历代志上 6 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

历代志上 6:1-81

利未的后裔

1利未的儿子是革顺哥辖米拉利2哥辖的儿子是暗兰以斯哈希伯仑乌薛3暗兰的儿子是亚伦摩西,女儿是米利暗亚伦的儿子是拿答亚比户以利亚撒以他玛4以利亚撒非尼哈非尼哈亚比书5亚比书布基布基乌西6乌西西拉希雅西拉希雅米拉约7米拉约亚玛利雅亚玛利雅亚希突8亚希突撒督撒督亚希玛斯9亚希玛斯亚撒利雅亚撒利雅约哈难10约哈难亚撒利雅——这亚撒利雅耶路撒冷所罗门建的圣殿里任祭司, 11亚撒利雅亚玛利雅亚玛利雅亚希突12亚希突撒督撒督沙龙13沙龙希勒迦希勒迦亚撒利雅14亚撒利雅西莱雅西莱雅约萨答15在耶和华借尼布甲尼撒掳掠犹大耶路撒冷人的时候,约萨答也一起被掳去了。

16利未的儿子是革顺哥辖米拉利17革顺的儿子一个叫立尼,一个叫示每18哥辖的儿子是暗兰以斯哈希伯仑乌薛19米拉利的儿子是抹利姆示。以上是利未人按宗族分的各家族。

20革顺的儿子是立尼立尼的儿子是雅哈雅哈的儿子是薪玛21薪玛的儿子是约亚约亚的儿子是易多易多的儿子是谢拉谢拉的儿子是耶特赖

22哥辖的儿子是亚米拿达亚米拿达的儿子是可拉可拉的儿子是亚惜23亚惜的儿子是以利加拿以利加拿的儿子是以比雅撒以比雅撒的儿子是亚惜24亚惜的儿子是他哈他哈的儿子是乌列乌列的儿子是乌西雅乌西雅的儿子是少罗25以利加拿的儿子是亚玛赛亚希摩26亚希摩的儿子是以利加拿以利加拿的儿子是琐菲琐菲的儿子是拿哈27拿哈的儿子是以利押以利押的儿子是耶罗罕耶罗罕的儿子是以利加拿以利加拿的儿子是撒母耳28撒母耳的长子是约珥,次子是亚比亚29米拉利的儿子是抹利抹利的儿子是立尼立尼的儿子是示每示每的儿子是乌撒30乌撒的儿子是示米亚示米亚的儿子是哈基雅哈基雅的儿子是亚帅雅

圣殿的歌乐手

31约柜安放在耶和华的殿中之后,大卫便派人在那里负责歌乐。 32他们按班次在会幕供职,一直到所罗门耶路撒冷建造了耶和华的殿。 33以下是负责歌乐的人及其后代:

哥辖的后代有希幔希幔约珥的儿子,约珥撒母耳的儿子, 34撒母耳以利加拿的儿子,以利加拿耶罗罕的儿子,耶罗罕以列的儿子,以列陀亚的儿子, 35陀亚苏弗的儿子,苏弗以利加拿的儿子,以利加拿玛哈的儿子,玛哈亚玛赛的儿子, 36亚玛赛以利加拿的儿子,以利加拿约珥的儿子,约珥亚撒利雅的儿子,亚撒利雅西番雅的儿子, 37西番雅他哈的儿子,他哈亚惜的儿子,亚惜以比雅撒的儿子,以比雅撒可拉的儿子, 38可拉以斯哈的儿子,以斯哈哥辖的儿子,哥辖利未的儿子,利未以色列的儿子。 39希幔的族兄和助手亚萨比利迦的儿子,比利迦示米亚的儿子, 40示米亚米迦勒的儿子,米迦勒巴西雅的儿子,巴西雅玛基雅的儿子, 41玛基雅伊特尼的儿子,伊特尼谢拉的儿子,谢拉亚大雅的儿子, 42亚大雅以探的儿子,以探薪玛的儿子,薪玛示每的儿子, 43示每雅哈的儿子,雅哈革顺的儿子,革顺利未的儿子。 44希幔亚萨的族兄和助手有米拉利的后代以探以探基示的儿子,基示亚伯底的儿子,亚伯底玛鹿的儿子, 45玛鹿哈沙比雅的儿子,哈沙比雅亚玛谢的儿子,亚玛谢希勒迦的儿子, 46希勒迦暗西的儿子,暗西巴尼的儿子,巴尼沙麦的儿子, 47沙麦末力的儿子,末力姆示的儿子,姆示米拉利的儿子,米拉利利未的儿子。 48希幔亚萨的同族弟兄利未人都奉派到会幕——上帝的殿中担任各种职务。

