但以理书 10 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

但以理书 10:1-21

底格里斯河边的异象

1波斯塞鲁士执政第三年,但以理,又名伯提沙撒,得到启示。这启示是真实的,是关于一场大争战的事。但以理通过异象明白了启示的意思。

2那时,我但以理悲伤了三个星期, 3期间没有吃过美味,没有尝过酒肉,没有抹过膏油。 4一月二十四日,我站在底格里斯河边, 5举目观看,见有一个人身穿细麻衣,腰束纯金的带子, 6身体如碧玉,面貌如闪电,眼睛如火炬,四肢如明亮的铜,声音如众人的呼喊。 7只有我但以理看见了这异象,跟我在一起的人都没有看见,但他们极其恐惧,纷纷逃匿, 8只剩下我一人观看这奇异的景象。我浑身无力,脸色苍白,精疲力尽。 9接着,我听见他说话的声音,一听见他的声音,我便俯伏在地上昏睡过去。 10忽然有一只手轻拍我,扶我用膝和手掌支撑起身体。 11他对我说:“倍受眷爱的但以理啊,要留心听我说,站起来吧,因为我是奉命到你这里来的。”他说完这话,我便战战兢兢地站起来。 12他说:“但以理啊,不要怕,从你在上帝面前谦卑地恳求明白这异象的第一天,你的祷告已蒙垂听。我是来答复你的。 13波斯国的守护神拦阻我二十一日。由于我滞留在波斯诸王那里,天使长米迦勒便来帮助我。 14我来是要使你明白将来你同胞的遭遇,因为这异象是关于将来的事。” 15他对我说话时,我低着头,说不出话。 16后来,有一位样子像人的用手摸我的嘴唇,我便开口对站在我面前的说:“我主啊,因为这异象,我痛苦不堪,毫无气力。 17仆人我怎能跟我主说话?我现在浑身无力,没有气息。”

18于是,那位样子像人的再次摸我,使我有力量。 19他对我说:“倍受眷爱的人啊,不要怕,愿你平安!要刚强勇敢。”我听到他的话,便有了力量,于是对他说:“我主啊,请说,因为你使我有了力量。” 20他说:“你知道我为什么要到你这里来吗?现在我要回去与波斯的守护神争战。我离开后,希腊的守护神就会来。 21除了你们的守护天使米迦勒以外,谁也不能帮助我抵挡他们。我来是要把记录在真理书上的事告诉你。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Danieli 10:1-21

Maono Ya Danieli Kuhusu Mtu

110:1 Dan 1:7, 21; 8:26Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, Danieli (ambaye aliitwa Belteshaza) alipewa ufunuo. Ujumbe wake ulikuwa kweli, nao ulihusu vita vikubwa. Ufahamu wa ujumbe ulimjia katika maono.

210:2 Ezr 9:4Wakati huo, mimi Danieli nikaomboleza kwa majuma matatu. 310:3 Dan 6:18Sikula chakula kizuri; nyama wala divai havikugusa midomo yangu; nami sikujipaka mafuta kamwe mpaka majuma matatu yalipotimia.

410:4 Mwa 2:14; Dan 2:15; 12:5Kwenye siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kwanza, nilipokuwa nimesimama kwenye ukingo wa mto mkubwa Hidekeli,10:4 Hedekeli ndio Mto Tigrisi. 510:5 Ezr 9:2; Ufu 15:6; Yer 10:9; Dan 8:3nikatazama juu, na mbele yangu alikuwepo mtu aliyevaa mavazi ya kitani na mshipi wa dhahabu safi kutoka ufazi kiunoni mwake. 610:6 Mt 17:2; 28:3; Ay 41:19; 19:12; Ufu 19:12; 1:15; Kut 28:20; Eze 1:24Mwili wake ulikuwa kama kito cha zabarajadi safi, uso wake kama umeme wa radi, macho yake kama mwali wa moto, mikono yake na miguu yake kama mngʼao wa shaba iliyosuguliwa sana, nayo sauti yake kama ya umati mkubwa wa watu.

