使徒行传 15 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

使徒行传 15:1-41

耶路撒冷会议

1有几个从犹太下来的人教导弟兄们说:“你们若不照着摩西的规条接受割礼,就不能得救。” 2保罗巴拿巴为这件事与他们激烈地辩论,最后大家决定派保罗巴拿巴和几个当地的信徒上耶路撒冷去跟使徒和长老讨论这件事。

3于是教会为他们送行。他们经过腓尼基撒玛利亚,沿途报告外族人悔改信主的消息,弟兄姊妹都大受鼓舞。 4他们到了耶路撒冷,受到教会、使徒和长老的接待,并详述了上帝借他们所做的一切事。 5有几个信了主的法利赛人站起来说:“外族的信徒必须接受割礼,而且还要遵守摩西的律法。”

6使徒和长老们聚集商议这个问题。 7经过许多辩论之后,彼得站起来对大家说:“弟兄们,你们都知道,上帝早已在你们当中拣选我去向外族人传道,让他们也可以听到福音并信主。 8洞悉人心的上帝把圣灵赐给他们,正如赐给我们一样,以表明祂也接纳外族人。 9上帝对他们和我们一视同仁,祂因他们的信心而洁净了他们的心灵。 10现在你们为什么要试探上帝,把我们祖先和我们不能负的重担强加在这些门徒身上? 11我们相信,他们和我们一样都是靠主耶稣的恩典得救。”

12众人都沉默不语,继续听巴拿巴保罗叙述上帝借着他们在外族人中所行的神迹奇事。 13他们报告完了,雅各站起来说:“弟兄们,请听我说。 14刚才西门讲述了上帝当初如何眷顾外族人,从他们当中拣选人归在祂的名下。 15这完全与众先知的话相符,正如圣经上说,

16“‘此后,我要回来重建已倾覆的大卫王朝,

将它从废墟中重建、恢复,

17好叫其余的百姓,

就是凡归在我名下的外族人都寻求主。’

这是上帝说的, 18祂从亘古就显明了这事。

19“所以,我认为不应该为难那些信上帝的外族人。 20我们只须写信吩咐他们远避被偶像玷污之物,不可淫乱,不可吃血和勒死的牲畜。 21因为自古以来,在各城都有人宣讲摩西的律法,每逢安息日,都有人在会堂里诵读。”

给外族信徒的信

22最后,使徒、长老和全教会都决定从他们当中选派代表,随保罗巴拿巴安提阿。他们选了别号巴撒巴犹大西拉,这两位都是教会的领袖。 23他们带去的书信这样说:“安提阿叙利亚基利迦的外族弟兄姊妹,你们的弟兄——众使徒和长老向你们问安!

24“听说有几个人从我们这里去了你们那里,教导你们必须接受割礼并遵守摩西的律法15:24 有古卷无“教导你们必须接受割礼并遵守摩西的律法。”。他们的言论使你们大感困惑。其实我们从来没有授权他们这样做。 25所以我们一致决定选派代表,随我们敬爱的巴拿巴保罗去你们那里。 26他们二人为我们主耶稣基督的缘故已将生死置之度外。 27我们选派犹大西拉两位代表跟他们一起去,向你们报告我们的决定。 28因为圣灵和我们都认为不应把重担加在你们身上。但请务必注意以下几件事, 29要远避祭拜偶像的事,不可吃血,不可吃勒死的牲畜,不可淫乱。你们一一遵守这些事就好了。祝平安!”

30他们奉命下到安提阿,召集众人,交付书信。 31众人读过这封信之后,都因信中劝勉的话而欢喜。 32犹大西拉也是先知,他们讲了许多勉励、坚立弟兄姊妹的话。 33住了些日子后,安提阿的弟兄姊妹以平安的祝福为他们送行,让他们回耶路撒冷复命。 34西拉决定留在那里。15:34 有古卷无“但西拉决定留在那里”。 35保罗巴拿巴则继续留在安提阿,与许多人一起教导、传扬上帝的道。

保罗与巴拿巴分手

36过了一些日子,保罗巴拿巴说:“我们回到曾传过福音的各城镇去探望弟兄姊妹吧,好知道他们的情况。” 37巴拿巴想要带约翰·马可同去, 38保罗坚持不带他同行,因为他在旁非利亚离开了他们,没有和他们一起做工。

39二人激烈地争执起来,僵持不下,只好分道扬镳。巴拿巴约翰·马可一同乘船去塞浦路斯40保罗则选了西拉同行,弟兄姊妹把他们交托在主的恩典中。 41保罗走遍了叙利亚基利迦,巩固当地的各教会。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Matendo 15:1-41

