民数记 33 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

民数记 33:1-56

从埃及到约旦河

1以下是以色列人在摩西亚伦的领导下离开埃及列队行军的路线。 2摩西遵照耶和华的吩咐记录启行的地点,以下是他们停留过的地方。

3一月十五日,即逾越节的第二天,埃及人眼睁睁地看着以色列人昂首挺胸地离开了兰塞4当时埃及人正埋葬他们的长子,耶和华击杀了他们的长子,并借此惩罚了他们的众神明。 5以色列人从兰塞启行,至疏割扎营; 6疏割启行,至旷野边界的以倘扎营; 7以倘启行,又折回巴力·洗分对面的比哈·希录,在密夺附近扎营; 8比哈·希录启行,经过红海到书珥旷野,在伊坦旷野走了三天,至玛拉扎营; 9玛拉启行,至以琳扎营,那里有十二股水泉和七十棵棕树; 10以琳启行,至红海岸边扎营; 11从红海启行,至旷野扎营; 12旷野启行,至脱加扎营; 13脱加启行,至亚录扎营; 14亚录启行,至利非订扎营,在那里民众没有水喝; 15利非订启行,至西奈旷野扎营; 16西奈旷野启行,至基博罗·哈他瓦扎营; 17基博罗·哈他瓦启行,至哈洗录扎营; 18哈洗录启行,至利提玛扎营; 19利提玛启行,至临门·帕烈扎营; 20临门·帕烈启行,至立拿扎营; 21立拿启行,至勒撒扎营; 22勒撒启行,至基希拉他扎营; 23基希拉他启行,至沙斐山扎营; 24沙斐山启行,至哈拉大扎营; 25哈拉大启行,至玛吉希录扎营; 26玛吉希录启行,至他哈扎营; 27他哈启行,至他拉扎营; 28他拉启行,至密加扎营; 29密加启行,至哈摩拿扎营; 30哈摩拿启行,至摩西录扎营; 31摩西录启行,至比尼·亚干扎营; 32比尼·亚干启行,至曷·哈吉甲扎营; 33曷·哈吉甲启行,至约巴他扎营; 34约巴他启行,至阿博拿扎营; 35阿博拿启行,至以旬·迦别扎营; 36以旬·迦别启行,至旷野的加低斯扎营; 37加低斯启行,至以东边界的何珥山扎营。

38以色列人离开埃及后的第四十年五月一日,亚伦祭司遵照耶和华的吩咐上了何珥山,并在那里离世, 39享年一百二十三岁。

40在南地的迦南亚拉得王得知了以色列人要来的消息。

41以色列人从何珥山启行,至撒摩拿扎营; 42撒摩拿启行,至普嫩扎营; 43普嫩启行,至阿伯扎营; 44阿伯启行,至摩押边境的以耶·亚巴琳扎营; 45以耶·亚巴琳启行,至底本·迦得扎营; 46底本·迦得启行,至亚门·低比拉太音扎营; 47亚门·低比拉太音启行,至尼波对面的亚巴琳山扎营; 48亚巴琳山启行,至耶利哥对面、约旦河边的摩押平原扎营。 49他们沿着约旦河在摩押平原扎营,营地从伯·耶施末一直延伸到亚伯·什亭

50耶和华在耶利哥对面、约旦河边的摩押平原对摩西说: 51“你告诉以色列人,‘你们过约旦河进了迦南以后, 52一定要赶走当地的居民,毁掉他们一切的石像和铸像,拆毁他们所有的丘坛。 53你们要占领那片土地,住在那里,因为我已经把那里赐给你们作产业了。 54你们要按宗族家系抽签分配土地,人口多的多分,人口少的少分,抽到哪块地就得哪块地。 55如果你们不赶走那里的居民,留下来的人必成为你们眼里的刺和肋旁的荆棘,在你们所居之地搅扰你们, 56我也会用预备对付他们的方法来对付你们。’”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hesabu 33:1-56

Vituo Katika Safari Ya Waisraeli

133:1 Kut 17:1; 40:36; Hes 1:1; Kut 4:16; 6:26Hivi ndivyo vituo katika safari ya Waisraeli walipotoka Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Mose na Aroni. 233:2 Kut 17:4Kwa agizo la Bwana, Mose aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao:

333:3 Hes 10:2; Mwa 47:11; Yos 5:10; Kut 14:8; 1:11; 12:37; 12:2; 13:4; Za 105:38; Isa 52:12; Kut 14:8Waisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote, 433:4 Kut 4:23; 2Nya 24:24; Yer 15:3; Eze 14:21; Kut 12:12; Isa 19:1; Sef 2:11; Ufu 12:8waliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao Bwana alikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwa Bwana alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao.

533:5 Kut 12:37Waisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi.

633:6 Kut 13:20; Mwa 33:17; Yos 13:27; Za 60:6Wakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa.

733:7 Kut 13:17, 18; 14:2, 9Wakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki ya Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli.

833:8 Kut 14:2; 14:22; 15:23Wakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari mpaka jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara.

933:9 Kut 15:27Wakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi.

1033:10 Kut 16:1Wakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu.

1133:11 Kut 16:1; 17:1Wakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini.

12Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka.

13Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi.

1433:14 Kut 15:22; 17:2Wakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji kwa ajili ya watu kunywa.

1533:15 Kut 17:1; 19:1Wakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika Jangwa la Sinai.

1633:16 Hes 11:34Wakaondoka katika Jangwa la Sinai na kupiga kambi huko Kibroth-Hataava.

1733:17 Hes 11; 35; Kum 9:22Wakaondoka Kibroth-Hataava na kupiga kambi huko Haserothi.

