列王纪上 11 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

列王纪上 11:1-43

所罗门背弃上帝

1除了埃及公主以外,所罗门王还宠爱许多外邦女子,有摩押人、亚扪人、以东人、西顿人和人。 2耶和华曾告诉以色列人不可跟这些外族人通婚,免得受引诱去随从他们的神明,所罗门却迷恋这些女子。 3他有七百个妻子,都是外国的公主,还有三百个妃嫔。这些女子使他的心背弃耶和华。 4所罗门年老的时候,他的嫔妃诱惑他的心去追随别的神明。他没有像他父亲大卫那样忠心顺服他的上帝耶和华。 5所罗门西顿人的女神亚斯她录亚扪人的可憎神明米勒公6他做了耶和华视为恶的事,没有像他父亲大卫那样忠心顺服耶和华。 7耶路撒冷东面的山上,所罗门摩押人可憎的神明基抹亚扪人可憎的神明摩洛修建丘坛。 8他又为所有的外邦妃嫔修建丘坛,供她们向自己的神明烧香献祭。

9-10所罗门背弃了曾两次向他显现的以色列的上帝耶和华,违背耶和华的命令去随从别的神明。所以,耶和华向他发怒, 11说:“你既然违背我的命令,不遵守我的约和律例,我必夺走你的国,将它赐给你的一个臣仆。 12然而,因你父大卫的缘故,我不会在你有生之年这样做,我要从你儿子手中把国夺走。 13但我不会全部夺走,为了我仆人大卫和我拣选的耶路撒冷,我会留下一个支派给你儿子。”

所罗门的敌人

14耶和华使以东王的后裔哈达兴起,与所罗门为敌。 15从前大卫征讨以东,元帅约押前去埋葬阵亡的人,将以东的男子都杀了。 16他率领以色列人在那里住了六个月,直到杀光了以东的男子。 17那时,哈达年纪还小,他和他父亲的几个以东臣仆一起逃往埃及18他们从米甸逃到巴兰,在那里招聚了一些人,然后又逃到埃及去见埃及王法老。法老赐他粮食、房屋和田地。 19法老非常喜欢哈达,将王后答比妮的妹妹许配给他。 20他们生了一个儿子,取名基努拔,由王后在宫中抚养,跟王子们在一起。 21后来,哈达知道大卫已与祖先同眠,约押元帅也死了,就求法老准他回国。 22法老问他:“你为什么要回国呢?你在我这里还缺什么吗?”哈达答道:“什么都不缺,但还是求王准我回国。” 23上帝又使以利亚大的儿子利逊兴起,与所罗门为敌。这人从他主人琐巴哈大底谢身边逃走后, 24招聚了一群匪徒,自己做头目。大卫征服琐巴人后,他又前往大马士革,在那里做王。 25所罗门活着的时候,哈达利逊不断为患。利逊统治亚兰,他憎恨以色列人。

耶罗波安叛变

26所罗门的一个臣仆耶罗波安也叛变了。他是以法莲支派洗利达尼八的儿子,母亲洗鲁阿是个寡妇。 27以下是他反叛所罗门的缘由:

当年所罗门建造米罗堡,修补大卫城的城墙时, 28发现年轻的耶罗波安勤奋能干,就提拔他监管约瑟家族的一切工程。

29有一次,耶罗波安出了耶路撒冷,在路上遇见身披新衣的示罗亚希雅先知。当时野外只有他们二人。 30亚希雅将身上的新衣撕作十二片, 31耶罗波安说:“你可以拿十片。以色列的上帝耶和华说,‘我必夺走所罗门的国,把十个支派赐给你。 32然而,为了我仆人大卫和我在以色列众支派中拣选的耶路撒冷城,我会留下一个支派给所罗门33所罗门背弃了我,去祭拜西顿人的女神亚斯她录摩押的神明基抹亚扪人的神明米勒公。他没有遵行我的道,没有做我视为正的事,也不像他父亲大卫那样遵守我的律例和典章。 34然而,我不会夺走他整个国,我会让所罗门终生为王,因为我所拣选的仆人大卫遵守我的诫命和律法。 35我必从他儿子手中把国夺走,将十个支派赐给你, 36只给他儿子留下一个支派,好使我仆人大卫有后裔留在我选为居所的耶路撒冷城。 37我要让你做王,使你如愿地统治以色列38若你像我仆人大卫一样听从我的一切吩咐,遵行我的道,做我视为正的事,遵守我的律例诫命,我就与你同在,巩固你的王朝,像巩固大卫的王朝一样,使你统治以色列39所罗门的所作所为,我必让大卫的后裔遭难,但不会永远如此。’”

40所罗门想杀耶罗波安,他就逃到埃及投奔埃及示撒,在那里一直住到所罗门过世。

41所罗门的其他事迹、作为和智慧都记在所罗门记上了。 42所罗门耶路撒冷统治以色列四十年, 43他与祖先同眠后葬在他父亲大卫的城里。他儿子罗波安继位。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wafalme 11:1-43

Wakeze Solomoni

111:1 Kut 34:16; 1Fal 12:21, 31Hata hivyo, Mfalme Solomoni akawapenda wanawake wengi wa kigeni zaidi, mbali na binti Farao: wanawake wa Wamoabu, Waamoni, Waedomu, Wasidoni na Wahiti. 211:2 Kut 34:16; 1Fal 16:31Walitoka katika mataifa ambayo Bwana aliwaambia Waisraeli, “Msije mkaoana nao, kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu mgeukie miungu yao.” Hata hivyo, Solomoni akakaza kuwapenda. 311:3 Mwa 22:24; Mit 31:3Alikuwa na wake 700 mabinti wa uzao wa kifalme, na masuria 300, nao wake zake wakampotosha. 411:4 Kut 34:16; 1Nya 29:19Kadiri Solomoni alivyozidi kuzeeka, wake zake wakaugeuza moyo wake kuelekea miungu mingine, na moyo wake haukujitolea kikamilifu kwa Bwana Mungu wake, kama ulivyokuwa moyo wa Daudi baba yake. 511:5 Amu 2:13Solomoni akafuata Ashtorethi mungu mke wa Wasidoni, na Moleki11:5 Moleki au Milkomu ni mungu aliyekuwa akiabudiwa na Waamoni; alikuwa chukizo kwa sababu watoto walitolewa kafara kwake. mungu aliyekuwa chukizo la Waamoni. 611:6 Kum 4:25Kwa hiyo Solomoni akafanya uovu machoni pa Bwana; hakumfuata Bwana kikamilifu kama alivyofanya Daudi baba yake.

711:7 2Fal 23:13; Hes 21:29; Mdo 7:43Kwenye kilima mashariki mwa Yerusalemu, Solomoni akajenga mahali pa juu kwa ajili ya Kemoshi chukizo la Wamoabu, na kwa Moleki mungu chukizo la Waamoni. 8Akafanya hivyo kwa wake zake wote wa kigeni, ambao walifukiza uvumba na kutoa dhabihu kwa miungu yao.

911:9 1Fal 3:5Bwana akamkasirikia Solomoni kwa sababu moyo wake uligeuka mbali na Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye alikuwa amemtokea mara mbili. 1011:10 1Fal 9:6; 6:12Ingawa alikuwa amemkataza Solomoni kufuata miungu mingine, Solomoni hakutii amri ya Bwana. 11Kwa hiyo Bwana akamwambia Solomoni, “Kwa kuwa hii ndiyo hali yako na hukushika Agano langu na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme kutoka kwako na kumpa mmoja wa walio chini yako. 12Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi baba yako, sitafanya jambo hili wakati wa uhai wako. Nitaurarua kutoka mikononi mwa mwanao. 1311:13 2Sam 7:15; Kum 12:11Lakini pia sitaurarua ufalme wote kutoka kwake, bali nitampa kabila moja kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu na kwa ajili ya Yerusalemu, ambao nimeuchagua.”

