但以理書 4 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

但以理書 4:1-37

尼布甲尼撒的第二個夢

1尼布甲尼撒王傳諭天下各族、各邦、各語種的人:「願你們大享平安! 2我樂意向你們述說至高的上帝對我所行的神蹟奇事。

3「祂的神蹟何其偉大!

祂的奇事何其可畏!

祂的國度永遠長存,

祂的統治直到萬代。

4「我尼布甲尼撒安居在家,在宮中享受榮華。 5但我做了一個夢,令我害怕。我躺在床上的時候,腦中出現的情景和異象使我恐懼。 6我便召巴比倫所有的智者來為我解夢。 7術士、巫師、占星家和占卜者都來了,我將夢告訴他們,他們卻不能給我解夢。 8最後但以理來到我面前,他又名伯提沙撒——取自我神明的名,他有聖潔神明的靈。我將夢告訴他,說, 9『術士的首領伯提沙撒啊,我知道你有聖潔神明的靈,任何奧秘都難不倒你。請你為我解釋我夢中所見的異象。

10「『以下是我躺在床上時腦中出現的異象:我看見大地中央有棵非常高大的樹。 11這樹長得蒼勁有力,高可參天,從地極都能看見。 12它的葉子美麗,果實纍纍,可作眾生的食物。野獸在它的蔭下躺臥,飛鳥在它的枝頭棲息,一切生靈都從它那裡得到食物。

13「『我躺在床上時腦中出現了異象,我看見一位聖潔的守望者從天而降。 14他大聲說,砍倒那棵樹,削掉它的枝子,剝光它的葉子,拋散它的果子,使野獸逃離樹下,飛鳥離開枝頭。 15但把樹丕留在地裡,用鐵環和銅環箍住他留在野地的青草中,讓他被天上的露水浸濕,與野獸一起吃草。 16要改變他的人心,給他一個獸心,達七年之久。 17這是守望者的命令,是聖者的決定,要讓眾生知道至高者主宰世上萬國,祂要把國賜給誰就賜給誰,即使是最卑微的人。』

18「這就是我尼布甲尼撒王所做的夢。伯提沙撒啊,你要為我解夢,因為我國中所有的智者都不能為我解夢。但是你能,因為你有聖潔神明的靈。」

但以理解夢

19但以理,又名伯提沙撒,一時非常驚訝,惶恐不安。王說:「伯提沙撒啊,不要因為這夢和夢的意思而惶恐不安。」伯提沙撒回答說:「我主啊,願這夢發生在恨你的人身上,夢的意思應驗在你的仇敵身上。 20你夢見的樹蒼勁有力,高可參天,從地極都能看見。 21它的葉子美麗,果實纍纍,可作眾生的食物。野獸住在它的蔭下,飛鳥宿在它的枝頭。 22王啊,這蒼勁有力的樹就是你,你的威名高達穹蒼,你的權柄延至地極。 23王看見聖潔的守望者從天而降,說,『將這樹砍倒、毀滅,但把樹丕用鐵環和銅環箍住留在野地的青草中,讓他被天上的露水浸濕,與野獸一起吃草,達七年之久。』

24「王啊,以下是夢的意思,是至高者裁定要臨到我主我王的事: 25你必從人群中被趕走,與野獸同住,像牛一樣吃草,被天上的露水浸濕,達七年之久,直到你知道至高者主宰世上萬國,祂要把國賜給誰就賜給誰。 26守望者命令留下樹丕,表示等到你承認上天掌權後,你將重掌國權。 27王啊,請接受我的勸諫,你要秉公行義,以斷絕罪惡;憐憫窮人,以除掉罪過。這樣,你的國運也許可以延續。」

夢兆應驗

28這一切事果然發生在尼布甲尼撒王身上。 29十二個月後,他在巴比倫王宮的屋頂散步時, 30說:「這宏偉的巴比倫豈不是我用大能建立為京都,以顯我的威嚴和榮耀嗎?」 31話未說完,天上就有聲音說:「尼布甲尼撒王啊,你聽著,你已失去王權。 32你必從人群中被趕走,與野獸同住,像牛一樣吃草,達七年之久,直到你知道至高者主宰世上萬國,祂要把國賜給誰就賜給誰。」 33這話立刻應驗在尼布甲尼撒身上。他從人群中被趕走,像牛一樣吃草,身體被天上的露水浸濕,直到他的頭髮長如鷹毛,指甲長如鳥爪。

