路加福音 5 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

路加福音 5:1-39

呼召门徒

1一天,耶稣站在革尼撒勒湖边,众人团团围着祂,要听上帝的道。 2祂看见湖边停着两条船,渔夫离了船正在洗网, 3就上了西门的那条船,请西门把船稍微划离岸边,然后坐在船上教导众人。 4耶稣讲完之后对西门说:“把船划到水深的地方去撒网捕鱼。”

5西门说:“老师,我们劳碌了一整夜,一无所获,但既然你这样吩咐,我就照你的话做。” 6他们把网撒下去,果然捕获很多鱼,差点把网撑破了, 7于是招呼另一条船上的同伴来帮忙。他们一起把两条船都装满了鱼,船几乎要沉下去了。

8西门·彼得见状,便跪倒在耶稣膝前说:“主啊,离开我,我是个罪人!” 9他和所有同伴们对捕到这么多鱼感到非常惊讶, 10包括西庇太的两个儿子雅各约翰。耶稣对西门说:“不要怕,从今以后,你将成为得人的渔夫。” 11于是他们把船靠岸后,撇下一切跟从了耶稣。

洁净麻风病人

12有一次,耶稣在一个小镇遇见一个浑身患麻风病的人,那人一看见耶稣,就俯伏在地上恳求说:“主啊,如果你肯,一定能使我洁净。”

13耶稣伸手摸他,说:“我肯,你洁净了吧!”他身上的麻风病立刻消失了。

14耶稣又嘱咐他:“不要把这事告诉别人,要去让祭司察看你的身体,照摩西的规定献上祭物,向众人证明你已经洁净了。”

15结果耶稣的名声传得更广了,成群的人聚集到祂那里听祂讲道、求祂医病。 16不过,祂还是常常退到旷野去祷告。

叫瘫子行走

17有一天,耶稣在教导人,旁边坐着来自加利利犹太耶路撒冷各地的法利赛人和律法教师,主的能力伴随着耶稣,使祂能医治病人。

18有人用担架抬着一个瘫痪的人想进到屋里,把他放在耶稣面前。 19可是人太挤了,无法进去,他们就爬上屋顶,掀开瓦片,把那病人连人带担架缒到耶稣面前。 20耶稣看见他们那么有信心,就对瘫子说:“朋友,你的罪得到赦免了!”

21那些法利赛人和律法教师开始议论起来:“这个说话亵渎上帝的人是谁啊?除了上帝以外,谁能够赦罪?”

22耶稣知道他们的想法,就问:“你们为什么心里议论呢? 23说‘你的罪得到赦免了’容易呢,还是说‘你起来行走’容易呢? 24如今我要让你们知道人子在世上有赦罪的权柄。”于是对瘫子说:“我吩咐你起来!收拾你的担架回家去吧。”

25那人立刻当众站了起来,拿起他躺卧的担架回家去了,不住地赞美上帝。 26众人都十分惊奇,一同赞美上帝,心里充满了敬畏,说:“今天我们看到神迹了!”

呼召利未

27后来耶稣外出时,看见一个名叫利未的税吏坐在收税站里,就对他说:“跟从我!” 28利未就起来,撇下一切跟从了耶稣。

29随后,他在家设宴款待耶稣,赴宴的人中有许多税吏和其他人。 30法利赛人和律法教师就向耶稣的门徒抱怨说:“你们为什么跟税吏和罪人一起吃喝呢?”

31耶稣答道:“健康的人不需要医生,有病的人才需要。 32我来不是要召义人悔改,乃是召罪人悔改。”

论禁食

33他们说:“约翰的门徒常常禁食祷告,法利赛人的门徒也是一样,可是你的门徒却又吃又喝。”

34耶稣说:“新郎还跟宾客在一起的时候,岂能让宾客禁食? 35但有一天新郎将被带走,那时他们就要禁食了。” 36耶稣又给他们讲了一个比喻,说:“没有人会从新衣服上撕下一块布来,补在旧衣服上。否则,不但新衣服撕破了,旧衣服和新补丁也不相称。 37同样,没有人把新酒装进旧皮囊里,否则新酒会把旧皮囊胀破,酒也漏了,皮囊也毁了。 38所以新酒一定要装在新皮囊里。 39但是,没有人喝过陈年老酒后,还愿意喝新酒,因为他会说,‘还是陈年老酒好。’”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Luka 5:1-39

