列王纪下 22 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

列王纪下 22:1-20

约西亚做犹大王

1约西亚八岁登基,在耶路撒冷执政三十一年。他母亲叫耶底大,是波斯加亚大雅的女儿。 2约西亚做耶和华视为正的事,事事效法他祖先大卫,不偏不离。

发现律法书

3约西亚执政第十八年,他派米书兰的孙子、亚萨利的儿子沙番书记去耶和华的殿,并吩咐他说: 4“你去见大祭司希勒迦,让他清点奉献到耶和华殿中的银子,那些银子是殿门守卫从民众收集来的。 5-6然后把银子交给负责修理耶和华殿的督工,他们就可以购买木料和凿好的石头,雇用木匠、建筑工人和石匠来修理耶和华的殿。 7你不用查核他们的账目,因为他们都是忠诚可靠的人。”

8大祭司希勒迦告诉书记沙番说:“我在耶和华的殿里找到了律法书。”希勒迦把书交给沙番看。 9沙番禀告王说:“你的臣仆已经把殿里的银子清点完毕,交给了殿里的督工和工人。” 10他又告诉王:“希勒迦祭司给了我一卷书。”沙番就在王面前诵读这书。 11王听了律法书上的话,就撕裂衣服, 12吩咐希勒迦祭司、沙番的儿子亚希甘米该亚的儿子亚革波、书记沙番和王的臣仆亚撒雅13“你们为我、为民众和整个犹大去求问耶和华有关这书卷上的话。耶和华的烈怒已经临到我们身上,因为我们的祖先没有遵守这书卷上的话,没有遵行这书卷上的吩咐。”

户勒妲的预言

14于是,希勒迦祭司、亚希甘亚革波沙番亚撒雅去求问女先知户勒妲。她是负责管理礼服的沙龙的妻子,沙龙哈珥哈斯的孙子、特瓦的儿子。户勒妲住在耶路撒冷第二区。他们向她说明来意。 15她对他们说:“以色列的上帝耶和华要你们回去告诉差你们来见我的人, 16耶和华说,‘我要照犹大王所读的那书上的一切话,降灾难给这地方及这里的居民。 17因为他们背弃我,给别的神明烧香,制造偶像惹我发怒,我的怒火要在这地方燃烧,绝不止息。 18你们告诉差你们来求问耶和华的犹大王,至于你所听见的那些话,以色列的上帝耶和华说, 19因为你听到我对这地方及其居民的警告,知道这地方要受咒诅、沦为荒场,便悔改,在我面前谦卑,撕裂衣服,向我哭泣。因此,我垂听了你的祷告。这是我耶和华说的。 20我会让你平安入土到你祖先那里。你不会看到我要降给这地方的一切灾难。’”他们便回去禀告王。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Wafalme 22:1-20

Yosia Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 34; 35:20-27)

122:1 Yer 1:2; Yos 15:39Yosia alikuwa na miaka minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka thelathini na mmoja. Mama yake aliitwa Yedida binti Adaya, kutoka Boskathi. 222:2 Kum 5:32Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana na kuenenda katika njia zote za Daudi baba yake. Hakugeuka upande wa kuume wala wa kushoto.

322:3 2Nya 34:20; Yer 39:14Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wake, Mfalme Yosia akamtuma mwandishi Shafani mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu, kwenda katika Hekalu la Bwana. Akasema: 422:4 Ezr 7:1; 2Fal 12:4-5“Panda uende kwa Hilkia, kuhani mkuu, umwambie ahesabu zile fedha ambazo zimeletwa katika Hekalu la Bwana, ambazo mabawabu wamekusanya kutoka kwa watu. 522:5 2Fal 12:5Waambie waikabidhi kwa watu walioteuliwa kusimamia kazi ya Hekalu. Waamuru watu hawa wawalipe wafanyakazi ambao wanakarabati Hekalu la Bwana: 622:6 2Fal 12:11-12wale maseremala, wajenzi na waashi. Waambie pia wanunue mbao na mawe yaliyochongwa ili kukarabati Hekalu. 722:7 2Fal 12:15Lakini hawahitajiki kutoa hesabu ya fedha walizokabidhiwa, kwa sababu wanafanya kwa uaminifu.”

