列王紀下 11 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

列王紀下 11:1-21

耶何耶大立約阿施為王

1亞哈謝的母親亞她利雅見兒子死了,便決定除掉王室後裔。 2約蘭王的女兒、亞哈謝的妹妹約示芭把亞哈謝的兒子約阿施從被殺的王子中偷出來,將他和乳母藏在一間臥室裡,才躲過亞她利雅,使約阿施沒有被殺。 3約阿施和他的乳母在耶和華的殿裡藏了六年,那時亞她利雅篡位當政。

4第七年,耶何耶大派人召迦利11·4 迦利人」指雇來保護王的外族衛兵。和衛兵的百夫長們到耶和華的殿裡,與他們立約,讓他們在耶和華的殿裡起誓,然後把約阿施王子帶到他們面前。 5耶何耶大吩咐他們說:「你們在安息日值班的,三分之一要守衛王宮, 6三分之一要守衛蘇珥門,三分之一要守住衛兵院後門。你們要輪流守衛。 7安息日沒有值班的兩隊要在耶和華的殿裡保護王, 8各人要手持兵器護衛在王周圍。凡擅自闖入者,都要處死。無論王去哪裡,你們都要緊隨左右。」 9眾百夫長依令而行,各自率領安息日值班和休班的隨從來見耶何耶大10耶何耶大把耶和華殿中大衛王的矛槍和盾牌交給百夫長。 11從殿右到殿左,在祭壇和殿周圍,衛兵都手持兵器護衛王。 12耶何耶大祭司領王子出來,給他戴上王冠,把律法書交給他,膏立他為王。眾人都鼓掌高呼:「願王萬歲!」

13亞她利雅聽見衛兵和眾人的歡呼聲,便走進耶和華的殿,眾人都聚集在那裡。 14她看見王照例站在柱旁,百夫長和吹號的人侍立在王左右,眾人都歡呼吹號,便撕裂衣服喊叫:「反了!反了!」 15耶何耶大祭司認為不可在耶和華的殿裡處死亞她利雅,便命令領兵的百夫長:「把她帶出去。凡跟隨她的,都要殺掉。」 16他們抓住她,把她帶到馬匹進出王宮的入口,在那裡殺了她。

17耶何耶大讓王及民眾與耶和華立約,做耶和華的子民,也讓王與民眾立約。 18於是,民眾出去拆毀了巴力廟,砸碎祭壇和偶像,在壇前殺了巴力的祭司瑪坦耶何耶大派守衛保護耶和華的殿, 19然後率領百夫長、迦利人、衛兵和民眾,護送王從耶和華的殿下來,經過衛兵院的門進入王宮。這樣,約阿施坐上了王位。 20民眾都歡喜快樂,城裡安定,因為亞她利雅已在王宮那裡被處死。 21約阿施七歲登基。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Wafalme 11:1-21

Athalia Na Yoashi

(2 Nyakati 22:10–23:21)

111:1 2Fal 8:18Wakati Athalia mamaye Ahazia alipoona kuwa mwanawe amekufa, akainuka na kuiangamiza jamaa yote ya mfalme. 211:2 2Fal 12:1Lakini Yehosheba, binti wa Mfalme Yehoramu, aliyekuwa pia dada yake Ahazia, akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Akamweka Yoashi pamoja na yaya wake ndani ya chumba cha kulala na kumficha humo ili Athalia asimwone; kwa hiyo hakuuawa. 3Alibaki amefichwa pamoja na yaya wake katika Hekalu la Bwana kwa muda wa miaka sita wakati Athalia alikuwa akitawala nchi.

