以斯帖記 5 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

以斯帖記 5:1-14

以斯帖為王和哈曼設宴

1第三天,以斯帖身穿朝服進入王宮內院,面對大殿站立,王在殿裡正面朝宮門坐在寶座上。 2王見以斯帖王后站在院內,就施恩給她,向她伸出手中的金杖,以斯帖便上前摸杖頭。 3王問道:「以斯帖王后啊,你有什麼事?你有何要求?就是半壁江山,也必賜給你!」 4以斯帖回答說:「王若願意,就請王今天帶哈曼來赴我預備的宴席。」 5王說:「快召哈曼來,我們好照以斯帖的話做。」於是王帶著哈曼以斯帖預備的宴席。 6席間,王對以斯帖說:「你要什麼?我必賜給你。你有何要求?就是半壁江山,也必為你成就。」 7以斯帖回答說:「王啊,我所要、我所求的就是, 8我若得到王的恩寵,王若願意賜我所要所求的,就請王明天帶哈曼再來赴我預備的宴席,到時我一定向王稟明。」

哈曼圖謀殺末底改

9那天哈曼出來,心中歡喜快樂。但他看見末底改在宮門前既不起身,也不對他表示畏懼,心中十分惱火。 10哈曼忍怒回到家中,把朋友和妻子細利斯叫來, 11向他們誇耀自己的榮華富貴和兒孫滿堂,以及王怎樣擢升他,使他位極人臣。 12哈曼又說:「還有,以斯帖王后只請了我隨王赴她預備的宴席。她還請我明天隨王赴宴。 13但只要我看見猶太末底改坐在宮門口,這一切對我都毫無意義。」 14他妻子細利斯和他所有的朋友對他說:「你可以叫人做一個二十三米高的木架,明天早上求王將末底改吊在上面,然後你可以快樂地隨王去赴宴。」哈曼喜歡這個提議,就叫人做了木架。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Esta 5:1-14

Ombi La Esta Kwa Mfalme

15:1 Eze 16:13; Mit 21:1Siku ya tatu, Esta alivaa mavazi yake ya kimalkia, naye akasimama katika ua wa ndani wa jumba la mfalme, mbele ya ukumbi wa mfalme. Naye mfalme alikuwa akiketi katika kiti chake cha kifalme katika ukumbi, akielekea langoni. 2Alipomwona Malkia Esta amesimama uani alipendezwa naye, akamnyooshea fimbo ya utawala ya dhahabu ile iliyokuwa mkononi mwake. Kwa hiyo Esta alikaribia na kuigusa ncha ya fimbo ya mfalme.

35:3 Es 7:2; Mk 6:23Kisha mfalme aliuliza, “Malkia Esta, ni nini? Ombi lako ni nini? Hata kama ni nusu ya ufalme, utapewa.”

4Esta akajibu, “Kama itampendeza mfalme, mfalme pamoja na Hamani waje leo katika karamu ambayo nimeiandaa kwa ajili yake.”

5Mfalme akasema, “Mleteni Hamani mara moja, ili tupate kufanya lile Esta analoomba.”

Kwa hiyo mfalme na Hamani walihudhuria karamu aliyoiandaa Esta. 65:6 Dan 5:16Walipokuwa wakinywa mvinyo mfalme akamuuliza Esta tena, “Sasa haja yako ni nini? Utapewa. Ombi lako ni nini? Hata nusu ya ufalme, utapewa.”

7Esta akajibu, “Haja yangu na ombi langu ni hili: 85:8 Es 2:15; 1Fal 3:15Kama mfalme ameona vyema, nami nimepata kibali kwake na kama ikimpendeza mfalme kunipa ombi langu na kunitimizia haja yangu, mfalme na Hamani waje kwangu kesho katika karamu nitakayowaandalia. Kisha nitajibu swali la mfalme.”

Ghadhabu Ya Hamani Dhidi Ya Mordekai

95:9 Mit 14:17Hamani alitoka siku hiyo kwa furaha na moyo mchangamfu. Lakini alipomwona Mordekai langoni mwa mfalme na kuona kwamba hakusimama wala hakuonyesha hofu mbele yake, alijawa na ghadhabu dhidi ya Mordekai. 105:10 Es 6:13Hata hivyo, Hamani alijizuia akaenda zake nyumbani.

Akawaita pamoja rafiki zake na Zereshi, mkewe. 115:11 Mit 13:16; Es 9:10, 13Hamani akajisifia kwao juu ya utajiri wake mwingi, wanawe wengi na kwa njia zote ambazo mfalme amemheshimu kwazo na jinsi alivyomweka juu ya wakuu na maafisa wengine. 12Hamani akaongeza, “Si hayo tu. Mimi ndiye mtu pekee ambaye Malkia Esta amemwalika kumsindikiza mfalme kwenye karamu aliyomwandalia. Naye amenialika pamoja na mfalme kesho. 13Lakini haya yote hayanipi kuridhika iwapo ninaendelea kumwona yule Myahudi Mordekai akiketi kwenye lango la mfalme.”

145:14 Es 7:9; Ezr 6:11Zereshi mkewe na rafiki zake wote wakamwambia, “Tengeneza mahali pa kuangika watu kimo chake dhiraa hamsini,5:14 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5. kisha kesho asubuhi mwombe mfalme Mordekai aangikwe juu yake. Ndipo uende na mfalme kwenye karamu kwa furaha.” Shauri hili lilimpendeza Hamani, naye akajenga mahali pa kuangika watu.