使徒行传 28 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

使徒行传 28:1-31

在马耳他岛

1我们安全上岸后,才知道那个岛的名字叫马耳他2岛上的居民对我们非常友善。因为下雨,天气又冷,他们就生火接待我们。 3保罗拿起一捆柴放进火堆里,不料有一条毒蛇经不住热钻了出来,咬住了他的手。 4那里的居民看见毒蛇吊在保罗手上,就交头接耳地说:“这人一定是个凶手,虽然侥幸没有淹死,天理却不容他活下去。” 5可是保罗把蛇甩进火里,并没有受伤。 6他们以为保罗的手一定会肿起来或者他会突然倒毙,但是等了很久,见他还是安然无恙,就改变了态度,说他是个神明。

7那个岛的首领名叫部百流,他的田产就在附近。他接待我们,热情款待了我们三天。 8当时,部百流的父亲患痢疾,正发热躺在床上。保罗去为他祷告,把手按在他身上治好了他。 9这事以后,岛上其他的病人都来了,他们都得了医治。 10他们处处尊敬我们,在我们启航的时候,又赠送我们途中所需用的物品。

保罗抵达罗马

11三个月后,我们搭乘一艘停在该岛过冬的船离开。这船叫“双神号”,来自亚历山大12我们先到叙拉古港,在那里停泊三天, 13然后继续前行,到达利基翁。第二天,起了南风,第三天我们抵达部丢利14在那里遇见几位弟兄姊妹,应邀和他们同住了七天,然后前往罗马15那里的弟兄姊妹听说我们来了,便到亚比乌三馆迎接我们。保罗见到他们后,就感谢上帝,心中受到鼓励。 16进了罗马城后,保罗获准在卫兵的看守下自己一个人住。

继续传道

17三天后,保罗请来当地犹太人的首领,对他们说:“弟兄们,虽然我没有做过任何对不起同胞或违背祖先规矩的事,却在耶路撒冷遭囚禁,又被交到罗马人的手里。 18罗马官员审讯了我,发现我没有什么该死的罪,想释放我, 19犹太人却反对,我不得已只好上诉凯撒。我并非有什么事要控告自己的同胞。 20为此,我才请你们来当面谈,我受捆绑是为了以色列人所盼望的那位。”

21他们说:“犹太境内的同胞没有给我们写信提及你的事,也没有弟兄到这里说你的坏话。 22不过,我们倒很想听听你的观点,因为我们知道你们这一派的人到处受人抨击。”

23于是,他们和保罗约定了会面的日期。那一天,很多人来到保罗住的地方。从早到晚,保罗向他们传扬上帝国的道,引用摩西律法和先知书劝他们相信有关耶稣的事。 24有些人听后相信了他的话,有些人不相信, 25他们彼此意见不一。在他们散去之前,保罗说了一句话:“圣灵借以赛亚先知对你们祖先所说的话真是一点不错, 26祂说,

“‘你去告诉百姓,

你们听了又听,却不明白;

看了又看,却不领悟。

27因为这百姓心灵麻木,

耳朵发背,眼睛昏花,

以致眼睛看不见,

耳朵听不见,心里不明白,无法回心转意,

得不到我的医治。’

28所以你们当知道,上帝的救恩已经传给了外族人,他们也必听。”

29听完保罗的话后,那些犹太人就回去了,他们中间起了激烈的争论。28:29 有古卷无“听完保罗的话后,那些犹太人就回去了,他们中间起了激烈的争论。”

30后来,保罗租了一间房子,在那里住了整整两年,接待所有到访的人。 31他勇敢地传讲上帝的国,教导有关主耶稣基督的事,没有受到任何拦阻。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Matendo 28:1-31

Paulo Kisiwani Malta

128:1 Mdo 16:10; 27:26, 39Baada ya kufika nchi kavu salama, ndipo tukafahamu kwamba jina la kile kisiwa ni Malta. 228:2 Mdo 27:3; 2Kor 11:27Wenyeji wa kile kisiwa wakatufanyia ukarimu usio wa kawaida. Waliwasha moto na kutukaribisha sisi sote kwa sababu mvua ilikuwa inanyesha na kulikuwa na baridi. 3Paulo alikuwa amekusanya mzigo wa kuni na alipokuwa anaweka kwenye moto kwa ajili ya joto, nyoka mwenye sumu akatoka humo na kujisokotea mkononi mwake. 428:4 Mk 16:18; Lk 13:2, 4Wale wenyeji wa kile kisiwa walipomwona yule nyoka akiningʼinia mkononi mwa Paulo, wakaambiana, “Huyu mtu lazima awe ni muuaji, ingawa ameokoka kutoka baharini, haki haijamwacha aishi.” 528:5 Lk 10:19Lakini Paulo akamkungʼutia yule nyoka ndani ya moto wala yeye hakupata madhara yoyote. 628:6 Mdo 14:11Watu walikuwa wanangoja avimbe au aanguke ghafula na kufa. Lakini baada ya kungoja kwa muda mrefu na kuona kwamba hakuna chochote kisicho cha kawaida kilichomtokea, wakabadili mawazo yao na kuanza kusema kwamba yeye ni mungu.

