耶利米书 40 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

耶利米书 40:1-16

基大利恩待耶利米

1耶利米带着锁链跟耶路撒冷犹大被掳的人一起被带往巴比伦,但护卫长尼布撒拉旦拉玛释放了他。这事之后,耶和华的话传给了耶利米2护卫长释放耶利米之前对他说:“你的上帝耶和华曾说要在这里降下灾祸, 3现在果然应验了。你们遭灾是因为你们得罪了耶和华,不听祂的话。 4现在我解除你手上的锁链,释放你。你可以跟我去巴比伦,我必善待你;如果你不想去,也可以。你看,整片土地都在你眼前,你想去哪里都可以。 5巴比伦王委任沙番的孙子、亚希甘的儿子基大利管理犹大的城邑,如果你想留下来,可以去他那里住在同胞中,或去其他你喜欢的地方。”于是,护卫长给耶利米干粮和礼物,放他离去。 6耶利米就到米斯巴基大利那里,居住在留下来的人当中。

基大利管理犹大

7躲在乡村的犹大将领和士兵听说巴比伦王委任亚希甘的儿子基大利管理犹大的穷人,就是没有被掳到巴比伦的男女妇孺, 8便来到米斯巴基大利。他们是尼探雅的儿子以实玛利加利亚的儿子约哈难约拿单单户篾的儿子西莱雅尼陀法以斐的儿子们、玛迦耶撒尼亚及他们的属下。 9沙番的孙子、亚希甘的儿子基大利对他们起誓说:“你们不要怕臣服于迦勒底人,只管住在这里做巴比伦王的臣民,你们会平安无事。 10至于我,我要留在米斯巴,代表你们与迦勒底人会面。你们要储备酒、夏天的果子和油,存放在器皿内,在你们所住的城邑生活。” 11摩押亚扪以东及各国的犹大人听说巴比伦王留下一些人,并委任沙番的孙子、亚希甘的儿子基大利管理他们, 12便从各地回到犹大,去米斯巴基大利。他们储备了大量的酒和夏天的果子。

13加利亚的儿子约哈难和在乡村的众将领来到米斯巴基大利14对他说:“亚扪巴利斯尼探雅的儿子以实玛利来杀你,你知道吗?”亚希甘的儿子基大利却不相信他们的话。 15后来,加利亚的儿子约哈难米斯巴私下对基大利说:“让我去杀掉尼探雅的儿子以实玛利吧!没人会知道。何必让他来杀害你,以致汇集到你这里的犹大余民再度分散、灭亡呢?” 16亚希甘的儿子基大利说:“你不可杀他,你说他要杀我这件事不是真的。”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 40:1-16

Yeremia Aachiwa Huru

140:1 Yer 39:14; Mt 2:18; Yos 18:25; Nah 3:10; 1Sam 8:4Neno likamjia Yeremia kutoka kwa Bwana baada ya Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme kumfungua huko Rama. Alikuwa amemkuta Yeremia akiwa amefungwa kwa minyororo miongoni mwa mateka wote kutoka Yerusalemu na Yuda waliokuwa wakipelekwa uhamishoni Babeli. 240:2 Yos 23:15; Yer 50:7; Mao 2:17; Rum 13:4; Isa 10:22; 2Nya 34:24; Za 18:18; Gal 6:7-8Kiongozi wa walinzi alipomwona Yeremia, akamwambia, “Bwana Mungu wako aliamuru maafa haya kwa mahali hapa. 340:3 Mit 13:21; Yak 1:15; Law 26:33; Mdo 7:39; Rum 6:23; Kum 29:24-28; Dan 9:14; Rum 2:5-9Sasa Bwana ameyaleta haya, amefanya sawasawa na vile alivyosema angefanya. Yote haya yametokea kwa sababu ninyi mlifanya dhambi dhidi ya Bwana na hamkumtii. 440:4 Mwa 13:9; Yer 39:11-12; Mwa 20:15; Za 105:18-20; Yer 37:14; Mao 3:7Lakini leo ninakufungua minyororo iliyo kwenye viwiko vya mikono yako. Twende pamoja mpaka Babeli ikiwa unataka, nami nitakutunza. Lakini kama hutaki, basi usije. Tazama, nchi yote iko mbele yako, nenda kokote unakotaka.” 540:5 2Fal 25:22; Yer 39:14; Yos 15:18; Mit 15:16; 2Fal 22:12-14; Neh 5:14; Zek 1:12Lakini kabla Yeremia hajageuka kuondoka, Nebuzaradani akaongeza kusema, “Rudi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemchagua awe juu ya miji ya Yuda, ukaishi naye miongoni mwa watu, au uende popote panapokupendeza.”

