列王纪上 21 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

列王纪上 21:1-29

葡萄园事件

1这事以后,又发生了一件事。耶斯列拿伯有个葡萄园,在撒玛利亚亚哈王宫附近。 2一天,亚哈拿伯说:“你的葡萄园靠近我的王宫,你把它让给我作菜园吧。我可以用更好的葡萄园来跟你交换,如果你愿意,我也可以按地价付你钱。” 3拿伯说:“耶和华不准我把祖先的产业给你。” 4亚哈不能如愿,就闷闷不乐地回到宫中,躺在床上生气,饭也不吃。

5他妻子耶洗别过来问他:“王为什么烦闷,不思饮食呢?” 6亚哈回答说:“我要耶斯列拿伯将他的葡萄园卖给我,如果他愿意,我也可以用别的葡萄园跟他交换,可是他不肯。” 7耶洗别说:“你忘了自己是以色列王吗?起来吃饭吧,高兴点,我必让你得到耶斯列拿伯的葡萄园。”

8于是,耶洗别亚哈王的名义写信,并盖上王印,送给跟拿伯同居一城的长老和贵族。 9信上说:“你们要宣告禁食,让拿伯在百姓中坐首位, 10叫两个无赖坐在他对面控告他咒诅上帝和君王,然后把他拉出去用石头打死。” 11拿伯同居一城的长老和贵族接到来信,便依照信里的指示行事。 12他们宣告禁食,让拿伯在百姓中坐首位, 13又叫两名无赖当众作证指控拿伯咒诅上帝和君王。然后众人把拿伯拖出城外,用石头打死了他。 14事情办好了以后,他们就派人去把拿伯被石头打死的消息告诉耶洗别

15耶洗别接到消息后,就告诉亚哈说:“耶斯列拿伯已经死了,你去占他不肯卖给你的葡萄园吧。” 16亚哈听说拿伯死了,就起来,下去霸占拿伯的葡萄园。

17耶和华对提斯比以利亚说: 18“你去撒玛利亚以色列亚哈,他正在拿伯的葡萄园,他到那里要霸占那葡萄园。 19你要对他说,‘耶和华说,你杀了人,还要夺他的产业吗?’然后告诉他,耶和华说,‘狗在哪里舔拿伯的血,也必在哪里舔你的血。’”

20亚哈见了以利亚,说:“我的对头啊,你又来了!”以利亚说:“我又来了,因为你一心做耶和华视为恶的事。 21耶和华说,‘我必降祸给你,彻底毁灭你,铲除你家中所有的男子,不管是奴隶还是自由人。 22我必使你一家的下场像尼八的儿子耶罗波安家和亚希雅的儿子巴沙家一样,因为你惹我发怒,并且使以色列人陷入罪中。’ 23至于耶洗别,耶和华说,‘狗必在耶斯列的城墙边吃耶洗别的肉。 24凡属亚哈的人,死在城中的必被狗吃,死在郊野的必被飞鸟吃。’”

25从来没有人像亚哈那样受妻子耶洗别唆使,一心做耶和华视为恶的事。 26他像被耶和华驱逐的亚摩利人一样祭拜神像,行为可憎。 27亚哈听了以利亚的话,就撕裂衣服,披麻禁食,睡觉也不脱下麻衣,垂头丧气地走来走去。 28耶和华对提斯比以利亚说: 29“你看见亚哈在我面前如何痛悔了吗?因为他在我面前痛悔,我不会在他有生之日降灾,我要等他儿子执政的时候,才降灾给他家。”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wafalme 21:1-29

Shamba La Mizabibu La Nabothi

121:1 2Fal 9:21; 1Sam 29:1Baada ya hayo, Nabothi, Myezreeli, alikuwa na shamba la mizabibu jirani na jumba la kifalme la Ahabu mfalme wa Samaria. 2Ahabu akamwambia Nabothi, “Nipe shamba lako la mizabibu nilitumie kwa bustani ya mboga, kwa kuwa liko karibu na jumba langu la kifalme. Badala yake, nitakupa shamba jingine la mizabibu zuri zaidi au, kama utapenda, nitakulipa kiasi chochote unachoona ni thamani yake.”

321:3 Law 25:23Lakini Nabothi akamjibu, “Bwana na apishe mbali kukupa wewe urithi wa baba zangu.”

421:4 1Fal 20:43; Isa 28:23Basi Ahabu akaenda nyumbani, mwenye huzuni na hasira kwa sababu ya yale ambayo Nabothi, Myezreeli, alikuwa amesema, “Sitakupa urithi wa baba zangu.” Akajinyoosha juu ya kitanda akisononeka, na akakataa kula.

5Yezebeli mke wake akaingia na akamuuliza, “Kwa nini unahuzunika hivi? Kwa nini huli chakula?”

