创世记 9 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

创世记 9:1-29

上帝与挪亚立约

1上帝赐福给挪亚和他的儿子们,对他们说:“你们要生养众多,遍布地面。 2你们要管理所有地上的走兽、空中的飞鸟、地上的爬虫和海里的鱼,它们都必惧怕你们。 3凡是活着的动物都可作你们的食物,就像菜蔬和谷物一样。 4只是你们不可吃带血的肉,因为血就是生命。 5凡是杀人害命的,无论人或兽,我必向他们追讨血债。凡杀人的,我必追讨他的血债。 6凡杀害人的,也必被人杀害,因为人是上帝照着自己的形象造的。 7你们要生养众多,使地上人口兴旺。”

8上帝又对挪亚和他的儿子们说: 9“我要跟你们和你们的后代, 10以及所有和你们在一起、从方舟出来的飞禽走兽和牲畜等各种动物立约。 11我与你们立约,不再叫洪水淹没一切生灵,也不再让洪水毁灭大地。” 12上帝说:“我与你们及各种生灵立世代永存的约,我要给这个约一个记号。 13我把彩虹放在云中,作为我跟大地立约的记号。 14我使云彩覆盖大地的时候,会有彩虹在云中出现。 15这样我会记得我与你们及一切生灵所立的约,水就不会再泛滥淹灭所有生灵。 16当我看见彩虹在云中出现的时候,就会记得我与地上一切生灵立的永约。” 17上帝对挪亚说:“彩虹是我与地上一切生灵立约的记号。”

挪亚和他的儿子

18挪亚一起出方舟的有他的儿子雅弗迦南的父亲。 19挪亚这三个儿子的后代遍布天下。

20挪亚做了农夫,他是第一个栽种葡萄园的人。 21一天,他喝葡萄酒喝醉了,赤裸着身体躺在帐篷里。 22迦南的父亲看见他父亲赤身露体,便去告诉外面的两个弟兄。 23于是,雅弗拿了一件衣服搭在肩上,倒退着走进帐篷,把衣服盖在父亲身上,他们背着脸不看父亲赤裸的身体。

24挪亚酒醒后,知道了小儿子做的事, 25就说:

迦南该受咒诅,

必做他弟兄的仆人的仆人。”

26又说:

的上帝耶和华当受称颂!

迦南要做的仆人。

27愿上帝扩张雅弗的疆界,

愿他住在的帐篷里,

迦南做他的仆人。”

28洪水以后,挪亚又活了三百五十年。 29挪亚一生共活了九百五十岁。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 9:1-29

Mungu Aweka Agano Na Noa

19:1 Mwa 1:22Ndipo Mungu akambariki Noa na wanawe, akiwaambia, “Zaeni mkaongezeke kwa idadi na mkaijaze tena dunia. 29:2 Mwa 1:26Wanyama wote wa duniani, ndege wote wa angani, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi, na samaki wote wa baharini wamekabidhiwa mikononi mwenu, nao watawaogopa na kuwahofu. 39:3 Mwa 1:29; Kol 2:16; Mdo 10:15Kila kitu chenye uhai kiendacho kitakuwa chakula chenu. Kama vile nilivyowapa mimea mbalimbali, sasa nawapa kila kitu.

49:4 Law 3:17; 7:26; 17:10-14; 19:26; Kum 12:16, 23-25; 15:23; 1Sam 14:33; Eze 33:25; Mdo 15:20, 29“Lakini kamwe msile nyama ambayo bado ina damu ya uhai wake, kwa maana damu ni uhai. 59:5 Mwa 4:10; 42:22; 50:15; 1Fal 2:32; 2Nya 24:22; Za 9:12; Kut 21:28-32Hakika damu ya uhai wenu nitaidai. Nitaidai kutoka kwa kila mnyama. Kutoka kwa kila mwanadamu pia nitaidai kwa ajili ya uhai wa mtu mwenzake.

69:6 Mwa 1:26; 4:14; Amu 9:24; Mt 26:52“Yeyote amwagaye damu ya mwanadamu,

damu yake itamwagwa na mwanadamu,

kwa kuwa katika mfano wa Mungu,

Mungu alimuumba mwanadamu.

79:7 Mwa 1:22; 9:19Kuhusu ninyi, zaeni mwongezeke kwa wingi, mzidi katika dunia na kuijaza.”

8Ndipo Mungu akamwambia Noa na wanawe pamoja naye: 99:9 Mwa 6:18“Sasa mimi ninaweka Agano langu nanyi, pamoja na uzao wenu baada yenu, 10pia na kila kiumbe hai kilichokuwa pamoja nanyi: Ndege, wanyama wa kufugwa na wanyama wote wa porini, wale wote waliotoka katika safina pamoja nanyi, kila kiumbe hai duniani. 119:11 Isa 24:5; 33:8; 54:9; Hos 6:7; Mwa 8:21Ninaweka Agano nanyi: Kamwe uhai hautafutwa tena kwa gharika, kamwe haitakuwepo tena gharika ya kuangamiza dunia.”

129:12 Mwa 17:11-12; Kut 12:14; Law 3:17; 6:18; 17:7; Hes 10:8Mungu akasema, “Hii ni ishara ya Agano ninalofanya kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, Agano kwa vizazi vyote vijavyo: 139:13 Eze 1:28; Ufu 4:3; 10:1Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya Agano nifanyalo kati yangu na dunia. 14Wakati wowote ninapotanda mawingu juu ya dunia na upinde wa mvua ukijitokeza mawinguni, 159:15 Mwa 8:1, 21; Kut 2:24; 6:5; 34:10; Law 26:42-45; Kum 7:9; Za 89:34; 103:18; 105:8; 106:45; Eze 16:60nitakumbuka Agano langu kati yangu na ninyi na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina. Kamwe maji hayatakuwa tena gharika ya kuangamiza uhai wote. 169:16 Mwa 17:7-13, 19; 2Sam 7:13; 23:5; Za 105:9-10; Isa 9:7; 54:10; 55:3; 59:21; 61:8; Yer 31:34; 32:40; 33:21; Eze 16:60; 37:26; Ebr 13:20Wakati wowote upinde wa mvua unapotokea mawinguni, nitauona na kukumbuka Agano la milele kati ya Mungu na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina duniani.”

17Hivyo Mungu akamwambia Noa, “Hii ndiyo ishara ya Agano ambalo nimelifanya kati yangu na viumbe vyote vilivyo hai duniani.”

Wana Wa Noa

189:18 Mwa 5:32; 10:6, 15; Lk 3:36Wana wa Noa waliotoka ndani ya safina ni: Shemu, Hamu na Yafethi. (Hamu ndiye alikuwa baba wa Kanaani.) 199:19 Mwa 5:32; 1:22; 10:32; 11:4-9Hawa ndio waliokuwa wana watatu wa Noa, kutokana nao watu walienea katika dunia.

20Noa akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu. 219:21 Mwa 19:35Alipokunywa huo mvinyo wake akalewa na akalala uchi kwenye hema lake. 229:22 Hab 2:15Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake na kuwaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. 23Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao.

24Noa alipolevuka kutoka kwenye mvinyo wake na kujua lile ambalo mwanawe mdogo kuliko wote alilokuwa amemtendea, 259:25 Mwa 27:12, 29-40; 25:23; 37:10; 49:8; Kut 20:5; Za 79:8; Isa 14:21; Yer 31:29; 32:18; Hes 24:18; Yos 9:23akasema,

“Alaaniwe Kanaani!

Atakuwa mtumwa wa chini sana

kuliko watumwa wote kwa ndugu zake.”

269:26 Mwa 14:20; Kut 18:10; Za 7:17; 1Fal 9:21Pia akasema,

“Abarikiwe Bwana, Mungu wa Shemu!

Kanaani na awe mtumwa wa Shemu.

279:27 Mwa 10:2-5; Efe 2:13-14; 3:6Mungu na apanue mipaka ya Yafethi;

Yafethi na aishi katika mahema ya Shemu,

na Kanaani na awe mtumwa wake.”

28Baada ya gharika Noa aliishi miaka 350. 299:29 Mwa 2:17Noa alikuwa na jumla ya miaka 950, ndipo akafa.