但以理書 11 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

但以理書 11:1-45

1瑪代大流士元年,我去幫助、護衛米迦勒2現在我要把真相告訴你。波斯將再有三位王興起,隨後的第四位王遠比其他王富有。他靠財富強盛後,便會煽動眾民去攻打希臘國。 3那時必有一位英勇的王興起,執掌大權,隨心所欲。 4但他興起後不久,他的國必土崩瓦解,在天下一分為四,既不歸他的後代統治,也不如他掌權時強盛。因為他的國必被連根拔除,歸給外人。

5「南方王必強盛,他的將領中將有一位比他更強盛,這人執掌王權,勢力強大。 6若干年後,南方王將與北方王聯盟。南方王的女兒將到北方王那裡締結盟約。但她必保不住自己的勢力,王權也無法長久。她和她的隨從、父親和輔佐者必遭殺害。

7「她家族中必有一人繼承王位,率軍攻打北方王,侵入他們的堡壘,擊敗他們, 8將他們的神像、鑄造的偶像及金銀寶器擄到埃及。此後數年,他不再去攻擊北方王。 9後來,北方王必侵入南方王的國土,但終必撤回本國。

10「北方王的兒子們必發動戰爭,召集大軍,如洪水席捲而來,直打到南方王的堡壘。 11南方王必大怒,出來迎戰北方王的大軍,並擊敗他們。 12南方王獲勝後必心高氣傲,殺戮成千上萬的人,但他的勝利不能持久。 13因為數年後,北方王必召集更龐大的軍隊,帶著大量裝備捲土重來。

14「那時,許多人必起來反抗南方王。你同胞中的殘暴之徒也必反叛,從而使異象應驗,但他們必失敗。 15北方王必修築高臺攻取南方王的堅城,南方的軍兵必無力抵擋,就是精兵也抵擋不住。 16北方王必為所欲為,所向無敵。他必侵佔佳美之地,手握毀滅之權。 17他決意傾全國之力而來,與南方王建立聯盟,並將自己的女兒嫁給南方王,旨在推翻他的國。但北方王的計劃必然失敗,毫無收益。

18「後來,他將轉而攻打沿海地區,征服許多地方。但一位將領必制止他的囂張氣焰,使他自取其辱。 19他將返回本國的堡壘,從此一蹶不振,銷聲匿跡。 20繼承他王位的人將派稅吏橫徵暴斂,以維持王國的榮耀。但不久他必滅亡,並非死於民怨,也非死於戰爭。

21「接著繼位的是一個卑鄙的人。他無權繼位,卻乘人不備用奸計奪取王位。 22他橫掃千軍,擊潰他們,包括盟國的王。 23他與人結盟後,必行欺詐,藉不多的人掌握大權。 24他必乘人不備入侵最富庶的地區,行他祖先從未行過的事,將擄掠的財物分給部下,並策劃攻打堡壘,但這都是短暫的。 25他集中力量,鼓起勇氣,率領大軍進攻南方王。南方王也率領強大的軍隊迎戰,卻敵不過他,因為有人暗算南方王。 26南方王必遭親信暗算,全軍潰敗,許多人被殺。 27兩個王心懷叵測,同席而坐,爾虞我詐,但都不成功,因為結局必在所定的時間到來。 28北方王必帶著大量財物回國,但他決意反對聖約,在回國的路上任意妄為。

29「到了所定的時間,他必再次攻打南方,但結果與上次不同, 30因為基提的戰船必來攻擊他,使他喪膽而回。他必向聖約之民發洩憤怒,任意妄為,支持背棄聖約的人。 31他的軍隊必褻瀆聖地,褻瀆那堡壘,廢除日常獻的祭,設立帶來毀滅的可憎之物。 32他必花言巧語籠絡違背聖約的人,但認識上帝的人必奮起反抗。 33那些智者必教導許多民眾,但他們將在一段時間內被刀劍殺戮,或被燒死,或被擄去,或被搶掠。 34他們敗亡時必得不到多少援助,許多人並非真心實意地加入他們的行列。 35有些智者將被害,但這是為了熬煉、淨化他們,使他們潔白無瑕,一直到末了。因為結局必在所定的時間到來。

