Chinese Contemporary Bible (Traditional)

歷代志上 22:1-19

1大衛說:「耶和華上帝的殿和以色列人獻燔祭的壇要在這裡。」

大衛籌備建殿

2大衛下令召集住在以色列的外族人,派他們採鑿建上帝殿用的石頭。 3大衛預備了大量的鐵,用來做門扇的釘子和鉤子,又預備了不計其數的銅。 4他還預備了無數的香柏木,都是西頓人和泰爾人給他運來的。

5大衛說:「為耶和華建造的殿宇必須宏偉輝煌,聞名於世,而我的兒子所羅門年紀還輕、閱歷尚淺,所以我要為這殿預備材料。」因此,大衛在去世前為建殿預備了許多材料。

6大衛召來兒子所羅門,囑咐他要為以色列的上帝耶和華建造殿宇。 7他對所羅門說:「兒啊,我本想為我的上帝耶和華的名建造一座殿宇。 8但耶和華對我說,『你殺了許多人,打了很多仗,在我眼前使許多人血灑大地,因此你不可為我的名建造殿宇。 9你將生一個兒子,我必使他安享太平,不受四圍的仇敵侵擾。他的名字要叫所羅門,他執政期間,我必使以色列太平安寧。 10他將為我的名建造殿宇,他要做我的兒子,我要做他的父親,我要使他的王朝在以色列永遠長存。』

11「兒啊,願耶和華與你同在,使你亨通,照你的上帝耶和華的吩咐去建造祂的殿。 12願耶和華賜你聰明和智慧,以便你照祂的律法治理以色列13你若謹遵耶和華藉摩西吩咐以色列的律例和典章,就必亨通。你要剛強勇敢,不可驚慌害怕。 14看啊,我歷盡艱辛,為耶和華的殿預備了三千四百五十噸金子、三萬四千五百噸銀子和不計其數的銅和鐵。我還預備了木料和石頭。你還要多加預備。 15你有許多工匠,如鑿石匠、砌石匠、木匠等各種能工巧匠, 16還有不計其數的金匠、銀匠、銅匠和鐵匠。現在動工吧,願耶和華與你同在。」

17大衛又吩咐以色列的眾首領幫助他兒子所羅門18他說:「你們的上帝耶和華與你們同在,使你們四境平安。祂將這地方的居民交在我手中,使這地方被祂和祂的子民治理。 19現在,你們要全心全意地尋求你們的上帝耶和華,去建造耶和華上帝的聖所,好將祂的約櫃和聖潔器皿都放在裡面。」

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Nyakati 22:1-19

122:1 Kum 12:5; Mwa 28:17; 1Nya 21:18-28; 2Nya 3:1; Kum 12:5; 2Sam 24:18Ndipo Daudi akasema, “Nyumba ya Bwana Mungu itakuwa mahali hapa, pia pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Israeli.”

Maandalizi Kwa Ajili Ya Hekalu

222:2 Kum 20:11; 1Fal 9:21; 5:17-18; Ezr 3:7Kwa hiyo Daudi akatoa amri wakusanyike wageni wote waliokuwa wanaishi Israeli, na kutoka miongoni mwao akaweka waashi ili kuchonga mawe kwa ajili ya kujenga nyumba ya Mungu. 322:3 1Fal 7:47Daudi akatoa chuma tele ili kutengenezea misumari kwa ajili ya mafungo ya malango ya nyumba na shaba tele isiyopimika. 422:4 1Fal 5:6Pia akatoa magogo ya mierezi yasiyohesabika, kwa kuwa Wasidoni na Watiro walikuwa wamemletea Daudi idadi kubwa ya mierezi.

522:5 1Fal 3:7; 1Nya 29:1Daudi akasema, “Mwanangu Solomoni bado ni mdogo wa umri na hana uzoefu. Nyumba itakayojengwa kwa ajili ya Bwana inatakiwa iwe yenye uzuri mwingi na sifa na fahari mbele ya mataifa yote. Kwa hiyo nitaifanyia matayarisho.” Daudi akafanya matayarisho makubwa kabla ya kifo chake.

