历代志下 9 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

历代志下 9:1-31

示巴女王拜访所罗门

1示巴女王听闻所罗门的名声,便来用难题考问他。她率领许多随从,用骆驼驮着香料、宝石和大量的黄金到耶路撒冷晋见所罗门王,与所罗门谈论她心中的疑问。 2所罗门王解答了她所有的问题,没有一样难得住他。 3示巴女王看见所罗门的智慧,又看见他建的宫殿、 4席上的美味、入座的群臣、侍立一旁的仆人、他们的服装、酒政、以及他在耶和华殿里献的燔祭,感到万分惊奇。 5她对所罗门王说:“我在本国听到的有关你的功业和智慧原来都是真的。 6若不是亲眼目睹,我不会相信。事实上,我听到的还不到一半!你的智慧远超过我听到的传闻。 7你的臣仆经常侍立在你面前聆听智慧之言,真有福气! 8你的上帝耶和华当受称颂!祂喜爱你,立你做王统治祂的子民。因为你的上帝爱以色列人,要使他们永远坚立,所以立你为他们的王,使你秉公行义。”

9示巴女王将四吨黄金、大量香料和宝石献给所罗门王。再无人像示巴女王那样献给所罗门王那么多香料。 10希兰的仆人和所罗门的仆人从俄斐运来黄金、檀香木和宝石。 11所罗门王用这些檀香木建造耶和华的殿和王宫的阶梯,又制作歌乐手的琴瑟。在犹大从来没有见过这样的物品。 12所罗门王满足了示巴女王的一切要求,回赠她的礼物超过了她带来的。之后,女王和随从就回示巴去了。

所罗门王的财富

13所罗门每年收到的黄金约二十三吨, 14此外还有商人、阿拉伯诸王和国内各总督送给他的金银。 15所罗门王用锤好的金子打造了二百面大盾牌,每面用七公斤金子; 16又用锤好的金子打造了三百面小盾牌,每面用三点五公斤金子,全部放在黎巴嫩林宫。 17王又造了一个象牙大宝座,外面用纯金包裹。 18这宝座有六级台阶,又有金脚凳与宝座相连,宝座两旁有扶手,扶手两边各站着一头狮子, 19六级台阶上共站着十二头狮子,每级台阶两端各站一头。这宝座举世无双。 20所罗门王所有的杯子都是金的,黎巴嫩林宫里所有的器皿都是纯金的,没有一件是用银子造的,因为所罗门年间银子不算什么。 21王有船队与希兰的仆人一起出海去他施,每三年就运回金银、象牙、猿猴和孔雀。 22所罗门王的财富和智慧超过天下诸王。 23天下的君王都纷纷来朝见所罗门,聆听上帝赐给他的智言慧语。 24他们年年都带来礼物,有金银器皿、衣服、兵器、香料和骡马。 25所罗门有四千个安置战车和马匹的棚,有一万二千名骑兵,驻扎在屯车城和他所在的耶路撒冷26所罗门统管从幼发拉底河到非利士地区,远至埃及边境的诸王。 27王使耶路撒冷的金银多如石头,使香柏木多如丘陵的无花果树。 28所罗门的马匹都是从埃及和其他国家运来的。

所罗门逝世

29所罗门一生的事迹,自始至终都记在拿单先知的史记、示罗亚希雅的《预言书》和易多先见论尼八的儿子耶罗波安的《启示书》中。 30所罗门耶路撒冷统治以色列四十年, 31他与祖先同眠后,葬在他父亲大卫的城里。他儿子罗波安继位。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Nyakati 9:1-31

Malkia Wa Sheba Amtembelea Solomoni

(1 Wafalme 10:1-13)

19:1 Mwa 10:7; Eze 20:49; Lk 11:31; Mt 12:42; 13:11, 35; Za 49:4; 78:2; Mit 1:5Malkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Solomoni, huyo malkia akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Alifika akiwa na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliobeba vikolezi, kiasi kikubwa cha dhahabu na vito vya thamani, alikuja kwa Solomoni na kuzungumza naye kuhusu yote ambayo alikuwa nayo moyoni mwake. 2Solomoni akamjibu maswali yake yote, wala hakukuwa na jambo lolote lililokuwa gumu kwake asiweze kumwelezea. 39:3 1Fal 5:12Malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Solomoni na jumba la kifalme alilokuwa amejenga, 4chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa alizotoa katika Hekalu la Bwana alipatwa na mshangao.

