罗马书 14 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

罗马书 14:1-23

体恤弱者

1你们要接纳信心软弱的弟兄姊妹,不要因为看法不同便彼此批评。 2有人相信什么都可以吃,但信心软弱的人只吃素菜。 3吃的人不可轻看不吃的人,不吃的人也不可批评吃的人,因为两者都蒙上帝接纳。 4你是谁,竟然批评别人的仆人?他做得是否合宜,自然有他的主人负责。他必能做得合宜,因为主能使他做得合宜。

5有人认为这日比那日好,有人认为天天都一样,各人应该照着自己的信念拿定主意。 6守日子的人是为主而守,吃的人是为主而吃,因为他感谢上帝;不吃的人是为主不吃,他也同样感谢上帝。 7因为我们没有人为自己活,也没有人为自己死。 8我们活是为主而活,死是为主而死。因此,我们无论生死都是属主的人。 9正是为这个缘故,基督死了,又复活了,好做死人和活人的主。

10那么,你为什么论断弟兄姊妹呢?为什么轻视弟兄姊妹呢?将来我们都要一同站在上帝的审判台前。 11圣经上说:“主说,‘我凭我的永恒起誓,万膝必向我跪拜,万口必称颂上帝。’” 12这样看来,我们各人都要在上帝面前陈明自己一切的事。

不要使人犯罪

13所以,我们不可再互相论断,要留心自己的言行,不要绊倒弟兄姊妹。 14我知道并靠着主耶稣深信,没有什么是不洁净的,但若有人以为某物不洁净,那物对他来说就不洁净。 15如果你吃的东西令弟兄姊妹不安,你就不是凭爱心行事。你不可因为一点食物而损害基督舍命救赎的人。 16所以,不要让你们认为好的事被别人诟病。 17因为上帝的国不是关乎吃什么喝什么,而是关乎公义、平安和圣灵所赐的喜乐。 18以这样的态度事奉基督的人才会得到上帝的喜悦和大家的称赞。

19所以,我们要努力追求和睦,彼此造就。 20不可因食物的问题而破坏上帝的工作。所有的食物固然都是洁净的,但人若因所吃的食物绊倒别人,就有罪了。 21无论是吃肉、喝酒还是做任何别的事,如果会绊倒别人,就应该一概不做。 22你有信心认为可以做的,只要你和上帝知道就可以了。人如果在自己认为可以做的事上问心无愧,就有福了。 23人如果心里疑惑,却仍然吃,就有罪了,因为他不是凭信心吃。凡不凭信心去做的,就是犯罪。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Warumi 14:1-23

Msiwahukumu Wengine

114:1 1Kor 8:9-12; 9:22Mkaribisheni yeye ambaye imani yake ni dhaifu, lakini si kwa kugombana na kubishana juu ya mawazo yake. 214:2 Rum 14:14; 1Kor 10:25; 1Tim 4:4; Tit 1:15Mtu mmoja imani yake inamruhusu kula kila kitu, lakini mwingine ambaye imani yake ni dhaifu, hula mboga tu. 314:3 Lk 18:9; Kol 2:16Yeye alaye kila kitu asimdharau yeye asiyekula. Wala yeye asiyekula kila kitu asimhukumu yule alaye kila kitu, kwa maana Mungu amemkubali. 414:4 Mt 7:1; Yak 4:12Wewe ni nani hata umhukumu mtumishi wa mtu mwingine? Kwa bwana wake tu anasimama au kuanguka. Naye atasimama kwa sababu Bwana anaweza kumsimamisha.

