使徒行傳 5 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

使徒行傳 5:1-42

欺騙聖靈

1一個名叫亞拿尼亞的人與妻子撒非喇也把田產賣了。 2他私自留下一部分錢,然後把其餘的拿去交給使徒,這件事他妻子也知道。 3彼得說:「亞拿尼亞,你為什麼讓撒旦充滿你的心,欺騙聖靈,私自留下一些賣地的錢呢? 4田產沒有賣的時候屬於你,即使賣了,賣地的錢也由你支配。你怎麼做出這種事呢?你不是欺騙人,你是欺騙上帝!」 5亞拿尼亞聽見這話,當場倒地而死。聽見這件事的人都非常懼怕。 6有幾個青年上前把他的屍體裹起來,抬出去埋葬了。

7大約過了三個小時,亞拿尼亞的妻子也進來了,她還不知道發生了什麼事。 8彼得問她:「你們賣田地的錢就這麼多嗎?」她說:「是的,就這麼多。」

9彼得說:「你們二人怎麼串通起來試探主的靈呢?埋葬你丈夫的人就到門口了,他們也要把你抬出去。」 10撒非喇立刻倒在彼得腳前死了。那些青年進來看見她已經死了,便把她抬出去葬在她丈夫的旁邊。 11整個教會和聽見這件事的人都非常懼怕。

神蹟奇事

12主藉著使徒們在百姓中行了許多神蹟奇事,大家同心合意地在所羅門廊那裡聚會。 13其他人不敢接近他們,不過百姓都很敬重他們。 14信主的人數不斷增加,男女都有。 15人們甚至把病人抬到街上,放在床上或墊子上,希望彼得路過時的影子可以落在病人身上。 16還有大群的人從耶路撒冷附近的城鎮帶著病人和被污鬼攪擾的人趕來,他們都得了醫治。

使徒受迫害

17大祭司和他的同黨撒都該人看見這情形,妒火中燒, 18便把使徒拘捕,關在監裡。 19當天晚上,有一位主的天使把獄門打開,領他們出來, 20說:「你們到聖殿去,把這生命之道傳給百姓。」 21使徒遵從命令,在黎明的時候來到聖殿開始教導眾人。

大祭司和他的同黨召集了所有公會5·21 公會是猶太人的最高立法與司法機關。的人和以色列的眾長老,然後派人去監獄把使徒押來受審。 22差役來到監獄時,發現使徒已經不見了,就回去稟告,說: 23「我們看見牢門緊鎖,守衛都站在門外,但打開門一看,裡面卻空無一人!」

24聖殿護衛長和祭司長聽後,都很困擾,不知道是怎麼回事。 25這時有人來報告說:「你們關押在牢裡的人正在聖殿裡教導人!」 26聖殿護衛長和差役再去把使徒抓回來。這次他們不敢動粗,生怕百姓會用石頭打他們。

27使徒被帶來後站在公會前,大祭司盤問他們,說: 28「我們不是嚴禁你們奉耶穌的名去教導百姓嗎?你們竟然在耶路撒冷各處傳道,還想把殺那人的血債歸到我們身上!」

29彼得和其他使徒申辯說:「我們要服從的是上帝,而非人。 30你們釘死在十字架上的耶穌,我們祖先的上帝已經使祂復活了。 31上帝把祂提升到自己的右邊,立祂為君王和救主,好賜給以色列人悔改的機會,使他們的罪得到赦免。 32我們就是這些事的見證人,上帝賜給順服祂之人的聖靈也同樣做見證。」

33他們聽了,怒氣衝天,打算殺掉使徒。 34公會中有一位名叫迦瑪列的法利賽人,是個德高望重的律法教師。他站起來,叫人把使徒暫且押到外面, 35然後說:「以色列人啊,你們應當慎重處置這些人。 36不久前,有個名叫杜達的人起來自立山頭,吸引了差不多四百個跟隨者,但他被殺之後,那些跟隨者就各奔東西,銷聲匿跡了。 37後來,又有個加利利猶大在戶口登記期間鼓動百姓跟隨他造反。他被殺之後,那些跟隨者也煙消雲散了。 38所以,像現在這種情形,我勸大家還是不要管他們,隨他們去吧。他們的計劃和行為如果是出於人意,終必失敗; 39但如果是出於上帝,你們不但無法阻止他們,恐怕反而是在抵擋上帝!」

40公會採納了他的意見,於是把使徒召回來打了一頓,再次警告他們不可奉耶穌的名傳道,才放了他們。 41使徒離開公會後,為自己有資格為主的名受辱而歡喜。 42他們每天在聖殿裡和各家各戶教導人,傳揚耶穌是基督。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Matendo 5:1-42

Anania Na Safira

1Lakini mtu mmoja jina lake Anania pamoja na mkewe Safira waliuza kiwanja. 25:2 Mdo 4:35-37Huku mkewe akijua kikamilifu, Anania alificha sehemu ya fedha alizopata, akaleta kiasi kilichobaki na kukiweka miguuni pa mitume.