34「七年後,我尼布甲尼撒舉目望天,恢復了神智,便稱頌至高者,讚美、尊崇永活者。

「祂的統治永無窮盡,

祂的國度直到萬代。

35世人都微不足道,

祂在天軍和世人中獨行其道,

無人能攔阻祂的手,

或質問祂的作為。

36「那時,我恢復了神智,也恢復了我的威嚴和榮耀,重現我國度的輝煌。我的謀士和大臣都來朝見我,我重掌國權,勢力比以前更大。 37現在我尼布甲尼撒頌讚、尊崇、敬奉天上的王,因為祂的作為公正,祂行事公平,能夠貶抑行為驕傲的人。」

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Danieli 4:1-37

Ndoto Ya Nebukadneza Ya Mti

14:1 Dan 3:4; 6:25Mfalme Nebukadneza,

Kwa kabila za watu, mataifa na watu wa kila lugha, wanaoishi katika ulimwengu wote:

Mafanikio yawe kwenu sana!

24:2 Dan 3:26; Za 74:9Ni furaha yangu kuwaambia kuhusu ishara za miujiza na maajabu ambayo Mungu Aliye Juu Sana amenifanyia.

34:3 Za 105:27; Dan 6:25-27; 2:44Ishara zake ni kuu aje,

na maajabu yake yana nguvu aje!

Ufalme wake ni ufalme wa milele;

enzi yake hudumu kutoka kizazi hadi kizazi.

44:4 Za 30:6; Isa 32:9Mimi, Nebukadneza, nilikuwa nyumbani katika jumba langu la kifalme, nikiwa ninaishi kwa raha na hali ya kufanikiwa. 54:5 Dan 2:1, 28; Za 4:4; Mwa 41:8; Ay 3:26; Dan 5:6; 2:3Niliota ndoto iliyoniogopesha. Nilipokuwa nimelala kitandani mwangu, njozi na maono yaliyopita mawazoni mwangu vilinitisha. 64:6 Dan 2:2Hivyo nikaagiza kwamba watu wote wenye hekima wa Babeli waletwe mbele yangu kunifasiria ndoto yangu. 74:7 Mwa 41:8; Isa 44:25; Dan 2:2, 10Walipokuja waganga, wasihiri, wanajimu na waaguzi, niliwaambia ndoto yangu, lakini hawakuweza kunifasiria. 84:8 Mwa 41:38; Dan 5:11-14; 1:7Mwishoni, Danieli alikuja mbele yangu nikamweleza hiyo ndoto. (Danieli anaitwa Belteshaza, kwa jina la mungu wangu, nayo roho ya miungu mitakatifu inakaa ndani yake.)

94:9 Dan 2:48; 5:11-12Nilisema, “Belteshaza, mkuu wa waganga, ninajua kuwa roho ya miungu mitakatifu iko ndani yako, wala hakuna siri iliyo ngumu kwako. Hii ndiyo ndoto yangu, nifasirie. 104:10 Za 4:4; Eze 31:3-4Haya ndiyo maono niliyoona nilipokuwa nimelala kitandani mwangu: Nilitazama, na mbele yangu ulisimama mti katikati ya nchi. Ulikuwa mrefu sana. 114:11 Eze 19:11; 31:5Mti ule ulikua, ukawa mkubwa na wenye nguvu, nayo ncha yake ikagusa anga; ulionekana mpaka miisho ya dunia. 124:12 Eze 17:23; Mt 13:32; Mao 4:20Majani yake yalikuwa ya kupendeza, matunda yake yalikuwa mengi, na juu yake kulikuwa na chakula kwa ajili ya wote. Chini ya kivuli chake wanyama wa kondeni walipata hifadhi, na ndege wa angani waliishi katika matawi yake. Kila kiumbe kililishwa kutokana na mti huo.

134:13 Dan 8:13; Kum 33:2; Dan 7:1“Katika maono niliyoyaona nikiwa nimelala kitandani mwangu, nilitazama, na mbele yangu alikuwepo mlinzi, aliye mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni. 144:14 Mt 3:10; Dan 5:20; Ay 24:20; Eze 31:2Akaita kwa sauti kubwa: ‘Kateni mti huu, myafyeke matawi yake; yaondoeni majani yake na kuyatawanya matunda yake. Wanyama na wakimbie kutoka chini yake na ndege waondoke kutoka matawi yake. 15Lakini acheni kisiki chake na mizizi, kikiwa kimefungwa kwa chuma na shaba, kibaki ardhini, kwenye majani ya kondeni.

