创世记 36 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

创世记 36:1-43

以扫的后代

1以下是以扫的后代,即以东的后代。

2以扫娶了迦南女子为妻,她们是以伦的女儿亚大希未祭便的孙女、亚拿的女儿阿何利巴玛3他还娶了以实玛利的女儿、尼拜约的妹妹巴实抹4亚大以扫生了以利法巴实抹生了流珥5阿何利巴玛生了耶乌施雅兰可拉。他们都是以扫的儿子,是在迦南出生的。

6以扫带着他在迦南所得的妻子、儿女和家中所有的人员,以及所有的牲畜和财产离开雅各,迁往别处。 7以扫雅各两家的财产和牲畜太多,那地方不够他们住, 8于是以扫,即以东,搬到了西珥山居住。

9以扫西珥山区以东人的祖先,以下是他的子孙。

10以扫的妻子亚大生了以利法巴实抹生了流珥11以利法的儿子是提幔阿抹洗玻迦坦基纳斯12以利法的妾亭纳为他生了亚玛力,他们都是以扫妻子亚大的子孙。 13流珥的儿子是拿哈谢拉沙玛米撒,他们都是以扫妻子巴实抹的子孙。 14以扫的妻子阿何利巴玛祭便的孙女、亚拿的女儿,她给以扫生了耶乌施雅兰可拉

15以下是以扫子孙中的族长。

以扫的长子以利法的子孙中有提幔族长、阿抹族长、洗玻族长、基纳斯族长、 16可拉族长、迦坦族长、亚玛力族长,他们都是以利法以东的后代,即亚大的子孙。 17以扫的儿子流珥的子孙中有拿哈族长、谢拉族长、沙玛族长、米撒族长,他们都是流珥以东的后代,即以扫的妻子巴实抹的子孙。 18以扫的妻子阿何利巴玛的子孙中有耶乌施族长、雅兰族长和可拉族长。这些都是以扫的妻子、亚拿的女儿阿何利巴玛子孙中的族长。

19这些族长都是以扫的子孙,以扫又名以东

20以下是住在以东境内何利西珥的子孙:罗坍朔巴祭便亚拿21底顺以察底珊。他们都是以东境内何利西珥的子孙中的族长。

22罗坍的儿子是何利希幔罗坍的妹妹是亭纳23朔巴的儿子是亚勒文玛拿辖以巴录示玻阿南24祭便的儿子是亚雅亚拿,在旷野为父亲放驴时发现温泉的就是亚拿25亚拿的儿子名叫底顺、女儿名叫阿何利巴玛26底顺的儿子是欣但伊是班益兰基兰27以察的儿子是辟罕撒番亚干28底珊的儿子是乌斯亚兰

29以下是何利人的族长:罗坍族长、朔巴族长、祭便族长、亚拿族长、 30底顺族长、以察族长、底珊族长。他们是西珥地区何利人各宗族的族长。

31以色列人还没有君王统治之前,在以东做王的人如下: 32比珥的儿子比拉以东做王,定都亭哈巴33比拉死后,波斯拉谢拉的儿子约巴继位。 34约巴死后,提幔地区的户珊继位。 35户珊死后,比达之子哈达继位,定都亚未得,他曾在摩押地区击败米甸人。 36哈达死后,玛士利加桑拉继位。 37桑拉死后,大河边的利河伯扫罗继位。 38扫罗死后,亚革波的儿子巴勒·哈南继位。 39巴勒·哈南死后,哈达继位,定都巴乌,他的妻子名叫米希她别,是米·萨合的孙女、玛特列的女儿。

40以下是按宗族在各地区做族长的以扫的后代:亭纳亚勒瓦耶帖41阿何利巴玛以拉比嫩42基纳斯提幔米比萨43玛基叠以兰。这些人在所住的以东各地做族长。以扫以东人的始祖。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 36:1-43

Wazao Wa Esau

(1 Nyakati 1:34-42)

136:1 Mwa 2:4; 25:30Hivi ndivyo vizazi vya Esau (yaani Edomu).

236:2 Mwa 26:34; 28:8-9Esau akaoa wake kutoka miongoni mwa wanawake wa Kanaani: Ada binti wa Eloni Mhiti, Oholibama binti wa Ana, mjukuu wa kike wa Sibeoni Mhivi, 3pia akaoa Basemathi binti wa Ishmaeli, dada yake Nebayothi.

436:4 1Nya 1:35Ada akamzalia Esau Elifazi, Basemathi akamzaa Reueli, 536:5 1Nya 1:35Oholibama akamzaa Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wana wa Esau waliozaliwa kwake huko Kanaani.