5Akamwambia mfalme, “Taarifa niliyosikia kwenye nchi yangu mwenyewe kuhusu mafanikio na hekima yako ni kweli. 69:6 2Nya 6:32Lakini sikuamini yaliyosemwa hadi nilipokuja na kuona kwa macho yangu mwenyewe. Naam, sikuambiwa hata nusu yake; katika hekima na mali umezidi sana kuliko ile taarifa niliyoisikia. 7Heri watu wako! Heri hawa maafisa wako wasimamao mbele yako daima na kusikia hekima yako! 89:8 1Fal 2:12; 1Nya 28:5; Za 72:8-9Ahimidiwe Bwana Mungu wako, ambaye amependezwa sana nawe, na akakuweka juu ya kiti chake cha ufalme utawale kwa niaba ya Bwana Mungu wako. Kwa sababu ya upendo wa Mungu wako kwa Israeli na shauku yake ya kuwadhibitisha milele, amekufanya wewe mfalme juu yao, ili kudumisha haki na uadilifu.”

99:9 2Nya 8:18Naye akampa mfalme talanta 1209:9 Talanta 120 za dhahabu ni sawa na tani 4.5. za dhahabu, kiasi kikubwa cha vikolezi na vito vya thamani. Haikuwahi kamwe kuletwa vikolezi vizuri kama vile Malkia wa Sheba alivyompa Mfalme Solomoni.

109:10 1Fal 5:2-6; 2Nya 8:18; 1Fal 9:27-28; 10:11; Za 72:10(Watumishi wa Hiramu na wa Solomoni wakaleta dhahabu kutoka Ofiri, tena wakaleta shehena kubwa ya miti ya msandali na vito vya thamani. 11Mfalme akatumia hiyo miti ya msandali kuwa ngazi kwa ajili ya Hekalu la Bwana na kwa jumba la kifalme, pia kwa kutengeneza vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Kiasi hicho kingi cha msandali hakijawahi kuingizwa Yuda tangu siku ile.)

12Mfalme Solomoni akampa Malkia wa Sheba kila kitu alichotamani na kukiomba, zaidi ya vile alivyokuwa amemletea mfalme. Kisha malkia akaondoka na kurudi katika nchi yake, yeye na watumishi wake.

Fahari Ya Solomoni

(1 Wafalme 10:14-25)

13Uzito wa dhahabu ambayo Solomoni alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666,9:13 Talanta 666 za dhahabu ni sawa na tani 25. 149:14 Isa 21:13; Eze 27:21; Yer 25:24; Isa 45:14; Za 68:29; 72:10; Isa 60:6mbali na mapato yaliyoletwa na wafanyabiashara na wachuuzi. Wafalme wote wa Arabuni na watawala wa nchi wakamletea Solomoni dhahabu na fedha.

15Mfalme Solomoni akatengeneza ngao kubwa 200 kwa dhahabu iliyofuliwa. Kila ngao ilikuwa na dhahabu yenye uzito wa shekeli 6009:15 Shekeli 600 za dhahabu ni sawa na kilo 3.5. 169:16 2Nya 12:9; 1Fal 7:2Akatengeneza pia ngao ndogo 300 za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa na uzito wa mane tatu9:16 Mane tatu za dhahabu ni sawa na kilo 1.7. za dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni.

