民数记 28 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

民数记 28:1-31

日常献祭的条例

1耶和华对摩西说: 2“你告诉以色列人,要在规定的时间献上蒙我悦纳的馨香火祭,作为我的食物。 3以下是他们要献给耶和华的火祭。

“每天两只毫无残疾、一岁的公羊羔作燔祭, 4早晨和傍晚各献一只, 5同时献上素祭——一公斤细面粉调上一升油。 6这是在西奈山上规定的日常燔祭,是献给耶和华的馨香火祭。 7与每只羊羔一同献上的还有一升酒,要将酒洒在圣所作为献给耶和华的奠祭。 8傍晚献羊羔时,也要像早上一样同时献上素祭和奠祭,作蒙耶和华悦纳的馨香火祭。

安息日献的祭

9“安息日,要献两只毫无残疾、一岁的公羊羔,同时献上奠祭以及两公斤调油的细面粉作素祭。 10这是在日常燔祭和奠祭以外安息日所献的燔祭。

初一献的祭

11“在朔日,要给耶和华献燔祭——两头公牛犊、一只公绵羊和七只一岁的公羊羔,都要毫无残疾。 12同时要献上调了油的细面粉作素祭,每头公牛需献三公斤素祭,每只公绵羊需献两公斤素祭, 13每只公羊羔需献一公斤素祭。这馨香的燔祭是献给耶和华的火祭。 14献燔祭时要同时献上奠祭,每头公牛需献二升奠酒,每只公绵羊需献一点二升奠酒,每只羊羔需献一升奠酒。这是朔日要献的燔祭,一年之中月月如此。 15除了日常的燔祭和奠祭以外,还要把一只公山羊献给耶和华作赎罪祭。

逾越节献的祭

16“一月十四日是耶和华的逾越节, 17十五日开始节庆,你们要连续七天吃无酵饼。 18第一天要举行圣会,不可做日常工作。 19你们要把毫无残疾的两头公牛犊、一只公绵羊和七只一岁的公羊羔献给耶和华作燔祭; 20同时要献上调了油的细面粉作素祭,每头公牛需献三公斤素祭,每只公绵羊需献两公斤素祭, 21每只公羊羔需献一公斤素祭; 22同时还要献一只公山羊作赎罪祭,为你们赎罪。 23除了早晨献的日常燔祭以外,要献上这些祭物。 24接连七天,除了日常的燔祭和同献的奠祭以外,还要照上面的规定给耶和华献上馨香的火祭。 25第七天,你们要举行圣会,不可做日常工作。

七七收获节献的祭

26“七七收获节庄稼初熟之日,就是你们把新素祭献给耶和华的日子,不可工作,要举行圣会。 27你们要把两头公牛犊、一只公绵羊和七只一岁的公羊羔献给耶和华作馨香的燔祭。 28同时要献上调了油的细面粉作素祭,每头公牛需献三公斤素祭,每只公绵羊需献两公斤素祭, 29每只公羊羔需献一公斤素祭。 30此外,还要献上一只公山羊作赎罪祭,为你们赎罪。 31除了日常的燔祭和同献的素祭以外,还要献上奠祭。祭牲不可有残疾。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hesabu 28:1-31

Sadaka Za Kila Siku

(Kutoka 29:38-46)

1Bwana akamwambia Mose, 228:2 Law 23:1-44; 3:11; 1:9; Mal 1:7-12“Wape Waisraeli agizo hili na uwaambie: ‘Hakikisheni kwamba mnaniletea mimi kwa wakati uliowekwa chakula kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, kama harufu nzuri ya kupendeza.’ 328:3 Kut 12:3; 29:38; Amo 4:4; Kut 29:38Waambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtolea Bwana: wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama sadaka ya kawaida ya kuteketezwa kila siku. 428:4 Kut 29:39; 12:6Andaa mwana-kondoo mmoja asubuhi na mwingine jioni, 528:5 Hes 29:6; Law 6:20; 2:1; Kut 16:36; 29:38-42; Hes 15:4kila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efa28:5 Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na kilo moja. ya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hini28:5 Robo ya hini ni sawa na lita moja. ya mafuta ya zeituni. 628:6 Law 1:3; Kut 19:3; Law 1:9Hii ni sadaka ya kawaida ya kuteketezwa iliyoanzishwa katika Mlima Sinai kama harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. 728:7 Hes 6:15; Law 10:9; 3:7; Hes 3:28; Kut 29:42; 30:9; Law 23:13; Hes 15:5-10; Isa 57:1Sadaka ya kinywaji itakayotolewa pamoja na kila mwana-kondoo ni robo ya hini ya kinywaji kilichochachuka. Mimina sadaka ya kinywaji kwa Bwana mahali patakatifu. 828:8 Kut 29:39; Law 23:7; 1:9Andaa yule mwana-kondoo wa pili jioni, pamoja na sadaka ya nafaka na sadaka ya kinywaji kama ulivyofanya kwa ile sadaka nyingine ya asubuhi. Hii ni sadaka iliyotolewa kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

