出埃及記 26 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

出埃及記 26:1-37

聖幕的做法

1「要用十幅幔子造聖幕,這些幔子要用細麻線和藍、紫、朱紅三種顏色的毛線織成,還要用精緻的手工繡上基路伯天使。 2每幅幔子的尺寸都一樣,長十二米、寬兩米。 3每五幅連在一起,形成兩幅大幔子。 4要在每幅大幔子邊緣釘上藍色的扣環, 5每幅大幔子釘五十個,扣環要兩兩相對, 6再做五十個金鉤,把兩幅大幔子連在一起,成為聖幕。

7「要用山羊毛織十一幅幔子作聖幕的罩棚, 8每幅長十三米、寬兩米。十一幅幔子的尺寸都要一樣。 9然後,你們要把五幅連成一大幅,其餘六幅連成一大幅,第六幅要在聖幕前疊起來。 10要在這兩幅幔子的邊緣各釘上五十個扣環, 11再做五十個銅鉤,把這兩幅大幔子扣在一起,成為一個完整的罩棚。 12鋪罩棚所剩下來的半幅幔子要垂到聖幕後面。 13兩旁餘下的幔子可垂在聖幕的兩邊,每邊長五十釐米,蓋著聖幕。 14罩棚上面要蓋一層染成紅色的公羊皮,再蓋一層海狗皮做頂蓋。

15「要用皂莢木做支撐聖幕的木板, 16每塊木板長四米,寬六十六釐米。 17每塊木板要有兩個接榫,好連接在一起。聖幕的所有木板都要這樣。 18聖幕的南面要有二十塊木板, 19在這些木板下面要造四十個帶凹槽的銀底座,每塊木板下面兩個,用來套在木板的兩個接榫上。 20聖幕北面也要有二十塊木板, 21這些木板下面也要裝上四十個帶凹槽的銀底座,每塊木板下面有兩個銀底座。 22聖幕後面,就是西面,要有六塊木板。 23聖幕後面的兩個拐角要各有兩塊木板, 24木板的下端連於底座26·24 連於底座」或譯「是雙層的」。,頂端用一個環固定。兩個拐角都要這樣做。 25這樣,兩端便共有八塊木板,每塊木板下面各有兩個帶凹槽的銀底座,一共有十六個銀底座。

26-27「要用皂莢木做橫閂,聖幕左右兩邊及後面的牆板上要各有五根橫閂, 28攔腰固定牆板的那根橫閂要從這端貫穿到那端。 29所有的木板和橫閂都要包上金,並要在木板上造金環,用來穿橫閂。 30要照著我在山上所指示你的樣式,把聖幕支搭起來。

造至聖所的條例

31「要用細麻線和藍色、紫色、朱紅色的線織成一幅幔子,上面用精緻的手工繡上基路伯天使。 32要把這幅幔子掛在四根包金的皂莢木柱上,木柱上面有金鉤,木柱立在四個帶凹槽的銀底座上面。 33要把整幅幔子掛在木柱的金鉤上,把約櫃抬進幔子裡。這幔子把聖幕分為兩個部分,幔子裡面是至聖所,外面是聖所。 34要把施恩座放在至聖所裡面的約櫃上。 35桌子要放在幔子的外面、聖所的北面,燈臺放在南面,跟桌子相對。 36要用細麻線和藍色、紫色、朱紅色的線繡製聖幕的門簾。 37要用皂莢木做五根掛門簾的柱子,柱子包上金,上面要有金鉤,並要為柱子造五個帶凹槽的銅底座。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kutoka 26:1-37

Maskani Ya Mungu

(Kutoka 36:8-38)

126:1 Kut 29:42; 40:2; Law 8:10; Hes 1:50; Yos 22:19-20; 2Sam 7:2; 1Fal 1:30; Mdo 7:44; Ebr 8:2-5; 13:10; Ufu 21:3; Kut 25:18“Tengeneza maskani kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi atatarizi makerubi kwenye mapazia hayo. 2Mapazia yote yatatoshana kwa ukubwa: kila moja litakuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane,26:2 Dhiraa 28 ni sawa na mita 13. na upana wa dhiraa nne26:2 Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8. 326:3 1Kor 12:4-12Unganisha mapazia matano pamoja; fanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano. 426:4 Efe 4:13; Kol 2:2, 19Tengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, na ufanye vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho. 5Fanya vitanzi hamsini katika pazia mmoja, na vitanzi vingine hamsini kwenye pazia la mwisho la fungu hilo lingine, nazo vitanzi vyote vielekeane. 6Kisha tengeneza vifungo hamsini vya dhahabu ili vitumike kufunga na kuunganisha mapazia pamoja kufanya Hema liwe kitu kimoja.