710:7 2Fal 6:17-20; Mdo 9:2Mimi Danieli, ni mimi peke yangu niliyeona hayo maono; watu waliokuwa pamoja nami hawakuyaona, lakini waligubikwa na hofu kuu, hata wakakimbia na kujificha. 810:8 Mwa 32:24; Ay 4:14; Dan 8:27; Hes 3:16; Ay 4:15; Hab 3:16Kwa hiyo niliachwa peke yangu, nikikodolea macho maono hayo makubwa; sikubakiwa na nguvu, na rangi ya uso wangu ikabadilika kama aliyekufa, nikakosa nguvu. 910:9 Dan 8:18; Mt 17:6; Wim 5:2Kisha nikamsikia akisema, nami nilipokuwa nikimsikiliza, nikalala kifudifudi, nikapatwa na usingizi mzito.

1010:10 Yer 1:9; Ufu 1:17Mkono ulinigusa, ukaninyanyua, na kuniweka nikipiga magoti na mikono yangu ikashika chini, huku nikiwa bado ninatetemeka. 11Akasema, “Danieli, wewe mtu upendwaye sana, fikiri kwa makini maneno ninayokwenda kunena nawe sasa; simama wima, kwa maana sasa nimetumwa kwako.” Naye aliponiambia haya, nikasimama nikitetemeka.

1210:12 Law 16:31; Dan 9:3, 20; Mt 14:27; Isa 65:24Ndipo akaendelea kusema, “Danieli, usiogope. Tangu siku ya kwanza ulipotia moyo wako ili kupata ufahamu na kujinyenyekeza mbele ya Mungu wako, maneno yako yalisikiwa, nami nimekuja ili kujibu maneno yako. 1310:13 Dan 12:1; Yud 9; Isa 24:21Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga kwa siku ishirini na moja. Ndipo Mikaeli, mmoja wa malaika wakuu, alikuja kunisaidia, kwa sababu nilikuwa nimezuiliwa huko na mfalme wa Uajemi. 1410:14 Dan 9:22; 2:28; Hab 2:3; Dan 8:26; Eze 12:27Sasa nimekuja kukuelezea mambo yatakayowatokea watu wako wakati ujao, kwa maana maono hayo yanahusu wakati ambao haujaja bado.”

1510:15 Eze 24:27; Lk 1:20; Dan 8:18Alipokuwa akinielezea haya, nilisujudu uso wangu ukiwa umeelekea chini, nikawa bubu. 1610:16 Isa 6:7; 21:3; Yer 1:9; Dan 8:15-18Ndipo mmoja aliyeonekana kama mwanadamu akanigusa midomo yangu, nami nikafungua kinywa changu, nikaanza kunena. Nikamwambia yule aliyesimama mbele yangu, “Nimepatwa na huzuni kubwa kwa sababu ya maono haya, bwana wangu, nami nimeishiwa nguvu. 1710:17 Dan 4:19Bwana wangu, mimi mtumishi wako nitawezaje kuzungumza na wewe? Nguvu zangu zimeniishia hata ninashindwa kupumua.”

1810:18 Dan 8:18Tena yule aliyeonekana kama mwanadamu akanigusa na kunitia nguvu. 1910:19 Kut 14:13; Amu 6:23; Isa 35:4; 6:1-8; Yos 1:9; Rum 8:31; Dan 9:23Akasema, “Ee mtu upendwaye sana, usiogope. Amani iwe kwako! Uwe na nguvu sasa; jipe nguvu.”

Alipozungumza nami, nilipata nguvu, nikasema, “Nena, bwana wangu, kwa kuwa umenipa nguvu.”

2010:20 Dan 8:21; 11:2Kwa hiyo akasema, “Je, unajua kwa nini nimekujia? Sasa hivi nitarudi kupigana dhidi ya mkuu wa Uajemi, nami nikienda, mkuu wa Uyunani atakuja. 2110:21 Dan 11:2; Yud 9Lakini kwanza nitakuambia kile kilichoandikwa katika Kitabu cha Kweli. (Hakuna hata mmoja anayenisaidia dhidi yao isipokuwa Mikaeli, mkuu wenu.