撒母耳记下 2 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

撒母耳记下 2:1-32

大卫做犹大王

1这事以后,大卫求问耶和华:“我可以回到犹大的城邑吗?”耶和华说:“可以。”大卫又问:“我应该回到哪一座城呢?”耶和华说:“希伯仑。” 2大卫就带着他的两个妻子耶斯列亚希暖迦密拿八的遗孀亚比该,一起上到希伯仑3他还把部下和他们的家属一起带去,住在希伯仑地区的城邑。 4犹大人到希伯仑膏立大卫犹大支派的王。

大卫听说是基列·雅比人埋葬了扫罗5就派人去告诉他们:“你们这样厚待你们的主人扫罗,把他安葬,愿耶和华赐福给你们! 6愿耶和华以慈爱和信实待你们,我也会厚待你们,因为你们做了这事。 7现在你们的主扫罗已经死了,犹大支派已经膏立我做他们的王,你们要刚强勇敢。”

大卫家与扫罗家争战

8那时,扫罗的元帅尼珥的儿子押尼珥带着扫罗的儿子伊施波设过河来到玛哈念9立他为王统治基列亚书利耶斯列以法莲便雅悯以色列其余的地方。 10扫罗的儿子伊施波设四十岁登基,统治以色列两年。犹大支派则跟随大卫11大卫希伯仑做王统治犹大支派七年半。

12有一次,尼珥的儿子押尼珥带领扫罗的儿子伊施波设的军队,从玛哈念前往基遍13洗鲁雅的儿子约押带领大卫的军队出来,在基遍池与他们相遇。一方坐在池这边,一方坐在池那边。 14押尼珥约押说:“让双方的青年起来在我们面前较量一下吧。”约押说:“好啊。” 15于是,双方都选了十二人出来, 16他们各自抓住对方的头发,用刀刺对方的肋旁,同归于尽。于是基遍的那个地方叫“刀田”。 17那天,两军恶战,押尼珥以色列人被大卫的人马杀败。 18当时,洗鲁雅的三个儿子约押亚比筛亚撒黑都在场。亚撒黑跑得飞快如鹿, 19他跟在押尼珥后面,不偏不离,穷追不舍。 20押尼珥回头问道:“你是亚撒黑吗?”亚撒黑说:“正是。” 21押尼珥说:“你去追赶别人,夺取他的兵器吧。”但亚撒黑还是穷追不舍。 22押尼珥又对他说:“快走开吧,非逼我杀你吗?我若杀了你,还有何颜面见你哥哥约押呢?” 23亚撒黑还是不肯罢休。押尼珥就用枪柄刺入他的肚腹,穿透了他的后背,他便倒地身亡。众人赶到那里,都停了下来。

24约押亚比筛却继续追赶押尼珥。太阳落山时,他们追到了基亚附近的亚玛山,通往基遍旷野的路旁。 25便雅悯人在押尼珥的带领下聚集在一个山头上。 26押尼珥约押喊道:“我们非要无休止地杀下去吗?难道你不知道这样下去必有苦果吗?你什么时候才命你的人停止追杀自己的同胞呢?” 27约押说:“我凭永活的上帝起誓,你要是不这样说,我们会一直追到天亮。” 28于是,约押吹响号角,所有的人便停止了战斗,不再追赶以色列的军队。

29押尼珥和随从连夜赶路,穿过了亚拉巴,过了约旦河,第二天又马不停蹄地走了一个上午,回到玛哈念30约押追赶押尼珥回来后细点人数,发现除亚撒黑外还损失了十九个人。 31大卫的军队杀了三百六十个跟随押尼珥便雅悯人。 32约押和他的随从把亚撒黑送到伯利恒,葬在他父亲的坟墓里。然后,他们整夜赶路,黎明的时候回到了希伯仑

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Samweli 2:1-32

Daudi Atiwa Mafuta Kuwa Mfalme Wa Yuda

12:1 1Sam 23:2, 11-12; Mwa 13:18; 23:19; 1Sam 30:31; Hes 27:21; 1Sam 23:2-9; 1Fal 2:11Ikawa baada ya mambo haya, Daudi akamuuliza Bwana, “Je, nipande kwenda katika mojawapo ya miji ya Yuda?”

Bwana akasema, “Panda.”

