uliyeinua sauti yako dhidi yake,

na kumwinulia macho yako kwa kiburi?

Ni dhidi ya yule Aliye Mtakatifu wa Israeli!

2319:23 Za 20:7; Eze 31:3Kupitia kwa wajumbe wako

umelundika matukano juu ya Bwana.

Nawe umesema,

“Kwa magari yangu mengi ya vita,

nimepanda juu ya vilele vya milima,

vilele vya juu sana katika Lebanoni.

Nami nimeiangusha mierezi yake mirefu,

misunobari yake iliyo bora sana.

Nimefikia sehemu zake zilizo mbali sana,

misitu yake iliyo mizuri sana.

24Nimechimba visima katika nchi za kigeni

na kunywa maji yake.

Kwa nyayo za miguu yangu

nimekausha vijito vyote vya Misri.”

2519:25 Isa 22:11; Mik 1:6“ ‘Je, hujasikia?

Zamani sana niliamuru hili.

Siku za kale nilipanga hili;

sasa nimelifanya litokee,

kwamba umegeuza miji yenye ngome

kuwa malundo ya mawe.

2619:26 Eze 7:17; Ay 8:12Watu wa miji hiyo wameishiwa nguvu,

wanavunjika mioyo na kuaibishwa.

Wao ni kama mimea katika shamba,

kama machipukizi mororo ya kijani,

kama majani yachipuayo juu ya paa la nyumba,

ambayo hukauka kabla ya kukua.

2719:27 Za 139:1-4“ ‘Lakini ninajua mahali ukaapo,

kutoka kwako na kuingia kwako,

na jinsi unavyoghadhibika dhidi yangu.

2819:28 2Nya 33:11; Eze 29:4Kwa sababu unaghadhibika dhidi yangu,

na ufidhuli wako umefika masikioni mwangu,

nitaweka ndoana yangu puani mwako

na hatamu yangu kinywani mwako,

nami nitakufanya urudi kwa njia ile uliyoijia.’

2919:29 Lk 2:12; Za 107:37“Hii ndiyo itakuwa ishara kwako, ee Hezekia:

“Mwaka huu utakula kile kiotacho chenyewe,

na mwaka wa pili utakula kutoka machipukizi yake.

Lakini katika mwaka wa tatu, panda na uvune,

panda mashamba ya mizabibu na ule matunda yake.

3019:30 Mwa 45:7; Amo 9:14Mara nyingine tena mabaki ya nyumba ya Yuda

wataeneza mizizi chini na kuzaa matunda juu.

3119:31 Mwa 45:7; Isa 9:7Kwa kuwa kutoka Yerusalemu watakuja mabaki,

na kutoka Mlima Sayuni kundi la walionusurika.

Wivu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote ndio utatimiza jambo hili.

32“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana kuhusu mfalme wa Ashuru:

“Hataingia katika mji huu

wala hatapiga mshale hapa.

Hatakuja mbele yake akiwa na ngao,

wala kupanga majeshi kuuzingira.

33Kwa njia ile aliyoijia, ndiyo atakayorudi;

hataingia katika mji huu,

asema Bwana.

3419:34 2Fal 20:6; 2Sam 7:15Nitaulinda mji huu na kuuokoa,

kwa ajili yangu mwenyewe,

na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu.”

3519:35 Ay 24:24Usiku ule, malaika wa Bwana akaenda, akawaua wanajeshi 185,000 katika kambi ya Waashuru. Wenzao walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali! 3619:36 Mwa 10:11Basi Senakeribu mfalme wa Ashuru akavunja kambi na kuondoka. Akarudi Ninawi na kukaa huko.

3719:37 2Fal 17:31; Mwa 8:4Siku moja, alipokuwa akiabudu katika hekalu la mungu wake Nisroki, wanawe Adrameleki na Shareza wakamuua kwa upanga, nao wakakimbilia nchi ya Ararati. Naye Esar-Hadoni mwanawe akawa mfalme badala yake.