以斯帖记 6 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

以斯帖记 6:1-14

王赐末底改尊荣

1那夜王睡不着觉,就吩咐人拿史书念给他听。 2刚好念到末底改揭发两位守门太监辟探提列谋害亚哈随鲁王的事, 3王便问:“末底改既行此事,可曾赐他什么尊荣和爵位吗?”服侍王的臣仆回答说:“没有赐他什么。” 4王问:“谁在院子里?”那时哈曼刚进到王宫外院,想请求王将末底改吊在他预备的木架上。 5服侍王的臣仆回答说:“是哈曼站在院子里。”王说:“让他进来。” 6哈曼进来后,王问他:“王愿意赏识一个人,该怎么做呢?”哈曼心想:“王愿意赏识的人不是我是谁呢?” 7于是,他就对王说:“王若愿意赏识一个人, 8可以拿来王穿过的袍子,牵来王骑过的戴冠的御马, 9交给王最尊贵的一位大臣,给王所愿意赏识的人穿上,让他骑着马在城中的广场上游行,并派人在他前面宣告,‘王愿意赏识谁,就会这样待他。’” 10王对哈曼说:“快去照你说的,把王袍和御马赐给在宫门供职的犹太末底改。你所说的一样也不可少。” 11于是,哈曼将袍子给末底改穿上,让他骑着马在城中的广场上游行,并在他前面宣告:“王愿意赏识谁,就会这样待他。”

12之后,末底改回到宫门那里,哈曼却悲伤地蒙着头匆匆回家去了。 13他将自己的遭遇详细告诉妻子细利斯和所有的朋友。他的谋士及其妻子细利斯对他说:“你开始在末底改面前败落。如果他是犹太人,你必胜不过他,终必在他面前败落。”

14他们正在谈论的时候,王的太监来催哈曼赶快去赴以斯帖预备的宴席。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Esta 6:1-14

Mordekai Anapewa Heshima

16:1 Dan 6:18; Es 2:23Usiku ule mfalme hakupata usingizi, hivyo akaagiza aletewe kitabu cha kumbukumbu za matukio ya utawala wake, asomewe. 2Kitabu hicho kilikutwa na kumbukumbu kwamba Mordekai alikuwa amefichua jinsi Bigthana na Tereshi, waliokuwa maafisa wawili wa mfalme, walinzi wa lango walivyokuwa wamepanga hila ya kumuua Mfalme Ahasuero.

36:3 Mhu 9:13-16Mfalme akauliza, “Je, ni heshima na shukrani gani Mordekai alipokea kwa ajili ya jambo hili?”

Watumishi wake wakajibu, “Hakuna lolote alilofanyiwa.”

4Mfalme akasema, “Ni nani yuko uani?” Wakati huo huo Hamani alikuwa ameingia ua wa nje wa jumba la mfalme kusema na mfalme kuhusu kumwangika Mordekai katika mahali pa kuangikia watu alipokuwa amepajenga kwa ajili yake.

5Watumishi wake wakamjibu, “Hamani amesimama uani.”

Mfalme akaamuru, “Mleteni ndani.”

6Hamani alipoingia, mfalme alimuuliza, “Afanyiwe nini mtu ambaye mfalme apenda kumheshimu?”

Basi Hamani akawaza moyoni mwake, “Ni nani mwingine ambaye mfalme angemheshimu kuliko mimi?” 7Kwa hiyo akamjibu mfalme, “Kwa mtu ambaye mfalme apenda kumheshimu, 86:8 Mwa 41:42; Isa 52:1aletewe joho la kifalme ambalo mfalme ameshalivaa na farasi ambaye mfalme alishampanda, ambaye amevikwa taji ya kifalme kichwani mwake. 96:9 Mwa 41:43Kisha joho na farasi vikabidhiwe kwa mmojawapo wa wakuu wa mfalme anayeheshimika sana. Nao wamvike mtu yule ambaye mfalme anapenda kumheshimu, na aongozwe akiwa juu ya farasi kupitia barabara za mji, wakitangaza mbele yake, ‘Hivi ndivyo anavyofanyiwa mtu ambaye mfalme apenda kumheshimu!’ ”

10Mfalme akamwamuru Hamani, “Nenda mara moja, chukua joho na farasi na ufanye kama vile ulivyopendekeza kwa Mordekai Myahudi, akaaye langoni mwa mfalme. Usipuuze kufanya kitu chochote ulichoshauri.”

11Hivyo Hamani akachukua joho na farasi.

Akamvika Mordekai, na kumpandisha juu ya farasi akamtembeza katika barabara za mji akitangaza mbele yake, “Hivi ndivyo anavyofanyiwa mtu ambaye mfalme anapenda kumheshimu!”

126:12 2Sam 15:30; Mik 3:7Baadaye Mordekai akarudi kwenye lango la mfalme. Lakini Hamani akakimbia nyumbani, akiwa amejaa huzuni, 136:13 Za 57:6; Mit 26:27naye akamweleza Zereshi mkewe pamoja na rafiki zake wote kila kitu ambacho kimempata.

Washauri wake pamoja na Zereshi mkewe wakamwambia, “Kwa kuwa Mordekai, ambaye mbele yake umeanza kuanguka ni wa asili ya Kiyahudi, huwezi kushindana naye; kwa hakika utaanguka!” 14Walipokuwa bado wakizungumza naye, matowashi wa mfalme wakaja na kumharakisha Hamani aende katika karamu aliyoiandaa Esta.