民数记 31 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

民数记 31:1-54

攻打米甸人

1耶和华对摩西说: 2“你要为以色列人向米甸人报仇,之后你将归到祖先那里。” 3于是,摩西对民众说:“你们男子要拿起兵器去攻打米甸,为耶和华报仇。 4以色列的每个支派要派一千人出战。” 5于是,他们从以色列每个支派选出一千人,武装了一万二千军兵。 6每个支派选出的一千军兵由摩西派遣出战,以利亚撒祭司的儿子非尼哈拿着圣所的器具和号角随行。 7他们照耶和华对摩西的吩咐去攻打米甸人,杀死了米甸的所有男子, 8包括以未利金苏珥户珥利巴五个王,还杀了比珥的儿子巴兰9以色列人虏获了米甸的妇女、孩子、牛羊和财物, 10将他们的城邑营寨付之一炬, 11带走了掳掠的人畜等战利品。 12他们来到耶利哥对面、约旦河边的摩押平原,把战利品交给摩西以利亚撒祭司和以色列全体会众。

13摩西以利亚撒祭司以及所有民众的首领都到营外迎接他们。 14摩西对回来的千夫长和百夫长发怒, 15说:“你们为什么让这些妇女活着? 16就是她们听了巴兰的指使在毗珥引诱以色列人背叛耶和华,以致瘟疫降在耶和华的会众身上。 17现在,你们要杀掉所有的男孩以及与男人发生过关系的女子, 18但可以留下那些处女。 19你们凡杀了人和碰过死人的都要在营外待七天。在第三天和第七天,你们要洁净自己及掳来的人, 20也要洁净自己所有的衣服、皮具、山羊毛织的物品和木器。” 21以利亚撒祭司对打仗回来的军兵说:“以下是耶和华借摩西颁布的律例。 22金、银、铜、铁、锡、铅, 23凡耐火之物都要用火来洁净,还要用除秽水加以洁净;不耐火之物要用水来洁净。 24第七天,你们洗完衣服后就洁净了,可以回营。”

25耶和华对摩西说: 26“你和以利亚撒祭司以及会众的各族长要统计俘虏和牲畜的数目, 27然后把这些战利品分成两份,一份给出征的战士,一份给会众。 28要从战士分得的俘虏、牛、驴和羊群中抽出五百分之一献给耶和华, 29要把那五百分之一交给以利亚撒祭司献给耶和华作举祭。 30要从会众分得的俘虏和牛、驴、羊等牲畜中抽出五十分之一交给在我圣幕司职的利未人。” 31摩西以利亚撒祭司遵命而行。

32战士虏获的战利品中有六十七万五千只羊, 33七万二千头牛, 34六万一千头驴, 35三万二千名处女。 36战士分得的战利品有三十三万七千五百只羊, 37其中六百七十五只献给耶和华; 38三万六千头牛,其中七十二头献给耶和华; 39三万零五百头驴,其中六十一头献给耶和华; 40一万六千名处女,其中三十二人献给耶和华。 41摩西照耶和华的吩咐,把献给耶和华的举祭交给以利亚撒祭司。

42以色列会众分得的那一半战利品,即摩西从出征之人的战利品中分出来给他们的, 43有三十三万七千五百只羊、 44三万六千头牛、 45三万零五百头驴、 46一万六千名处女。 47摩西照耶和华的吩咐,从中抽出五十分之一交给在圣幕里司职的利未人。

48统领军队的千夫长和百夫长来见摩西49说:“仆人们统计了手下出征的战士,未失一兵一卒。 50现在我们把各自虏获的臂环、镯子、图章戒指、耳环、项链等金器都带来献给耶和华,作为我们生命的赎价。” 51摩西以利亚撒祭司收了他们所献的各种金制物品。 52千夫长和百夫长献给耶和华作举祭的金子约二百公斤。 53战士则保留了自己虏获的财物。 54摩西以利亚撒祭司就把千夫长和百夫长献的金子带进会幕,在耶和华面前作以色列人的纪念。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hesabu 31:1-54

Kulipiza Kisasi Juu Ya Wamidiani

1Bwana akamwambia Mose, 231:2 Mwa 25:2; Hes 20:26; 25:17; Kum 32:35, 43; Mwa 15:15“Uwalipize kisasi Wamidiani kwa ajili ya Waisraeli. Halafu baada ya hayo, utakufa.”