Kuitwa Kwa Wanafunzi Wa Kwanza

(Mathayo 4:18-22; Marko 1:16-20)

15:1 Mk 4:14; Ebr 4:12Siku moja Yesu alipokuwa amesimama karibu na Ziwa la Genesareti,5:1 Yaani Bahari ya Galilaya. watu wengi wakiwa wanasongana kumzunguka ili wapate kusikia neno la Mungu, 2akaona mashua mbili ukingoni mwa ziwa, zikiwa zimeachwa hapo na wavuvi waliokuwa wanaosha nyavu zao. 35:3 Mt 13:2Akaingia katika mojawapo ya hizo mashua ambayo ilikuwa ya Simoni, akamwomba aisogeze ndani ya maji kidogo kutoka ufuoni. Kisha akaketi na kufundisha watu akiwa mle ndani ya mashua.

45:4 Yn 21:6Alipomaliza kunena, akamwambia Simoni, “Sasa peleka mashua hadi kilindini kisha mshushe nyavu zenu mkavue samaki.”

55:5 Lk 9:33, 49; 17:13; Yn 21:3Simoni akamjibu, “Bwana, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha na hatukuvua chochote. Lakini, kwa neno lako nitazishusha nyavu.”

65:6 Yn 21:11Nao walipozishusha nyavu zao, wakavua samaki wengi sana, nyavu zao zikajaa zikaanza kukatika. 7Wakawaashiria wavuvi wenzao kwenye ile mashua nyingine ili waje kuwasaidia. Wakaja, wakajaza mashua zote mbili samaki hata zikaanza kuzama.

85:8 Mwa 18:27; Ay 42:6Simoni Petro alipoona haya yaliyotukia, alianguka miguuni mwa Yesu na kumwambia, “Bwana, ondoka kwangu. Mimi ni mtu mwenye dhambi!” 9Kwa kuwa yeye na wavuvi wenzake walikuwa wameshangazwa sana na wingi wa samaki waliokuwa wamepata. 105:10 Mt 14:27Vivyo hivyo wenzake Simoni, yaani Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, walishangazwa pia.

Ndipo Yesu akamwambia Simoni, “Usiogope, tangu sasa utakuwa mvuvi wa watu.” 115:11 Mt 4:11Hivyo wakasogeza mashua zao mpaka ufuoni mwa bahari, wakaacha kila kitu na kumfuata.

Yesu Amtakasa Mtu Mwenye Ukoma

(Mathayo 8:1-4; Marko 1:40-45)

125:12 Mt 8:12Ikawa siku moja Yesu alipokuwa katika mji fulani, mtu mmoja mwenye ukoma mwili mzima akamjia. Alipomwona Yesu, alianguka chini mpaka uso wake ukagusa ardhi, akamsihi akisema, “Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.”

13Yesu akanyoosha mkono wake, akamgusa yule mtu, akamwambia, “Nataka. Takasika!” Na mara ukoma wake ukatakasika.

145:14 Mt 8:4Yesu akamwagiza akisema, “Usimwambie mtu yeyote, bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani na ukatoe sadaka alizoagiza Mose kwa utakaso wako, ili kuwa ushuhuda kwao.”

155:15 Mt 9:26Lakini habari zake Yesu zikazidi sana kuenea kotekote kuliko wakati mwingine wowote. Makutano makubwa ya watu yalikuwa yakikusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. 165:16 Mt 14:23Lakini mara kwa mara Yesu alijitenga nao ili kwenda mahali pa faragha kuomba.

Yesu Amponya Mtu Mwenye Kupooza

(Mathayo 9:1-8; Marko 2:1-12)

175:17 Mt 15:1; Lk 2:46; Mk 5:30; Lk 6:19Siku moja Yesu alipokuwa akifundisha, Mafarisayo na walimu wa sheria, waliokuwa wametoka kila kijiji cha Galilaya na kutoka Uyahudi na Yerusalemu, walikuwa wameketi huko. Nao uweza wa Bwana ulikuwa juu yake kuponya wagonjwa. 185:18 Mt 9:2; Mk 2:8Wakaja watu wamembeba mgonjwa aliyepooza kwenye mkeka. Wakajaribu kumwingiza ndani ili wamweke mbele ya Yesu. 19Walipokuwa hawawezi kufanya hivyo kwa sababu ya umati wa watu, wakapanda juu ya paa, wakaondoa baadhi ya matofali, wakamteremsha yule mgonjwa kwa mkeka wake hadi katikati ya ule umati pale mbele ya Yesu.