Kisha huyo kiongozi akampa posho yake na zawadi, akamwacha aende zake. 640:6 Amu 20:1; 1Sam 7:5-17Kwa hiyo Yeremia akaenda kwa Gedalia mwana wa Ahikamu huko Mispa, na kuishi naye miongoni mwa watu walioachwa katika nchi.

Gedalia Auawa

(2 Wafalme 25:22-26)

740:7 Yer 39:10; Mdo 24:17; Mwa 41:41; Neh 5:14; Yak 2:5; 2Fal 24:14Maafisa wote wa jeshi na watu wao waliokuwa bado wapo kwenye eneo la wazi waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemteua Gedalia mwana wa Ahikamu kuwa mtawala wa nchi, na amemweka kuwa kiongozi wa wanaume, wanawake na watoto waliokuwa maskini zaidi katika nchi ambao hawakuchukuliwa kwenda uhamishoni Babeli, 840:8 Yer 41:1-2; 2Sam 23:28; Kum 3:14wakamjia Gedalia huko Mispa. Hawa walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani na Yonathani wana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi, wana wa Efai Mnetofathi, na Yezania mwana wa Mmaaka, pamoja na watu wao. 940:9 Yer 5:19; Efe 6:5-8; Yer 38:20; Rum 13:1-2; Eze 23:23Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani akaapa ili kuwatia moyo wao na watu wao. Akasema: “Msiogope kuwatumikia Wakaldayo. Kaeni katika nchi na kumtumikia mfalme wa Babeli, na itakuwa vyema kwenu. 1040:10 Kum 1:39; 16:13; Mwa 27:28; Kut 7:19; 23:16; 2Kor 4:7Mimi mwenyewe nitakaa Mispa ili kuwawakilisha mbele ya Wakaldayo wanaotujia, lakini ninyi mtavuna divai, matunda ya kiangazi na mafuta, nanyi mtaweka katika vyombo vyenu vya kuhifadhia, na kuishi katika miji mliyojitwalia.”

1140:11 Hes 21:11; 25:1; Isa 16:4; Mao 1:14; Yer 24:9; Mwa 25:30; Yer 12:14Wayahudi wote waliokuwa Moabu, Amoni, Edomu na nchi nyingine zote waliposikia kwamba mfalme wa Babeli ameacha mabaki ya watu katika Yuda na amemweka Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani kuwa mtawala wao, 1240:12 Yer 43:5wakarudi wote katika nchi ya Yuda kwa Gedalia huko Mispa, kutoka nchi zote ambazo walikuwa wametawanywa. Nao wakavuna divai na matunda tele wakati wa kiangazi.

13Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wote wa jeshi waliokuwa bado wapo kwenye eneo la wazi wakamjia Gedalia huko Mispa 1440:14 Mwa 19:38; 2Sam 10:1-19; Amo 1:13; Yer 41:10; 25:21; 49:1na kumwambia, “Je, hujui kwamba Baalisi mfalme wa Waamoni amemtuma Ishmaeli mwana wa Nethania akuue?” Lakini Gedalia mwana wa Ahikamu hakuwaamini.

1540:15 Kum 5:17; Mt 5:21-22; Mwa 11:4; Mt 26:31; Yn 11:52; Rum 11:5; 2Fal 21:15Kisha Yohanani mwana wa Karea akamwambia Gedalia kwa siri huko Mispa, “Acha niende nikamuue Ishmaeli mwana wa Nethania, wala hakuna atakayejua. Kwa nini akuue na kusababisha Wayahudi wote waliokuzunguka watawanyike, na mabaki wa Yuda waangamie?”

1640:16 Yer 43:2Lakini Gedalia mwana wa Ahikamu akamwambia Yohanani mwana wa Karea, “Usifanye jambo kama hilo! Unalosema kuhusu Ishmaeli si kweli.”