Daudi akauliza, “Je, niende wapi?”

Bwana akajibu, “Nenda Hebroni.”

22:2 1Sam 25:42-43; 30:5Basi Daudi akakwea kwenda huko pamoja na wake zake wawili, Ahinoamu wa Yezreeli na Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli. 32:3 1Sam 27:2; 1Nya 12:22; Mwa 13:18; 23:2; 37:14Pia Daudi akawachukua watu waliokuwa pamoja naye, kila mmoja na jamaa yake, nao wakaishi huko Hebroni na miji yake. 42:4 1Sam 30:31; 2:35; 2Sam 5:3-5; 1Nya 12:23-40; Amu 21:8; 1Sam 11:1; 31:11-13Ndipo watu wa Yuda wakaja Hebroni, huko wakamtia Daudi mafuta awe mfalme juu ya nyumba ya Yuda.

Daudi alipoambiwa kuwa ni watu wa Yabeshi-Gileadi waliomzika Sauli, 52:5 Amu 17:2; 1Sam 23:21; 2Tim 1:16; Za 115:15akatuma wajumbe kwa watu wa Yabeshi-Gileadi kuwaambia, “Bwana awabariki kwa kuonyesha wema huu kwa kumzika Sauli bwana wenu. 62:6 Kut 34:6; 2Tim 1:16; Mt 5:44Sasa Bwana na awaonyeshe wema na uaminifu, nami pia nitawaonyesha wema ule ule kwa kuwa mmefanya jambo hili. 72:7 Yos 1:6; Amu 5:21Sasa basi, kuweni hodari na mashujaa, kwa maana bwana wenu Sauli amekufa, nayo nyumba ya Yuda imenitia mafuta niwe mfalme juu yao.”

Vita Kati Ya Nyumba Ya Daudi Na Sauli

82:8 1Sam 14:50; 2Sam 3:27; 4:5; 1Nya 8:33; 9:36-39; Mwa 32:2; 1Sam 17:55; 2Sam 17:27Wakati huo Abneri mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Sauli, alikuwa amemchukua Ish-Boshethi mwana wa Sauli na kumleta hadi Mahanaimu. 92:9 Hes 32:26; Yos 19:24-31; 1Nya 12:29; Amu 1:32Akamweka awe mfalme juu ya nchi ya Gileadi, Waasheri,2:9 Waasheri hapa ni kabila moja la Israeli. Yezreeli, Efraimu, Benyamini na Israeli yote.

10Ish-Boshethi2:10 Ish-Boshethi maana yake Mtu wa Aibu, pia anaitwa Esh-Baali maana yake Mtu wa Baali (1Nya 8:33; 9:39). mwana wa Sauli alikuwa na umri wa miaka arobaini alipoanza kutawala Israeli, naye akatawala miaka miwili. Hata hivyo, nyumba ya Yuda ikamfuata Daudi. 112:11 2Sam 5:5Muda ambao Daudi alikuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda huko Hebroni ilikuwa miaka saba na miezi sita.

122:12 Yos 9:3; 18:25; Isa 28:21Abneri mwana wa Neri, pamoja na watu wa Ish-Boshethi mwana wa Sauli, wakatoka Mahanaimu kwenda Gibeoni. 132:13 2Sam 8:16; 19:13; 1Fal 1:17; 1Nya 2:16; 22:6; 27:34; Yer 41:12Yoabu mwana wa Seruya na watu wa Daudi wakatoka na kukutana nao kwenye bwawa la Gibeoni. Kikundi kimoja kiliketi upande mmoja wa bwawa, na kikundi kingine upande wa pili.

142:14 Mit 10:23; 13:10Ndipo Abneri akamwambia Yoabu, “Tuwaweke baadhi ya vijana wasimame na wapigane ana kwa ana mbele yetu.”

Yoabu akasema, “Sawa, na wafanye hivyo.”

15Kwa hiyo vijana wakasimama, wakahesabiwa: watu wa Benyamini na wa Ish-Boshethi mwana wa Sauli kumi na wawili, na upande wa Daudi kumi na wawili. 162:16 Amu 3:21Kisha kila mtu akakamatana na mpinzani wake kichwani na kuchomana kwa upanga, nao wakaanguka chini pamoja. Kwa hiyo mahali pale katika Gibeoni pakaitwa Helkath-Hasurimu.2:16 Helkath-Hasurimu maana yake Uwanja wa Mapambano.