205:20 Lk 7:48-49Yesu alipoiona imani yao, akamwambia yule mgonjwa, “Rafiki, dhambi zako zimesamehewa.”

215:21 Isa 43:25; Lk 7:49; Yn 5:12Mafarisayo na wale walimu wa sheria wakaanza kuuliza, “Ni nani mtu huyu anayesema maneno ya kukufuru? Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?”

22Yesu akijua mawazo yao akawauliza, “Kwa nini mnawaza hivyo mioyoni mwenu? 23Je, ni lipi lililo rahisi zaidi, kumwambia, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uende’? 245:24 Mt 8:20Lakini ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi…” Akamwambia yule aliyepooza, “Nakuambia, inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani kwako.” 25Mara yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama mbele yao wote, akachukua mkeka wake, akaenda zake nyumbani, huku akimtukuza Mungu. 265:26 Mt 9:8Kila mmoja akashangaa na kumtukuza Mungu. Wakajawa na hofu ya Mungu, wakasema, “Leo tumeona mambo ya ajabu.”

Yesu Amwita Lawi

(Mathayo 9:9-13; Marko 2:13-17)

275:27 Mt 4:19Baada ya haya, Yesu alitoka na kumwona mtoza ushuru mmoja jina lake Lawi akiwa amekaa forodhani, mahali pake pa kutoza ushuru. Akamwambia, “Nifuate.” 285:28 Lk 5:11; Mt 4:19Naye Lawi akaacha kila kitu, akaondoka, akamfuata.

295:29 Lk 15:1Kisha Lawi akamfanyia Yesu karamu kubwa nyumbani kwake, nao umati mkubwa wa watoza ushuru na watu wengine walikuwa wakila pamoja nao. 305:30 Mdo 23:9; Mt 9:11Lakini Mafarisayo na walimu wa sheria waliokuwa wa dhehebu lao wakawalalamikia wanafunzi wa Yesu, wakisema, “Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na ‘wenye dhambi’?”

31Yesu akawajibu, “Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa. 325:32 Yn 3:17Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.”

Yesu Aulizwa Kuhusu Kufunga

(Mathayo 9:14-17; Marko 2:18-22)

335:33 Lk 7:18; Yn 1:35; 3:25-26; Mt 14:17; Mk 2:18-22Wakamwambia Yesu, “Wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo mara kwa mara hufunga na kuomba, lakini wanafunzi wako wanaendelea kula na kunywa.”

345:34 Yn 3:29; Mt 14:17; Mk 2:18-22Yesu akawajibu, “Je, mnaweza kuwafanya wageni wa bwana arusi kufunga wakati yuko pamoja nao? 355:35 Lk 9:22; 7:22; Mt 14:17; Mk 2:18-22Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao. Hapo ndipo watakapofunga.”

365:36 Mt 14:17; Mk 2:18-22; Mt 9:16, 17; Mk 2:21, 22Yesu akawapa mfano huu, akawaambia: “Hakuna mtu achanaye kiraka kutoka kwenye nguo mpya na kukishonea kwenye nguo iliyochakaa. Akifanya hivyo, atakuwa amechana nguo mpya, na kile kiraka hakitalingana na ile nguo iliyochakaa. 375:37 Mt 14:17; Mk 2:18-22Hakuna mtu awekaye divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Akifanya hivyo, hiyo divai mpya itavipasua hivyo viriba, nayo yote itamwagika. 385:38 Mt 14:17; Mk 2:18-22Divai mpya lazima iwekwe kwenye viriba vipya. 395:39 Mt 14:17; Mk 2:18-22Wala hakuna mtu anayependelea divai mpya baada ya kunywa divai ya zamani, bali husema, ‘Ile ya zamani ni nzuri zaidi.’ ”