使徒行传 3 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

使徒行传 3:1-26

彼得医治瘸腿的乞丐

1一天,在下午三点祷告的时间,彼得约翰去圣殿。 2有一个生来瘸腿的人天天被人抬到圣殿美门的外面,向进殿的人乞讨。 3他看见彼得约翰要进殿,就求他们施舍。 4二人定睛看他,彼得说:“看着我们!” 5那人就紧盯着他们,期盼能有所收获。

6彼得说:“金子、银子我都没有,但是我把我有的给你。我奉拿撒勒人耶稣基督的名,命令你起来行走!”

7彼得拉着他的右手扶他起来,那人的脚和踝骨立刻变得强健有力。 8他跳了起来,站稳后开始行走,跟着彼得约翰进入圣殿,走着跳着赞美上帝。 9大家看见他一边走一边赞美上帝, 10认出他就是那个在美门外面的乞丐,都为发生在他身上的事而感到惊奇、诧异。 11那乞丐紧紧拉着彼得约翰的手走到所罗门廊,众人都跑过来,啧啧称奇。

彼得传扬基督

12彼得看见这情形,就对大家说:“以色列人啊,何必惊奇呢?为什么一直盯着我们呢?你们以为我们是凭自己的能力和虔诚叫这人行走吗? 13亚伯拉罕以撒雅各的上帝,就是我们祖先的上帝,已经使祂的仆人耶稣得了荣耀。你们把耶稣交给彼拉多,尽管彼拉多想释放祂,你们却在彼拉多面前弃绝祂! 14你们弃绝了那圣洁公义者,竟然要求彼拉多释放一个凶手。 15你们杀了生命之主,上帝却使祂从死里复活了。我们都是这事的见证人。 16你们认识的这个乞丐因为相信耶稣的名,得到了医治。你们都看见了,他能痊愈是因为他信耶稣。

17“弟兄们,我知道你们的所作所为是出于无知,你们的官长也是一样。 18但是上帝早已借众先知预言基督要受害,这事果然应验了。 19所以你们要悔改,归向上帝,祂将除去你们一切的罪恶, 20赐给你们焕然一新的日子,也将差遣祂预先为你们选立的基督耶稣降临。 21基督必须留在天上,直到万物更新的时候,这是上帝自古以来借圣先知的口说的。 22摩西曾经说,‘主——你们的上帝将要在你们中间兴起一位像我一样的先知。你们要留心听祂的话, 23凡不听的,必将他从民中铲除。’

24“从撒母耳到后来的所有先知都宣告过这些日子。 25你们是先知的子孙,也承受了上帝和你们祖先所立的约。上帝曾对亚伯拉罕说,‘天下万族必因你的后裔而蒙福。’ 26上帝兴起祂的仆人,首先差遣祂到你们中间赐福给你们,使你们脱离罪恶。”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Matendo 3:1-26

Petro Amponya Mlemavu Kwa Jina La Yesu

13:1 Lk 22:8; Mdo 2:46; Za 55:17; Mdo 10:30Siku moja Petro na Yohana walikuwa wanapanda kwenda Hekaluni kusali yapata saa tisa alasiri. 23:2 Mdo 14:8; Lk 16:20; Yn 9:8Basi palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa kiwete tangu kuzaliwa. Alichukuliwa na kuwekwa kwenye lango la Hekalu liitwalo Zuri, kila siku ili aombe msaada kwa watu wanaoingia Hekaluni. 3Huyu mtu alipowaona Petro na Yohana wakikaribia kuingia Hekaluni, akawaomba wampe sadaka. 43:4 Mdo 14:9Wakamkazia macho, kisha Petro akamwambia, “Tutazame sisi.” 5Hivyo yule mtu akawatazama, akitazamia kupata kitu kutoka kwao.

63:6 Mk 1:24; Mdo 14:10Ndipo Petro akamwambia, “Sina fedha wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, tembea!” 7Petro akamshika yule mtu kwa mkono wa kuume akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikapata nguvu. 83:8 Isa 35:6; Mdo 14:10Akaruka juu na kusimama, akaanza kutembea. Kisha akaingia Hekaluni pamoja na Petro na Yohana, huku akitembea na kurukaruka na kumsifu Mungu. 93:9 Mdo 4:16, 21Watu wote walipomwona akitembea na kumsifu Mungu, 103:10 Mdo 3:2; Yn 9:8wakamtambua kuwa ni yule mtu aliyekuwa akiketi nje ya Hekalu penye lango liitwalo Zuri akiomba msaada, nao wakajawa na mshangao, wakastaajabu juu ya yale yaliyomtukia.