36「北方王必任意妄為,自高自大,自以為超越一切神明,肆意詆譭萬神之神。他必亨通,一直到上帝發烈怒的日子結束。因為所定的必然成就。 37他不尊崇他祖先的神明,也不尊崇婦女們愛慕的神明或其他任何神明,因為他自認為超越一切。 38他反倒祭拜他祖先不認識的堡壘之神,向它獻上金銀寶石及貴重的禮物。 39他必靠外族神明的幫助攻打堅固的堡壘,將尊榮賜給順從他的人,派他們治理民眾,分給他們土地作獎賞。

40「到了末後,南方王必與北方王交戰。北方王必率領戰車、騎兵和大批戰船攻擊他,又如洪水般橫掃列國。 41他必侵入佳美之地,殺死成千上萬的人,只有以東摩押亞捫人的首領得以逃脫。 42他必攻擊列國,埃及也無法倖免。 43他必掌管埃及的金銀財寶,利比亞人和古實人必歸順他。 44但從東方和北方傳來的消息必令他震驚,他必大怒,出兵殺戮、毀滅許多人。 45他必在海和榮美的聖山之間搭起他宮殿般的帳幕。但他必滅亡,無人相助。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Danieli 11:1-45

111:1 Dan 5:31Nami katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Dario Mmedi, nilisimama kumsaidia na kumlinda.)

Wafalme Wa Kusini Na Wa Kaskazini

211:2 Dan 10:20-21“Sasa basi, ninakuambia kweli: Wafalme watatu zaidi watatokea Uajemi, kisha atatokea mfalme wa nne, ambaye atakuwa tajiri sana kuliko wengine wote. Wakati atakapokuwa amekwisha kujipatia nguvu kwa utajiri wake, atamchochea kila mmoja dhidi ya ufalme wa Uyunani. 311:3 Dan 8:4, 21Ndipo mfalme mwenye nguvu atatokea, ambaye atatawala kwa nguvu nyingi na kufanya anavyopenda. 411:4 Dan 7:2; 8:22; Yer 42:10Baada ya kujitokeza, milki yake itavunjwa na kugawanyika katika pande nne za mbinguni. Hautakwenda kwa wazao wake, wala hautakuwa na nguvu alizotumia, kwa sababu milki yake itangʼolewa na kupewa wengine.

5“Mfalme wa Kusini atakuwa na nguvu, lakini mmoja wa majemadari wake atakuwa na nguvu zaidi kuliko mfalme, naye atatawala ufalme wake mwenyewe kwa nguvu nyingi. 6Baada ya miaka kadha, wataungana. Binti wa mfalme wa Kusini ataolewa kwa mfalme wa Kaskazini ili kuimarisha mapatano, lakini huyo binti nguvu zake hazitadumu; hata mfalme hatadumu wala nguvu zake. Katika siku hizo atafukuzwa, pamoja na hao wasindikizaji wake wa kifalme, watoto wake, na yeyote aliyemuunga mkono.

7“Mmoja kutoka jamaa ya huyo binti atainuka na kuchukua nafasi yake. Atashambulia majeshi ya mfalme wa Kaskazini na kuingia katika ngome yake; atapigana dhidi yao naye atashinda. 811:8 Isa 37:19; 46:1-2; Yer 43:12Tena ataitwaa miungu yao, vinyago vyao vya chuma, na vitu vyao vya thamani vya fedha na dhahabu, na kuvichukua hadi Misri. Kwa miaka kadha atamwacha mfalme wa Kaskazini bila kumsumbua. 9Kisha mfalme wa Kaskazini atashambulia nchi ya mfalme wa Kusini, lakini atarudi nyuma hadi kwenye nchi yake. 1011:10 Isa 8:8; Yer 46:8; Dan 9:26Wana wa mfalme wa Kaskazini watajiandaa kwa vita na kukusanya jeshi kubwa, ambalo litafagia nchi kama mafuriko yasiyozuilika na kuendelea na vita hadi kwenye ngome ya mfalme wa Kusini.

1111:11 Dan 8:7-8“Kisha mfalme wa Kusini atatoka kwa ghadhabu na kupigana dhidi ya mfalme wa Kaskazini, ambaye ataunda jeshi kubwa, lakini litashindwa. 12Wakati jeshi litakapokuwa limechukuliwa, mfalme wa Kusini atajawa na kiburi na atachinja maelfu mengi, hata hivyo hatabaki na ushindi. 13Kwa maana mfalme wa Kaskazini atakusanya jeshi jingine kubwa kuliko lile la kwanza; na baada ya miaka kadha, atasonga mbele na jeshi kubwa mno lililoandaliwa vizuri.

