出埃及記 23 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

出埃及記 23:1-33

公義與憐憫

1「不可散佈謠言,也不可與惡人一起作偽證陷害別人。 2不可隨眾行惡。在法庭作證時不可附和多數人,顛倒是非。 3在訴訟的事上不可偏袒窮人。

4「倘若看見仇人的牛或驢走迷了路,總要牽回去交給他。 5倘若遇見仇人的驢被馱的重物壓倒,不可逕自走開,總要幫助仇人抬開重物。

6「不可在訴訟案中冤枉窮人。 7不可誣告別人,不可殺害正直無辜的人,因為我必懲罰作惡之人。 8不可收受賄賂,因為賄賂蒙蔽人的眼目,使人顛倒是非。 9不可欺凌在你們中間寄居的人,因為你們也曾經在埃及寄居,知道身在異鄉的滋味。

安息年和安息日

10「六年之內你要耕種收割, 11第七年要讓土地休息,不耕不種,你們當中的窮人可以吃田中長出來的,剩下的可以留給動物吃。你也要這樣耕作葡萄園和橄欖園。 12六天之內,你要工作,但第七天要休息。這樣,牛、驢可以歇息,你家裡的奴僕和寄居的也可以休息。 13你們要謹慎遵從我對你們說的話。不可提其他神明的名字,不可從你口中聽到它們的名字。

三大節期

14「你每年要向我守三個節期。 15要守除酵節,照我的吩咐在每年亞筆月所定的日期連續吃七天的無酵餅,因為你是在這個月離開了埃及。誰也不可空手來朝拜我。 16要在耕種後、收取初熟之物的時候守收割節。要在年終從田間收取勞動成果時守收藏節。 17以色列所有的男子都要在這三個節期上來朝見主耶和華。

18「不可把祭牲的血和有酵的餅一起獻給我,也不可把祭牲的脂肪留到第二天早晨。 19要把田中最好的初熟之物送到你們的上帝耶和華的殿中。不可用母山羊的奶煮牠的小羊羔。

應許賜迦南

20「看啊,我要差遣天使走在你前面,在路上保護你,帶領你平安地到達我為你預備的地方。 21他是奉我的名來的,你們要謹遵他的話,不可悖逆,不然他必不赦免你們的過犯。

22「你若認真聽從他的吩咐,遵行我的話,我就與你的仇敵為敵,與你的對頭作對。 23我的天使要走在你前面,帶領你去亞摩利人、人、比利洗人、迦南人、希未人和耶布斯人所住的地方,我會把他們全部消滅。 24不可叩拜他們的神明,不可供奉它們,也不可效法他們的行為,要徹底拆毀神像,打碎他們的神柱。 25你們要事奉你們的上帝耶和華,我必賜給你日用的飲食,使你們身體健康,不受疾病的侵害, 26在你境內必沒有人流產或不育,我會使你壽終正寢。 27你所到之處,我必使那裡的人惶恐不安,使你一切的仇敵都在你面前轉身逃跑。 28我要派黃蜂做你的先鋒,趕走那些希未人、迦南人和人。 29我不會在一年之內把這些人全部趕走,免得土地荒涼,野獸肆虐。 30我會逐漸地趕走他們,直到你們人丁興旺,可以佔據那片土地。 31我給你定下國界,從紅海到非利士海岸,從曠野到幼發拉底河。我要把其中所有的人都交在你手中,你要把他們全部趕出去。 32不可跟這些民族及其神明立約, 33也不可讓這些民族住在你的土地上,免得他們使你得罪我,你若供奉他們的神明,必因此而陷入網羅。」

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kutoka 23:1-33

Sheria Za Haki Na Rehema

123:1 Mwa 36:7; Mt 19:18; Lk 3:14; Kut 20:16; Kum 5:20; 19:16-21; Za 27:12; 35:11; Mit 19:5; Mdo 6:11“Usieneze habari za uongo. Usimsaidie mtu mwovu kwa kuwa shahidi mwenye nia ya kudhuru wengine.

223:2 Law 19:15, 33; Kum 1:17; 27:19; 1Sam 8:3; Kum 24:17; 16:19; Ay 31:34“Usifuate umati wa watu katika kutenda mabaya. Unapotoa ushahidi kwenye mashtaka, usipotoshe haki ukijumuika na umati wa watu, 323:3 Rum 12:20; Law 6:2-3; 19:11; Kum 22:1-2nawe usimpendelee mtu maskini katika mashtaka yake.