Adui Za Solomoni

14Kisha Bwana akamwinua adui dhidi ya Solomoni, Hadadi, Mwedomu, kutoka ukoo wa ufalme wa Edomu. 1511:15 1Nya 18:12Huko nyuma wakati Daudi alipokuwa akipigana na Edomu, Yoabu jemadari wa jeshi, aliyekuwa amekwenda kuzika waliouawa, alikuwa amewaua wanaume wote waliokuwako Edomu. 16Yoabu na Waisraeli wote walikaa huko kwa miezi sita, mpaka walipomaliza kuwaangamiza wanaume wote huko Edomu. 17Lakini Hadadi, akiwa bado mvulana mdogo, alikimbilia Misri akiwa na baadhi ya maafisa wa Kiedomu waliokuwa wakimhudumia baba yake. 1811:18 Hes 10:12Wakaondoka Midiani wakaenda Parani. Basi wakichukua pamoja nao wanaume kutoka Parani, wakaenda Misri, kwa Farao mfalme wa Misri, ambaye alimpa Hadadi nyumba, ardhi na akampatia chakula.

19Farao akapendezwa sana na Hadadi hata akampa ndugu wa mkewe mwenyewe, Malkia Tapenesi, ili aolewe na Hadadi. 20Huyo ndugu wa Tapenesi akamzalia mwana aliyeitwa Genubathi, ambaye alilelewa na Tapenesi katika jumba la kifalme. Huko Genubathi aliishi pamoja na watoto wa Farao mwenyewe.

21Alipokuwa huko Misri, Hadadi alisikia kwamba Daudi amepumzika na baba zake na ya kwamba pia Yoabu aliyekuwa jemadari wa jeshi amekufa. Ndipo Hadadi akamwambia Farao, “Niruhusu niende ili niweze kurudi katika nchi yangu.”

22Farao akauliza, “Umekosa nini hapa, kwamba unataka kurudi katika nchi yako?”

Hadadi akajibu, “Hakuna, lakini niruhusu niende!”

2311:23 1Fal 5:4; 2Sam 8:3Mungu akamwinua adui mwingine dhidi ya Solomoni, Rezoni mwana wa Eliada, ambaye alikuwa amemkimbia bwana wake Hadadezeri, mfalme wa Soba. 2411:24 2Sam 8:5Akawakusanya watu, naye akawa kiongozi wa kundi la waasi, wakati Daudi alipoangamiza majeshi ya Soba; waasi walikwenda Dameski, mahali walipokaa na kumiliki. 2511:25 Mwa 10:22; 2Sam 10:19Rezoni alikuwa adui wa Israeli kwa muda wote alioishi Solomoni, ukiongezea matatizo yaliyosababishwa na Hadadi. Kwa hiyo Rezoni akatawala katika Aramu11:25 Yaani Shamu (ambayo leo ni Syria). na alikuwa mkatili kwa Israeli.

Yeroboamu Anaasi Dhidi Ya Solomoni

2611:26 2Nya 13:6Pia, Yeroboamu mwana wa Nebati aliasi dhidi ya mfalme. Alikuwa mmoja wa maafisa wa Solomoni, Mwefraimu kutoka Sereda, ambaye mama yake alikuwa mjane aliyeitwa Serua.

2711:27 1Fal 9:24Haya ndiyo maelezo ya jinsi alivyomwasi mfalme: Solomoni alikuwa amejenga Milo11:27 Milo maana yake Boma la Ngome. naye akawa ameziba mwanya katika ukuta wa mji wa Daudi baba yake. 2811:28 Rut 2:1; Mit 22:29Basi Yeroboamu alikuwa mtu shujaa na hodari, naye Solomoni alipoona jinsi kijana alivyofanya kazi yake, akamweka kuwa kiongozi wa kazi yote ya mikono ya nyumba ya Yosefu.