“ ‘Mwacheni aloweshwe na umande wa mbinguni, naye aachwe aishi pamoja na wanyama miongoni mwa mimea ya dunia. 16Akili yake na ibadilishwe kutoka ile ya mwanadamu na apewe akili ya mnyama, mpaka nyakati saba zipite juu yake.

174:17 Za 83:18; Rum 13:1; Mt 23:12; Dan 11:21; Za 83:18; Yer 27:5-7; Za 103:19“ ‘Uamuzi huu umetangazwa na walinzi, hukumu imetangazwa na watakatifu, ili walio hai wajue kuwa Aliye Juu Sana ndiye anayetawala juu ya falme zote za wanadamu, naye humpa yeyote amtakaye na kumtawaza juu yake hata yeye aliye mnyonge sana miongoni mwa wanadamu.’

184:18 Mwa 41:8; Dan 5:8, 15; 1:20; Mwa 41:38; Dan 1:20“Hii ndiyo ndoto niliyoipata mimi, Mfalme Nebukadneza. Sasa Belteshaza, niambie maana yake, kwa maana hakuna hata mmoja wa wenye hekima katika ufalme wangu anayeweza kunifasiria. Bali wewe waweza, kwa sababu roho ya miungu mitakatifu imo ndani yako.”

Danieli Anafasiri Ndoto

194:19 Mwa 41:15; Dan 10:16-17; 2Sam 18:32; Mwa 41:8; 40:12; Dan 7:15, 28; 8:27Ndipo Danieli (aliyeitwa pia Belteshaza) alipofadhaika sana kwa muda, nayo mawazo yake yakamtia hofu. Basi mfalme akasema, “Belteshaza, usiruhusu ndoto wala maana yake kukutia hofu.”

Belteshaza akamjibu, “Bwana wangu, laiti ndoto hii ingehusu adui zako, na maana yake iwahusu watesi wako! 20Mti uliouona, uliokua ukawa mkubwa na wenye nguvu, nayo ncha yake ikagusa anga na kuonekana duniani kote, 214:21 Eze 31:6ukiwa na majani ya kupendeza na matunda mengi, ukitoa chakula kwa wote, na ukiwapa hifadhi wanyama wa kondeni na kuwa mahali pa viota katika matawi yake kwa ajili ya ndege wa angani. 224:22 2Sam 12:7; Yer 27:7; Dan 2:37-38; Ay 20:5; Dan 5:18-19Ee mfalme, wewe ndiwe ule mti! Umekuwa mkubwa na mwenye nguvu, nao ukuu wako umekua mpaka kufika juu angani, nayo mamlaka yako yameenea mpaka miisho ya dunia.

234:23 Dan 8:13; 5:21; Eze 31:3-4“Ee mfalme, wewe ulimwona mlinzi, aliye mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni na kusema, ‘Ukateni mti na kuuangamiza, lakini kiacheni kisiki kikiwa kimefungwa kwa chuma na kwa shaba, kwenye majani ya kondeni, wakati mizizi yake inabaki ardhini. Mwacheni aloweshwe na umande wa mbinguni, mwacheni aishi kama wanyama pori mpaka nyakati saba zipite juu yake.’

244:24 Ay 40:12; Yer 40:2; Ay 34:19; Isa 46:10-11; Za 107:40“Ee mfalme, hii ndiyo tafsiri, na hii ni amri ya Aliye Juu Sana aliyoitoa dhidi ya bwana wangu mfalme: 254:25 Za 83:18; Yer 27:5; Dan 2:47; Ay 24:8; Dan 5:21; Za 83:18Wewe utafukuzwa mbali na wanadamu, nawe utaishi pamoja na wanyama pori; utakula manyasi kama ngʼombe, na kuloana kwa umande wa mbinguni. Nyakati saba zitapita juu yako, mpaka utakapokubali kuwa Yeye Aliye Juu Sana ndiye anayetawala juu ya falme za wanadamu, naye humtawaza yeyote amtakaye. 264:26 Dan 2:37; Lk 15:18Amri ya kuacha kisiki pamoja na mizizi yake inamaanisha kwamba ufalme wako utarejezwa kwako utakapokubali kwamba Mbingu ndizo zitawalazo. 274:27 Isa 55:6-7; Kum 24:13; 1Fal 21:29; Mdo 8:22; Za 41:3; Mit 28:13; Yer 29:7; Eze 18:22Kwa hiyo, ee mfalme, uwe radhi kupokea shauri langu: Acha dhambi zako kwa kutenda yaliyo haki, ukaache uovu wako, na uwe na huruma kwa walioonewa. Hivyo itawezekana baada ya hayo, mafanikio yako yakaendelea.”