514:5 Gal 4:10; Kol 2:16Mtu mmoja anaitukuza siku fulani kuwa ni bora kuliko nyingine, na mwingine anaona kuwa siku zote ni sawa. Basi kila mmoja awe na hakika na yale anayoamini. 614:6 Mt 14:19; 1Tim 4:3, 4Yeye anayehesabu siku moja kuwa takatifu kuliko nyingine, hufanya hivyo kwa kumheshimu Bwana. Naye alaye nyama hula kwa Bwana, kwa maana humshukuru Mungu, naye akataaye kula nyama hufanya hivyo kwa Bwana na humshukuru Mungu. 714:7 2Kor 5:15; Gal 2:20Kwa kuwa hakuna hata mmoja wetu anayeishi kwa ajili yake mwenyewe, wala hakuna hata mmoja wetu afaye kwa ajili yake mwenyewe. 814:8 Flp 1:20; Gal 2:20; 1The 5:10; Lk 20:38Kama tunaishi, tunaishi kwa Bwana, nasi pia tukifa tunakufa kwa Bwana. Kwa hiyo basi, kama tukiishi au kama tukifa, sisi ni mali ya Bwana.

914:9 Ufu 1:18; 2:8; Mdo 10:42; 2Kor 5:15Kwani kwa sababu hii hasa, Kristo alikufa na akawa hai tena kusudi apate kuwa Bwana wa wote, yaani, waliokufa na walio hai. 1014:10 2Kor 5:10; Mdo 17:31; Mt 25:31, 32; 7:1; 2Kor 5:10Basi kwa nini wewe wamhukumu ndugu yako? Au kwa nini wewe unamdharau ndugu yako? Kwa kuwa sote tutasimama mbele ya kiti cha Mungu cha hukumu. 1114:11 Isa 45:23; Flp 2:10, 11Kwa kuwa imeandikwa:

“ ‘Kama vile niishivyo,’ asema Bwana,

‘kila goti litapigwa mbele zangu,

na kila ulimi utakiri kwa Mungu.’ ”

1214:12 Mt 12:36; 1Pet 4:5Hivyo basi kila mmoja wetu atatoa habari zake mwenyewe kwa Mungu.

Usimfanye Ndugu Yako Ajikwae

1314:13 Mt 7:1; Rum 14:1; 2Kor 8:9, 13Kwa hiyo tusiendelee kuhukumiana: Badala yake mtu asiweke kamwe kikwazo au kizuizi katika njia ya ndugu mwingine. 1414:14 Mdo 10:15; 1Kor 8:7Ninajua tena nimehakikishiwa sana katika Bwana Yesu kwamba hakuna kitu chochote ambacho ni najisi kwa asili yake. Lakini kama mtu anakiona kitu kuwa ni najisi, basi kwake huyo kitu hicho ni najisi. 1514:15 Efe 5:2; 1Kor 8:7Kama ndugu yako anahuzunishwa kwa sababu ya kile unachokula, basi huenendi tena katika upendo. Usiruhusu kile unachokula kiwe sababu ya kumwangamiza ndugu yako ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. 1614:16 1Kor 10:30; Tit 2:5; Rum 12:17Usiruhusu kile ambacho unakiona kuwa chema kisemwe kuwa ni kiovu. 1714:17 1Kor 8:8; Gal 5:22Kwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu. 1814:18 Lk 2:52; Mdo 24:16Kwa sababu mtu yeyote anayemtumikia Kristo kwa jinsi hii, anampendeza Mungu na kukubaliwa na wanadamu.

1914:19 Za 34:14; 1Kor 7:15; Rum 15:2; Efe 4:12, 29Kwa hiyo na tufanye bidii kutafuta yale yaletayo amani na kujengana sisi kwa sisi. 2014:20 Rum 14:15; Mt 15:11; Mdo 10:15; Tit 1:15Usiiharibu kazi ya Mungu kwa ajili ya chakula. Hakika vyakula vyote ni safi, lakini ni kosa kula kitu chochote kinachomsababisha ndugu yako ajikwae. 2114:21 1Kor 8:13; Mt 15:29Ni afadhali kutokula nyama wala kunywa divai au kufanya jambo lingine lolote litakalomsababisha ndugu yako ajikwae.

2214:22 1Yn 3:21; Mt 15:29Je, wewe unayo imani? Ile imani uliyo nayo, uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiye na sababu ya kujihukumu nafsi yake kwa ajili ya kile anachokifanya. 23Lakini kama mtu ana shaka kuhusu kile anachokula, amehukumiwa, kwa sababu hakula kwa imani. Kwa kuwa chochote kinachofanywa pasipo imani ni dhambi.