Baraza La Yerusalemu

115:1 Gal 2:12; 5:2, 3; Mdo 6:14Baadhi ya watu wakashuka Antiokia kutoka Uyahudi, nao wakawa wanawafundisha wandugu: “Msipotahiriwa kufuatana na desturi aliyofundisha Mose, hamwezi kuokoka.” 215:2 Gal 2:2; Mdo 11:30Baada ya Paulo na Barnaba kutokubaliana nao kukawa na mabishano makali, Paulo na Barnaba na baadhi ya wengine miongoni mwao wakachaguliwa kwenda Yerusalemu ili kujadiliana jambo hili na mitume na wazee. 315:3 Mdo 14:27Hivyo wakasafirishwa na kanisa, wakiwa njiani wakapitia nchi ya Foinike na Samaria, wakawaeleza jinsi watu wa Mataifa walivyookoka. Habari hizi zikaleta furaha kubwa kwa ndugu wote. 415:4 Mdo 21:19Walipofika Yerusalemu, walipokelewa na kanisa na mitume pamoja na wazee, ndipo Paulo na Barnaba wakawaarifu kila kitu Mungu alichokuwa amefanya kupitia kwao.

515:5 Mdo 5:17; Mt 3:7; Mdo 15:1Ndipo baadhi ya walioamini wa madhehebu ya Mafarisayo wakasimama na kusema, “Hao watu wa Mataifa lazima watahiriwe na waagizwe kutii sheria ya Mose.”

6Mitume na wazee wakakutana pamoja ili kufikiri jambo hili. 715:7 Mdo 10:20; 11:12; 10:1-48Baada ya majadiliano mengi, Petro akasimama na kusema, “Ndugu zangu, mnajua kwamba siku za kwanza Mungu alinichagua ili kwa midomo yangu watu wa Mataifa wapate kusikia ujumbe wa Injili na kuamini. 815:8 Mdo 1:24; Ufu 2:23; Mdo 10:44, 47Mungu, yeye ajuaye mioyo, alionyesha kwamba anawakubali kwa kuwapa Roho Mtakatifu kama vile alivyotupa sisi. 915:9 Mdo 10:28, 34; 11:12; 10:43Mungu hakutofautisha kati yetu na wao, bali alitakasa mioyo yao kwa imani. 1015:10 Mt 23:4; Gal 5:1Sasa basi, mbona mnataka kumjaribu Mungu kwa kuweka kongwa shingoni mwa wanafunzi ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulibeba? 1115:11 Gal 2:16; Efe 2:5-8Lakini sisi tunaamini ya kuwa tunaokolewa kwa neema ya Bwana Yesu Kristo, kama wao wanavyookolewa.”

1215:12 Yn 4:48; Mdo 14:27; 21:19Kusanyiko lote likakaa kimya, wakawasikiliza Paulo na Barnaba wakieleza jinsi Mungu alivyowatumia kutenda ishara na maajabu kwa watu wa Mataifa. 1315:13 1Kor 15:7; Gal 1:19Walipomaliza kunena, Yakobo akasema, “Ndugu zangu, nisikilizeni. 1415:14 2Pet 1:1; Mdo 15:7; Lk 1:68Simoni amekwisha kutueleza jinsi Mungu, kwa mara ya kwanza alivyoonyesha kuhusika kwa kujichagulia watu kutoka watu wa Mataifa kwa ajili ya Jina lake. 1515:15 Amo 9:11-12Maneno ya manabii yanakubaliana na jambo hili, kama ilivyoandikwa:

1615:16 Amo 9:11-12“ ‘Baada ya mambo haya nitarudi,

nami nitajenga upya

nyumba ya Daudi iliyoanguka.

Nitajenga tena magofu yake

na kuisimamisha,

1715:17 Amo 9:11, 12ili wanadamu wengine wote

wapate kumtafuta Bwana,

hata wale watu wa Mataifa wote

ambao wanaitwa kwa Jina langu,

asema Bwana, afanyaye mambo haya’

1815:18 Isa 45:21ambayo yamejulikana tangu zamani.