726:7 Kut 36:14“Tengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika maskani. 8Mapazia hayo kumi na moja yatakuwa na kipimo kimoja, yaani urefu wa dhiraa thelathini,26:8 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5. na upana wa dhiraa nne. 9Unganisha hayo mapazia matano yawe fungu moja, na hayo mengine sita yawe fungu lingine. Kunja hilo pazia la sita mara mbili mbele ya maskani. 10Tengeneza vitanzi hamsini kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu moja, na vivyo hivyo kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu hilo lingine. 11Kisha tengeneza vifungo hamsini vya shaba, uviingize katika vile vitanzi ili kukaza hema pamoja kuwa kitu kimoja. 12Kuhusu kile kipande cha ziada cha pazia la Hema, nusu ya hilo pazia lililobaki litaningʼinizwa upande wa nyuma wa Hema. 13Mapazia ya hema yatakuwa na urefu wa dhiraa moja zaidi pande zote, sehemu itakayobaki itaningʼinia pande zote za Hema ili kuifunika. 1426:14 Kut 36:19; Hes 3:25; 4:25Tengeneza kifuniko cha hema kwa ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.26:14 Pomboo hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili.

15“Tengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani. 16Kila mhimili uwe na urefu wa dhiraa kumi26:16 Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5. na upana wa dhiraa moja na nusu, 17zikiwa na ndimi mbili zilizo sambamba kila mmoja na mwingine. Tengeneza mihimili yote ya maskani jinsi hii. 18Tengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa maskani, 1926:19 Kut 38:27kisha tengeneza vitako arobaini vya fedha vya kuweka chini ya hiyo mihimili, vitako viwili kwa kila mhimili, kimoja chini ya kila ulimi. 20Kuhusu upande wa kaskazini wa maskani, tengeneza mihimili ishirini 21na vitako arobaini vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. 22Kisha tengeneza mihimili sita kwa mwisho ulio mbali, yaani upande wa magharibi wa maskani, 23na pia utengeneze mihimili miwili ya pembe za upande ulio mbali. 24Katika pembe hizi mbili ni lazima mihimili yake iwe miwili kuanzia chini mpaka juu, na iingizwe kwenye pete moja; mihimili ya pembe hizi mbili itafanana. 25Kwa hiyo itakuwepo mihimili minane, na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila mhimili.

2626:26 Kut 36:31; Rum 15:1; Gal 6:2“Pia tengeneza mataruma ya mti wa mshita: matano kwa ajili ya mihimili ya upande mmoja wa maskani, 27matano kwa ajili ya mihimili ya upande mwingine, na matano kwa ajili ya mihimili ya upande wa magharibi, mwisho kabisa mwa maskani. 28Taruma la katikati litapenya katikati ya mihimili kutoka mwisho mmoja hadi mwisho mwingine. 29Funika hiyo mihimili kwa dhahabu, kisha tengeneza pete za dhahabu ambazo zitashikilia hayo mataruma. Pia funika hayo mataruma kwa dhahabu.

3026:30 Kut 40:2; 25:9; Hes 9:15; Ebr 8:5; Mdo 7:44; Ebr 8:5“Simamisha Hema sawasawa na mfano ulioonyeshwa kule mlimani.

3126:31 Hes 4:5; 2Nya 3:14; Mt 27:51; Lk 23:45; Ebr 9:3; Kut 25:18; 36:35; Law 16:2; Kut 25:18; 36:35“Tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, naye fundi stadi atirizi makerubi kwenye hilo pazia. 32Litundike kwa kulabu za dhahabu kwenye nguzo nne za mti wa mshita ambazo zimefunikwa kwa dhahabu, zikiwa zimesimamishwa kwenye vitako vinne vya fedha. 3326:33 Kut 27:21; 35:12; 40:2-3, 21; Law 16:2; Hes 3:31; 4:5; 2Nya 3:14; Law 16:2, 16; 1Fal 6:16; 7:50; 8:6; 2Nya 3:8; 5:7; Eze 41:5; Ebr 9:2-3Ningʼiniza pazia hilo kwenye vifungo, kisha weka Sanduku la Ushuhuda nyuma ya pazia. Pazia litatenganisha Mahali Patakatifu kutoka Patakatifu pa Patakatifu. 3426:34 Kut 25:21; 30:6; 37:6; Law 16:2; Ebr 9:5Weka kifuniko cha kiti cha rehema juu ya Sanduku la Ushuhuda ndani ya Patakatifu pa Patakatifu. 3526:35 Kut 25:23; Ebr 9:2; Kut 25:31Weka meza nje ya pazia upande wa kaskazini wa Hema, kisha weka kinara cha taa upande wa kusini wa Hema.

3626:36 Kut 35:15; 40:5; 28; Za 45:14; Eze 16:10; 26:16; 27:7“Kwa ajili ya ingilio la hema, tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. 3726:37 Kut 38:1Tengeneza kulabu za dhahabu kwa ajili ya hilo pazia, na nguzo tano za mshita zilizofunikwa kwa dhahabu. Kisha mimina vitako vitano vya shaba kwa ajili yake.