4“Kama ukikutana na maksai au punda wa adui yako anapotea, hakikisha umemrudisha kwake. 523:5 Kum 22:4Ukiona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, usimwache hapo alipoangukia; hakikisha kuwa umemsaidia.

623:6 Kum 23:16; Mit 22:22“Usiwanyime haki watu wako walio maskini katika mashtaka yao. 723:7 Kut 20:16; Efe 4:24-25; Mt 27:4; Mwa 18:23; Kut 34:7; Kum 19:18; 25:1Ujiepushe na mashtaka ya uongo, wala usimuue mtu asiye na hatia au mtu mwaminifu, kwa maana sitamhesabia hana hatia yeye aliye na hatia.

823:8 Kut 18:21; Law 9:15; Kum 10:17; 27:25; Ay 15:34; 36:18; Za 26:10; Mit 6:35; 15:27; 17:8; Isa 1:23; 5:23; Mik 3:11; 7:3“Usipokee rushwa, kwa kuwa rushwa hupofusha wale waonao, na kupinda maneno ya wenye haki.

923:9 Kut 22:21; Law 19:33-34; Eze 22:7“Usimwonee mgeni; ninyi wenyewe mnajua jinsi mgeni anavyojisikia, kwa sababu mlikuwa wageni Misri.

Sheria Za Sabato

10“Kwa muda wa miaka sita mtapanda mashamba yenu na kuvuna mazao, 1123:11 Law 25:1-7; Neh 10:31lakini katika mwaka wa saba usiilime ardhi wala kuitumia, ili watu walio maskini miongoni mwenu waweze kupata chakula kutoka kwenye hayo mashamba, nao wanyama pori wapate chakula kwa yale mabaki watakayobakiza. Utafanya hivyo katika shamba lako la mizabibu na la mizeituni.

1223:12 Kut 20:9; Lk 13:14; Mwa 2:2-3“Kwa siku sita fanya kazi zako, lakini siku ya saba usifanye kazi, ili maksai wako na punda wako wapate kupumzika, naye mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwako, pamoja na mgeni, wapate kustarehe.

1323:13 Kum 4:9, 23; 1Tim 4:16; Kum 12:3; Yos 23:7; Za 16:4; Zek 13:2; Kum 18:20; Hos 2:17“Uzingatie kutenda kila kitu nilichokuambia. Usiombe kwa majina ya miungu mingine, wala usiyaruhusu kusikika kinywani mwako.

Sikukuu Tatu Za Mwaka

(Kutoka 34:18-26; Kumbukumbu 16:1-17)

1423:14 Kut 12:14; 34:23-24; Kum 16:16; 1Fal 9:25; 2Nya 8:13; Eze 46:9“Mara tatu kwa mwaka utanifanyia sikukuu.

1523:15 Kut 12:17; Mt 26:17; Lk 22:1; Mdo 12:3; Kut 12:2; 22:29“Utaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu; kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu kama nilivyokuagiza. Fanya jambo hili kwa wakati uliopangwa katika mwezi wa Abibu, ndio mwezi wa nne, kwa sababu katika mwezi huo ulitoka Misri.

“Mtu yeyote asije mbele yangu mikono mitupu.

1623:16 Law 23:15-21; Hes 28:26; Kum 16:9; 2Nya 8:13; Kut 22:29; 34:22; Law 23:34, 42; Kum 16:16; 31:10; Ezr 3:4; Neh 8:14; Zek 14:16; Yer 40:10; Kum 16:13“Utaadhimisha Sikukuu ya Mavuno kwa malimbuko ya mazao yako uliyopanda katika shamba lako.

“Utaadhimisha Sikukuu ya Kukusanya mavuno mwishoni mwa mwaka, unapokusanya mavuno yako toka shambani.

17“Mara tatu kwa mwaka wanaume wote watakuja mbele za Bwana Mwenyezi.

1823:18 Kut 34:25; Law 2:11; Kut 12:8“Msitoe damu ya dhabihu kwangu pamoja na kitu chochote kilicho na chachu.

“Mafuta ya mnyama wa sadaka ya sikukuu yangu yasibakizwe mpaka asubuhi.

19“Utaleta malimbuko bora ya ardhi yako katika nyumba ya Bwana Mungu wako.

