Chinese Contemporary Bible (Traditional)

箴言 26:1-28

1愚人得尊榮本不合宜,

如夏天降雪、收割時下雨。

2麻雀翻飛,燕子翱翔,

咒詛不會無端降臨。

3鞭子打馬,韁繩勒驢,

棍棒責打愚人的背。

4別照愚人的愚昧回答他,

免得你像他一樣。

5要照愚人的愚昧回答他,

免得他自以為有智慧。

6靠愚人傳信,

如同砍斷自己的腳,

自討苦吃。

7愚人口中說箴言,

如同跛子空有腿。

8把尊榮給愚人,

就像把石子綁在甩石器上。

9愚人口中說箴言,

如同醉漢握荊棘。

10雇用愚人或路人,

如同弓箭手亂箭傷人。

11愚人一再重複愚昧事,

就像狗回頭吃所吐的。

12自以為有智慧的人,

還不如愚人有希望。

13懶惰人說:「路上有獅子,

街上有猛獅。」

14懶惰人賴在床上滾來滾去,

就像門在門軸上轉來轉去。

15懶惰人手放在餐盤,

卻懶得送食物進嘴。

16懶惰人自以為比七個善於應對的人更有智慧。

17插手他人的糾紛,

猶如揪狗的耳朵。

18-19欺騙鄰舍還說是開玩笑,

如同瘋子亂拋火把、亂射箭。

20沒有木柴,火自然熄滅;

沒有閒話,爭端便平息。

21好鬥之人煽動爭端,

如同餘火加炭、火上加柴。

22閒言閒語如可口的美食,

輕易進入人的五臟六腑。

23火熱的嘴,邪惡的心,

猶如瓦器鍍了層銀。

24怨恨人的用美言掩飾自己,

心中卻藏著詭詐。

25縱然他甜言蜜語,你也不可信他,

因為他心中充滿各種可憎之事。

26雖然他用詭計掩飾怨恨,

他的邪惡必被會眾揭穿。

27挖陷阱的,必自陷其中;

滾石頭的,必自傷己身。

28撒謊的舌恨它所害的人,

諂媚的嘴帶來毀滅。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mithali 26:1-28

126:1 Isa 32:6; 1Sam 12:17; Mit 19:10Kama theluji wakati wa kiangazi au mvua wakati wa mavuno,

ndivyo asivyostahili heshima mpumbavu.

226:2 Hes 23:8; Kum 23:5Kama shomoro apigapigavyo mabawa yake

au mbayuwayu katika kuruka kwake kasi,

ndivyo ilivyo laana isiyo na sababu haimpati mtu.

326:3 Za 32:9; Mit 10:13Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda,

nayo fimbo kwa migongo ya wapumbavu!

426:4 Isa 36:21Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake,

ama wewe mwenyewe utakuwa kama yeye.

526:5 Mt 16:14; 21:24-27; Mit 3:7Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake,

ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe.

626:6 Mit 10:26Kama vile ilivyo kujikata miguu au kunywa hasara,

ndivyo ilivyo kutuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu.

726:7 Mit 26:9Kama miguu ya kiwete inavyoningʼinia

ndivyo ilivyo mithali katika kinywa cha mpumbavu.

826:8 Mit 26:1Kama kufunga jiwe kwenye kombeo,

ndivyo ilivyo kumpa mpumbavu heshima.

926:9 Mit 26:7Kama mwiba kwenye mkono wa mlevi

ndivyo ilivyo mithali kinywani mwa mpumbavu.

10Kama mpiga upinde ambaye hujeruhi ovyo,

ndivyo alivyo yeye aajiriye mpumbavu au yeyote apitaye njiani.

1126:11 Kut 8:15; Za 85:8; 2Pet 2:22Kama mbwa ayarudiavyo matapiko yake,

ndivyo mpumbavu arudiavyo upumbavu wake.

1226:12 Ufu 3:17; Mit 29:20Je, unamwona mtu ajionaye mwenye hekima

machoni pake mwenyewe?

Liko tumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake.

1326:13 Mit 6:6-11; 24:30-34; 22:13Mvivu husema, “Yuko simba barabarani,

simba mkali anazunguka mitaa!”

1426:14 Mit 6:9Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake,

ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake.

1526:15 Mit 19:24Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani,

naye huchoka kuupeleka kwenye kinywa chake.

16Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe,

kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.

17Kama yeye amkamataye mbwa kwa masikio,

ndivyo alivyo mtu apitaye njiani na kujiingiza kwenye ugomvi usiomhusu.

18Kama mtu mwendawazimu

atupaye vijinga vya moto au mishale ya kufisha,

1926:19 Efe 5:4ndivyo alivyo mtu amdanganyaye jirani yake na kusema,

“Nilikuwa nikifanya mzaha tu!”

2026:20 Mit 22:10Bila kuni moto huzimika;

pasipo uchongezi ugomvi humalizika.

2126:21 Mit 14:17Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, na kama kuni kwenye moto,

ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuchochea ugomvi.

2226:22 Mit 18:8; Eze 22:9Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu;

huingia sehemu za ndani sana za mtu.

2326:23 Lk 22:48Kama rangi ingʼaayo iliyopakwa kwenye vyombo vya udongo

ndivyo ilivyo midomo laini pamoja na moyo mbaya.

2426:24 Za 31:18; 41:6; Mit 10:18; Za 31:18; 41:6Mtu mwenye nia ya kudhuru wengine hujificha kwa maneno ya midomo yake,

lakini moyoni mwake huficha udanganyifu.

2526:25 Za 28:3; Yer 9:4-8Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini,

kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake.

26Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu,

lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko.

2726:27 Za 7:15-16; 35:8; Mhu 10:8; Mit 28:10; Es 6:13; 7:9Kama mtu akichimba shimo, atatumbukia ndani yake,

kama mtu akivingirisha jiwe, litamrudia.

2826:28 Mit 13:6; 29:5; Za 12:3Ulimi wa uongo, huwachukia wale unaowaumiza,

nacho kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.