撒母耳记下 16 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

撒母耳记下 16:1-23

大卫和洗巴

1大卫刚越过了山顶,就看见米非波设的仆人洗巴牵着两头驴,驴背上驮着二百个面饼、一百个葡萄饼、一百个夏天的果饼和一皮袋酒来迎接他。 2王问洗巴说:“你带这些来做什么?”洗巴说:“驴是给王的家眷骑的,饼和夏天的水果是给你的随从吃的,酒是供他们在旷野疲惫时喝的。” 3王又问他:“你主人的孙子米非波设在哪里?”洗巴说:“他在耶路撒冷,因为他相信现在以色列人会把他祖父的国归还给他。” 4王就对洗巴说:“米非波设的一切现在都归你了。”洗巴说:“愿我在我主我王面前蒙恩!”说着,便叩拜大卫王。

示每咒诅大卫

5大卫王来到巴户琳时,扫罗家族基拉的儿子示每出来对着大卫破口大骂, 6还朝大卫和他的臣仆扔石头,无视大卫身边的众多部下和勇士。 7示每大卫:“滚吧!滚吧!你这个杀人凶手,你这个败类! 8你杀扫罗的家人,夺其王位,耶和华报应了你,把江山交给了你儿子押沙龙。你这杀人凶手是自食恶果!”

9洗鲁雅的儿子亚比筛对王说:“这死狗竟敢辱骂我主我王,让我过去砍掉他的头!” 10王却说:“洗鲁雅的儿子啊,不要管我的事。如果是耶和华叫他来咒骂我,谁能干涉他呢?” 11大卫亚比筛和他所有臣仆说:“我的亲生儿子尚且要取我的命,何况这个便雅悯人呢?由他去吧!因为这是耶和华的意思。 12也许耶和华会体察我的困苦,因我今天所受的咒骂而赐福给我。” 13于是,大卫和随从继续赶路,示每也沿着对面的山坡边走边骂,向他们扔石头,撒灰尘。 14王和众人来到约旦河边时,疲惫不堪,便在那里歇息。

15押沙龙以色列众人进了耶路撒冷亚希多弗也和他在一起。 16大卫的朋友亚基户筛去见押沙龙,对他说:“愿王万岁!愿王万岁!” 17押沙龙户筛说:“这就是你对朋友的忠诚吗?你为什么不跟你的朋友去呢?” 18户筛说:“我不去,谁是耶和华和全体以色列人民所拣选的,我就归属谁,留在谁那里。 19再说,我应当服侍谁呢?难道不该服侍王的儿子吗?我要像服侍你父亲一样服侍你。”

20押沙龙亚希多弗下一步应该怎么办。 21亚希多弗说:“你父亲留下几个妃嫔看守宫殿,你要跟她们同寝,叫所有的以色列人知道你与父亲誓不两立,这样支持你的人会更坚定。” 22于是,他们便为押沙龙在殿顶盖了一座帐篷,他就当着所有以色列人的面与父亲的妃嫔同寝。 23那时,亚希多弗出的主意如同是来自上帝的话,大卫曾对他言听计从,现在押沙龙也是一样。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Samweli 16:1-23

Daudi Na Siba

116:1 2Sam 9:1-3; 1Sam 25:18; 1Nya 12:40; 2Sam 15:30Daudi alipokuwa amekwenda umbali mfupi kupita kilele cha mlima, akamkuta huko Siba, msimamizi wa shughuli za Mefiboshethi, akingojea kumlaki Daudi. Alikuwa na punda wawili wakiwa wametandikwa na kupakiwa mikate mia mbili, maandazi mia ya zabibu kavu, maandazi mia ya tini na kiriba cha divai.

216:2 2Sam 17:27-29; Amu 5:10; 10:4; 1Sam 25:27; 2Sam 15:23; Mit 15:23; 31:6; Za 104:15; 1Tim 5:23Mfalme Daudi akamuuliza Siba, “Kwa nini umeleta vitu hivi?”

Siba akamjibu, “Punda ni kwa ajili ya watu wa nyumba ya mfalme kupanda, mikate na matunda ni kwa ajili ya watu kula, nayo divai ni kwa kuwaburudisha watakaochoka jangwani.”

316:3 2Sam 9:9-10; 19:26-27Kisha mfalme akauliza, “Yuko wapi mwana wa bwana wako?”

Siba akamwambia, “Anakawia Yerusalemu, kwa sababu anafikiri, ‘Leo nyumba ya Israeli itanirudishia utawala wa baba yangu.’ ”

416:4 2Sam 4:4; 14:10-11; Mit 18:13Ndipo mfalme akamwambia Siba, “Yote yaliyokuwa mali ya Mefiboshethi sasa ni mali yako.”

Siba akasema, “Nasujudu kwa unyenyekevu. Naomba nipate kibali mbele yako, bwana wangu mfalme.”