35:3 Mt 4:10; Yn 13:2, 27Petro akamuuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na kiwanja? 45:4 Kum 23:22; Law 6:2Je, kabla hujauza hicho kiwanja si kilikuwa mali yako? Hata baada ya kukiuza, fedha ulizopata si zilikuwa kwenye uwezo wako? Kwa nini basi umewaza hila hii moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Wewe hukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu.”

55:5 Za 5:6; Mdo 5:10Anania aliposikia maneno haya akaanguka chini na kufa. Hofu kuu ikawapata wote waliosikia jambo lililokuwa limetukia. 65:6 Yn 19:40Vijana wakaja, wakaufunga mwili wake sanda, wakamchukua nje kumzika.

7Saa tatu baadaye mkewe Anania akaingia, naye hana habari ya mambo yaliyotukia. 85:8 Mdo 5:2Petro akamuuliza, “Niambie, je, mliuza kiwanja kwa thamani hii?” Akajibu, “Ndiyo, tuliuza kwa thamani hiyo.”

95:9 Mdo 5:3; Mt 4:7Ndipo Petro akamwambia, “Imekuwaje mkakubaliana kumjaribu Roho wa Bwana? Tazama! Nyayo za vijana waliomzika mumeo ziko mlangoni, wewe nawe watakuchukua nje.”

105:10 Mdo 5:5, 6Saa ile ile akaanguka chini miguuni mwake na kufa. Nao wale vijana wakaingia, wakamkuta amekufa, wakamchukua wakamzika kando ya mumewe. 115:11 Mdo 19:7Hofu kuu ikalipata kanisa lote pamoja na watu wote waliosikia juu ya matukio haya.

Mitume Waponya Wengi

125:12 Yn 4:48; Mdo 2:43; 4:32; Yn 10:23Mitume wakafanya ishara nyingi na miujiza miongoni mwa watu. Walioamini wote walikuwa wakikusanyika katika ukumbi wa Solomoni. 135:13 Mdo 2:47; 4:21; Yn 9:22; 12:42; 19; 18Hakuna mtu mwingine aliyethubutu kuambatana nao ijapokuwa waliheshimiwa sana na watu. 145:14 Mdo 2:41, 47; 6; 7; 21:20Hata hivyo, waliomwamini Bwana wakazidi kuongezeka, wanaume na wanawake. 155:15 Mdo 19; 12Hata wakawa wanawaleta wagonjwa na kuwalaza kwenye magodoro na kwenye vitanda barabarani ili yamkini Petro akipita kivuli chake kiwaguse baadhi yao. 165:16 Mt 8:16; Mk 16:17Pia watu wakakusanyika kutoka miji iliyokuwa karibu na Yerusalemu, wakileta wagonjwa na watu walioteswa na pepo wachafu. Hao wote wakaponywa.

Mitume Washtakiwa

175:17 Mdo 15:5; 4:1Kisha kuhani mkuu na wenzake wote waliokuwa pamoja naye, waliokuwa wa kundi la Masadukayo, wakajawa na wivu. 18Wakawakamata mitume na kuwatia gerezani. 195:19 Kut 3:2; Mt 28:2; Mdo 16:26Lakini wakati wa usiku, malaika wa Bwana akaja, akafungua milango ya gereza na akawatoa nje. Akawaambia, 205:20 Yn 6:63-68; 17:3; 1Yn 5:11“Nendeni, mkasimame Hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya uzima huu mpya.”

215:21 Mdo 4:5-6; Mt 5:22Waliposikia haya wakaenda Hekaluni alfajiri wakaendelea kufundisha watu.