49亚伦和他的后代在祭坛和香坛上献祭烧香,负责至圣所里的各种工作,为以色列人赎罪,正如上帝的仆人摩西的吩咐。 50以下是亚伦的后代:以利亚撒非尼哈亚比书51布基乌西西拉希雅52米拉约亚玛利雅亚希突53撒督亚希玛斯

利未人住的地方

54以下是哥辖族人亚伦的后代分到的地方:

他们抽中第一签, 55得到了犹大境内的希伯仑城及其周围的草场, 56但城外的田地和村庄分给了耶孚尼的儿子迦勒57亚伦的子孙得到避难城希伯仑立拿及其周围的草场、雅提珥以实提莫及其周围的草场、 58希仑底璧59亚珊伯·示麦及这些城邑周围的草场。 60他们还得到了便雅悯支派的迦巴阿勒篾亚拿突及这些城邑周围的草场。他们各宗族所得的城邑共十三座。

61哥辖族其余的人从玛拿西半个支派中抽签分到了十座城。 62革顺各宗族的人从以萨迦亚设拿弗他利支派以及玛拿西支派的巴珊地区分到了十三座城。 63米拉利各宗族的人从吕便迦得西布伦支派抽签分到十二座城。 64以色列人把这些城邑及其周围的草场分给了利未人。 65以上提到的犹大西缅便雅悯支派的城邑也是用抽签的方式分给他们的。 66哥辖的一些宗族从以法莲支派分到城邑, 67其中有以法莲山区的避难城示剑及其周围的草场,还有基色68约缅伯·和仑69亚雅仑迦特·临门及这些城邑周围的草场。 70哥辖族其余的人从玛拿西半个支派中得到了亚乃比连城及其周围的草场。 71革顺族从玛拿西半个支派中得到了巴珊哥兰及其周围的草场,亚斯她录及其周围的草场。 72他们从以萨迦支派得到了基低斯大比拉73拉末亚念及这些城邑周围的草场。 74他们从亚设支派得到了玛沙押顿75户割利合及这些城邑周围的草场。 76他们从拿弗他利支派得到了加利利基低斯哈们基列亭及这些城邑周围的草场。 77米拉利族的人从西布伦支派得到了临摩挪他泊城及其周围的草场; 78约旦河东岸、耶利哥对面的吕便支派得到了旷野中的比悉雅哈撒79基底莫米法押及这些城邑的草场; 80迦得支派得到了基列拉末及其周围的草场、玛哈念81希实本雅谢及这些城邑周围的草场。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Nyakati 6:1-81

Wana Wa Lawi

16:1 Mwa 29:34; Kut 6:16Wana wa Lawi walikuwa:

Gershoni, Kohathi na Merari.

2Wana wa Kohathi walikuwa:

Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

36:3 Law 10:1–20:2; Kut 6:23; 24:1Amramu alikuwa na wana:

Aroni, Mose, na Miriamu.

Aroni alikuwa na wana:

Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

4Eleazari akamzaa Finehasi,

Finehasi akamzaa Abishua,

5Abishua akamzaa Buki,

Buki akamzaa Uzi,

6Uzi akamzaa Zerahia,

Zerahia akamzaa Merayothi,

7Merayothi akamzaa Amaria,

Amaria akamzaa Ahitubu,

86:8 2Sam 15:27; Ezr 7:2; 2Sam 8:17Ahitubu akamzaa Sadoki,

Sadoki akamzaa Ahimaasi,

9Ahimaasi akamzaa Azaria,

Azaria akamzaa Yohanani,

106:10 1Fal 6:1; 2Nya 3:1; 26:17-18Yohanani akamzaa Azaria (ndiye alifanya kazi ya ukuhani katika Hekalu alilojenga Mfalme Solomoni huko Yerusalemu),

116:11 Ezr 7:3Azaria akamzaa Amaria,

Amaria akamzaa Ahitubu,

12Ahitubu akamzaa Sadoki,

Sadoki akamzaa Shalumu,

136:13 2Fal 22:5-20; 2Nya 35:8Shalumu akamzaa Hilkia,

Hilkia akamzaa Azaria,

146:14 Ezr 2:2; Neh 11:11Azaria akamzaa Seraya,

Seraya akamzaa Yehosadaki.

