诗篇 62 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

诗篇 62:1-12

第 62 篇

唯上帝是拯救

大卫作的训诲诗,交给乐长,照耶杜顿的做法。

1我的心默默等候上帝,

祂是我的拯救者。

2唯有祂才是我的磐石,

我的拯救,我的堡垒,

我必不致动摇。

3我就像一面摇摇欲坠的墙壁、行将倒塌的篱笆,

你们要攻击我、置我于死地到何时呢?

4你们千方百计把我从高位拉下。

你们善于说谎,嘴上祝福,

心却咒诅。(细拉)

5我的心啊!要默默等候上帝,

因为我的盼望从祂而来。

6唯有祂才是我的磐石,

我的拯救,我的堡垒,

我必不致动摇。

7上帝是我的拯救者,

是我的荣耀,

祂是我的坚固磐石,

是我的避难所。

8众百姓啊,

要时刻信靠上帝,

向祂倾心吐意,

因为祂是我们的避难所。(细拉)

9卑贱人不过是一丝气息,

尊贵人不过是一场幻影,

把他们放在天平上一秤,

比空气还轻,毫无分量。

10不要敲诈勒索,

不要妄想靠偷盗发财,

即使财富增多,也不要倚靠它。

11上帝再三告诉我:

祂拥有权能,

12充满慈爱。

主啊,你必照各人的行为来施行赏罚。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 62:1-12

Zaburi 62

Mungu Kimbilio La Pekee

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi.

162:1 Za 5:3Kwa Mungu peke yake nafsi yangu inapata pumziko;

wokovu wangu watoka kwake.

262:2 Kut 15:2; Za 18:31; 89:26; 59:9; Ay 29:18Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu;

yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe.

362:3 Isa 30:13Mtamshambulia mtu hata lini?

Je, ninyi nyote mtamtupa chini,

ukuta huu ulioinama na uzio huu unaotikisika?

462:4 Za 28:3; 55:21Walikusudia kikamilifu kumwangusha

toka mahali pake pa fahari;

wanafurahia uongo.

Kwa vinywa vyao hubariki,

lakini ndani ya mioyo yao hulaani.

562:5 Mik 7:7, 10; Za 62:1Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake,

tumaini langu latoka kwake.

6Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu;

ndiye ngome yangu, sitatikisika.

762:7 Za 61:3Wokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu,

ndiye mwamba wangu wenye nguvu

na kimbilio langu.

862:8 Isa 26:4; 1Sam 1:15; Za 37:5; 42:4; Mt 26:36-46Enyi watu, mtumainini yeye wakati wote,

miminieni mioyo yenu kwake,

kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu.

962:9 Za 49:2; Ay 7:7; Isa 40:15Binadamu wa ngazi ya chini ni pumzi tu,

nao wa ngazi ya juu ni uongo tu;

wakipimwa kwenye mizani, si chochote;

wote kwa pamoja ni pumzi tu.

1062:10 Za 12:5; Isa 61:8; 26:4; 1Tim 6:17; Eze 22:29; Nah 3:1; Lk 12:15; Ay 31:25; Mt 19:23, 24; 1Tim 6:6-10; Mk 10:23Usitumainie vya udhalimu

wala usijivune kwa vitu vya wizi;

ingawa utajiri wako utaongezeka,

usiviwekee moyo wako.

1162:11 1Nya 29:11; Ufu 19:1Jambo moja Mungu amelisema,

mambo mawili nimeyasikia:

kwamba, Ee Mungu,

wewe una nguvu,

1262:12 Za 130:7; 103:8; 86:5; 28:4; Ay 21:31; Mt 16:27; Rum 2:6; 1Kor 3:8; Kol 3:25; 1Pet 1:17na kwamba, Ee Bwana,

wewe ni mwenye upendo.

Hakika utampa kila mtu thawabu

kwa kadiri ya alivyotenda.