Petro Anashuhudia Kuwa Yesu Anaponya

113:11 Lk 22:8; Yn 10:23; Mdo 5:12Aliyeponywa alipokuwa akiambatana na Petro na Yohana, watu wote walishangaa mno, wakaja wakiwakimbilia pale ukumbi wa Solomoni. 12Petro alipoona watu wamekusanyika akawaambia, “Enyi Waisraeli, kwa nini mnastaajabu kuhusu jambo hili? Mbona mnatukazia macho kwa mshangao kana kwamba ni kwa uwezo wetu au utakatifu wetu tumemfanya mtu huyu kutembea? 133:13 Mdo 7:32; 22:14; Mt 27; 2; Lk 23:4Mungu wa Abrahamu na Isaki na Yakobo, Mungu wa baba zetu amemtukuza Mwanawe Yesu, ambaye ninyi mlimtoa ahukumiwe kifo na mkamkana mbele ya Pilato, ingawa yeye alikuwa ameamua kumwachia aende zake. 143:14 Mdo 4:27; 7:52; Mk 15:11; Lk 23:18-25Ninyi mlimkataa huyo Mtakatifu na Mwenye Haki mkaomba mpewe yule muuaji. 153:15 Mdo 2:24; 2:32Hivyo mkamuua aliye chanzo cha uzima, lakini Mungu akamfufua kutoka kwa wafu. Sisi tu mashahidi wa mambo haya. 163:16 Mt 9:22; Mdo 4:10; 14:9Kwa imani katika jina la Yesu, huyu mtu mnayemwona na kumfahamu ametiwa nguvu. Ni kwa jina la Yesu na imani itokayo kwake ambayo imemponya kabisa huyu mtu, kama ninyi wote mnavyoona.

173:17 Lk 23:34; Mdo 13:27“Sasa ndugu zangu, najua ya kuwa ninyi mlitenda bila kujua, kama walivyofanya viongozi wenu. 183:18 Mdo 17:2-3; Lk 24:27; Mdo 26:22-27Lakini kwa njia hii Mungu alitimiza kile ambacho alikuwa ametabiri kwa vinywa vya manabii wake wote, kwamba Kristo3:18 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. atateswa. 193:19 Za 5:11; Mdo 2:38Tubuni basi mkamgeukie Mungu, dhambi zenu zifutwe, ili zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwepo kwake Bwana, 203:20 Lk 2:11naye apate kumtuma Kristo, ambaye ameteuliwa kwa ajili yenu, yaani Yesu. 213:21 Mdo 1:11; Mt 17:11; Lk 1:70Ilimpasa mbingu zimpokee mpaka wakati wa kufanywa upya kila kitu, kama Mungu alivyoahidi zamani kupitia kwa vinywa vya manabii wake watakatifu. 223:22 Kum 18:15-18; Mdo 7:37Kwa maana Mose alisema, ‘Bwana Mungu wenu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Itawapasa kumtii huyo kwa kila jambo atakalowaambia. 233:23 Kum 18:19; Law 23:29Mtu yeyote ambaye hatamsikiliza huyo nabii, atatupiliwa mbali kabisa na watu wake.’

243:24 Lk 24:27“Naam, manabii wote tangu Samweli na waliokuja baada yake, wote walitabiri kuhusu siku hizi. 253:25 Mdo 2:39; Rum 9:4-5; Mwa 22:18; 28:14Ninyi ndio wana wa manabii na wa Agano ambalo Mungu alifanya na baba zenu, akimwambia Abrahamu, ‘Kupitia kwa uzao wako, watu wote wa ulimwengu watabarikiwa.’ 263:26 Mdo 2:24; 13:46; Rum 1:16Mungu alipomfufua Yesu Mwanawe, alimtuma kwenu kwanza, ili awabariki kwa kumgeuza kila mmoja wenu kutoka njia yake mbaya.”