使徒行传 12 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

使徒行传 12:1-25

希律王的暴行

1那时,希律王下手残害教会的一些人, 2杀了约翰的哥哥雅各3他见这样做能取悦犹太人,便又在除酵节期间拘捕了彼得4把他关在监里,由四班卫兵,每班四人轮流看守,想等逾越节12:4 除酵节为期七天,逾越节是其中的第一天,参见出埃及记12章。过后当众惩办他。 5彼得被囚期间,教会都迫切地为他向上帝祷告。

彼得神奇出狱

6在被希律提审前一夜,彼得被两条铁链锁着睡在两个卫兵中间,门外警卫森严。 7忽然,有一位主的天使站在彼得身旁,监牢内一片光明,天使拍他的肋旁,把他叫醒,说:“赶快起来!”铁链就从他手上脱落下来。 8天使对他说:“束上腰带,穿好鞋子。”彼得一一照办。天使又说:“披上外衣,跟我来!” 9他跟着天使走出牢房,不知道这一切都是真的,还以为自己看到了异象。 10他们一路穿过第一道和第二道守卫,来到通往城里的铁门,那门竟自动打开了。他们就出来,走过一条街之后,天使便离开了彼得

11彼得这才如梦初醒,说:“现在我确定,主派了天使来救我脱离希律的魔掌,不让犹太人的期望得逞。” 12他清醒后,便到约翰·马可的母亲玛丽亚家,很多人正聚集在那里祷告。

13彼得在外面敲门,有一个叫罗大的婢女出来应门。 14她听出是彼得的声音,喜出望外,竟然没有开门就跑进去告诉大家:“彼得在门外!” 15他们说:“你一定疯了。”她坚持说:“是真的!”他们就说:“是他的天使吧!”

16彼得不住地敲门。他们开门看见他,都大吃一惊! 17彼得摆手示意他们安静,然后把主怎样领他出狱的经过告诉大家,又说:“把这事告诉雅各和其他弟兄姊妹。”交待完了,他便离开那里,往其他地方去了。

18天亮后,监狱的守卫发现彼得不见了,顿时一片骚动。 19希律派人四处搜捕,一无所获,于是亲自审问看守彼得的卫兵,下令处决他们。后来希律离开犹太,下到凯撒利亚,并住在那里。

希律的下场

20希律泰尔西顿的人非常恼火。于是,他们联合起来去见他,先取得宫廷总管伯拉斯都的支持,然后向他求和,因为他们两地需要从他的辖区获得粮食。

21到了约定的日子,希律穿上王袍,坐在宝座上向众人致词。 22致词完毕,众人齐声高呼:“这是神明在说话,不是凡人在说话!” 23希律没有把荣耀归给上帝,主的天使立刻惩罚他,他当场被虫子咬死了。

24上帝的道日见兴旺,越传越广。

25巴拿巴扫罗把款项送到以后,就带着约翰·马可耶路撒冷回去。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Matendo 12:1-25

Yakobo Auawa, Petro Atiwa Gerezani

112:1 Mt 14:1Wakati huo huo Mfalme Herode Agripa aliwakamata baadhi ya watu wa kanisa. 212:2 Mt 4:21; Mk 10:39Akaamuru Yakobo, ndugu yake Yohana, auawe kwa upanga. 312:3 Mdo 24:27; 25:9; Kut 12:15; 23:15; Mdo 20:6Alipoona jambo hilo limewapendeza Wayahudi, akaendelea, akamkamata pia Petro. Hii ilitokea wakati wa Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. 412:4 Yn 11:15Baada ya kumkamata alimtia gerezani, chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari, vyenye askari wanne kila kimoja. Herode alikuwa amekusudia kumtoa na kumfanyia mashtaka mbele ya watu baada ya Pasaka.

512:5 Mdo 1:14; Efe 6:18Kwa hiyo Petro akawekwa gerezani, lakini kanisa lilikuwa likimwombea kwa Mungu kwa bidii.

612:6 Mdo 21:33Usiku ule kabla ya siku ambayo Herode Agripa alikuwa amekusudia kumtoa na kumfanyia mashtaka, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili, akiwa amefungwa kwa minyororo miwili. Nao walinzi wa zamu walikuwa wakilinda penye lango la gereza. 712:7 Mdo 5:19; Za 107:14; Mdo 16:26Ghafula malaika wa Bwana akatokea na nuru ikamulika mle ndani ya gereza. Yule malaika akampiga Petro ubavuni na kumwamsha, akisema, “Ondoka upesi!” Mara ile minyororo ikaanguka kutoka mikononi mwa Petro.