331:3 Amu 11:36; 1Sam 24:12; 2Sam 4:8; 22:48; Za 94:1; 149:7; Isa 34:8; Yer 11:20; 46:10; Eze 25:17; Kum 32:35; Yer 50:28; Za 94:1; Rum 12:19; Ebr 10:30Kwa hiyo Mose akawaambia watu, “Waandaeni baadhi ya wanaume wenu waende vitani kupigana na Wamidiani ili wawalipize kisasi cha Bwana. 4Peleka wanaume 1,000 vitani kutoka kila kabila la Israeli.” 5Kwa hiyo waliandaliwa wanaume 12,000 kwa vita, wanaume 1,000 kutoka kila kabila, walitolewa kutoka koo za Israeli. 631:6 Kut 6:25; Hes 14:44; 10:2; 10:9Mose aliwatuma vitani, watu 1,000 kutoka kila kabila, pamoja na Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, ambaye alichukua vyombo vya mahali patakatifu na tarumbeta za kuashiria.

731:7 Hes 25:16; Kum 20:13; Amu 21:11; 1Fal 11:15; 1Sam 27:9; 1Fal 11:15-16; Kum 20:13; Amu 21:11; 6:2, 33; 6:1Walipigana dhidi ya Wamidiani, kama Bwana alivyomwagiza Mose, nao waliua kila mwanaume. 831:8 Yos 13:21; Hes 25:15; 22:5; 24:14; Yos 13:22; Za 9:12; Yud 11; Ufu 2:14; 19:20Miongoni mwa watu waliouawa walikuwepo wafalme watano wa Midiani, nao ni Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba. Vilevile walimuua Balaamu mwana wa Beori kwa upanga. 931:9 Mwa 34:29Waisraeli waliwateka wanawake wa Kimidiani pamoja na watoto wao na walichukua makundi ya ngʼombe, kondoo na mali zao kama nyara. 1031:10 Yos 6:24; 8:28; 11:11; Amu 18:27; Mwa 25:16; 1Nya 6:54; Za 69:25; Eze 25:4Walichoma moto miji yote ambayo Wamidiani walikuwa wanaishi, pamoja na kambi zao zote. 1131:11 Kum 20:14; 2Nya 28:8Walichukua nyara zote na mateka, pamoja na watu na wanyama, 1231:12 Mwa 49:27; Kut 15:9; Hes 27:2nao waliwaleta wafungwa mateka na nyara kwa Mose na kwa kuhani Eleazari, nao Waisraeli walikusanyika kwenye kambi zao katika tambarare za nchi ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko.

13Mose, kuhani Eleazari na viongozi wote wa jumuiya wakatoka kuwalaki nje ya kambi. 1431:14 Kut 18:21; Kum 1:15; 2Sam 18:1Mose aliwakasirikia maafisa wa jeshi, yaani hao wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, ambao walirudi kutoka vitani.

1531:15 Kum 2:34; 20:13; Yos 6:21; 8:25; 1Sam 15:3; Yos 10:40; 11:14Mose akawauliza, “Je, mmewaacha wanawake wote hai?” 1631:16 Hes 22:5; 24:14; 2Pet 2:15; Hes 23:25; 25:1-9; 14:37; Yos 22:17; Za 106:28-29; Hos 9:10; Mik 6:5; Ufu 2:14“Wanawake hao ndio waliofuata ushauri wa Balaamu, nao ndio waliowasababisha Waisraeli wamwasi Bwana kwa kile kilichotokea kule Peori, na kwa hiyo pigo liliwapata watu wa Bwana. 1731:17 Kum 7:2; 20:16; Amu 21:11Sasa waue wavulana wote. Pia muue kila mwanamke ambaye alikwisha fanya tendo la ndoa, 18lakini mwacheni hai kwa ajili yenu kila msichana ambaye kamwe hajawahi kuzini na mwanaume.

1931:19 Hes 5:2; 9:6, 10; 19:11, 12, 16; Law 21:1“Ninyi nyote ambao mmeua mtu yeyote au kumgusa mtu yeyote ambaye ameuawa, lazima mkae nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Katika siku ya tatu na ya saba lazima mjitakase wenyewe pamoja na wafungwa wenu. 2031:20 Hes 19:19; Law 11:32Takaseni kila vazi pamoja na kila kitu kilichotengenezwa kwa ngozi, kwa singa za mbuzi au kwa mti.”

