Забур 116 – CARST & NEN

Священное Писание (Восточный перевод), версия для Таджикистана

Забур 116:1-2

Песнь 116

1Славьте Вечного, все народы,

хвалите Его, все племена!

2Потому что велика милость Вечного к нам

и верность Его пребудет вовеки.

Славьте Вечного!

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 116:1-19

Zaburi 116

Shukrani Kwa Kuokolewa Kutoka Mauti

1116:1 Za 18:1; 31:22; 40:1; 6:9; 28:2Ninampenda Bwana kwa maana amesikia sauti yangu;

amesikia kilio changu ili anihurumie.

2116:2 Za 5:1Kwa sababu amenitegea sikio lake,

nitamwita siku zote za maisha yangu.

3116:3 2Sam 22:6; Za 18:4-5Kamba za mauti zilinizunguka,

maumivu makuu ya kuzimu yalinipata,

nikalemewa na taabu na huzuni.

4116:4 Za 80:2, 18; 118:5Ndipo nikaliitia jina la Bwana:

“Ee Bwana, niokoe!”

5116:5 Kut 22:27; 9:27; Ezr 9:15; Za 11:7; 86:15; 2Nya 12:6; Neh 9:8; Yer 12:1; Mao 1:18; Ufu 16:5Bwana ni mwenye neema na haki,

Mungu wetu ni mwingi wa huruma.

6116:6 Za 79:8; 18:3; 22:5; 107:13Bwana huwalinda wanyenyekevu,

nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa.

7116:7 Za 13:6; 106:1; 142:7; 46:10; 62:1; 131:2; Mt 11:29; Yer 6:16Ee nafsi yangu, tulia tena,

kwa kuwa Bwana amekuwa mwema kwako.

8116:8 Za 86:13Kwa kuwa wewe, Ee Bwana,

umeniokoa nafsi yangu na mauti,

macho yangu kutokana na machozi,

miguu yangu kutokana na kujikwaa,

9116:9 Mwa 5:22; Za 56:13; 89:15; 27:13; Ay 28:13; Isa 38:11; Yer 11:9ili niweze kutembea mbele za Bwana,

katika nchi ya walio hai.

10116:10 Za 9:18; 72:2; 107:17; 119:67, 71, 75; 2Kor 4:13Niliamini, kwa hiyo nilisema,

“Mimi nimeteseka sana.”

11116:11 Yer 9:3-5Katika taabu yangu nilisema,

“Wanadamu wote ni waongo.”

12116:12 Za 103:2; 106:1Nimrudishie Bwana nini

kwa wema wake wote alionitendea?

13116:13 Za 105:1Nitakiinua kikombe cha wokovu

na kulitangaza jina la Bwana.

14116:14 Hes 30:2; Za 66:13Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana

mbele za watu wake wote.

15116:15 Za 72:14; Hes 23:10; Ay 5:26; Lk 16:22; Ufu 14:13Kifo cha watakatifu kina thamani

machoni pa Bwana.

16116:16 Za 119:125; 143:12; 86:16; Ay 12:18Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako,

mimi ni mtumishi wako,

mwana wa mjakazi wako;116:16 Au: mwanao mwaminifu.

umeniweka huru

toka katika minyororo yangu.

17116:17 Law 7:12; Ezr 1:4Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru

na kuliita jina la Bwana.

18116:18 Za 116:14; Law 22:18Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana

mbele za watu wake wote,

19116:19 Za 102:21; 92:13; 135:2; 96:8; 100:4katika nyua za nyumba ya Bwana,

katikati yako, ee Yerusalemu.

Msifuni Bwana.