历代志下 31 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

历代志下 31:1-21

希西迦的改革

1当一切都办妥后,所有在场的以色列人就前往犹大各城邑,打碎神柱,砍倒亚舍拉神像,又拆毁犹大便雅悯以法莲玛拿西境内所有的丘坛和祭坛,然后各自返回自己的城邑和家园。

2希西迦分派祭司和利未人的班次,使他们各司其职,献上燔祭和平安祭,在耶和华殿门内事奉,称谢、颂赞耶和华。 3王又从自己的产业中划分出一部分作为早晚的燔祭,以及安息日、朔日及耶和华律法规定的其他节期的燔祭。

4他又吩咐耶路撒冷的居民将祭司和利未人当得的份交给他们,好使他们专心执行耶和华的律法。 5谕旨一出,以色列人就献出许多初熟的五谷、新酒、新油、蜂蜜、田间的出产及各样物品的十分之一,数量极多。 6住在犹大各城的以色列人和犹大人也送来牛羊的十分之一,以及献给他们的上帝耶和华的圣物,就是十一奉献,把它们堆积成堆。 7他们从三月开始堆积,到七月才结束。 8希西迦与众官员来了,看见堆积起来的供物,就称颂耶和华,又为耶和华的以色列子民祝福。 9希西迦向祭司和利未人询问这些供物的事, 10撒督家族的亚撒利雅大祭司回答说:“自从民众把这些供物送到耶和华的殿里以来,我们不但吃得饱,还剩下许多。因为耶和华赐福给祂的子民,所以才有这么多剩余。”

11于是,希西迦下令在耶和华的殿里预备库房。他们预备好后, 12便忠心地把供物、十一奉献和圣物放进库房。利未歌楠雅总管这事,他的兄弟示每做助手。 13耶歇亚撒细雅拿哈亚撒黑耶利末约撒拔以列伊斯玛基雅玛哈比拿雅做监督协助歌楠雅和他兄弟示每,他们都是希西迦王和管理上帝殿的亚撒利雅指派的。 14看守东门的利未人音拿的儿子可利,负责管理民众自愿献给上帝的礼物,以及分发献给耶和华的供物和至圣之物。 15伊甸珉雅珉耶书亚示玛雅亚玛利雅示迦尼雅在祭司所在的各城忠心地协助可利,按照班次,不分老幼,将物品分给他们的弟兄。 16此外,他们还分给三岁及三岁以上、姓名记在家谱上、每天在耶和华的殿中按班次供职的男子, 17并分给按宗族登记在家谱上的祭司,按班次和职任分给二十岁及二十岁以上的利未人, 18也按照家谱分给他们的妻子儿女,因为他们诚心洁净自己。 19至于住在各城郊野做祭司的亚伦子孙,各城都有指定的人把应得之份分给祭司中所有的男子和登记在家谱上的利未人。

20希西迦犹大全境都如此行,做他的上帝耶和华视为良善、正直和忠心的事。 21无论是在上帝的殿中事奉,还是遵行律法和诫命,他都寻求他的上帝,尽心去做。因此,他行事顺利。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Nyakati 31:1-21

Sehemu Za Ibada Za Kipagani Zaondolewa

131:1 2Fal 18:4; Isa 36:7; 2Nya 13:14Baada ya mambo haya yote kumalizika, Waisraeli ambao walikuwako huko wakaenda kwenye miji ya Yuda, wakayavunja yale mawe ya kuabudia na kuzikatakata zile nguzo za Ashera. Wakabomoa mahali pa juu pa kuabudia miungu pamoja na madhabahu zake kila mahali katika Yuda na Benyamini na katika Efraimu na Manase. Baada ya kuviharibu hivi vyote, Waisraeli wakarudi katika miji yao wenyewe na kwenye milki zao.

231:2 2Nya 29:9; Za 71:22; 1Nya 23:28-32; 15:2Hezekia akawapanga makuhani na Walawi katika migawanyo, kila mgawanyo kulingana na wajibu wao, kama ni makuhani au Walawi, ili kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, kuhudumu, kushukuru na kuimba sifa katika malango ya makao ya Bwana. 331:3 1Nya 29:3; Eze 45:17; Hes 28:1; 29:40Mfalme akatoa matoleo kutoka mali zake mwenyewe kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa za asubuhi na za jioni na sadaka za kuteketezwa kwa siku za Sabato, kwa Sikukuu za Mwezi Mwandamo na kwa ajili ya sikukuu zilizoamriwa kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Bwana. 431:4 Neh 13:10-12; Mal 2:7; 1Kor 9:13; Hes 18:8Akawaagiza watu wanaoishi Yerusalemu watoe sehemu iliyo haki ya makuhani na Walawi ili waweze kujitoa kikamilifu kutimiza wajibu wao katika Sheria ya Bwana. 531:5 Neh 13:12; Eze 44:30; Kum 12:17; 1Kor 15:20; Kut 22:29; 23:19; Hes 18:12; Eze 20:40; Yak 1:18; Mit 3:9Mara tu baada ya kutolewa tangazo hilo, Waisraeli wakatoa kwa ukarimu malimbuko ya nafaka zao, divai mpya, mafuta na asali pamoja na vyote vilivyotoka mashambani. Wakaleta kiasi kikubwa cha fungu la kumi la kila kitu. 631:6 Law 27:30; Neh 13:10-12; Kum 14:28; Rut 3:7Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda wakaleta pia fungu la kumi la makundi yao ya ngʼombe na makundi ya kondoo na mbuzi pia na fungu la kumi la vitu vitakatifu vilivyowekwa wakfu kwa ajili ya Bwana Mungu wao na kuvikusanya katika malundo. 731:7 Kut 23:16Wakaanza kufanya haya katika mwezi wa tatu na kumaliza katika mwezi wa saba. 831:8 Za 144:13-15; Mwa 14:19; 2Sam 6:18; Kum 33:29; 1Fal 8:55-56; 2Nya 6:3; Za 33:12; 144:15Wakati Hezekia na maafisa wake walipokuja na kuona yale malundo, wakamsifu Bwana na kuwabariki watu wake Israeli.