1915:19 Mdo 15:28; 1The 1:9“Kwa hivyo uamuzi wangu ni kwamba, tusiwataabishe watu wa Mataifa wanaomgeukia Mungu. 2015:20 1Kor 8:7-13; Ufu 2:14, 20; 1Kor 10:7-8; Ufu 2:14; 20; Mwa 9:4; Law 7:26Badala yake, tuwaandikie kwamba wajiepushe na vyakula vilivyonajisiwa kwa kutolewa sanamu, wajiepushe na uasherati, au kula mnyama aliyenyongwa, na damu. 2115:21 Mdo 13:15; 2Kor 3:14-15Kwa maana katika kila mji kwa vizazi vilivyopita, Mose amekuwa na wale wanaotangaza sheria yake kwa kuwa imekuwa ikisomwa kwa sauti kubwa katika masinagogi kila Sabato.”

Barua Kwa Waumini Wa Mataifa

2215:22 Mdo 11:30; 16:19, 25, 26; 2Kor 1:19; 1The 1:1; 1Pet 5:12Mitume na wazee pamoja na kanisa lote, wakaamua kuwachagua baadhi ya watu wao na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba. Wakamchagua Yuda aitwaye Barsaba pamoja na Sila, watu wawili waliokuwa viongozi miongoni mwa ndugu. 2315:23 Mdo 20:23Wakatumwa na barua ifuatayo:

Sisi mitume na wazee, ndugu zenu,

Kwa ndugu Mataifa mlioamini mlioko Antiokia, Shamu na Kilikia:

Salamu.

2415:24 Mdo 15:1; Gal 1:7; 5:10Tumesikia kwamba kuna baadhi ya watu waliokuja huko kutoka kwetu bila ruhusa yetu na kuwasumbua, wakiyataabisha mawazo yenu. 25Hivyo tumekubaliana wote kuwachagua baadhi ya watu na kuwatuma kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paulo, 2615:26 Mdo 11:19; 11:23; 15:40; 13:13watu ambao wamehatarisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana wetu Yesu Kristo. 2715:27 Mdo 15:22Kwa hiyo tunawatuma Yuda na Sila, kuthibitisha kwa maneno ya mdomo mambo haya tunayowaandikia. 2815:28 Mdo 5:32Kwa maana imempendeza Roho Mtakatifu na sisi tusiwatwike mzigo wowote mkubwa zaidi ya mambo haya yafuatayo ambayo ni ya lazima: 2915:29 Mdo 21:25Kwamba mjiepushe na vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, au kula nyama ya mnyama aliyenyongwa, na mjiepushe na uasherati. Mkiyaepuka mambo haya, mtakuwa mmefanya vyema.

Kwaherini.

30Hivyo wakaagwa, wakashuka kwenda Antiokia. Baada ya kulikusanya kanisa pamoja, wakawapa ile barua. 31Nao hao watu wakiisha kuisoma, wakafurahishwa sana kwa ujumbe wake wa kutia moyo. 3215:32 Mdo 14:22; 18:23Yuda na Sila, ambao wenyewe walikuwa manabii, wakanena maneno mengi ya kuwatia moyo na kuwajenga katika imani wale ndugu walioamini. 3315:33 1Sam 1:17; Lk 7:50Baada ya kukaa huko Antiokia kwa muda, wakaagwa kwa amani na wale ndugu ili waende kwa wale waliowatuma. [ 3415:34 Mdo 4:36; 13:40Lakini Sila bado akaendelea kukaa huko.] 3515:35 Mdo 8:4Lakini Paulo na Barnaba walibaki Antiokia ambako wao pamoja na wengine wengi walifundisha na kuhubiri neno la Bwana.

Safari Ya Pili Ya Paulo Kueneza Injili

(15:36–18:22)

Paulo Na Barnaba Wagawanyika

3615:36 Mdo 13:4, 13, 14, 51; 14:1, 6, 24; 25Baada ya muda, Paulo akamwambia Barnaba, “Turudi tukawatembelee ndugu katika miji yote tuliyohubiri neno la Bwana tuone jinsi wanavyoendelea.” 3715:37 Mdo 12:12Barnaba alitaka wamchukue Yohana aitwaye Marko waende naye. 3815:38 Mdo 13:13Lakini Paulo aliona si vyema kwa sababu aliwahi kuwaacha walipokuwa huko Pamfilia, hakutaka kuendelea kufanya kazi naye. 39Pakatokea ubishi mkali kati ya Paulo na Barnaba kuhusu jambo hili, hivyo wakagawanyika. Barnaba akamchukua Yohana Marko wakasafiri baharini kwenda Kipro. 4015:40 Mdo 11:23; 15:41; Lk 2:2; Mdo 6:9; 16:5Lakini Paulo akamchagua Sila na akaondoka baada ya ndugu kuwatakia neema ya Bwana. 41Akapitia Shamu na Kilikia, akiimarisha makanisa ya huko.