14“Katika nyakati hizo wengi watainuka dhidi ya mfalme wa Kusini. Watu wenye ghasia miongoni mwa watu wako mwenyewe wataasi ili kutimiza maono, lakini bila mafanikio. 1511:15 Eze 4:2; Za 33:16Ndipo mfalme wa Kaskazini atakuja na kuuzunguka mji kwa majeshi, na kuuteka mji wa ngome. Majeshi ya Kusini yatakosa nguvu za kuyazuia; naam, hata vikosi vyao vya askari vilivyo bora zaidi, havitakuwa na nguvu ya kuwakabili. 1611:16 Dan 8:4-7, 9; Yos 1:5Huyo mvamia nchi atafanya apendavyo; hakuna yeyote atakayeweza kumpinga. Atajiimarisha katika Nchi ya Kupendeza, na atakuwa na uwezo wa kuiangamiza. 1711:17 Za 20:4; 2Nya 20:3Ataamua kuja na nguvu za ufalme wake wote na kufanya mapatano ya amani na mfalme wa Kusini. Naye atamtoa binti yake aolewe naye ili kuuangusha ufalme, lakini mipango yake haitafanikiwa wala kumsaidia. 1811:18 Isa 66:19; Yer 25:22; Hos 12:14Ndipo atabadili nia yake kupigana na nchi za pwani na ataziteka nyingi, lakini jemadari mmoja atakomesha ufidhuli wake na kurudisha ufidhuli wake juu yake. 1911:19 Za 27:2; 46:2; 37:36; Eze 26:21Baada ya hili atazigeukia ngome za nchi yake mwenyewe, lakini atajikwaa na kuanguka, wala hataonekana tena.

2011:20 Isa 60:17“Atakayetawala baada yake atamtuma mtoza ushuru ili kudumisha fahari ya kifalme. Hata hivyo, baada ya miaka michache ataangamizwa, lakini si katika hasira wala katika vita.

2111:21 Dan 4:17; 8:25; 2Sam 15:6“Atakayetawala baada yake atakuwa mtu wa kudharauliwa ambaye hajapewa heshima ya kifalme. Atauvamia ufalme wakati watu wake wanapojiona wako salama, naye atautwaa kwa hila. 2211:22 Dan 8:10-11; Isa 28:15Ndipo jeshi kubwa litafagiliwa mbele yake; jeshi pamoja na mkuu mmoja wa agano wataangamizwa. 2311:23 Dan 8:25Baada ya kufanya mapatano naye, atatenda kwa udanganyifu, na akitumia watu wachache tu ataingia madarakani. 2411:24 Neh 9:25Wakati majimbo yaliyo tajiri sana yanajiona salama, atayavamia, naye atafanikisha kile ambacho baba zake wala babu zake hawakuweza. Atagawa nyara, mateka na utajiri miongoni mwa wafuasi wake. Atafanya hila ya kupindua miji yenye maboma, lakini kwa muda mfupi tu.

25“Pamoja na jeshi kubwa atachochea nguvu zake na ushujaa wake dhidi ya mfalme wa Kusini. Mfalme wa Kusini atafanya vita na jeshi lenye nguvu sana, lakini hataweza kusimama kwa sababu ya kwa hila zilizofanywa dhidi yake. 26Wale wanaokula kutoka kwenye ruzuku za mfalme watajaribu kumwangamiza; jeshi lake litafagiliwa mbali, nao wengi watakufa vitani. 2711:27 Za 64:6; 12:2; Yer 9:5; Hab 2:3Wafalme hawa wawili, mioyo yao ikiwa imekusudia mabaya, wataketi kwenye meza moja na kudanganyana wao kwa wao, lakini pasipo faida, kwa sababu bado mwisho utakuja katika wakati ulioamriwa. 28Mfalme wa Kaskazini atarudi katika nchi yake na utajiri mwingi, lakini atakuwa ameukaza moyo wake kinyume na agano takatifu. Atachukua hatua dhidi ya hilo agano, kisha atarudi nchi yake.

