民数记 19 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

民数记 19:1-22

红母牛的灰

1耶和华对摩西亚伦说: 2“要吩咐以色列人遵行我颁布的以下律法条例。

以色列人要牵来一头毫无残疾、从未负过轭的红母牛。 3你们要把牛交给以利亚撒祭司,然后牵到营外,当着他的面把牛宰了。 4以利亚撒祭司要用指头蘸牛血,向会幕前面弹七次。 5然后,要当着他的面焚烧红母牛,牛的皮、肉、血和粪都要烧掉。 6祭司要把香柏木、牛膝草、朱红色线扔进烧牛的火里。 7之后,祭司要洗衣沐浴,才能回营,但要等到傍晚才能洁净。 8负责烧牛的人也要洗衣、沐浴,并且要等到傍晚才能洁净。 9要由洁净的人把红母牛灰收起来,放在营外洁净的地方,用于给以色列会众制作除秽水,作除罪之用。 10收起牛灰的人也要洗净衣服,等到傍晚才能洁净。以色列人和寄居的外族人都要永远遵行这定例。

11“碰过尸体的人,七天不洁净。 12他要在第三天和第七天用除秽水自洁,才能洁净,否则就不能洁净。 13若有人碰过尸体却不自洁,他就玷污了耶和华的圣幕,要将他从以色列人中铲除,因为除秽水没有洒在他身上,污秽还留在他身上。 14若有人死在帐篷里,当时走进帐篷的或在场的人都七天不洁净。 15帐篷里没有盖的敞口器皿都不洁净。 16人若在野外碰过被杀或自然死亡之人的尸体,或碰过死人的骸骨或坟墓,就七天不洁净。 17要拿些除罪用的红母牛灰,放在器皿里,倒上清水, 18然后由洁净的人拿牛膝草蘸这水洒在帐篷及里面所有的人和器具上,也要洒在碰过骸骨、坟墓、被杀者尸体或自然死亡者尸体的人身上。 19要由洁净的人在第三天和第七天把水洒在不洁净的人身上。到第七天,接受洁净礼的人要洗衣、沐浴,等到傍晚才能洁净。 20若有人沾了污秽却没有用除秽水自洁,他就不洁净,要将他从会众中铲除,因为他玷污了耶和华的圣所。 21你们要永远遵行这定例。洒除秽水的人要洗净衣服。碰过除秽水的人要等到傍晚才能洁净。 22不洁净的人碰过的东西都不洁净,碰过这些东西的人傍晚之前都不洁净。”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hesabu 19:1-22

Maji Ya Utakaso

1Bwana akamwambia Mose na Aroni: 219:2 Mwa 15:9; Ebr 9:13; Law 22:19-25; Kum 21:3; 1Sam 6:7“Hivi ndivyo sheria ambayo Bwana ameagiza itakavyo: Waambie Waisraeli wakuletee mtamba mwekundu asiye na dosari wala waa, na ambaye hajapata kufungwa nira. 319:3 Hes 3:4; Kut 29:14Mpeni kuhani Eleazari huyo mtamba; naye atatolewa nje ya kambi na kuchinjwa mbele yake huyo kuhani. 419:4 Law 4:17Kisha kuhani Eleazari atachukua baadhi ya damu yake kwenye kidole chake na kuinyunyiza mara saba kuelekea upande wa mbele ya Hema la Kukutania. 519:5 Kut 29:14Wakati angali akitazama, mtamba huyo atateketezwa: ngozi yake, nyama yake, damu na sehemu zake za ndani. 619:6 Za 51:7; Law 14:4Kuhani atachukua kuni za mti wa mwerezi, hisopo na sufu nyekundu, na kuvitupa kwenye huyo mtamba anayeungua. 719:7 Law 11:25; 14:8Baada ya hayo, kuhani lazima afue nguo zake, na aoge mwili wake kwa maji. Kisha anaweza kurudi kambini, lakini atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada mpaka jioni. 8Mtu amchomaye huyo mtamba lazima naye pia afue nguo zake na kuoga kwa maji, naye pia atakuwa najisi mpaka jioni.