172:17 2Sam 3:1; 1Sam 17:8; 1Fal 20:11Siku hiyo vita vilikuwa vikali sana, naye Abneri na watu wa Israeli wakashindwa na watu wa Daudi.

182:18 2Sam 3:39; 16:10; 19:22; 3:30; 10:7; 11:1; 14:1; 18:14; 20:8; 24:3; 1Fal 1:7; 2:5, 34; 1Sam 26:6; 2Sam 23:24; 2Nya 2:16; 1Nya 11:26; 27:1; 12:8; Za 6:5; Wim 2:9Wana watatu wa Seruya walikuwako huko: nao ni Yoabu, Abishai na Asaheli. Basi huyo Asaheli alikuwa na mbio kama paa. 19Asaheli akamfukuza Abneri, pasipo kugeuka kulia wala kushoto wakati akimfuata. 20Abneri akaangalia nyuma na kumuuliza, “Ni wewe, Asaheli?”

Akamjibu, “Ndiyo.”

212:21 1Sam 17:42Ndipo Abneri akamwambia, “Geuka upande wa kulia au kushoto. Mchukue mmoja wa vijana wa kiume na umvue silaha zake.” Lakini Asaheli hakuacha kumfukuza.

222:22 2Sam 3:27Abneri akamwonya tena Asaheli akimwambia, “Acha kunifukuza! Kwa nini nikuue? Je, nitawezaje kumtazama ndugu yako Yoabu usoni?”

232:23 2Sam 3:27; 4:6; 20:17Lakini Asaheli alikataa kuacha kumfuatia, kwa hiyo Abneri akamchoma Asaheli tumboni kwa ncha butu ya mkuki wake, mkuki ukamtoboa ukatokea mgongoni mwake. Akaanguka na kufa papo hapo. Ikawa kila mtu alisimama alipofika mahali pale Asaheli alipoanguka na kufa.

242:24 Yos 9:3; 10:2Lakini Yoabu na Abishai walimfuata Abneri, na jua lilipokuwa linatua, wakafika kwenye kilima cha Ama, karibu na Gia kwenye njia ya kuelekea kwenye nyika ya Gibeoni. 25Ndipo watu wa kabila la Benyamini wakakusanyika tena nyuma ya Abneri. Wakaunda kikosi na kujiimarisha juu ya kilima.

262:26 Kum 32:42; Yer 46:10, 14; Nah 2:13; 3:15; Ay 18:2; 19:2; Za 4:2; Mdo 7:16Abneri akamwita Yoabu, akamwambia, “Je, ni lazima upanga uendelee kuangamiza milele? Hutambui kwamba jambo hili litaishia katika uchungu? Utaacha kuwaagiza watu wako waache kuwafuatilia ndugu zao hata lini?”

272:27 Mit 17:14; 20:18; Lk 14:31-32Yoabu akajibu, “Hakika kama aishivyo Mungu, kama hukusema, hawa watu wangeendelea kuwafuatia ndugu zao mpaka asubuhi.”

282:28 2Sam 18:16; 20:23; Amu 3:27Basi Yoabu akapiga tarumbeta, nao watu wote wakasimama, hawakuwafuata Israeli tena, wala hawakuwapiga tena.

292:29 Kum 3:17; Mwa 32:2; Wim 2:17; Yos 21:38; 2Sam 17:24Usiku ule wote Abneri na watu wake wakatembea kupitia Araba. Wakavuka Mto Yordani, wakaendelea wakipitia nchi yote ya Bithroni wakafika Mahanaimu.

30Basi Yoabu akarudi kutoka kumfuatia Abneri, na kuwakusanya watu wake wote. Pamoja na Asaheli, watu kumi na tisa wa Daudi walikuwa wamepotea. 31Lakini watu wa Daudi walikuwa wamewaua watu wa kabila la Benyamini 360 waliokuwa pamoja na Abneri. 322:32 Mwa 49:29; 47:29-30; Amu 8:32; 2Sam 17:24Wakamchukua Asaheli, wakamzika katika kaburi la baba yake huko Bethlehemu. Kisha Yoabu na watu wake wakatembea usiku kucha na kufika huko Hebroni wakati wa mapambazuko.