历代志下 21 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

历代志下 21:1-20

1约沙法与祖先同眠后,葬在大卫城他的祖坟里。他儿子约兰继位。

犹大王约兰

2亚撒利雅耶歇撒迦利雅亚撒列夫米迦勒示法提雅约兰的兄弟、犹大约沙法的儿子。 3他们的父亲赐给他们许多金银、财宝和犹大境内的坚城,但将王位赐给了约兰,因为他是长子。 4约兰登基,巩固了王位后,就用刀杀了他所有的兄弟和一些以色列首领。 5约兰三十二岁登基,在耶路撒冷执政八年。 6他与亚哈家一样步以色列诸王的后尘,因为他娶了亚哈的女儿为妻,做耶和华视为恶的事。 7但耶和华不愿毁灭大卫家,因为祂曾与大卫立约,应许让大卫和他的子孙永远做王。

8约兰执政期间,以东人反叛犹大,自己立王。 9约兰率将领及所有战车前去讨伐,结果被以东人包围。但他们乘夜突出重围。 10以东人至今仍脱离犹大的统治,立拿人也在那时候叛变了,因为约兰背弃了他祖先的上帝耶和华。 11约兰犹大的山上修建丘坛,引诱耶路撒冷的居民和犹大人与假神苟合。

12以利亚先知写信给约兰说:“你祖先大卫的上帝耶和华这样说,‘因为你没有效法你父亲约沙法,也没有效法犹大亚撒13而是重蹈以色列诸王的覆辙,与亚哈家一样,引诱犹大人和耶路撒冷的居民与假神苟合,还杀了比你好的兄弟。 14因此,耶和华要降大灾祸给你的人民、儿女、妻妾及一切所有。 15你必患严重的肠病,并且日益加重,直到你的肠子掉出来。’”

16耶和华驱使非利士人和古实附近的阿拉伯人攻打约兰17他们起兵攻打犹大,侵入境内,掳走了王宫里的所有财物以及约兰的儿子和妻妾,只留下他最小的儿子约哈斯

18这事以后,耶和华使约兰患了无法医治的肠病, 19日益加重,两年后肠子掉了出来,他痛苦地死去了。他的百姓没有像对待他祖先那样向他焚火致哀。 20约兰三十二岁登基,在耶路撒冷执政八年。他死后无人向他致哀。他葬在大卫城,但没有葬在王陵里。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Nyakati 21:1-20

Yehoramu Atawala

(2 Wafalme 8:17-24)

121:1 1Nya 3:11Yehoshafati akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Mwanawe Yehoramu akawa mfalme baada yake. 2Ndugu zake Yehoramu, wana wa Yehoshafati walikuwa: Azaria, Yehieli, Zekaria, Azaria, Mikaeli na Shefatia. Hawa wote walikuwa wana wa Yehoshafati mfalme wa Israeli21:2 Yaani Yuda. 321:3 2Nya 11:23; 11:10Baba yao alikuwa amewapa zawadi nyingi za fedha na dhahabu na vitu vya thamani, pamoja na miji yenye ngome huko Yuda, bali ufalme akampa Yehoramu kwa sababu alikuwa mwanawe mzaliwa wa kwanza.

421:4 1Fal 2:12; Amu 9:5; Mwa 4:8; 1Yn 3:12Baada ya Yehoramu kujiimarisha katika ufalme wa baba yake, akawaua kwa upanga ndugu zake wote pamoja na baadhi ya wakuu wa Israeli. 5Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka minane. 621:6 1Fal 12:28-30; 2Nya 18:1; 22:3; Neh 13:26; 2Fal 8:18Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa imefanya, kwa kuwa alimwoa binti wa Ahabu. Akatenda maovu machoni pa Bwana. 721:7 2Sam 7:13-15; 2Nya 23:3; 2Sam 21:17; 2Fal 8:19; 1Fal 11:36; Za 132:11Hata hivyo, kwa sababu ya Agano ambalo Bwana alikuwa amefanya na Daudi, Bwana hakuwa radhi kuangamiza nyumba ya Daudi. Mungu alikuwa ameahidi kuidumisha taa kwa ajili yake na wazao wake milele.

821:8 2Nya 20:22-23; Mwa 27:40; 2Fal 8:20; 9:22; Za 106:39; Ufu 17:1-5Wakati wa Yehoramu, Edomu waliasi dhidi ya Yuda na kujiwekea mfalme wao wenyewe. 9Basi Yehoramu akaenda huko pamoja na maafisa wake na magari yake ya vita. Waedomu wakamzunguka yeye na majemadari wake wa magari yake ya vita, lakini akaondoka, akapenya usiku na kuwashambulia Waedomu. 1021:10 Hes 33:20; Mwa 27:40Hadi leo Edomu wameasi dhidi ya Yuda.

Libna pia wakaasi wakati huo huo kwa sababu Yehoramu alikuwa amemwacha Bwana, Mungu wa baba zake. 1121:11 Law 17:7; 20:5Alikuwa pia ametengeneza mahali pa juu pa kuabudia miungu katika vilima vya Yuda na akawa amewasababisha watu wa Yerusalemu kufanya uzinzi na akawa amewapotosha watu wa Yuda.

1221:12 Kut 34:13; 1Fal 22:4321:12 2Fal 1:16-17; 2Nya 17:3-6; 14:2Yehoramu akapokea barua kutoka kwa nabii Eliya iliyosema:

“Hili ndilo Bwana, Mungu wa Daudi baba yako, asemalo: ‘Hukuenenda katika njia za Yehoshafati baba yako au za Asa mfalme wa Yuda. 1321:13 1Fal 16:29-33; 2:32; Kut 34:15; 2Fal 9:22Lakini umeenenda katika njia za wafalme wa Israeli, nawe umewaongoza Yuda na watu wa Yerusalemu kuzini, kama vile nyumba ya Ahabu ilivyofanya. Pia umewaua ndugu zako mwenyewe, watu wa nyumbani mwa baba yako, watu waliokuwa bora kuliko wewe. 14Hivyo basi Bwana yu karibu kuwapiga watu wako, wanao, wake zako na kila kitu kilicho chako, kwa pigo zito. 1521:15 Hes 12:10Wewe mwenyewe utaugua sana kwa ugonjwa wa tumbo kwa muda mrefu, hadi ugonjwa utakaposababisha matumbo yako kutoka nje.’ ”

1621:16 2Nya 22:1; 26:7; 2Sam 24:1; 1Fal 11:14, 23Bwana akaamsha chuki ya Wafilisti na ya Waarabu walioishi karibu na Wakushi dhidi ya Yehoramu. 1721:17 2Fal 12:18; 2Nya 24:7; Yoe 3:5Wakaishambulia Yuda, wakaivamia na kuchukua mali zote zilizopatikana katika jumba la mfalme pamoja na wanawe na wake zake. Hakubakiziwa mwana yeyote isipokuwa Ahazia aliyekuwa mdogo wa wote.

18Baada ya mambo haya yote, Bwana akampiga Yehoramu kwa ugonjwa usioponyeka wa matumbo. 1921:19 2Nya 16:14Ikawa baada ya muda, mwisho wa mwaka wa pili, matumbo yake yakatoka nje kwa sababu ya ugonjwa, naye akafa katika maumivu makali sana. Watu wake hawakuwasha moto kwa heshima yake, kama walivyokuwa wamewafanyia baba zake.

2021:20 2Nya 33:20; Yer 22:18, 28Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipokuwa mfalme, naye akatawala huko Yerusalemu miaka minane. Akafa, bila kusikitikiwa na mtu yeyote, naye akazikwa katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme.