创世记 8 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

创世记 8:1-22

洪水消退

1上帝眷顾挪亚及方舟里的野兽和牲畜,使风吹在大地上,水便开始消退。 2深渊的泉源和天上的水闸都关闭了,大雨也停了。 3地上的洪水慢慢消退,过了一百五十天,水退下去了。 4七月十七日,方舟停在亚拉腊山上。 5水继续消退,到十月一日,山顶都露出来了。

6又过了四十天,挪亚打开方舟的窗户, 7放出一只乌鸦。它一直在空中飞来飞去,直到地上的水都干了。 8后来,挪亚放出一只鸽子,以便了解地面的水是否已经消退。 9但遍地都是水,鸽子找不到歇脚的地方,就飞回了方舟,挪亚伸手把鸽子接进方舟里。 10过了七天,挪亚再把鸽子放出去。 11到了黄昏,鸽子飞回来,嘴里衔着一片新拧下来的橄榄叶,挪亚便知道地上的水已经退了。 12等了七天,他又放出鸽子,这一次,鸽子没有回来。

13挪亚六百零一岁那年的一月一日,地上的水干了。挪亚打开方舟的盖观望,看见地面都干了。 14到了二月二十七日,大地完全干了。 15上帝对挪亚说: 16“你与妻子、儿子和儿媳可以出方舟了。 17你要把方舟里的飞禽走兽及爬虫等所有动物都带出来,让它们在地上多多繁殖。” 18于是,挪亚与妻子、儿子和儿媳都出了方舟。 19方舟里的飞禽走兽和爬虫等所有地上的动物,都按种类出了方舟。

挪亚献祭

20挪亚为耶和华筑了一座坛,在上面焚烧各种洁净的牲畜和飞鸟作为燔祭。 21耶和华闻到这燔祭的馨香,心想:“虽然人从小就心存恶念,但我再不会因为人的缘故而咒诅大地,再不会毁灭一切生灵。 22只要大地尚存,播种收割、夏热冬寒、白昼黑夜必永不停息。”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 8:1-22

Mwisho Wa Gharika

18:1 Mwa 9:15; 19:29; 21:1; 30:22; Kut 2:23-24; Ay 12:15; 14:13; Rut 4:13; Nah 1:4; 1Sam 1:11, 19; 2Fal 20:3; 1Nya 16:15; Neh 1:8; 5:19; 13:11-31; Hes 10:9; Za 66:6; 105:42; 106:4; Lk 1:54, 72; Kut 14:21; Yos 2:10; 3:16; Isa 11:15; 44:27Mungu akamkumbuka Noa na wanyama wote wa porini na wa kufugwa waliokuwa naye ndani ya safina, akatuma upepo ukavuma katika dunia, nayo maji yakaondoka. 28:2 Mwa 7:4, 11Zile chemchemi zilizo chini sana ya ardhi pamoja na malango ya mafuriko ya mbinguni yakawa yamefungwa nayo mvua ikawa imekoma kunyesha kutoka angani. 38:3 Mwa 7:24Maji yakaendelea kupungua taratibu katika nchi. Kunako mwisho wa siku ya 150, maji yalikuwa yamepungua, 48:4 Mwa 7:11, 20; 2Fal 19:37; Yer 51:27katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa saba, safina ikatua katika milima ya Ararati. 5Maji yakaendelea kupungua hadi mwezi wa kumi, na siku ya kwanza ya mwezi wa kumi, vilele vya milima vikaonekana.

6Baada ya siku arobaini Noa akafungua dirisha alilokuwa amelifanya katika safina 78:7 Amu 11:15; Kum 14:14; 1Fal 17:4-6; Ay 38:41; Za 147:9; Mit 30:17; Isa 34:11; Lk 12:24na akamtoa kunguru, akawa akiruka kwenda na kurudi mpaka maji yalipokwisha kukauka juu ya nchi. 88:8 Ay 30:31; Za 55:6; 74:19; Wim 2:12-14; Isa 38:14; 59:11; 60:8; Yer 48:28; Eze 7:16; Nah 2:7; Hos 7:11; 11:11; Mt 3:16; 10:16; Yn 1:32Kisha akamtoa hua ili aone kama maji yameondoka juu ya uso wa ardhi. 9Lakini hua hakupata mahali pa kutua kwa kuwa maji yalienea juu ya uso wa dunia yote, kwa hiyo akarudi kwa Noa ndani ya safina. Noa akanyoosha mkono akamchukua yule hua akamrudisha ndani ya safina. 10Noa akangojea siku saba zaidi kisha akamtoa tena hua kutoka safina. 11Wakati hua aliporejea kwa Noa jioni, alikuwa amechukua katika mdomo wake jani bichi la mzeituni, lililochumwa wakati ule ule! Ndipo Noa akajua ya kuwa maji yameondoka juu ya uso wa dunia. 12Akangojea siku saba zaidi na akamtuma tena hua, lakini wakati huu hua hakurudi tena kwa Noa.

138:13 Mwa 5:32Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza ya mwaka 601, wa kuishi kwake Noa, maji yalikuwa yamekauka duniani. Kisha Noa akafungua mlango wa safina akaona ya kuwa uso wa ardhi ulikuwa umekauka. 148:14 Mwa 7:11Katika siku ya ishirini na saba ya mwezi wa pili dunia ilikuwa imekauka kabisa.

15Ndipo Mungu akamwambia Noa, 168:16 Mwa 7:13“Toka ndani ya safina, wewe na mkeo na wanao na wake zao. 178:17 Mwa 1:22Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe: Ndege, wanyama na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia.”

188:18 1Pet 3:20; 2Pet 2:5Kwa hiyo Noa akatoka nje pamoja na mkewe, wanawe na wake zao. 19Wanyama wote na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi na ndege wote, kila kitu kiendacho juu ya nchi, aina moja baada ya nyingine vikatoka katika safina, kila aina ya kiumbe, kimoja baada ya kingine.

Noa Atoa Dhabihu

208:20 Mwa 12:7-8; 13:18; 22:9; 26:25; 33:20; 35:7; 7:8; 22:2-13; Kut 17:15; 24:4; 10:25; 20:24; 40:29; Ay 42:8; Law 1:3; 4:29; 6:8-13; Hes 6:11; Amu 6:26; 11:31; 1Sam 20:29Kisha Noa akamjengea Bwana madhabahu, akachukua baadhi ya wale wanyama na ndege wote walio safi, akatoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. 218:21 Kut 29:18, 25; Law 1:9, 13; 2:9; 4:31; Hes 15:3, 7; 2Kor 2:15; Mwa 3:17; 6:5; 9:11-15; Yer 17:9; Za 51:5; Mt 15:19; Rum 1:21; Yer 44:11; Isa 54:9Bwana akasikia harufu nzuri ya kupendeza, naye akasema moyoni mwake, “Kamwe sitailaani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, hata ingawa kila mwelekeo wa moyo wake ni mbaya tangu ujana. Kamwe sitaangamiza tena viumbe hai vyote kama nilivyofanya.

228:22 Yos 3:15; Za 67:6; 74:17; Yer 5:24; Zek 14:8; Mwa 1:14“Kwa muda dunia idumupo,

wakati wa kupanda na wa kuvuna,

wakati wa baridi na wa joto,

wakati wa kiangazi na wa masika,

usiku na mchana

kamwe havitakoma.”