9Hezekia akawauliza makuhani na Walawi kuhusu yale malundo, 1031:10 2Sam 8:17; Kut 36:5; Hag 2:19; Mal 3:10-12naye Azaria aliyekuwa kuhani mkuu, kutoka jamaa ya Sadoki, akajibu, “Tangu watu walipoanza kuleta sadaka zao katika Hekalu la Bwana tumekuwa na chakula cha kutosha na vingi vya kuweka akiba kwa sababu Bwana amewabariki watu wake, hivyo tumekuwa na kiasi kingi kilichobaki.”

Kutambuliwa Kwa Makuhani Na Walawi

11Hezekia akatoa agizo la kutengeneza vyumba vya ghala katika Hekalu la Bwana nalo hili likafanyika. 1231:12 2Nya 35:9; Neh 13:13Kisha kwa uaminifu wakaleta sadaka zao, mafungu yao ya kumi na vitu vilivyowekwa wakfu. Konania Mlawi, ndiye alikuwa msimamizi wa vitu hivi na Shimei ndugu yake ndiye alikuwa msaidizi wake. 13Yehieli, Azazia, Nahathi, Asaheli, Yeremothi, Yozabadi, Elieli, Ismakia, Mahathi na Benaya walikuwa waangalizi chini ya Konania na Shimei ndugu yake, waliokuwa wamewekwa na Mfalme Hezekia na Azaria, afisa msimamizi wa Hekalu la Mungu.

14Kore mwana wa Imna, Mlawi, bawabu wa Lango la Mashariki, alikuwa msimamizi wa sadaka za hiari zilizotolewa kwa Mungu, akiyagawanya hayo matoleo yaliyotolewa kwa Bwana na pia zile sadaka zilizowekwa wakfu. 1531:15 2Nya 29:12; Yos 21:9-19Edeni, Miniamini, Yeshua, Shemaya, Amaria na Shekania walimsaidia kwa uaminifu katika miji ya makuhani, wakiwagawia makuhani wenzao kufuatana na migawanyo yao, wazee kwa vijana sawasawa.

1631:16 1Nya 23:3; Ezr 3:4Zaidi ya hao wakawagawia wanaume wenye umri wa miaka mitatu au zaidi ambao majina yao yalikuwa kwenye orodha ya vizazi, wale wote ambao wangeingia katika Hekalu la Bwana ili kufanya kazi zao mbalimbali za kila siku kulingana na wajibu katika mgawanyo wao. 1731:17 1Nya 23:24, 27Kuandikishwa kwa makuhani kulikuwa kwa kufuata chimbuko la nyumba za baba zao na Walawi kuanzia umri wa miaka ishirini au zaidi ilikuwa kufuatana na huduma zao, kwa migawanyo yao. 18Makuhani waliandikishwa pamoja na watoto wao wadogo, wake zao, watoto wao wa kiume na wa kike, jamii yote iliandikishwa kwa kufuata orodha ya vizazi vyao. Kwa kuwa walikuwa waaminifu katika kujitakasa.

1931:19 Law 25:34; 2Nya 31:12-15; Hes 35:2Kuhusu makuhani, wazao wa Aroni walioishi kwenye mashamba yaliyozunguka miji yao au katika miji mingine yoyote, watu walitajwa majina ili kumgawia kila mwanaume miongoni mwao na kwa wote waliokuwa katika orodha ya vizazi vya Walawi.

2031:20 2Fal 20:3; 22:2; 1The 2:10; 1Fal 15:5; Yn 1:47Hivi ndivyo Hezekia alivyofanya katika Yuda yote, akifanya lile lililo jema, sawa na la uaminifu mbele za Bwana Mungu wake. 2131:21 Kum 29:9; Mit 3:9; Yos 4:7; Mal 3:10; 1Tim 4:8Naye katika kila kitu alichofanya katika huduma kwenye Hekalu la Mungu na katika utii kwa sheria na amri, alimtafuta Mungu wake na kufanya kazi kwa moyo wake wote. Naye hivyo akafanikiwa.