Kuhani mkuu na wale waliokuwa pamoja nao walipowasili, alikusanya baraza na wazee wote wa Israeli wakatuma wale mitume waletwe kutoka gerezani. 225:22 Mdo 12:18, 19Lakini wale walinzi wa Hekalu walipokwenda gerezani hawakuwakuta mitume mle. Kwa hiyo wakarudi na kutoa habari. 23Wakasema, “Tumekuta milango ya gereza imefungwa sawasawa na askari wa gereza wamesimama nje ya mlango, lakini tulipofungua milango hakuwepo mtu yeyote ndani.” 245:24 Lk 22:4; Mdo 4:1Basi mkuu wa walinzi wa Hekalu na viongozi wa makuhani waliposikia haya, wakafadhaika na kushangaa sana kwa ajili yao kwamba jambo hili litakuwaje.

25Ndipo mtu mmoja akaja akawaambia, “Tazameni watu mliowatia gerezani wako Hekaluni wakiwafundisha watu.” 265:26 Mdo 4:21Ndipo yule mkuu wa walinzi wa Hekalu wakaenda pamoja na askari wakawaleta wale mitume, lakini bila ghasia kwa sababu waliogopa kupigwa mawe na watu.

275:27 Mt 5:22Wakiisha kuwaleta mitume wakawaamuru kusimama mbele ya baraza ili kuhani mkuu awahoji. 285:28 Mdo 4:18; Mt 23:35; 27:25“Tuliwaonya kwa nguvu msifundishe kwa jina hili, lakini ninyi mmeijaza Yerusalemu yote mafundisho yenu na tena mmekusudia kuleta damu ya mtu huyu juu yetu.”

295:29 Kut 1:17; Mdo 4:19Petro na wale mitume wengine wakajibu, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. 305:30 Mdo 3:13; 2:24; Gal 3:13; 1Pet 2:24Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu kutoka kwa wafu, ambaye ninyi mlimuua kwa kumtundika kwenye msalaba. 315:31 Mk 16:19; Lk 2:11; Mdo 2:23Mungu alimtukuza, akamweka mkono wake wa kuume kuwa Kiongozi na Mwokozi ili awape Israeli toba na msamaha wa dhambi. 325:32 Lk 24:48; Yn 15:26Nasi tu mashahidi wa mambo haya, vivyo hivyo na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wale wanaomtii.”

335:33 Mdo 2:37; 7:54Wale wajumbe wa baraza la wazee waliposikia haya, walijawa na ghadhabu, wakataka kuwaua mitume. 345:34 Mdo 22:3; Lk 2:46; 5:17Lakini Farisayo mmoja, jina lake Gamalieli, aliyekuwa mwalimu wa sheria, aliyeheshimiwa na watu wote, akasimama mbele ya baraza akaamuru mitume watolewe nje kwa muda. 35Ndipo alipowaambia wajumbe wa baraza, “Enyi watu wa Israeli, fikirini kwa uangalifu mnayotaka kuwatendea watu hawa. 365:36 Mdo 21:38Kwa maana wakati uliopita, aliinuka mtu mmoja jina lake Theuda, alijidai kuwa yeye ni mtu maarufu, akapata wafuasi wapatao 400 walioambatana naye. Lakini aliuawa, na wafuasi wake wote wakatawanyika, wakawa si kitu. 375:37 Lk 2:2Baada yake, alitokea Yuda Mgalilaya wakati wa kuorodhesha watu, naye akaongoza kundi la watu kuasi. Yeye pia aliuawa, nao wafuasi wake wakatawanyika. 385:38 Lk 15:13Kwa hiyo, kwa habari ya jambo hili nawashauri, jiepusheni na watu hawa. Waacheni waende zao! Kwa maana kama kusudi lao na shughuli yao imetokana na mwanadamu, haitafanikiwa. 395:39 2Nya 13:12; Mdo 11:17Lakini ikiwa imetoka kwa Mungu, hamtaweza kuwazuia watu hawa. Badala yake mtajikuta mnapigana na Mungu.”

405:40 Mt 10:17Wakapokea ushauri wa Gamalieli. Wakawaita mitume ndani, wakaamuru wachapwe mijeledi, kisha wakawaagiza wasinene tena kwa jina la Yesu, wakawaachia waende zao.

415:41 Mt 5:12; Mk 15:21Nao mitume wakatoka nje ya baraza, wakiwa wamejaa furaha kwa sababu wamehesabiwa kustahili kupata aibu kwa ajili ya jina la Yesu. 425:42 Mdo 2:46; 4:20, 29; 9:22; 13:32Kila siku, Hekaluni na nyumba kwa nyumba, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema kwamba Yesu ndiye Kristo.5:42 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.