636:6 Mwa 12:5; 1Nya 1:35Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike na wote wa nyumbani mwake, mifugo yake pamoja na wanyama wake wengine wote na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata akiwa Kanaani, akahamia katika nchi iliyo mbali na Yakobo ndugu yake. 736:7 Mwa 13:6; 27:39Mali zao zilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja, nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao. 836:8 Kum 2:4Kwa hiyo Esau (ambaye ni Edomu) aliishi katika nchi ya kilima huko Seiri.

936:9 Mwa 2:4Hawa ndio wazao wa Esau, baba wa Waedomu, katika nchi ya kilima cha Seiri.

1036:10 Mwa 36:3Haya ndiyo majina ya wana wa Esau:

Elifazi, mwana wa Esau ambaye mkewe Ada alimzalia; na Reueli, mwana wa Esau ambaye mkewe Basemathi alimzalia.

1136:11 1Nya 1:45Wana wa Elifazi ni:

Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi.

1236:12 Kut 17:8, 16; 1Sam 15:2Elifazi mwana wa Esau alikuwa pia na suria aliyeitwa Timna, ambaye alimzalia Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Ada mke wa Esau.

1336:13 Mwa 36:3Wana wa Reueli ni:

Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Basemathi mkewe Esau.

1436:14 Mwa 36:2Wana wa Oholibama binti Ana, mkewe Esau, aliyekuwa mjukuu wa Sibeoni, aliomzalia Esau ni:

Yeushi, Yalamu na Kora.

1536:15 Mwa 36:19-40; Kut 15:15Hawa ndio waliokuwa wakuu miongoni mwa wazao wa Esau:

Wakuu wa wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau ni:

Temani, Omari, Sefo, Kenazi, 1636:16 Mwa 32:3Kora, Gatamu na Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wakuu waliotoka kwa Elifazi huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Ada.

1736:17 1Nya 1:37Wakuu wa wana wa Reueli, mwana wa Esau ni:

Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa Reueli huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Basemathi mkewe Esau.

1836:18 Mwa 36:2Wakuu wa wana wa Esau ambao mkewe Oholibama alimzalia ni:

Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa mke wa Esau, Oholibama binti Ana.

1936:19 1Nya 1:35Hawa ndio waliokuwa wana wa Esau (ndiye Edomu), na hawa ndio waliokuwa wakuu wao.

2036:20 Mwa 14:6Hawa ndio walikuwa wana wa Seiri, Mhori, waliokuwa wakiishi katika nchi ile:

Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, 2136:21 Mwa 36:30Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio wana wa Seiri huko Edomu waliokuwa wakuu kwa Wahori.

22Wana wa Lotani walikuwa:

Hori na Homamu. Timna alikuwa dada yake Lotani.

23Wana wa Shobali walikuwa:

Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.

2436:24 Mwa 36:2Wana wa Sibeoni walikuwa:

Aiya na Ana. Huyu Ana ndiye aligundua chemchemi ya maji moto jangwani alipokuwa akichunga punda za Sibeoni baba yake.

2536:25 Mwa 36:2Watoto wa Ana walikuwa:

Dishoni na Oholibama binti wa Ana.

26Wana wa Dishoni walikuwa:

Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.

27Wana wa Eseri walikuwa:

Bilhani, Zaavani na Akani.

28Wana wa Dishani walikuwa:

Usi na Arani.

2936:29 Mwa 36:20Hawa ndio waliokuwa wakuu wa Wahori:

Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, 3036:30 Mwa 36:21Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Wahori, kufuatana na makundi yao, katika nchi ya Seiri.

Watawala Wa Edomu

(1 Nyakati 1:43-54)

3136:31 Mwa 17:6Wafuatao ni wafalme waliotawala Edomu kabla ya mfalme yeyote wa Israeli kutawala:

32Bela mwana wa Beori alikuwa mfalme wa Edomu. Mji wake uliitwa Dinhaba.

3336:33 Isa 34:6Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.

3436:34 Yer 49:7Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.

3536:35 Rut 1:1, 6; Mwa 19:37Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.

36Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.

3736:37 Mwa 26:22Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati akawa mfalme baada yake.

38Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.

39Baal-Hanani mwana wa Akbori alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu.

4036:40 Mwa 36:15Hawa ndio wakuu waliotokana na Esau, kwa majina, kufuatana na koo zao na nchi zao:

Timna, Alva, Yethethi, 41Oholibama, Ela, Pinoni, 42Kenazi, Temani, Mibsari, 4336:43 Mwa 36:9Magdieli na Iramu. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Edomu, kufuatana na makazi yao katika nchi waliyoimiliki.

Huyu ndiye alikuwa Esau, baba wa Waedomu.