919:9 Ebr 9:13; Kut 29:31; Law 4:12; Hes 8:1; Mwa 35:2“Mtu ambaye ni safi atakusanya majivu ya mtamba huyo na kuyaweka mahali ambapo ni safi nje ya kambi kwa taratibu za kiibada. Yatahifadhiwa na jumuiya ya Kiisraeli kwa matumizi katika maji ya utakaso; ni kwa ajili ya kutakasa kutoka dhambini. 1019:10 Law 15:10; 14:46; 3:17; 22:18Mtu akusanyaye majivu ya huyo mtamba ni lazima pia afue nguo zake, kadhalika naye pia atakuwa najisi hadi jioni. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa Waisraeli na kwa wageni wanaoishi miongoni mwao.

1119:11 Law 21:1; 8:33; Hes 31:19“Mtu yeyote agusaye maiti ya mtu yeyote atakuwa najisi kwa siku saba. 1219:12 Hes 31:19; 2Nya 26:21Ni lazima ajitakase mwenyewe kwa maji katika siku ya tatu na siku ya saba, ndipo atakuwa safi. Lakini kama hatajitakasa mwenyewe katika siku ya tatu na ya saba, hatakuwa safi. 1319:13 Law 21:11; 15:31; 2Nya 36:14; Za 79:1; Law 22:3; 7:20; Hag 2:13Mtu yeyote agusaye maiti ya mtu yeyote na kushindwa kujitakasa mwenyewe hunajisi Maskani ya Bwana. Mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na Israeli. Kwa sababu hajanyunyiziwa maji ya utakaso, yeye ni najisi; unajisi wake unabaki juu yake.

14“Hii ndiyo sheria itumikayo wakati mtu amekufa ndani ya hema: Yeyote aingiaye ndani ya hema hilo na yeyote aliye ndani yake watakuwa najisi kwa muda wa siku saba, 1519:15 Law 6:28nacho kila chombo kisicho na kifuniko juu yake kitakuwa najisi.

1619:16 Hes 31:19; 1Fal 13:2; 2Fal 23:14; Eze 6:5; 2Fal 23:6; Mt 23:27; Law 5:3“Mtu yeyote aliyeko nje mahali pa wazi agusaye mtu aliyeuawa kwa upanga au mtu aliyekufa kwa kifo cha kawaida, au mtu yeyote agusaye mfupa wa mtu aliyekufa au kaburi, atakuwa najisi kwa siku saba.

1719:17 Hes 8:7“Kwa mtu aliye najisi, weka majivu ya sadaka ya utakaso wa dhambi ndani ya chombo, umimine maji safi juu yao. 1819:18 Kut 12:22; Law 4:17Kisha mtu aliye safi kwa kawaida za kiibada atachukua hisopo, achovye ndani ya maji, na kunyunyizia hema na vifaa vyote pamoja na watu ambao walikuwamo. Pia ni lazima amnyunyizie mtu yeyote ambaye amegusa mfupa wa mtu aliyekufa, au kaburi, au mtu ambaye ameuawa, au mtu ambaye amekufa kifo cha kawaida. 1919:19 Law 16:14-15; Hes 31:19; Eze 36:25; Ebr 10:22; Mwa 35:2Mtu ambaye ni safi ndiye atakayemnyunyizia yeyote ambaye ni najisi siku ya tatu na siku ya saba, na katika siku ya saba atamtakasa mtu huyo. Mtu ambaye ametakaswa lazima afue nguo zake na kuoga kwa maji, na jioni ile atakuwa safi. 2019:20 Za 14:7; Law 15:31; 14:8Lakini ikiwa mtu ambaye ni najisi hakujitakasa mwenyewe, ni lazima akatiliwe mbali na jumuiya, kwa sababu ameinajisi Maskani ya Bwana. Maji ya utakaso hayajanyunyizwa juu yake, naye ni najisi. 2119:21 Kut 27:21Hii ni sheria ya kudumu kwao.

“Mtu yeyote ambaye ananyunyiza yale maji ya utakaso lazima pia afue nguo zake, na yeyote ambaye hugusa maji ya utakaso atakuwa najisi mpaka jioni. 2219:22 Law 5:2; 15:4-12Kitu chochote anachogusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi, na yeyote akigusaye huwa najisi mpaka jioni.”