8Yule malaika akamwambia, “Vaa nguo zako na viatu vyako.” Petro akafanya hivyo. Kisha akamwambia, “Jifunge vazi lako na unifuate.” 912:9 Mdo 9:10Petro akatoka mle gerezani akiwa amefuatana na yule malaika. Hakujua wakati huo kuwa yaliyokuwa yakitukia yalikuwa kweli. Alidhani kuwa anaona maono. 1012:10 Mdo 5:19; 16:26Wakapita lindo la kwanza na la pili, ndipo wakafika kwenye lango la chuma linaloelekea mjini. Lango likawafungukia lenyewe, nao wakapita hapo wakatoka nje. Baada ya kutembea umbali wa mtaa mmoja, ghafula yule malaika akamwacha Petro.

1112:11 Lk 15:17; Za 34:7; Dan 3:28; 6:22; 2Kor 11:10; 2Pet 2:9Ndipo Petro akarudiwa na fahamu, akasema, “Sasa ninajua bila shaka yoyote kuwa Bwana amemtuma malaika wake na kuniokoa kutoka makucha ya Herode Agripa na kutoka matazamio yote ya Wayahudi.”

1212:12 Mdo 12:25; 15:37; Kol 4:10; 2Tim 4:11; 1Pet 5:13Mara Petro alipotambua hili alikwenda nyumbani kwa Maria, mama yake Yohana aliyeitwa pia Marko, ambako watu wengi walikuwa wamekutana kwa maombi. 1312:13 Yn 18:16Petro alipobisha hodi kwenye lango la nje, mtumishi wa kike jina lake Roda, akaja kumfungulia. 1412:14 Lk 24:41Alipoitambua sauti ya Petro, alifurahi mno akarudi bila kufungua na kuwaeleza kwamba, “Petro yuko langoni!”

1512:15 Mt 18:10Wakamwambia yule mtumishi wa kike, “Umerukwa na akili.” Alipozidi kusisitiza kuwa ni kweli, wakasema, “Lazima awe ni malaika wake.”

16Lakini Petro aliendelea kugonga langoni, nao walipofungua lango na kumwona Petro, walistaajabu sana. 1712:17 Mdo 19:33; 21:40Yeye akawaashiria kwa mkono wake wanyamaze kimya, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa gerezani. Naye akaongeza kusema, “Waelezeni Yakobo na ndugu wengine habari hizi.” Kisha akaondoka akaenda sehemu nyingine.

1812:18 Mdo 5:21, 22Kulipokucha kukawa na fadhaa kubwa miongoni mwa wale askari kuhusu yaliyomtukia Petro. 1912:19 Mdo 8:1-4; 16:27; 8:40Baada ya Herode kuamuru atafutwe kila mahali na bila kumpata, aliwahoji wale askari walinzi kisha akatoa amri wauawe. Basi Herode Agripa akatoka Uyahudi akaenda Kaisaria, akakaa huko kwa muda.

Kifo Cha Herode Agripa

2012:20 Mt 11:21; 1Fal 5:9, 11; Eze 27:17Basi Herode Agripa alikuwa amekasirishwa sana na watu wa Tiro na Sidoni. Hivyo watu wa miji hiyo miwili wakaungana pamoja wakatafuta kukutana naye. Wakiisha kuungwa mkono na Blasto, mtumishi maalum wa Mfalme Herode Agripa aliyeaminika, wakaomba mapatano ya amani maana nchi zao zilitegemea nchi ya huyo mfalme kwa mahitaji yao ya chakula.

21Katika siku iliyochaguliwa Herode Agripa akavaa mavazi yake ya kifalme, akaketi kwenye kiti chake cha enzi na kuwahutubia watu. 2212:22 Eze 28:2Watu waliokuwa wamekusanyika wakapiga kelele, wakisema, “Hii si sauti ya mwanadamu, bali ni ya Mungu.” 2312:23 Mdo 5:19; 1Sam 25:38; 2Sam 24:16; 2Fal 19:35Ghafula, kwa kuwa Herode hakumpa Mungu utukufu, malaika wa Bwana akampiga, naye akaliwa na chango, akafa.

2412:24 Ebr 4:12; Mdo 6:7; 19:20Lakini neno la Mungu likaendelea mbele na kuenea, nao wengi wakaambatana nalo.

2512:25 Mdo 4:36; 11:30; 12:12Barnaba na Sauli walipomaliza ile huduma yao iliyowapeleka, wakarudi Yerusalemu wakiwa pamoja na Yohana aitwaye Marko.