列王纪下 16 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

列王纪下 16:1-20

亚哈斯做犹大王

1利玛利的儿子比加执政第十七年,犹大约坦的儿子亚哈斯登基。 2他二十岁登基,在耶路撒冷统治十六年。他没有效法他祖先大卫做耶和华视为正的事, 3反而步以色列诸王的后尘,效法耶和华在以色列人面前赶走的外族人的可憎行径,把自己的儿子焚烧献作祭物。 4他在丘坛、山冈和绿树下献祭烧香。

5亚兰利汛利玛利的儿子以色列比加前来攻打耶路撒冷,围住亚哈斯,但屡攻不下。 6当时,亚兰利汛收复以拉他,赶走城内的犹大人。亚兰人至今居住在那里。 7亚哈斯差遣使者去见亚述提革拉·毗列色,对他说:“我是你的仆人、你的儿子,现在亚兰王和以色列王攻打我,求你从他们手中拯救我。” 8亚哈斯把耶和华殿里和王宫库房里的金银送给亚述王。 9亚述王答应了他,起兵攻陷大马士革,杀了利汛,把城中的居民掳到吉珥

10亚哈斯王在大马士革亚述提革拉·毗列色的时候,看到一座坛,便派人将坛的模型和详细的制造方法送到乌利亚祭司那里。 11乌利亚祭司按照送来的模型,在亚哈斯王返回之前建造了一座坛。 12王从大马士革回来,看见那座坛,就到上面献祭。 13他在上面献上燔祭、素祭和奠祭,又将平安祭祭牲的血洒在坛上。 14他把献给耶和华的铜坛从耶和华的殿前搬到新坛的北边,铜坛原来放在殿和新坛之间。 15他吩咐乌利亚祭司:“要在这座大坛上献早晨的燔祭、晚上的素祭,王的燔祭、素祭,国中民众的燔祭、素祭和奠祭,燔祭牲和平安祭牲的血也要洒在上面,但铜坛要供我个人求问之用。” 16乌利亚祭司遵命而行。

17亚哈斯王拆掉盆座的镶板,搬走盆,将铜海从铜牛背上搬下来,放在铺石的地上。 18为了亚述王,他挪走耶和华殿里为安息日而盖的走廊,封闭了王从外面进耶和华殿的入口。

19亚哈斯其他的事都记在犹大的列王史上。 20亚哈斯与祖先同眠后,葬在大卫城他的祖坟里。他儿子希西迦继位。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Wafalme 16:1-20

Ahazi Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 28)

116:1 Isa 1:1; Hos 1:1Katika mwaka wa kumi na saba wa utawala wa Peka mwana wa Remalia, Ahazi mwana wa Yothamu mfalme wa Yuda alianza kutawala. 2Ahazi alikuwa na miaka ishirini alipoanza kutawala, akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na sita. Tofauti na Daudi baba yake, hakufanya yaliyo mema machoni pa Bwana, Mungu wake. 316:3 Law 18:21; Kum 9:4Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, na hata akamtoa mwanawe kafara katika moto, akifuata njia za machukizo za mataifa ambayo Bwana alikuwa ameyafukuza mbele ya Waisraeli. 416:4 Kum 12:2; Eze 6:13Akatoa kafara na kufukiza uvumba katika mahali pa juu pa kuabudia miungu, juu ya vilima, na chini ya kila mti uliotanda.

516:5 2Fal 15:37Kisha Resini mfalme wa Aramu na Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli wakaondoka kwenda kupigana dhidi ya Yerusalemu na kumzunguka Ahazi kwa jeshi, lakini hawakuweza kumshinda. 616:6 Isa 9:12; 1Fal 9:26Wakati ule, Resini mfalme wa Aramu akaurudisha Elathi kwa Aramu kwa kuwafukuza watu wa Yuda. Kisha Waedomu wakahamia Elathi, nao wanaishi huko mpaka leo.

716:7 2Fal 15:29; Hos 10:6Ahazi akatuma wajumbe kumwambia Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru kwamba, “Mimi ni mtumishi na mtumwa wako. Njoo na uniokoe kutoka mkononi mwa mfalme wa Aramu na wa mfalme wa Israeli, ambao wananishambulia.” 816:8 2Fal 12:18; 12:18Naye Ahazi akachukua fedha na dhahabu zilizopatikana ndani ya Hekalu la Bwana na katika hazina ya jumba la mfalme, na kuzituma kama zawadi kwa mfalme wa Ashuru. 916:9 Mwa 14:15; Amo 1:5Mfalme wa Ashuru akamwitikia kwa kushambulia Dameski na kuiteka. Akawahamishia wenyeji wake huko Kiri, na kumuua Resini.

1016:10 Isa 6:2Kisha Mfalme Ahazi akaenda Dameski kukutana na Tiglath-Pileseri wa Ashuru. Akaona madhabahu huko Dameski, naye akamtumia Uria kuhani mchoro wa hayo madhabahu, pamoja na maelezo ya mpango kamili wa ujenzi wake. 11Kwa hiyo Uria kuhani akajenga madhabahu kulingana na mipango yote ambayo Mfalme Ahazi alikuwa ameituma kutoka Dameski, na akamaliza ujenzi kabla ya Mfalme Ahazi kurudi. 1216:12 2Nya 26:16Mfalme aliporudi kutoka Dameski na kuona hayo madhabahu, akayasogelea na kutoa sadaka juu yake. 13Akatoa sadaka yake ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka, akamimina sadaka ya kinywaji na kunyunyizia damu ya sadaka zake za amani juu ya hayo madhabahu. 1416:14 Kut 40:6; 1Fal 8:64Mfalme Ahazi akayaondoa madhabahu ya zamani ya shaba kutoka hapo mbele ya Hekalu la Bwana, yaliyokuwa yamesimama kati ya ingilio la Hekalu na hayo madhabahu mapya, naye akayaweka upande wa kaskazini mwa hayo madhabahu mapya.

1516:15 Kut 29:38-41Ndipo Mfalme Ahazi akatoa amri zifuatazo kwa Uria kuhani: “Juu ya hayo madhabahu kubwa mapya, toa sadaka ya asubuhi ya kuteketezwa na sadaka ya jioni ya nafaka, sadaka ya mfalme ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, sadaka ya kuteketezwa ya watu wote wa nchi, pamoja na sadaka yao ya nafaka na sadaka yao ya kinywaji. Unyunyize juu ya hayo madhabahu damu yote ya sadaka za kuteketezwa na dhabihu. Lakini mimi nitatumia hayo madhabahu ya zamani ya shaba kwa ajili ya kutafuta uongozi.” 16Naye Uria kuhani akafanya kama Mfalme Ahazi alivyoagiza.

1716:17 1Fal 7:27Mfalme Ahazi akaondoa mbao za pembeni na kuondoa masinia kwenye vile vishikilio vilivyohamishika. Akaondoa ile Bahari kutoka kwenye mafahali wa shaba walioishikilia, na kuiweka kwenye kitako cha jiwe. 1816:18 Eze 16:28Kwa heshima ya mfalme wa Ashuru, akaliondoa pia pazia la Sabato lililokuwa limewekwa ndani ya Hekalu, na akaondoa ile njia ya kifalme ya kuingia kwenye Hekalu la Bwana.

19Matukio mengine ya utawala wa Ahazi na yale aliyoyafanya, je hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 2016:20 Isa 14:28Ahazi akalala na baba zake, naye akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Naye Hezekia mwanawe akawa mfalme baada yake.