6Akamjibu, “Kwa sababu nilimwambia Nabothi, Myezreeli, ‘Niuzie shamba lako la mizabibu, au kama ukipenda, nitakupa shamba jingine la mizabibu badala yake.’ Lakini akasema, ‘Sitakupa shamba langu la mizabibu.’ ”

721:7 1Sam 8:14Yezebeli mke wake akasema, “Hivi ndivyo unavyofanya, nawe ni mfalme katika Israeli yote? Inuka na ule! Changamka. Nitakupatia shamba la mizabibu la Nabothi, Myezreeli.”

821:8 Mwa 38:18Kwa hiyo akaandika barua kwa jina la Ahabu akaweka muhuri wake juu ya hizo barua, akazipeleka kwa wazee na kwa watu wenye cheo walioishi katika mji pamoja na Nabothi. 9Katika barua hizo aliandika:

“Tangazeni siku ya watu kufunga na mkamketishe Nabothi mahali pa wazi miongoni mwa watu. 1021:10 Kut 22:28; Law 24:15-16; Mdo 6:11Lakini waketisheni watu wawili wabaya kabisa mkabala naye, nao washuhudie kuwa yeye amemlaani Mungu na mfalme. Kisha mtoeni nje na kumpiga kwa mawe hadi afe.”

11Hivyo wazee na watu wenye cheo walioishi katika mji wa Nabothi wakafanya kama Yezebeli alivyoelekeza katika barua aliyowaandikia. 1221:12 Isa 58:4Wakatangaza mfungo na kumketisha Nabothi mahali pa wazi miongoni mwa watu. 1321:13 Law 24:16Kisha watu wawili wabaya kabisa wakaja wakaketi mkabala naye, nao wakaleta mashtaka dhidi ya Nabothi mbele ya watu, wakisema, “Nabothi amemlaani Mungu na mfalme.” Kwa hiyo wakamtoa nje na kumpiga kwa mawe hadi akafa. 14Kisha wakatuma ujumbe kwa Yezebeli, kusema, “Nabothi amepigwa mawe na amekufa.”

1521:15 1Sam 8:14Mara tu Yezebeli aliposikia kwamba Nabothi amepigwa mawe na amekufa, akamwambia Ahabu, “Amka na uchukue lile shamba la mizabibu la Nabothi, Myezreeli, ambalo alikataa kukuuzia. Hayuko hai tena, bali amekufa.” 16Ahabu aliposikia Nabothi amekufa, akainuka na kushuka ili kulichukua shamba la mizabibu la Nabothi.

17Kisha neno la Bwana likamjia Eliya, Mtishbi: 18“Shuka ukakutane na Ahabu mfalme wa Israeli, anayetawala Samaria. Sasa yuko katika shamba la mizabibu la Nabothi, ambapo amekwenda alimiliki. 1921:19 Ay 24:6; 1Fal 22:38Umwambie, ‘Hivi ndivyo Bwana asemavyo: Je, hujamuua mtu na kuitwaa mali yake?’ Kisha umwambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana: Mahali ambapo mbwa waliramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba damu yako, naam, yako wewe!’ ”

2021:20 1Fal 18:17; Rum 7:14Ahabu akamwambia Eliya, “Kwa hiyo umenipata, wewe adui yangu!”

Akajibu, “Ndiyo, nimekupata. Kwa sababu umejiuza mwenyewe kufanya uovu mbele ya macho ya Bwana. 21‘Nitaleta maafa juu yako. Nitaangamiza uzao wako na kukatilia mbali kutoka kwa Ahabu kila mzaliwa wa mwisho wa kiume katika Israeli, wa mtumwa au wa mtu huru. 2221:22 1Fal 16:3Nitaifanya nyumba yako kama ile ya Yeroboamu mwana wa Nebati na ile ya Baasha mwana wa Ahiya, kwa sababu umenighadhibisha kwa kuwa umesababisha Israeli kutenda dhambi.’

2321:23 2Fal 9:10, 34-36“Pia kwa habari ya Yezebeli Bwana anasema, ‘Mbwa watamla Yezebeli karibu na ukuta wa Yezreeli.’

2421:24 1Fal 14:11; Mwa 40:19“Mbwa watawala wale wa nyumba ya Ahabu watakaofia mjini, nao wale watakaofia mashambani wataliwa na ndege wa angani.”

25(Hapajapata kamwe kuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza mwenyewe kutenda uovu machoni mwa Bwana, akiwa anachochewa na Yezebeli mkewe. 2621:26 Mwa 15:16Alitenda kwa uovu sana katika kuabudu sanamu, kama wale Waamori ambao Bwana aliowafukuza mbele ya Israeli.)

2721:27 Mwa 37:34; Yer 4:8; Isa 38:15Ahabu aliposikia maneno haya, akararua nguo zake, akavaa nguo za gunia na kufunga. Akalala na kujifunika nguo za gunia na kwenda kwa unyenyekevu.

28Ndipo neno la Bwana lilipomjia Eliya Mtishbi kusema, 2921:29 Kut 32:14; 2Fal 9:26“Umeona jinsi Ahabu alivyojinyenyekeza mbele zangu? Kwa kuwa amejishusha mwenyewe, sitaleta maafa haya wakati akiwa hai, lakini nitayaleta juu ya nyumba yake katika siku za mwanawe.”