2911:29 1Fal 12:15; 14:2Karibu na wakati ule Yeroboamu alikuwa anatoka nje ya Yerusalemu, Ahiya nabii Mshiloni akakutana naye njiani, akiwa amevaa joho jipya. Hawa wawili walikuwa peke yao mashambani, 3011:30 1Sam 15:27naye Ahiya akachukua joho jipya alilokuwa amevaa akalirarua vipande kumi na viwili. 3111:31 1Fal 11:11; 1Sam 15:27Kisha akamwambia Yeroboamu, “Chukua vipande kumi kwa ajili yako, kwa kuwa hivi ndivyo Bwana, Mungu wa Israeli asemavyo: ‘Tazama, ninakwenda kuuchana ufalme kutoka mikononi mwa Solomoni na kukupa wewe makabila kumi. 3211:32 2Sam 7:15Lakini kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi na mji wa Yerusalemu, ambao nimeuchagua miongoni mwa makabila yote ya Israeli, atakuwa na kabila moja. 3311:33 Amu 2:13; 1Fal 3:3Nitafanya hivi kwa sababu wameniacha mimi na kuabudu Ashtorethi mungu mke wa Wasidoni, Kemoshi mungu wa Wamoabu, na Moleki mungu wa Waamoni, nao hawakwenda katika njia zangu ili kufanya yaliyo sawa machoni pangu, wala kushika amri na sheria zangu kama Daudi, babaye Solomoni, alivyofanya.

34“ ‘Lakini sitauondoa ufalme wote kutoka mikononi mwa Solomoni, nimemfanya mtawala siku zote za maisha yake kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, niliyemchagua na ambaye aliyatunza maagizo na amri zangu. 35Nitauondoa ufalme kutoka mikononi mwa mwanawe na kukupa wewe makabila kumi. 3611:36 1Fal 12:17Nitampa mwanawe kabila moja ili kwamba Daudi mtumishi wangu awe na taa mbele zangu daima katika Yerusalemu, mji ambao nimeuchagua kuweka Jina langu. 3711:37 1Fal 14:7; 2Sam 3:21Hata hivyo, kukuhusu wewe Yeroboamu, nitakutwaa, nawe utatawala juu ya yote yale moyo wako unayotamani, utakuwa mfalme juu ya Israeli. 3811:38 Kum 12:25; 2Sam 3:15; Kut 1:21Ikiwa utafanya kila nitakalokuamuru, kuenenda katika njia zangu na kufanya yaliyo sawa mbele za macho yangu kwa kuzishika amri zangu na maagizo yangu kama alivyofanya Daudi mtumishi wangu, nitakuwa pamoja nawe. Nitakujengea ufalme utakaodumu kama ule niliomjengea Daudi, nami nitakupa Israeli. 39Nitawatesa wazao wa Daudi kwa ajili ya hili, lakini siyo milele.’ ”

4011:40 1Fal 12:2; 2Nya 10:2; 12:2Solomoni akajaribu kumuua Yeroboamu, lakini Yeroboamu akakimbilia Misri, kwa Mfalme Shishaki, naye akakaa huko mpaka Solomoni alipofariki.

Kifo Cha Solomoni

(2 Nyakati 9:29-31)

41Kwa habari za matukio mengine ya utawala wa Solomoni, yote aliyoyafanya na hekima aliyoionyesha, je hayakuandikwa yote katika kitabu cha matendo cha Solomoni? 42Solomoni alitawala Israeli yote miaka arobaini, akiwa Yerusalemu. 43Kisha Solomoni akalala pamoja na baba zake, naye akazikwa katika mji wa Daudi baba yake. Naye Rehoboamu mwanawe akawa mfalme baada yake.