622:6 Mdo 7:47Kisha akamwita Solomoni mwanawe akamwagiza kujenga nyumba kwa ajili ya Bwana, Mungu wa Israeli. 722:7 1Nya 17:2; 2Sam 7:2; 1Fal 8:17; Kum 12:5-11; Mdo 7:48Daudi akamwambia Solomoni: “Mwanangu, nilikuwa na jambo hili ndani ya moyo wangu kujenga nyumba kwa ajili ya Jina la Bwana Mungu wangu. 822:8 1Fal 5:3; 1Nya 28:3Lakini neno hili la Bwana likanijia, kusema: ‘Wewe umemwaga damu nyingi na kupigana vita vingi. Wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu. 922:9 Yos 14:15; 2Sam 12:24; 1Fal 4:20; 5:4; 1Nya 28:5Lakini utakuwa na mwana ambaye atakuwa mtu wa amani na utulivu nami nitampa utulivu mbele ya adui zake wote pande zote. Jina lake ataitwa Solomoni, nami nitawapa Israeli amani na utulivu wakati wa utawala wake. 1022:10 1Nya 17:12; 2Sam 7:13-14; 2Nya 6:15; 1Fal 5:5; 1Nya 28:6; Za 89:26-27; Ebr 1:5Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu. Yeye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake. Nami nitakifanya imara kiti chake cha enzi cha utawala wake katika Israeli milele.’

1122:11 1Sam 18:12; Rum 8:31“Sasa, mwanangu, Bwana awe pamoja nawe, nawe uwe na mafanikio upate kuijenga nyumba ya Bwana Mungu wako, kama alivyosema utafanya. 1222:12 1Fal 3:11; 2Nya 1:10; Kum 4:6Bwana na akupe hekima na ufahamu wakati atakuweka juu ya Israeli, ili uweze kuishika sheria ya Bwana Mungu wako. 1322:13 1Nya 28:7; Kum 31:6-7; Yos 1:6-9; 1Fal 6:12-13; 9:4-5; Isa 3:10; 1Nya 28:20Ndipo utakapofanikiwa, ikiwa utakuwa na bidii kutii amri na sheria Bwana alizompa Mose kwa ajili ya Israeli. Uwe hodari na ushujaa. Usiogope wala usikate tamaa.

1422:14 1Nya 29:2-5, 19“Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la Bwana: talanta 100,00022:14 Talanta 100,000 za dhahabu ni sawa na tani 3,750. za dhahabu, talanta 1,000,00022:14 Talanta 1,000,000 za fedha ni sawa na tani 37,500. za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza. 15Unao wafanyakazi wengi: Wachonga mawe, waashi na maseremala, pamoja na watu walio na ustadi katika kila kazi 16wa kufua dhahabu, fedha, shaba na chuma, mafundi wasiohesabika. Sasa basi anza kazi hii, naye Bwana awe pamoja nawe.”

1722:17 1Nya 28:1-6Kisha Daudi akawaamuru viongozi wote wa Israeli wamsaidie Solomoni mwanawe. 1822:18 1Fal 8:6; Kum 12:10; Yos 22:4Akawaambia, “Je, Bwana Mungu wenu si yuko pamoja na ninyi? Pia si amewapa raha pande zote? Kwa maana amewatia wenyeji wa nchi mkononi mwangu, nayo nchi iko chini ya Bwana na watu wake. 1922:19 2Nya 20:3; 1Fal 8:6; 2Nya 5:7; 6:11Sasa itoeni mioyo yenu na nafsi zenu katika kumtafuta Bwana Mungu wenu. Anzeni kujenga Maskani ya Bwana Mungu, ili mweze kulileta Sanduku la Agano la Bwana na vyombo vitakatifu vya Mungu katika Hekalu litakalojengwa kwa ajili ya Jina la Bwana.”