21Kisha kuhani Eleazari aliwaambia askari waliokuwa wamekwenda vitani, “Haya ndiyo matakwa ya sheria ambayo Bwana alimpa Mose: 2231:22 Yos 6:19; 22:8Dhahabu, fedha, shaba, chuma, bati, risasi, 2331:23 1Kor 3:13; Hes 8:7; 19:9, 17na kitu kingine chochote ambacho kinaweza kuhimili moto lazima mkipitishe kwenye moto, kisha kitakuwa safi. Lakini ni lazima pia kitakaswe kwa maji ya utakaso. Kitu chochote kisichoweza kuhimili moto lazima kipitishwe kwenye yale maji ya utakaso. 2431:24 Law 11:25; 14:8; Hes 19:10, 22; Za 51:2; Efe 5:26; Ebr 9:9-10Katika siku ya saba fueni nguo zenu, nanyi mtakuwa safi. Kisha mtaweza kuingia kambini.”

Kugawanya Mateka

25Bwana akamwambia Mose, 2631:26 Hes 1:4; 1:19“Wewe na kuhani Eleazari pamoja na viongozi wa jamaa ya jumuiya mtahesabu watu wote na wanyama ambao walitekwa. 2731:27 Yos 22:8; 1Sam 25:13; 30:24; Za 68:12Gawanyeni hizo nyara kati ya askari ambao walishiriki katika vita na kwa jumuiya. 2831:28 Hes 18:21; 2Sam 8:11; 1Nya 8:11; 26:27; Isa 18:7; 23:18; Mt 22:21Kutoka fungu la wale waliokwenda kupigana vitani, tenga kama ushuru kwa ajili ya Bwana kitu kimoja kati ya kila mia tano, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo au mbuzi. 29Chukua ushuru huu kutoka fungu lao, umpe kuhani Eleazari kama sehemu ya Bwana. 3031:30 Hes 3:7; 16:3Kutoka fungu la Waisraeli, chukua kitu kimoja kati ya kila hamsini, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo, mbuzi au wanyama wengine. Hivyo uwape Walawi, ambao wanawajibika kutunza Maskani ya Bwana.” 31Kwa hiyo Mose na kuhani Eleazari wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Mose.

32Nyara zilizobaki kutoka mateka ambayo askari walichukua ni kondoo 675,000, 33ngʼombe 72,000, 34punda 61,000, 35na wanawake 32,000 ambao hawakumjua mume kwa kufanya tendo la ndoa.

36Nusu ya fungu la wale waliokwenda kupigana vitani lilikuwa:

Kondoo 337,500 3731:37 Law 25:23; Kum 10:14; Za 50:12; Mk 12:17; Lk 20:25; 1Kor 10:26ambayo ushuru kwa ajili ya Bwana ilikuwa kondoo 675;

38ngʼombe 36,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa ngʼombe 72;

39punda 30,500 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa punda 61;

40Watu 16,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa watu 32.

4131:41 Hes 5:9; 18:8, 19Mose alimpa kuhani Eleazari ushuru kama sehemu ya Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

42Ile nusu iliyokuwa ya Waisraeli, ambayo Mose aliitenga kutoka kwa ile ya watu waliokwenda vitani, 43nusu iliyokuwa ya jumuiya, ilikuwa kondoo 337,500, 44ngʼombe 36,000, 45punda 30,500, 46na wanadamu 16,000. 47Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Mose alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kama Bwana alivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani ya Bwana.

48Kisha maafisa waliokuwa juu ya vikosi vya jeshi, wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, walimwendea Mose 4931:49 Hes 1:19; Yer 23:4; Kut 23:7; Law 26:7-9; Za 72:14; 116:15; 1Sam 30:19na kumwambia, “Watumishi wako wamehesabu askari walio chini ya amri yetu na hakuna hata mmoja aliyekosekana. 5031:50 Kut 30:16; Law 17:11; Mt 20:28; Rum 3:25Kwa hiyo tumeleta kama sadaka kwa Bwana vyombo vya dhahabu kila mmoja wetu alivyopata, yaani vikuku, bangili, pete za muhuri, vipuli na mikufu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yetu mbele za Bwana.”

51Mose na kuhani Eleazari wakapokea kutoka kwao dhahabu, yaani vyombo vyote vilivyonakshiwa. 52Dhahabu yote kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia ambavyo Mose na kuhani Eleazari walimletea Bwana kama zawadi ilikuwa shekeli 16,75031:52 Shekeli 16,750 ni sawa na kilo 200. 5331:53 Mwa 34:29; Kum 20:14Kila askari alikuwa amejichukulia nyara zake binafsi. 5431:54 Kut 27:21; 40:2; 28:12; Hes 16:40; Kut 30:16; Yos 4:7; Zek 6:14; Lk 22:19; Mdo 1:4Mose na kuhani Eleazari walipokea dhahabu kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, wakazileta katika Hema la Kukutania kama ukumbusho kwa Waisraeli mbele za Bwana.