Ndoto Inatimia

284:28 Hes 23:19; 2Sam 22:28; Dan 5:20Haya yote yalimpata Mfalme Nebukadneza. 29Miezi kumi na miwili baadaye, mfalme alipokuwa akitembea juu ya paa la jumba la kifalme la Babeli, 304:30 Mit 16:18; Isa 37:24-25; Hab 1:11; Isa 13:19; 10:13; Dan 5:20alisema, “Je, huu si Babeli mji mkuu nilioujenga kama makao ya kifalme, kwa uwezo wangu mkubwa, na kwa ajili ya utukufu wa enzi yangu?”

314:31 2Sam 22:28; Dan 5:20Maneno hayo yalikuwa bado katika midomo yake wakati sauti ilipokuja kutoka mbinguni, ikisema, “Mfalme Nebukadneza, hiki ndicho kilichoamriwa kwa ajili yako: Mamlaka yako ya ufalme yameondolewa kutoka kwako. 324:32 Ay 9:12Utafukuzwa mbali na wanadamu, ukaishi pamoja na wanyama pori, na utakula manyasi kama ngʼombe. Nyakati saba zitapita juu yako, mpaka utakapokubali kuwa Yeye Aliye Juu Sana ndiye anayetawala juu ya falme za wanadamu, naye humtawaza yeyote amtakaye.”

334:33 Ay 20:5; Dan 5:20-21; Ay 24:8Papo hapo yale yaliyokuwa yamesemwa kuhusu Nebukadneza yakatimia. Alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ngʼombe. Mwili wake uliloweshwa kwa umande wa mbinguni mpaka nywele zake zikakua kama manyoya ya tai na kucha zake kama makucha ya ndege.

344:34 Dan 12:7; Ufu 4:10; Lk 1:33; Ay 12:20; Isa 37:16; Dan 6:26; Za 145:13; Dan 2:44; 5:21Mwisho wa huo wakati, mimi Nebukadneza, niliinua macho yangu kuelekea mbinguni, nazo fahamu zangu zikanirudia. Ndipo nikamsifu Yeye Aliye Juu Sana, nikamheshimu na kumhimidi yeye aishiye milele.

Utawala wake ni utawala wa milele;

ufalme wake hudumu kutoka kizazi na kizazi.

354:35 Isa 40:17; Kum 21:8; Yon 1:14; Ay 9:4; Rum 9:20; Isa 14:24; 45:9; Za 115:3; 136:6; Kum 32:39; Dan 5:21Mataifa yote ya dunia

yanahesabiwa kuwa si kitu.

Hufanya kama atakavyo

kwa majeshi ya mbinguni,

na kwa mataifa ya dunia.

Hakuna anayeweza kuuzuia mkono wake

au kumwambia, “Umefanya nini wewe?”

364:36 Mit 22:4; Dan 5:18; Ay 42:12Wakati huo huo fahamu zangu ziliponirudia, nikarudishiwa heshima yangu na fahari yangu kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu. Washauri wangu na wakuu wangu walikuja kunitafuta, nami nikarudishwa kwenye kiti changu cha ufalme hata nikawa mkuu kuliko mwanzoni. 374:37 Kum 32:4; Za 33:4-5; Kut 18:11; Mt 23:12; Kut 15:2; Za 18:27; 34:3; Ay 31:4; 40:11-12; Isa 13:11; Dan 5:23; Za 119:21Basi mimi, Nebukadneza, humhimidi, na humtukuza na kumsifu Mfalme wa mbinguni, kwa sababu kila kitu afanyacho ni haki, na njia zake zote ni adili. Nao waendao kwa kiburi anaweza kuwashusha.