156:15 2Fal 25:18; Zek 6:11; 2Nya 36:17-21Yehosadaki alihamishwa wakati Bwana aliwapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Mfalme Nebukadneza.

166:16 Mwa 29:34; Kut 6:16; Hes 26:57Wana wa Lawi walikuwa:

Gershoni, Kohathi na Merari.

17Haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni:

Libni na Shimei.

18Wana wa Kohathi walikuwa:

Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

196:19 Mwa 46:11; 1Nya 23:21; Hes 3:33Wana wa Merari walikuwa:

Mahli na Mushi.

Zifuatazo ni koo za Walawi zilizoorodheshwa kufuatana na baba zao:

20Wazao wa Gershoni:

Gershoni akamzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi,

Yahathi akamzaa Zima, 216:21 1Nya 6:41-42Zima akamzaa Yoa,

Yoa akamzaa Ido, Ido akamzaa Zera,

Zera akamzaa Yeatherai.

226:22 Kut 6:24Wazao wa Kohathi:

Kohathi akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Kora,

Kora akamzaa Asiri, 23Asiri akamzaa Elikana,

Elikana akamzaa Ebiasafu, Ebiasafu akamzaa Asiri,

246:24 1Nya 15:5Asiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli,

Urieli akamzaa Uzia, Uzia akamzaa Shauli.

25Wazao wa Elikana walikuwa:

Amasai na Ahimothi,

26Ahimothi akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Sofai,

Sofai akamzaa Nahathi, 276:27 1Sam 1:1; 1:20Nahathi akamzaa Eliabu,

Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elikana,

Elikana akamzaa Samweli.

286:28 1Nya 6:33; 1Sam 8:2Wana wa Samweli walikuwa:

Yoeli mzaliwa wake wa kwanza,

na Abiya mwanawe wa pili.

29Wafuatao ndio wazao wa Merari:

Merari akamzaa Mahli, Mahli akamzaa Libni,

Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza,

30Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia,

Hagia akamzaa Asaya.

Waimbaji Wa Hekalu

316:31 2Nya 29:25-26; Neh 12:45; Ezr 3:10; Za 68:29; 1Nya 16:1; 2Sam 6:17; 1Fal 8:4Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Bwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. 32Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

336:33 1Fal 4:31; 1Nya 15:17; Mit 28Wafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao:

Kutoka ukoo wa Kohathi walikuwa:

Hemani, mpiga kinanda,

alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli,

346:34 1Sam 1:1mwana wa Elikana, mwana wa Yerohamu,

mwana wa Elieli, mwana wa Toa,

35mwana wa Sufu, mwana wa Elikana,

mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai,

36mwana wa Elikana, mwana wa Yoeli,

mwana wa Azaria, mwana wa Sefania,

376:37 Kut 6:24mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri,

mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora,

386:38 Kut 6:21mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi,

mwana wa Lawi, mwana wa Israeli;

396:39 2Nya 29:13; Neh 11:17; 1Nya 15:17na msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume:

Asafu mwana wa Berekia, mwana wa Shimea,

40mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya,

mwana wa Malkiya, 41mwana wa Ethni,

mwana wa Zera, mwana wa Adaya,

42mwana wa Ethani, mwana wa Zima,

mwana wa Shimei, 43mwana wa Yahathi,

mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.

44Na kutoka kwa walioshirikiana nao, Wamerari, mkono wake wa kushoto:

Ethani mwana wa Kishi, mwana wa Abdi,

mwana wa Maluki, 45mwana wa Hashabia,

mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia,

46mwana wa Amsi, mwana wa Bani,

mwana wa Shemeri, 47mwana wa Mahli,

mwana wa Mushi, mwana wa Merari,

mwana wa Lawi.

486:48 1Nya 23:32Ndugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu. 496:49 Kut 27:1-8; 30:1-7, 10; 2Nya 26:18; Kut 29:38; Hes 3:10; 18:7; Ebr 5:1; 1Sam 2:28; 1Nya 23:13Lakini Aroni na uzao wake ndio waliokuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Mose mtumishi wa Mungu.