1833:18 Hes 12:16; Kum 1:1Wakaondoka Haserothi na kupiga kambi huko Rithma.

19Wakaondoka Rithma na kupiga kambi huko Rimon-Peresi.

2033:20 Yos 10:29; 12:15; 15:42; 21:13; 2Fal 8:22; 19:8; 23:31; 1Nya 6:57; 2Nya 21:10; Isa 37:8; Yer 52:1Wakaondoka Rimon-Peresi na kupiga kambi huko Libna.

21Wakaondoka Libna na kupiga kambi huko Risa.

22Wakaondoka Risa na kupiga kambi huko Kehelatha.

23Wakaondoka Kehelatha na kupiga kambi kwenye mlima Sheferi.

24Wakaondoka kwenye mlima Sheferi na kupiga kambi huko Harada.

25Wakaondoka Harada na kupiga kambi huko Makelothi.

26Wakaondoka Makelothi na kupiga kambi huko Tahathi.

27Wakaondoka Tahathi na kupiga kambi huko Tera.

28Wakaondoka Tera na kupiga kambi huko Mithka.

29Wakaondoka Mithka na kupiga kambi huko Hashmona.

3033:30 Kum 10:6Wakaondoka Hashmona na kupiga kambi Moserothi.

3133:31 Kum 10:6Wakaondoka Moserothi na kupiga kambi huko Bene-Yakani.

3233:32 Mwa 36:27; Kum 10:6; 1Nya 1:42Wakaondoka Bene-Yakani na kupiga kambi huko Hor-Hagidgadi.

3333:33 Kum 10:7Wakaondoka Hor-Hagidgadi na kupiga kambi huko Yotbatha.

34Wakaondoka Yotbatha na kupiga kambi huko Abrona.

3533:35 Kum 2:8; 1Fal 9:26; 22:48Wakaondoka Abrona na kupiga kambi huko Esion-Geberi.

3633:36 Hes 13:21; 20:1; Kum 32:51; Yos 15:1Wakaondoka Esion-Geberi na kupiga kambi huko Kadeshi katika Jangwa la Sini.

3733:37 Hes 20:22; Mwa 36:16; Hes 20:16Wakaondoka Kadeshi na kupiga kambi kwenye Mlima Hori, mpakani mwa Edomu. 3833:38 Hes 27:13; Kut 16:35; Hes 20:25-28; Kum 10:6; 32:50Kwa amri ya Bwana, kuhani Aroni alipanda Mlima Hori, mahali alipofia katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arobaini baada ya Waisraeli kutoka Misri. 39Aroni alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na umri wa miaka 123.

4033:40 Mwa 10:18; Hes 21:1; Mwa 12:9; Amu 1:16Mfalme Mkanaani wa Aradi, ambaye aliishi huko Negebu ya Kanaani, akasikia kwamba Waisraeli wanakuja.

41Wakaondoka kwenye mlima Hori na kupiga kambi huko Salmona.

42Wakaondoka Salmona, wakapiga kambi huko Punoni.

4333:43 Hes 21:10Wakaondoka Punoni, wakapiga kambi huko Obothi.

4433:44 Hes 21:11Wakaondoka Obothi, wakapiga kambi huko Iye-Abarimu, mipakani mwa Moabu.

4533:45 Hes 32:34Wakaondoka Iye-Abarimu, wakapiga kambi huko Dibon-Gadi.

4633:46 Yer 48:22; Eze 6:14Wakaondoka Dibon-Gadi na kupiga kambi huko Almon-Diblathaimu.

4733:47 Hes 27:12; 32:3; Kum 32:49Wakaondoka Almon-Diblathaimu na kupiga kambi katika milima ya Abarimu, karibu na Nebo.

4833:48 Hes 27:12; 26:3; Mwa 13:10; Hes 22:1; Yos 12:9Wakaondoka kwenye milima ya Abarimu na kupiga kambi kwenye tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko. 4933:49 Yos 12:3; 13:20; Eze 25:9; Hes 21:16Huko kwenye tambarare za Moabu walipiga kambi kandokando ya Mto Yordani, kuanzia Beth-Yeshimothi mpaka Abel-Shitimu.

5033:50 Hes 33:48; 34:2Katika tambarare za Moabu kando ya Yordani kuvukia Yeriko, Bwana akamwambia Mose, 5133:51 Kum 7:1; 9:1; Yos 3:17“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapovuka Mto Yordani kuingia Kanaani, 5233:52 Law 26:1; Za 106:34-36; Kut 23:24; 34:12-17; Kum 7:2-5, 25, 26; Yos 11:12; 23:7; Amu 2:2wafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kuyeyusha chuma, na kupabomoa mahali pao pa ibada. 5333:53 Kum 11:31; 17:14; Yos 1:11; 21:43; Za 24:1; Ay 14:11; Dan 4:35Mtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki. 5433:54 Law 16:8; Hes 36:2; 26:54; 35:8; Yos 18:10Mtaigawanya nchi hiyo kwa kupiga kura, kufuatana na koo zenu. Kwa kundi kubwa zaidi toa urithi mkubwa zaidi, na kwa kundi dogo zaidi urithi mdogo zaidi. Chochote kinachowaangukia kwa kura kitakuwa chao. Mtaigawanya nchi kufuatana na makabila ya babu zenu.

5533:55 Yos 23:13; Amu 2:3; Za 106:36; Isa 55:13; Eze 2:6; 28:24; Mik 7:4; 2Kor 12:7; Kut 23:33; Mwa 17:8; Kum 1:7; Za 78:55; 105:11“ ‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wakaao katika nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama sindano kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi. 5633:56 Hes 14:28Kisha nitawatenda ninyi kile ambacho nimepanga kuwatenda wao.’ ”