179:17 1Fal 22:39Kisha mfalme akatengeneza kiti kikubwa cha kifalme kwa kutumia pembe za ndovu na kukifunika kwa dhahabu safi. 18Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na mahali pa kuwekea miguu vyote vya dhahabu. Pande zote za kiti kulikuwa na mahali pa kuegemeza mikono, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono. 19Simba kumi na wawili walisimama kwenye ngazi sita, mmoja katika kila upande wa kila ngazi. Hakuna kitu kama hicho kilichokuwa kimefanyika kwenye ufalme mwingine wowote. 20Vikombe vyote vya Mfalme Solomoni vya kunywea vilikuwa vya dhahabu na vyombo vyote vya nyumbani katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hakukuwa na kitu kilichotengenezwa kwa fedha, kwa sababu fedha ilionekana ya thamani ndogo wakati wa Solomoni. 219:21 1Fal 10:22; Isa 2:16; Yer 10:9; Yn 1:3; 1Fal 22:48; Za 48:7; Isa 60:9; Za 72:10Mfalme alikuwa na meli nyingi za biashara9:21 Au: za Tarshishi (ona pia 1Fal 10:22; 22:48; 2Nya 20:36; Isa 2:16; 60:9). baharini zilizoendeshwa na watu wa Hiramu. Kwa mara moja kila miaka mitatu zilirudi, zikiwa zimebeba dhahabu, fedha, pembe za ndovu na nyani wakubwa na wadogo.

229:22 1Fal 3:13; 2Nya 1:12; Kol 2:2-3; Mt 12:42; 1Fal 10:23-24; Za 89:27Mfalme Solomoni alikuwa mkuu zaidi kwa utajiri na hekima kuliko wafalme wote wa dunia. 239:23 1Fal 4:34Wafalme wote wa dunia wakatafuta kukutana na Solomoni ili kusikia hekima ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake. 249:24 Za 45:12; Isa 18:7; Za 72:10-15Mwaka baada ya mwaka, kila mmoja ambaye alikuja, alileta zawadi, vyombo vya fedha na dhahabu, majoho, silaha na vikolezi, farasi na nyumbu.

259:25 1Sam 8:11; 1Fal 4:26; 10:26; 2Nya 1:14Solomoni alikuwa na mabanda 4,000 kwa ajili ya farasi na magari ya vita, farasi 12,000 ambao aliwaweka katika miji ya magari ya vita na katika Yerusalemu pamoja naye. 269:26 1Fal 2:21; Za 72:8-9; Mwa 15:18-21; 1Fal 4:21Solomoni akatawala juu ya wafalme wote kuanzia Mto Frati mpaka kwenye nchi ya Wafilisti na kuendelea hadi mpaka wa Misri. 279:27 1Fal 10:27Mfalme akafanya fedha kuwa kitu cha kawaida kama mawe huko Yerusalemu, mierezi akaifanya kuwa mingi kama mikuyu vilimani. 289:28 Kum 17:16; 1Fal 10:26; Isa 31:1; 2:7; 2Nya 1:16Farasi wa Solomoni waliletwa kutoka Misri na kutoka nchi nyingine zote.

Kifo Cha Solomoni

(1 Wafalme 11:41-43)

299:29 2Sam 7:2; 1Nya 29:29; 1Fal 11:29; 2Nya 10:2; 12:15; 13:22Kwa habari za matukio mengine ya utawala wa Solomoni, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Nathani, katika unabii wa Ahiya Mshiloni na katika maono ya Ido mwonaji kuhusu Yeroboamu mwana wa Nebati? 309:30 1Fal 11:42-43Solomoni alitawala Israeli yote miaka arobaini, akiwa Yerusalemu. 319:31 1Fal 2:10Kisha Solomoni akalala pamoja na baba zake, naye akazikwa katika mji wa Daudi baba yake. Naye Rehoboamu mwanawe akawa mfalme baada yake.