“Usimchemshe mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

Malaika Wa Mungu Kuandaa Njia

2023:20 Mwa 16:7; Kut 15:17; 32:34“Tazama, ninamtuma malaika akutangulie mbele yako akulinde njiani na kukuleta mpaka mahali nilipoandaa. 2123:21 Kum 18:19; Yer 13:15; Kum 29:20; 2Fal 24:4; Mao 1:17; Hes 17:10; Kum 9:7; 31:27; Yos 24:19; Za 25:7; 78:8, 40; 106:33; 107; 11; 1Yn 5:16; Kut 3:15Mtamtii na kusikiliza kile anachokisema. Usiasi dhidi yake; hatakusamehe uasi wako, kwa maana Jina langu limo ndani yake. 2223:22 Kut 15:26; Mwa 12:3; Isa 41:11; Yer 30:20Kama ukitii kweli kweli kile asemacho na kufanya yote nisemayo, nitakuwa adui wa adui zako, na nitawapinga wale wakupingao. 2323:23 Hes 13:29; 21:21; Yos 3:10; 24:8-10; 24:8-11; Ezr 9:1Malaika wangu atatangulia mbele yako na kukuleta katika nchi ya Waamori, Wahiti, Waperizi, Wakanaani, Wahivi na Wayebusi, nami nitawafutilia mbali. 2423:24 Kut 20:5; Law 18:3; 20:23; Kum 9:4; 12:30-31; Yer 10:2; Kut 34:13; Hes 33:52; Kum 7:5; 12:3; Amu 2:2; 2Fal 18:4; 23:14; Kum 16:22; 1Fal 14:23; 3:2; 10:26; 17:20; 2Nya 14:2-3; Isa 27:9Usiisujudie miungu yao, au kuiabudu, wala kufuata desturi yao. Utayabomoa kabisa na kuvunjavunja mawe yao ya ibada vipande vipande. 2523:25 Mt 4:10; Law 26:3-13; Kum 7:12-15; 28:1-14; Kut 15:26Utamwabudu Bwana Mungu wako, na baraka zake zitakuwa juu ya vyakula vyako na maji yako. Nami nitaondoa maradhi miongoni mwako, 2623:26 Law 26:3-4; Kum 7:14; 28:4; Mal 3:11; Mwa 15:15; Kum 4:1, 40; 21:12na hakuna atakayeharibu mimba wala atakayekuwa tasa katika nchi yako. Nami nitakupa maisha makamilifu.

2723:27 Mwa 35:5; Kut 15:14; 14:24; Kum 7:23; 2Sam 22:41; Za 18:40; 21:12“Nitapeleka utisho wangu mbele yako na kufadhaisha kila taifa utakalolifikia. Nitafanya adui zako wote wakupe kisogo na kukimbia. 2823:28 Kum 7:20; Yos 24:12; Kut 33:2; 34:11, 24; Hes 13:29; Kum 4:38; 11:23; 18:12; Yos 3:10; 24:11; Za 78:55Nitatanguliza manyigu mbele yako kuwafukuza Wahivi, Wakanaani na Wahiti waondoke njiani mwako. 2923:29 Kum 7:22Lakini sitawafukuza kwa mara moja, kwa sababu nchi itabaki ukiwa na wanyama pori watakuwa wengi mno kwako. 3023:30 Yos 23:5Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, mpaka uwe umeongezeka kiasi cha kutosha kuimiliki nchi.

3123:31 Mwa 2:14; Kum 34:2; Ezr 4:20; Kum 7:24; 9:3; Yos 21:44; 24:12-18; Za 80:8“Nitaweka mipaka ya nchi yako kuanzia Bahari ya Shamu hadi Bahari ya Wafilisti, na kuanzia jangwani hadi Mto Frati. Nitawatia watu wanaoishi katika nchi hizo mikononi mwako, nawe utawafukuza watoke mbele yako. 3223:32 Mwa 26:28; Kut 34:12; Kum 7:2; Yos 9:7; Amu 2:2; 1Sam 11:1; 1Fal 15:19; 20:34; Eze 17:13Usifanye agano lolote nao wala na miungu yao. 3323:33 Kut 10:7; Za 106:36Usiwaache waishi katika nchi yako, la sivyo watakusababisha utende dhambi dhidi yangu, kwa sababu ibada ya miungu yao hakika itakuwa mtego kwako.”