29“Wakati ulioamriwa, atavamia tena Kusini, lakini wakati huu matokeo yake yatakuwa tofauti na yale ya wakati wa kwanza. 3011:30 Hes 24:24; Mwa 10:4; 1Sam 17:32; Ay 15:13Meli za nchi ya Kitimu zitampinga, naye atavunjika moyo. Ndipo atarudi nyuma na kutoa wazi hasira yake dhidi ya agano takatifu. Atarudi na kuonyesha fadhili kwa wale waliachao agano takatifu.

3111:31 Yer 19:4; Mt 24:15; Hos 3:4; Dan 8:11-13; 9:27; Mk 13:14“Majeshi yake yenye silaha yatainuka ili kunajisi ngome ya Hekalu, na kuondolea mbali sadaka ya kuteketezwa ya kila siku. Ndipo watalisimamisha chukizo la uharibifu lisababishalo ukiwa. 3211:32 1Nya 28:9; Mik 5:7-9Kwa udanganyifu atapotosha wale walionajisi agano, lakini watu wanaomjua Mungu wao watampinga kwa uthabiti.

3311:33 Dan 12:3; Mal 2:7; Yn 16:2; Ebr 11:32-38; Mt 24:9“Wenye hekima watawafundisha wengi, ingawa kwa kitambo watauawa kwa upanga au kuchomwa moto, au kukamatwa au kufanywa mateka. 3411:34 Mt 7:15; Rum 16:18Watakapoanguka, watapokea msaada kidogo, nao wengi ambao si waaminifu wataungana nao. 3511:35 Ay 28:1; Yn 15:2; Za 78:38; Isa 48:10; Dan 12:10; Zek 13:9Baadhi ya wenye hekima watajikwaa, ili waweze kusafishwa, kutakaswa na kufanywa wasio na waa mpaka wakati wa mwisho, kwa maana bado litakuja kwa wakati ulioamriwa.

Mfalme Ajikwezaye Mwenyewe

3611:36 1The 2:4; Ufu 13:5-6; Kum 10:17; Isa 26:20; Yud 16; Dan 7:25; Isa 10:25“Mfalme atafanya apendavyo. Atajikweza na kujitukuza juu ya kila mungu, naye atasema mambo ambayo hayajasikiwa dhidi ya Mungu wa miungu. Atafanikiwa hadi wakati wa ghadhabu utimie, kwa maana kile kilichokusudiwa lazima kitokee. 37Hataonyesha heshima kwa miungu ya baba zake au kwa yule aliyetamaniwa na wanawake, wala hatajali mungu yeyote, bali atajikweza mwenyewe juu yao wote. 38Badala ya kuwajali miungu, ataheshimu mungu wa ngome; mungu ambaye hakujulikana na baba zake ndiye atamheshimu kwa dhahabu na fedha, kwa vito vya thamani na zawadi za thamani kubwa. 39Atashambulia ngome zenye nguvu mno kwa msaada wa mungu wa kigeni naye atawaheshimu sana wale watakaomkubali yeye. Atawafanya watawala juu ya watu wengi, na atagawa nchi kwa gharama.

4011:40 Isa 21:1; 5:28; Eze 38:4; Isa 8:7“Katika wakati wa mwisho, mfalme wa Kusini atapigana naye vita, naye mfalme wa Kaskazini atamshambulia kwa magari ya vita, askari wapanda farasi, na idadi kubwa ya meli. Atavamia nchi nyingi na kuzikumba nchi hizo kama mafuriko. 4111:41 Isa 11:14; Yer 48:47; Mal 3:12; Eze 20:6Pia ataivamia Nchi ya Kupendeza. Nchi nyingi zitapinduliwa, bali Edomu, Moabu na viongozi wa Amoni wataokolewa kutoka mkono wake. 42Atapanua mamlaka yake juu ya nchi nyingi; hata Misri haitaepuka. 4311:43 Eze 30:4; 2Nya 12:3; Nah 3:9Atamiliki hazina za dhahabu, fedha na utajiri wote wa Misri, pamoja na Walibia na Wakushi kwa kujisalimisha. 44Lakini taarifa kutoka mashariki na kaskazini zitamshtua, naye ataondoka kwa ghadhabu nyingi ili kuangamiza na kuharibu kabisa wengi. 4511:45 Isa 2:2-4; Dan 8:9Atasimika hema zake za ufalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa kupendeza. Hata hivyo, atafikia mwisho wake, wala hakuna yeyote atakayemsaidia.