Shimei Amlaani Daudi

516:5 2Sam 3:16; 19:16-23; 1Fal 2:8, 36, 44; Kut 22:28; 2Sam 19:16Mfalme Daudi alipokuwa anakaribia Bahurimu, mtu mmoja kutoka ukoo huo huo kama jamaa ya Sauli, akatoka humo, ambaye jina lake ni Shimei mwana wa Gera; akawa analaani alipokuwa akitoka. 6Akamtupia Daudi na maafisa wote wa mfalme mawe, ingawa vikosi vyote na walinzi maalum walikuwa kulia na kushoto mwa Daudi. 7Shimei alivyokuwa akilaani, akasema, “Toka hapa, toka hapa, wewe mtu wa damu, wewe mtu mbaya kabisa! 816:8 2Sam 19:28; 21:9; 19:19; Za 55:3; Amu 9:24; 1Fal 2:32-33; Ufu 16:6Bwana amekulipiza kwa ajili ya damu yote uliyomwaga ya watu wa nyumba ya Sauli, ambaye nafasi yake umeimiliki wewe. Bwana amekabidhi ufalme mkononi mwa mwanao Absalomu. Maangamizi yamekupata kwa sababu wewe ni mtu wa damu!”

916:9 1Sam 26:6; 2Sam 3:8, 39; Lk 9:54; Kut 22:28Ndipo Abishai mwana wa Seruya akamwambia mfalme, “Kwa nini huyu mbwa mfu amlaani bwana wangu mfalme? Niruhusu nivuke nikatilie mbali kichwa chake.”

1016:10 2Sam 2:18; 19:22; Rum 9:20; 2Sam 3:39; 1Pet 2:23; 1Fal 18:25; Mao 3:38Lakini mfalme akamwambia, “Mna nini nami, enyi wana wa Seruya? Ikiwa analaani kwa sababu Bwana amemwambia, ‘Mlaani Daudi,’ nani awezaye kuuliza, ‘Kwa nini unafanya hivi?’ ”

1116:11 2Sam 12:11; Mwa 45:5; 1Sam 26:17Ndipo Daudi akamwambia Abishai na maafisa wake wote, “Mwanangu, yeye ambaye ametoka viunoni mwangu mwenyewe, anajaribu kuuondoa uhai wangu. Je, si zaidi sana kwa huyu Mbenyamini! Mwacheni, acha alaani, kwa maana Bwana amemwambia afanye hivyo. 1216:12 Za 4:1; 25:18; Kum 23:5; Rum 8:28; Mwa 29:32; Za 37:7; Yer 24:5-7; Mao 3:22-26; Mt 5:11-12; 2Kor 4:17Inawezekana kwamba Bwana ataona dhiki yangu na kunilipa mema kwa ajili ya laana ninayopokea leo.”

13Kwa hiyo Daudi na watu wake wakaendelea na safari yao barabarani, huku Shimei akiwa anatembea pembezoni mwa kilima sambamba na Daudi, huku akimlaani na kumtupia Daudi mawe na kumrushia mavumbi. 1416:14 Za 109:28; 2Sam 17:2Mfalme na watu wote aliokuwa pamoja nao wakafika kwenye kituo chao wakiwa wamechoka. Mfalme akajiburudisha hapo.

Shauri La Hushai Na Ahithofeli

1516:15 2Sam 15:37; 15:12Wakati huo, Absalomu pamoja na watu wote wa Israeli wakafika Yerusalemu, naye Ahithofeli alikuwa pamoja naye. 1616:16 2Sam 15:32Ndipo Hushai, Mwariki, rafiki wa Daudi, akamwendea Absalomu na kumwambia, “Mfalme aishi maisha marefu! Mfalme aishi maisha marefu!”

1716:17 2Sam 19:24-25; Mit 17:17; 2Sam 15:32Absalomu akamuuliza Hushai, “Je, huu ndio upendo unaomwonyesha rafiki yako? Kwa nini hukufuatana na rafiki yako?”

18Hushai akamwambia Absalomu, “La hasha, yeye aliyechaguliwa na Bwana, aliyechaguliwa na watu hawa, atakayechaguliwa tena na watu wote wa Israeli, huyu ndiye nitakayekuwa wake, nami nitabakia pamoja naye. 1916:19 2Sam 15:34; 1Sam 28:2Zaidi ya hayo, nimtumikie nani? Je, nisimtumikie mwana? Kama vile nilivyomtumikia baba yako, ndivyo nitakavyokutumikia wewe.”

2016:20 Kut 1:10; Za 37:12-15; Mit 21:30; Mt 27:1Absalomu akamwambia Ahithofeli, “Tupe shauri lako. Tufanye nini?”

2116:21 Mwa 35:22; 2Sam 12:11; 15:16; Zek 8:13; Law 8:18; 20:11; Kum 22:30; 27:20; Mit 28:7; Isa 3:9; Mik 7:3-6Ahithofeli akamjibu, “Kutana kimwili na masuria wa baba yako aliowaacha kutunza jumba la kifalme. Ndipo Israeli yote itakaposikia kwamba umejifanya chukizo kwa baba yako, nayo mikono ya kila mmoja aliye pamoja nawe itatiwa nguvu.” 2216:22 2Sam 3:7; 12:11-12; 15:16Kwa hiyo wakasimika hema kwa ajili ya Absalomu juu ya paa, naye akakutana kimwili na masuria wa baba yake mbele ya Israeli wote.

2316:23 2Sam 17:14, 23; 15:12Ilikuwa katika siku hizo shauri lililotolewa na Ahithofeli lilikuwa kama lile ambalo limeulizwa kwa Mungu. Ndivyo Daudi na Absalomu walivyoyaheshimu mashauri yote ya Ahithofeli.