Sadaka Za Sabato

928:9 Kut 20:10; Mt 12:5; Law 23:13; Eze 46:4; 40:4“ ‘Siku ya Sabato, utatoa sadaka ya wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari pamoja na sadaka yake ya kinywaji na sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu mbili za kumi za efa28:9 Sehemu mbili za kumi za efa ni sawa na kilo 2. za unga laini uliochanganywa na mafuta. 1028:10 Law 23:38; 1Sam 20:5; 1Nya 23:31; Neh 10:33; Isa 1:13-14; Eze 45:17; Hos 2:11; Kol 2:16Hii ni sadaka ya kuteketezwa itakayotolewa kwa ajili ya kila Sabato, pamoja na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya kinywaji.

Sadaka Za Kila Mwezi

1128:11 Hes 10:10; 7:15; Law 5:15; 1:3“ ‘Siku ya kwanza ya kila mwezi, mtamletea Bwana sadaka ya kuteketezwa ya fahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasiokuwa na dosari. 1228:12 Hes 15:6; 29:3; 15:9Pamoja na kila fahali, kutakuwa na sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa,28:12 Sehemu tatu za kumi za efa ni sawa na kilo 3. uliochanganywa na mafuta, pamoja na kondoo dume mmoja, sadaka ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta; 1328:13 Law 6:14; Hes 15:3; Law 1:9pamoja na kila mwana-kondoo, sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta. Hii ni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri, sadaka ya kuteketezwa iliyotolewa kwa moto kwa Bwana. 1428:14 Hes 15:11; 2Nya 2:4; Eze 3:5Pamoja na kila fahali kutakuwa na sadaka ya kinywaji nusu ya hini28:14 Nusu ya hini ni sawa na lita 2. ya divai; pamoja na kila kondoo dume, theluthi moja ya hini,28:14 Theluthi moja ya hini ni sawa na lita 1.2. na pamoja na kila mwana-kondoo robo hini. Hii ni sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi itakayotolewa kila mwandamo wa mwezi kwa mwaka. 1528:15 Hes 4:3; 29:16Zaidi ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya kinywaji, mbuzi mmoja dume atatolewa kwa Bwana kama sadaka ya dhambi.

Pasaka

(Walawi 23:5-14)

1628:16 Kut 12:11; 2Nya 30:13; 35:1; Kut 12:6; Law 23:5; Lk 22:7“ ‘Katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, itafanyika Pasaka ya Bwana. 1728:17 Kut 12:19; 12:15Katika siku ya kumi na tano ya mwezi huo itakuwa sikukuu; kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu. 1828:18 Kut 12:16; Law 23:7Katika siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu, msifanye kazi za kawaida. 1928:19 Law 1:9; 22:20; Hes 29:8; Kum 15:21Leteni mbele za Bwana sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo dume saba wenye umri wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 2028:20 Law 14:10Pamoja na kila fahali, andaa sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa; 21pia pamoja na kila mmoja wa wale wana-kondoo saba, andaa sehemu ya kumi ya efa. 2228:22 Law 4:2; 8:3; Hes 15:28; Law 16:18; Rum 8:3; Gal 4:4; Ebr 9:12; 10:1Pia mtoe beberu mmoja kama sadaka ya dhambi ambaye atafanya upatanisho kwa ajili yenu. 23Andaa hizi licha ya zile sadaka za kawaida za kuteketezwa za kila asubuhi. 2428:24 Law 1:9; 2Kor 2:15; Efe 5:2Kwa njia hii andaa chakula cha sadaka ya kuteketezwa kila siku, kwa siku saba kama harufu nzuri impendezayo Bwana. Hii itaandaliwa licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa ya kila siku pamoja na sadaka yake ya kinywaji. 2528:25 Kut 12:16; 13:6; Law 23:8Siku ya saba mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida.

Sikukuu Ya Majuma

(Walawi 23:15-22)

2628:26 Kut 34:2; 23:16; Law 23:10; Kum 16:10; Mit 3:9; Mdo 2:1“ ‘Siku ya malimbuko, mnapomletea Bwana sadaka ya nafaka mpya wakati wa Sikukuu ya Majuma, mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida. 2728:27 Law 23:18-19Mlete sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja, na pia wana-kondoo saba wenye umri wa mwaka mmoja, kama harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. 28Pamoja na kila fahali itatolewa sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa za unga laini; 29na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba. 30Ongeza beberu mmoja kwa kufanya upatanisho kwa ajili yenu. 31Andaa hizi sadaka pamoja na sadaka zake za vinywaji, kuwa nyongeza ya sadaka za kawaida za kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka. Hakikisha kuwa wanyama hao hawana dosari.