7Basi karibu na sehemu ile, palikuwa na shamba kubwa la mtu mmoja kiongozi wa kile kisiwa, aliyeitwa Publio. Alitupokea na akatuhudumia kwa ukarimu mkubwa kwa muda wa siku tatu. 828:8 Yak 5:14, 15; Mdo 9:40Baba yake Publio alikuwa mgonjwa kitandani, akiwa anaumwa homa na kuhara damu. Paulo akaingia ndani ili kumwona na baada ya maombi, akaweka mikono juu yake na kumponya. 9Jambo hili lilipotukia, watu wote wa kisiwa kile waliokuwa wagonjwa wakaja, nao wakaponywa. 1028:10 Mt 15:6; 1Tim 5:17; Za 15:4Wakatupa heshima nyingi, nasi tulipokuwa tayari kusafiri kwa njia ya bahari, wakapakia melini vitu vyote tulivyokuwa tunavihitaji.

Paulo Awasili Rumi

1128:11 Mdo 27:6Miezi mitatu baadaye tukaanza safari kwa meli iliyokuwa imetia nanga kwenye kisiwa hicho kwa ajili ya majira ya baridi. Hii ilikuwa meli ya Iskanderia yenye alama ya miungu pacha waitwao Kasta na Poluksi. 12Kituo chetu cha kwanza kilikuwa Sirakusa na tukakaa huko siku tatu. 13Kisha tukangʼoa nanga, tukafika Regio. Siku iliyofuata, upepo mkali wa kusi ukavuma, na siku ya pili yake tukafika Puteoli. 1428:14 Mdo 1:16Huko tukawakuta ndugu, nasi tukakaribishwa tukae nao kwa siku saba. Hivyo tukaendelea na safari mpaka Rumi. 1528:15 Mdo 1:16Ndugu wa huko Rumi waliposikia habari zetu, walikuja mpaka Soko la Apio na mahali paitwapo Mikahawa Mitatu kutulaki. Paulo alipowaona, alimshukuru Mungu akatiwa moyo. 1628:16 Mdo 24:23; 27:3Tulipofika Rumi, Paulo aliruhusiwa kuishi peke yake akiwa na askari wa kumlinda.

Paulo Ahubiri Rumi Chini Ya Ulinzi

1728:17 Mdo 25:2; 22:5; 25:8; 6:14Siku tatu baadaye Paulo akawaita pamoja viongozi wa Kiyahudi. Walipokwisha kukusanyika akawaambia, “Ndugu zangu, ingawa sikufanya jambo lolote dhidi ya watu wetu au dhidi ya desturi za baba zetu, lakini nilikamatwa huko Yerusalemu nikakabidhiwa kwa Warumi. 1828:18 Mdo 22:24; 26:31, 32; 23:9Wao walipokwisha kunihoji, wakataka kuniachia huru kwa sababu hawakuona kosa lolote nililolifanya linalostahili adhabu ya kifo. 1928:19 Mdo 25:11; 26:32Lakini Wayahudi walipopinga uamuzi huo, nililazimika kukata rufaa kwa Kaisari, ingawa sikuwa na lalamiko lolote juu ya taifa langu. 2028:20 Mdo 26:6, 7; 21:33Basi hii ndiyo sababu nimewatumania, ili niseme nanyi. Kwa kuwa ni kwa ajili ya tumaini la Israeli nimefungwa kwa minyororo.”

2128:21 Mdo 22:5Wakamjibu, “Hatujapokea barua zozote kutoka Uyahudi zinazokuhusu, wala hapana ndugu yeyote aliyekuja hapa ambaye ametoa taarifa au kuzungumza jambo lolote baya juu yako. 2228:22 Mdo 24:5, 14Lakini tungependa kusikia kutoka kwako unalofikiri kwa sababu tunajua kwamba kila mahali watu wanazungumza mabaya kuhusu jamii hii.”

2328:23 Mt 3:2; Mdo 19:8; 17:3; 8:35Baada ya kupanga siku ya kuonana naye, watu wengi wakaja kuanzia asubuhi hadi jioni akawaeleza na kutangaza kuhusu Ufalme wa Mungu akijaribu kuwahadithia juu ya Yesu kutoka Sheria ya Mose na kutoka Manabii. 2428:24 Mdo 14:4Baadhi wakasadiki yale aliyosema, lakini wengine hawakuamini. 25Hivyo hawakukubaliana, nao walipokuwa wanaondoka, Paulo akatoa kauli moja zaidi: “Roho Mtakatifu alinena kweli na baba zenu aliposema mambo yale yaliyomhusu Bwana Yesu kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba:

2628:26 Isa 6:9; Yer 5:21; Eze 12:2; Mt 13:14, 15; Mk 4:12; Lk 8:10; Yn 12:40; Rum 11:8“ ‘Nenda kwa watu hawa na useme,

“Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa;

na pia mtatazama, lakini hamtaona.”

2728:27 Za 119:70; Isa 6:9, 10Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu;

hawasikii kwa masikio yao,

na wamefumba macho yao.

Wasije wakaona kwa macho yao,

na wakasikiliza kwa masikio yao,

wakaelewa kwa mioyo yao,

na kugeuka nami nikawaponya.’

2828:28 Lk 2:30; Mdo 13:46“Basi na ijulikane kwenu kwamba, huu wokovu wa Mungu umepelekwa kwa watu wa Mataifa, nao watasikiliza.” [ 29Naye akiisha kusema maneno haya, Wayahudi wakaondoka wakiwa na hoja nyingi miongoni mwao.]

30Kwa miaka miwili mizima Paulo alikaa huko kwa nyumba aliyokuwa amepanga. Akawakaribisha wote waliokwenda kumwona. 3128:31 Mdo 4:29; Mt 4:23; Mdo 4:29; 28:23; Mt 4:23; Mdo 4:23; 4:23; 4:31; Efe 6:19Akahubiri Ufalme wa Mungu na kufundisha mambo yale yaliyomhusu Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri wote na bila kizuizi chochote.