506:50 Kut 6:23; Hes 3; 2; 26:60; 1Nya 24:1; Ezr 7:2-5Hawa ndio waliokuwa wazao wa Aroni:

Aroni akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi,

Finehasi akamzaa Abishua, 51Abishua akamzaa Buki,

Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Zerahia,

52Zerahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria,

Amaria akamzaa Ahitubu, 536:53 2Sam 8:17Ahitubu akamzaa Sadoki,

Sadoki akamzaa Ahimaasi.

546:54 Hes 31:10; 35:1-9; Yos 21:9-19Zifuatazo ni sehemu walizopewa ziwe nchi yao kwa ajili ya makazi yao (walipewa wazao wa Aroni waliotoka katika ukoo wa Wakohathi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):

556:55 Yos 21:11-12Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda pamoja na sehemu ya malisho inayouzunguka. 566:56 Yos 14:13; 15:13Lakini mashamba pamoja na vijiji vilivyouzunguka mji alipewa Kalebu mwana wa Yefune.

576:57 Hes 33:20; Yos 15:48; 21:13Kwa hiyo wazao wa Aroni walipewa miji ifuatayo pamoja na eneo la malisho: Hebroni (mji wa makimbilio), Libna, Yatiri, Eshtemoa, 586:58 Yos 10:42Hileni, Debiri, 596:59 Yos 15:42; 21:16Ashani, Yuta na Beth-Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho. 606:60 Yer 1:1Kutoka kabila la Benyamini walipewa Gibeoni, Geba, Alemethi na Anathothi, pamoja na maeneo yake ya malisho.

Miji hii kumi na mitatu iligawanywa miongoni mwa koo za Wakohathi.

61Wazao waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za nusu ya kabila la Manase.

62Wazao wa Gershoni, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na mitatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.

636:63 Yos 21:7, 34Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.

646:64 Hes 35:1-8; Yos 21:3, 41-42Kwa hiyo Waisraeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yake ya malisho. 65Kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini walipewa miji iliyotajwa hapo juu.

66Baadhi ya koo za Wakohathi walipewa kama nchi yao miji kutoka kabila la Efraimu.

676:67 Yos 10:33; Mwa 33:19; Yos 21:21Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji wa makimbilio) na Gezeri, 686:68 1Fal 4:12; Yos 10:10Yokmeamu, Beth-Horoni, 696:69 Yos 10:12; 19:45Aiyaloni na Gath-Rimoni, pamoja na maeneo yake ya malisho.

70Kutoka nusu ya kabila la Manase, Waisraeli waliwapa koo za Wakohathi waliobaki miji ya Aneri na Bileamu pamoja na maeneo yake ya malisho.

716:71 1Nya 23:7; Yos 20:8; 21:27Wagershoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho:

Katika nusu ya kabila la Manase:

walipewa Golani katika Bashani na pia Ashtarothi.

726:72 Yos 19:12Kutoka kabila la Isakari

walipokea Kedeshi, Daberathi, 73Ramothi na Anemu, pamoja na maeneo yake ya malisho.

746:74 Yos 19:28Kutoka kabila la Asheri

walipokea Mashali, Abdoni, 756:75 Yos 19:34; Hes 13:21Hukoki na Rehobu, pamoja na maeneo yake ya malisho.

76Kutoka kabila la Naftali

walipokea Kedeshi katika Galilaya, Hamoni na Kiriathaimu pamoja na maeneo yake ya malisho.

77Wamerari (Walawi waliobakia) walipokea miji ifuatayo:

kutoka kabila la Zabuloni

walipokea Yokneamu, Karta, Rimoni na Tabori pamoja na maeneo yake ya malisho.

786:78 Yos 20:8Kutoka kabila la Reubeni, ngʼambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko

walipokea Bezeri ulioko jangwani, Yahasa, 796:79 Kum 2:26Kedemothi na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho.

806:80 Yos 20:8; Mwa 32:2Na kutoka kabila la Gadi

walipokea Ramothi huko Gileadi, Mahanaimu, 816:81 Hes 21:32; 2Nya 11:14; Kum 2:24; Yos 13:10; Isa 15:4; Yer 48:34Heshboni na Yazeri, pamoja na maeneo yake ya malisho.