约拿书 4 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

约拿书 4:1-11

1这事令约拿十分不悦,非常恼怒。 2他向耶和华祷告说:“耶和华啊,我在家乡的时候岂不早就说过你会这样做吗?我知道你是一位有恩典、有怜悯的上帝,不轻易发怒,充满慈爱,不忍心降灾,所以我才急速逃往他施3耶和华啊,求你收回我的性命吧,我死了比活着还好!” 4耶和华对他说:“你这样大发脾气合理吗?”

5于是,约拿跑到城外,在城东为自己搭了一个棚,坐在棚下荫凉处,要看看尼尼微城究竟会怎样。 6后来,耶和华上帝安排了一棵蓖麻迅速地长起来,为约拿遮荫,使他的头免受日晒。约拿因有这棵蓖麻而非常欢喜。 7第二天黎明的时候,上帝却安排了一条虫来咬这棵蓖麻,蓖麻就枯萎了。 8太阳出来的时候,上帝刮起燥热的东风,烈日把约拿晒得发昏,他就再次求死说:“我死了比活着还好!”

9上帝对约拿说:“你为这棵蓖麻大发脾气合理吗?”约拿回答说:“我就是气死了也合理。” 10耶和华说:“这棵蓖麻不是你种的,也不是你栽培的,它在一夜之间长成,又在一夜之间死去,你尚且如此爱惜, 11我怎能不爱惜这尼尼微大城呢?城中单是连左右手都分不清的人就有十二万多,还有许多的牲畜。”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yona 4:1-11

Hasira Ya Yona Kwa Ajili Ya Huruma Ya Bwana.

14:1 Mt 20:11; 20:15; Lk 15:28Lakini Yona alichukizwa sana akakasirika. 24:2 Yer 20:7-8; Kum 4:31; Za 103:8; Kut 34:6; 22:27; Hes 14:18; Yoe 2:13Akamwomba Bwana, “Ee Bwana, hili si lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii ndiyo sababu niliharikisha kukimbilia Tarshishi. Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa. 34:3 Hes 11:15; Ay 7:15; Yer 8:3; 1Fal 19:4Sasa, Ee Bwana, niondolee uhai wangu, kwa kuwa ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”

44:4 Mwa 4:6; Mt 20:11-15Lakini Bwana akamjibu, “Je unayo haki yoyote kukasirika?”

5Yona akatoka nje akaketi mahali upande wa mashariki wa mji. Hapo akajitengenezea kibanda, akaketi kwenye kivuli chake na kungojea ni nini kitakachotokea katika mji. 64:6 Yon 1:17Ndipo Bwana, Mungu akaweka tayari mzabibu na kuufanya uote, kumpa Yona kivuli kilichomfunika kichwa ili kuondoa taabu yake, naye Yona akafurahi sana kwa ajili ya ule mzabibu. 74:7 Yoe 1:12Lakini kesho yake asubuhi na mapema Mungu akaamuru buu, autafune mzabibu huo nao ukanyauka. 84:8 Za 121:6; 1Fal 19:4Wakati jua lilipochomoza, Mungu akautuma upepo wa hari wa mashariki, nalo jua likawaka juu ya kichwa cha Yona mpaka akazimia. Akatamani kufa, naye akasema, “Ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”

9Lakini Mungu alimwambia Yona, “Je, unayo haki kukasirika kuhusu mzabibu huo?”

Akasema, “Ndiyo, ninayo haki. Nimekasirika kiasi cha kufa.”

10Lakini Bwana akamwambia, “Wewe unakasirika kwa ajili ya mzabibu huu, nawe hukuusababisha kuota wala kuutunza. Uliota usiku mmoja, nao ukafa usiku mmoja. 114:11 Eze 33:11; Kum 1:39; Za 36:6; Yon 1:2; 3:2; 3:1Lakini Ninawi ina zaidi ya watu 120,000 ambao hawawezi kupambanua kulia au kushoto, pamoja na ngʼombe wengi. Je, hainipasi kufikiri juu ya mji ule mkubwa?”