822:8 Kum 31:24; Gal 3:10Hilkia kuhani mkuu akamwambia Shafani mwandishi, “Nimekipata Kitabu cha Sheria ndani ya Hekalu la Bwana.” Akampa Shafani, ambaye alikisoma. 9Kisha Shafani mwandishi akamwendea mfalme na kumpa taarifa akisema: “Maafisa wako wametoa ile fedha ambayo ilikuwa ndani ya Hekalu la Bwana na imekabidhiwa mikononi mwa wasimamizi wa marekebisho ya Hekalu.” 1022:10 Yer 36:21Ndipo Shafani mwandishi akampasha mfalme habari kwamba: “Hilkia kuhani amenipa kitabu hiki.” Naye Shafani akakisoma kile kitabu mbele ya mfalme.

11Mfalme aliposikia maneno ya kile Kitabu cha Sheria, akararua mavazi yake. 1222:12 2Fal 25:22; Isa 8:14Akatoa maagizo haya kwa Hilkia kuhani, Ahikamu mwana wa Shafani, Akbori mwana wa Mikaya, Shafani mwandishi, na Asaya mtumishi wa mfalme: 1322:13 Kum 29:24-28; Amo 2:4“Nendeni mkamuulize Bwana kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu na Yuda wote kuhusu yale yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki ambacho kimepatikana. Hasira ya Bwana ni kubwa inayowaka dhidi yetu kwa sababu baba zetu hawakuyatii maneno ya kitabu hiki. Hawajatenda kulingana na yale yote yaliyoandikwa humo kutuhusu sisi.”

1422:14 Kut 15:20Hilkia kuhani, Ahikamu, Akbori, Shafani na Asaya wakaenda kuongea na nabii mke Hulda, ambaye alikuwa mke wa Shalumu mwana wa Tikwa, mwana wa Harhasi mtunzaji wa chumba cha mavazi. Hulda aliishi Yerusalemu katika Mtaa wa Pili.

15Akawaambia, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana, Mungu wa Israeli: Mwambieni yule mtu aliyewatuma ninyi kwangu, 1622:16 Yos 23:15; Dan 9:11‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana: Nitaleta maafa juu ya mahali hapa na watu wake, kulingana na kila kitu kilichoandikwa katika kitabu hicho mfalme wa Yuda alichosoma. 1722:17 1Fal 9:9Kwa sababu wameniacha mimi na kufukiza uvumba kwa miungu mingine, na kunighadhibisha kwa sanamu zote zilizotengenezwa kwa mikono yao, hasira yangu itawaka dhidi ya mahali hapa, wala haitatulizwa.’ 1822:18 Yer 21:2Mwambieni mfalme wa Yuda, ambaye amewatuma kumuuliza Bwana, ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana, Mungu wa Israeli, kuhusu maneno uliyoyasikia: 1922:19 Isa 37:15; Yer 26:6; Law 26:31Kwa kuwa moyo wako ulikuwa msikivu na ulijinyenyekeza mbele za Bwana uliposikia kile nilichosema dhidi ya mahali hapa na watu wake, kwamba wangelaaniwa na kuachwa ukiwa, basi kwa sababu uliyararua mavazi yako na kulia mbele zangu, nimekusikia, asema Bwana. 2022:20 Isa 47:11; 1Fal 21:29Kwa hiyo nitakukusanya kwa baba zako, nawe utazikwa kwa amani. Macho yako hayataona maafa yote nitakayoleta juu ya mahali hapa.’ ”

Basi wakapeleka jibu lake kwa mfalme.