411:4 2Fal 11:19Katika mwaka wa saba, Yehoyada akatumania wakuu wa vikundi vya mamia, na Wakari,11:4 Yaani Wakerethi (ona 1Sam 30:14; Eze 25:16; Sef 2:5, 6). na walinzi, nao wakaletwa kwake katika Hekalu la Bwana. Alifanya agano nao na kuwaapisha katika Hekalu la Bwana. Ndipo akawaonyesha mwana wa mfalme. 511:5 1Nya 9:25Akawaamuru akisema, “Hivi ndivyo iwapasavyo kufanya: Ninyi ambao mko makundi matatu mnaoingia zamu siku ya Sabato, theluthi yenu inayolinda jumba la kifalme, 6theluthi nyingine Lango la Suri, na theluthi nyingine lango lililo nyuma ya walinzi, ambao hupeana zamu kulinda Hekalu, 7nanyi ambao mko katika makundi mengine mawili ambao kwa kawaida hupumzika Sabato, wote mtalinda Hekalu kwa ajili ya mfalme. 8Jipangeni kumzunguka mfalme, kila mtu akiwa na silaha yake mkononi. Yeyote anayesogelea safu zenu lazima auawe. Kaeni karibu na mfalme popote aendapo.”

9Wakuu wa vikosi vya mamia wakafanya kama vile kuhani Yehoyada aliagiza. Kila mmoja akawachukua watu wake, wale waliokuwa wakiingia zamu siku ya Sabato na wale waliokuwa wakienda mapumziko, nao wakaja kwa kuhani Yehoyada. 1011:10 2Sam 8:7Ndipo akawapa wale wakuu mikuki na ngao zilizokuwa za Mfalme Daudi, zilizokuwa ndani ya Hekalu la Bwana. 11Wale walinzi, kila mmoja akiwa na silaha yake mkononi mwake, wakajipanga kumzunguka mfalme, karibu na madhabahu na Hekalu, kuanzia upande wa kusini hadi upande wa kaskazini mwa Hekalu.

1211:12 Kut 25:16; 1Sam 10:24; Isa 55:12Yehoyada akamtoa mwana wa mfalme na kumvika taji, akampa nakala ya agano, na kumtangaza kuwa mfalme. Wakamtia mafuta, nao watu wakapiga makofi na kupaza sauti, wakisema, “Mfalme aishi maisha marefu!”

13Athalia aliposikia kelele iliyofanywa na walinzi pamoja na watu, akawaendea watu pale penye Hekalu la Bwana. 1411:14 1Fal 1:39; Mwa 37:29; 2Fal 9:23Akaangalia, na tazama alikuwako mfalme, akiwa amesimama karibu na nguzo, kama ilivyokuwa desturi. Maafisa na wapiga tarumbeta walikuwa pembeni mwa mfalme, nao watu wote wa nchi walikuwa wakifurahi na kupiga tarumbeta. Ndipo Athalia akararua mavazi yake na kulia, “Uhaini! Uhaini!”

15Kuhani Yehoyada akawaagiza majemadari wa vikosi vya mamia, waliokuwa viongozi wa jeshi, “Mleteni nje kati ya safu, na mkamuue kwa upanga yeyote anayemfuata.” Kwa kuwa kuhani alikuwa amesema, “Hatauawa ndani ya Hekalu la Bwana.” 16Basi wakamkamata Athalia, na alipofika mahali ambapo farasi huingilia katika viwanja vya jumba la mfalme, wakamuulia hapo.

1711:17 Kut 24:8; Yer 34:8Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya Bwana na mfalme na watu kwamba watakuwa watu wa Bwana. Akafanya pia agano kati ya mfalme na watu. 1811:18 Kum 12:3; 1Fal 18:40; 2Fal 10:25Watu wote wa nchi wakaenda kwenye hekalu la Baali na kulibomoa. Wakavunjavunja madhabahu na sanamu, na kumuua Matani kuhani wa Baali mbele ya hayo madhabahu.

Kisha Yehoyada kuhani akawaweka walinzi kwenye Hekalu la Bwana. 1911:19 2Fal 11:4Pamoja naye akawachukua majemadari wa mamia, Wakari, walinzi na watu wote wa nchi, nao kwa pamoja wakamteremsha mfalme kutoka Hekalu la Bwana na kwenda kwenye jumba la mfalme, wakiingilia njia ya lango la walinzi. Ndipo mfalme akachukua nafasi yake kwenye kiti cha enzi, 2011:20 Mit 11:10nao watu wote wa nchi wakafurahi. Mji ukatulia, kwa sababu Athalia alikuwa ameuawa kwa upanga nyumbani kwa mfalme.

21Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala.